johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,105
- 164,483
Tumefika mahali inakuwa vigumu kumtofautisha mchungaji na mganga wa kienyeji.Leo gazeti la msemakweli limeripoti uwepo wa wachungaji wanaowanywesha waumini wao oil chafu ya magari kama njia ya kuwaponya,Tumefika mahali matendo ya wachungaji yanatia kinyaa,Nikuombe Dr Mwakyembe fanya utaratibu wa kuziweka hadharani katiba za makanisa na vikundi vya huduma za kiroho ili tuweze kuyafahamu yawapasayo kufanya na kuyaoanisha na yale wayatendayo.Pia nikuombe Mh Mwigulu ukiwa kama msajili wa hizi taasisi, zifanyie ukaguzi maana nyingine zinawageuza watu kuwa kama misukule.Ambazo hazistahili kuwepo zifute kabisa kwenye usajili kwa maslahi mapana ya taifa letu!