Katibu CCM afichua Siri ya Mnyika kumzushia Mama Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu CCM afichua Siri ya Mnyika kumzushia Mama Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Habarindiyohiyo, Apr 25, 2012.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katibu Msaidizi wa Idara ya Siasa na Uhusiano ya CCM Charles Charles amemuumbua Mbunge wa Ubungo John Mnyika kutokana na madai yake ya uongo bungeni dhidi ya mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

  Katibu huyo amefichua siri kuwa Mnyika alitoa madai ya uongo ya WAMA kutumiwa kwenye kampeni ili kuficha ukweli NGO nyingi zimekuwa zikitumiwa na CHADEMA kuishambulia serikali ya CCM na kuwakashifu viongozi wake.

  Amefichua siri nzito kuwa hata kauli za kutishia kuitisha maandamano nchi nzima zinazotolewa na NGO hizo zinatokana na CHADEMA.

  Katibu huyo wa CCM amempongeza Sophia Simba kwa majibu yake na kuwaomba wananchi wapuuze uzushi unaosambazwa dhidi ya mke wa Rais.

  Chanzo: Gazeti Kongwe la Chama
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Najua wewe ndiyo Charles Charles.Nakuhurumia sana kwani upeo wako ni sawa na Lusinde
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Gaziti gani hili? Maana kama ni lile la udaku wa kisiasa, limeshapoteza umaarufu.
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mnyika ana ushahidi wa gazeti ambapo wakati wa kampeni ilitolewa ahadi kuwa JK akichaguliwa WAMA itasomesha watoto 5 bure.
   
 5. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  DUhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!samahani kwa kujaza saver....
   
 6. s

  simon james JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM mnatapatapa hakuna mwenye akili atakaye puuza hoja ya mnyika
   
 7. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe na gazeti lako UHARO jifunzeni ustaarabu wa kuandika habari za ukweli. Siri ipi wakati ilizungumziwe kwenye Bunge Live?
   
 8. Y

  Young zee JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 398
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tangu lini magamba wakakubali ukweli? Na gazeti hilo halina jina?
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wamekutuma? Huna tofauti na Wasira na Lusinde!!!? Hakuna cha NGO hapa, sasa kuna watanzania ambao mwamko wa kisiasa wanao na wanajua kibaya na kizuri. Hawadanganyiki tena!!!
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kaongea nini sasa!?
  magamba ni magamba tuu kweli chama changu ccm kinatakiwa kife tuu,
  naye anaona anaandika utetezi kumba hamna kitu!
   
 11. k

  kajembe JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  hahahahahahahahahshahhahaha! gazeti la Uhuru,sijasoma gaziti hilo miaka mingi kweli aisee kumbe lipo duh!
   
 12. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Sasa hiyo siri ya huyo kila kilaza juu ya Mnyika iko wapi?! Kama sio upuuzi tu wa kulopoka na kutaka cheap popularity kupitia watu makini kama Mnyika, Tatizo la magamba hamna Mungu ndio maana hata midomo yenu haina speeed governor.
   
 13. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  For real???? Nani asiiyejua WAMA ni ufisadi mtupu...NGO za kujinufaisha kifamilia. Mnyika hakusema uongo ila huyo sijui katibu ndiye anayesema uongo.
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  siku zote magamba ni wezi
  wanapenda kukanusha yanayowaumbua na kuwahadaa wananchi ili wajisafishe
  sawa na ikulu wanavopenda kukanusha haraka habari za ukweli
  lakini mambo ya msingi hayatolewi ufafanuzi
  ukweli uko pale pale WAMA ilitumika ktk kampeni na mama jk alitumia rasilimali za nchi kumkampenia mr wake
  tuajua haya yote sisi sio wajinga tumeelimika vema kwa hivo mda wa kudanganya umekwisha
  subirini tsunami iwakaushe.tukishindwa sisi Mungu atawezesha kama alivomtoa rais korofi wa Malawi
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,782
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Njaa kiboko. Inakufanya unapoteza akili na kuongea maneno ya ajabu!
   
 16. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bwana charles charles mbona umeumbuka mwenyewe na gazeti lako la chama chako siri gani uliyofichua kama sio uzushi kama vipi lala.
   
 17. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hivi nani kati yetu anaweza kusimama na kuitetea CCM na Serikali???
   
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Ni mtanzania gani anaweza kusahau kwamba kampeni za urais wa ccm zilisimamiwa na familia yake kwa kutumia fedha za UMA.
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]RITA yakumbwa na kigugumizi kuzungumzia WAMA [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 23 September 2010 21:47 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Abdallah Bakari na Beatrice John

  WAKALA wa Ufilisi na Udhamini (Rita) imepatwa na kigugumizi kuzungumzia madai yaliyoibuka hivi karibuni dhidi ya mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), mama Salma Kikwete kutumia taasisi hiyo kufanya kampeni dhidi ya mgombea wa urais wa CCM, Jakaya Kikwete

  Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Philip Saliboko amesema kwa sasa ni mapema kujua iwapo mwenyekiti huyo yupo sahihi au anavunja sheria.

  “Nahitaji muda kufuatilia katika nyaraka za WAMA kuona kama malengo ya usajili wake, yanatoa fursa ya kushiriki katika kampeni za kisiasa au laa…. Hata hivyo tutahitaji kujiridhisha na madai hayo pasipo na shaka, hadi Alhamisi wiki ijayo nitakuwa tayari kusema juu ya madai hayo,” alisema Saliboko

  Salma Kikwete ni mwenyekiti wa WAMA, ambaye amekuwa akishiriki katika kumpigia kampeni za urais mumewe (Jakaya Kikwete) na kuzua mjadala unaohoji kama anaruhusiwa kutumia rasilimali za serikali na za WAMA kumfanyia kampeni mume wake.

  Saliboko alisema sheria ya usajili wa ufilisi na udhamini kifungu kidogo namba 318 ya mwaka 2002 inatoa mamlaka kwa Rita kuzifuta taasisi zinazofanya shughuli zake kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.

  “Si asasi zote, mashirika au taasisi zinazokatazwa kujiingiza katika siasa, zipo zilizoanzishwa kwa misingi ya kisiasa, hizo hatuna tatizo nazo ila zile ambazo zinatumia fursa zilizopo kujiingiza katika siasa tutazishughulikia,” alisema ofisa huyo.

  Alionya kuwa mashirika, asasi za kiraia na taasisi zisizo za kiserikali hazina budi kujiweka kando na siasa iwapo malengo ya kuanzishwa kwake hayashabiani ya siasa, zitajiingiza kwenye matatizo yanayoweza kusababisha zitafutiwa usajili wake.

  Alisema kwa mujibu wa sheria taasisi zote zinapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia malengo ya usajili wake na si kinyumecho na kwamba kujiingiza katika masula nje ya yaliyobainishwa katika usajili ni kuvunja sheria.

  “Iwapo tutajiridhisha kuwa asasi, shirika au taasisi zisizo za kiserikali zinajihusisha katika masuala ya kisiasa, ikiwemo kukipigia kampeni chama au mgombea fulani kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake tutazifuta kwa mujibu wa sheria,” alisema Saliboko na kuongeza;

  Hadi sasa hakuna taarifa rasmi za kuwepo kwa taasisi zinazojihusisha na kampeni kinyume cha sheria, ila tunaratibu hilo na pale tutakapothibitisha kuwapo kwa vitendo hivyo hatutasita kuchukua hatua,” alisema Saliboko.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 20. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ivi huyo charles charles ni yule jamaa mwenye C&C, hapo kinondoni?
   
Loading...