Katiba zibadilishwe, Watoto wanahitaji uhuru wa maamuzi yao, mahari inatumika kuwafanya watumwa

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Kila mwaka Juni 16 huwa ni siku ya kukumbuka watoto waliouawa katika Kitongoji cha Soweto, Nchini Afrika Kusini wakati wakiandamana kupinga ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendeshwa na utawala wa wakati huo wa Makaburu.

Mauaji yalifanyika mwaka 1976 wakati watoto hao waliokuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za kibinadamu.

Kutokana na kutokea kwa mauaji hayo mnamo mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) (Sasa Umoja wa Afrika) ulipitisha Azimio la kuwakumbuka watoto.

Kila mwaka Tanzania huwa inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hiyo ili kukumbusha umuhimu wa kumlinda mtoto dhidi ya vikwazo vinavyoweza kukwamisha ndoto yake ya baadaye.

Wakati mwingine wakati wa kuadhimisha siku hii kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, mtu hautakiwi kupiga picha na mtoto na kuituma kwenye mtandao wa kijamii akionyesha kuwa hupo tayari kumlinda mtoto ili aweze kutimiza ndoto yake.

Kila mwaka wakati wa kuadhimisha kumbukumbu hiyo ni lazima Nchi za Afrika zikatafakari mifumo mbalimbali ya kisheria inayochangia ukatili dhidi ya watoto.

Mfano mzuri tatizo la ndoa za utotoni. Kwa Afrika ndoa hizi za utotoni zinatokana na sheria za kiraia, kimila na kidini kutokana na kuwa zinaingiliana. Mkanganyiko huo umesababisha kukosekana ufumbuzi wa moja kwa moja wa kukomesha ndoa za utotoni.

Kutokana na ukubwa wa tatizo wa ndoa za utotoni Septemba, miaka ya karıbunı viongozi wa Afrıka walijiunga na Mataita mengine na kupitisha Mpango wa Malengo wa Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), ambao mpango wake ni kukomesha ndoa za utotoni kipindi cha miaka 15 ijayo.

Mikataba ya Haki za Binadamu hususani kwa wanawake na watoto hasa za Serikali za Kiafrika zilikubalina kwamba umri wa chini wa kuolewa uwe miaka 18.

Katika mkutano wa kwanza kuhusu mwisho wa ndoa za utotoni, Umoja wa Afrika ulikubaliana kufanyike mageuzi ya kisheria pamoja na nchi hizo kubadilishana taarifa kuhusu mbinu bora za kumaliza ndoa za utotoni.

Utafiti uliofanywa na Waangalizi wa Haki za Binadamu katika nchini Malawi, Sudan Kusini, Tanzania na Zimbabwe umeonesha kuwa kukosekana kwa mikakati ya kina ya kitaifa juu ya ndoa za utotoni, utaratibu duni miongoni mwa wizara za Serikali na mashirika kunadhoofisha ufanisi wa jitihada za Serikali za Afrika kutokomeza ndoa za utotoni.

Hii inatoa picha kwamba Serikalı za Afrika zinapaswa kutoa ahadi ya mabadiliko kwenye sheria za kiraia, kimila na kidini. Tanzania ikiwa ni moja ya nchi za Afrika zınazoathiriwa na ndoa za utotoni imekuwa kikwamishwa na upungufu uliomo kwenye sheria za kimila, kidini na kiraia.

Mfano, kwa Tanzania sheria za kimila (sheria ya hali za watu) katika tangazo la Serikali namba 279 la mwaka 1963 linaruhusu kila kabila kufuata na kufanya uamuzi kulingana na kabila lake na kuruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya umri mdogo pale mila na utamaduni zinaporuhusu.

Lakini pia kichocheo kingıne kwa Tanzania cha ndoa za utotoni ni sheria ya Ndoa ya mwaka 1971. Sheria hii inatoa fursa kwa mtoto wa kike chini ya miaka 18 kuolewa.

Ingawa wadau wamefanya jitihada kubwa ili kumaliza ndoa za utotoni, lakini vitendo hivyo bado vinaendelea na hivyo kuhitajika mkakati unaojumuisha wadau wote ili kuondokana na matatizo hayo yanayotokana na tamaduni potofu.

Pamoja na tangazo la Serikali namba 279 la mwaka 1963 kuruhusu kila kabila kufuata utamaduni wake na kufanya uamuzi kutokana na kabila linavyoona ikiwa ni pamoja na kuruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya umri mdogo pale mila na utamaduní zinaporuhusu, jambo hilo linatakiwa liangaliwe upya.

Baadhi ya tamaduni zinaweza kubadilishwa, hususani pale zinapodhuru watu, jamii na taifa. Inahitaji mikakati Madhubuti kutokomeza ndoa za utotoni kwa kujumuisha wadau wa sekta ya umma na binafsi, viongozi wa kimila na kidini, walimu na watu wengine wanaoheshimika ndani ya jamii.

Ikiwezekana Katiba ziwe rafiki kuangalia haki za Watoto, kutegemea maamuzi yaliyopitishwa zamani au kuangalia zaidi katika tamaduni itakuwa ni kuendeelea kuwaumiza. Mataifa ya Afrika yaweke msisitizo kwenye katiba zao juu ya masuala kama haya.

Vita ya ndoa za utotoni inahitaji ushirikiano ikiwa ni pamoja kuondoa kwenye vitabu vya sheria vifungu vinavyobariki ndoa za aina hiyo.

Lengo lazima liwe ni moja la kuhakikisha watoto wote, hususan wa kike wanapata elimu na ndoa za utotoni zinamalizika nchini kote.

Jitihada zinazofanywa na Serikali kutokomeza ndoa hizo zionekane kwa vitendo lakini sio kusema kwamba imeongeza jitihada za kutoa elimu kwa watoto wa kike na jamii kwa ujumla kuhusu madhara ya ndoa za utotoni wakati hata bajeti maalumu kwa ajili hiyo hatuijui.

Ili mafanikio makubwa yapatikane, ni muhimu kuwa na mikakati inayojumuisha watunga sera, viongozi wa kidini na jamii zinazojihusisha na vitendo vya ndoa za utotoni.

Elimu ambayo imekuwa ikitolewa ndani ya jamii kupitia tafiti na kisha jamii kuelimishwa athari za vitendo hivyo kupitia vyombo vya habari, imeonekana mapinduzi makubwa zaidi ya kutegemea sheria peke yake.

Ndoa hizi katika umri mdogo zinapigwa vita kwa sababu zinaongeza kiwango kwa kiwango kikubwa. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti, ilibainika kwamba kulikuwa na mabadiliko ndani ya jamii tofauti na ilivyokuwa mwaka 2011.

Ndoa za utotoni zina athari nyingi katika jami. athari za ndoa hizo kuongeza kiwango cha vifo vya mama na mtoto, tofauti ya ndoa za utotoni zinaongeza athari za maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI, hakuna msaada kwa wasichana walioathiriwa na ndoa za aina hiyo badala yake wameishia kutengwa na ukosefu wa stadi za kazi zinazohitajika katika ajira.

Pia mara nyingi wanakuwa katika hatari ya kukimbiwa na wanaume kutokana na kuwategemea mno kwa kila kitu na wakati mwingine nda hizo zinakuwa na hatari ya kukumbwa na migogoro.


Chanzo: Majira
 
Back
Top Bottom