Katika hali ya kushitua! katibu kata wa CCM kata Mbugani wilaya ya Tabora Mjini, Bwana Kasimu Idrisa amefarika Dunia dakika chache zilizopita baada ya kupokea barua ya kusimamishwa uongozi uliosababishwa na yeye kupoteza mitaa mingi kama kiongozi. Kata ya Mbugani yenye jumla ya mitaa 11 katika uchaguzi wa mitaa uliomalizika siku chache zilizopita CCM walipata mitaa 5 CUF 5 na UDP 1. kwa matokeo hayo katibu wa CCM mkoa wa Tabora alimsimamisha uongozi katibu kata huyo hasa baada ya kupewa taarifa zisizo rasmi na Diwani wa kata ambaye pia ni katibu wa siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Tabora Bwana Kapama, habari ninazoendelea kuzipata ni kuwa mahusiano ya Mh Diwani kapama na katibu kata hayakuwa mazuri hivyo baada ya matokeo hayo Diwani alimshitaki katibu kata wake CCM mkoa kuwa ndiye aliyesababisha kupotea kwa mitaa mingi hali ilisababisha katibu kata huyo kupewa barua ya kusimamishwa jana na leo asubuhi kuugua ghafla na kupelekwa Hospitali ya Kalunde ambapo amefariki Dunia.