Katiba ya Zanzibar ni Gari Letu la Mwisho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba ya Zanzibar ni Gari Letu la Mwisho!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Dec 2, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on December 1, 2011 by zanzibaryetu
  [​IMG]Mwandishi wa Makala hii ni Dk Harith Ghassany akiwa amekaa katika bustani ya kuvutia wanamazingira wanataka kuwe na hali kama hiyo inavyojionesha hapo chini alipoketi Dk Harith. bila ya shaka tukitunza mazingira tutafanikiwa kupata mandhari kama hayo khasa kwa kuzingatia tuna utajiri wa mandhari ya kuvutia katika visiwa vyetu vya Zanzibar

  Na Dk Harith Ghassany
  Katiba yetu ya Zanzibar ndio dira! Kama kuongeza au kupunguza ni ndani ya Katiba ya Zanzibar. Tukiishadidia Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni sawa na kuutawadhisha ubatili wa Muungano.Ni sawa na kuambiwa nguruwe ni haramu ukasema utamtawadhisha na utakapomchinja utaelekea kibla. Ni sawa na kufunga mwezi wa Ramadhani na inapofika saa tisa ya mchana na ubao wa njaa unakuuma ukaamua kufunga mapazia ili kiingie kiza upate kufuturu.
  Mbona sie mbumbumbu wa mambo ya Katiba na ya Kisheria, ambao ndio wengi zaidi, tunaiona hii lakini wanasheria wetu hawaiulizi na wakionyeshwa hawataki kuiona? Kulikoni? Sawa, tuliungana ndani ya Muungano, lakini na nani na yuwapi? Tukikubali kuendelea kujiita Tanzania/Watanzania kuwa ni sawa na Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni sawa na mke aliezaa udogoni kesha yule mwanawe akaja hamia kwako na kwa sababu ni mtoto wako wa kwanza akaja kusimamia mirathi yako dhidi ya wanao halali.
  Kiislam hiyo ni batili lakini jamii inasema inamuonea huruma kizuka ambae ni mamae aliemzaa! Ukiwauliza wale watoto wako halali, maslahi na mustakbali wao jee? Jawabu wote ni ndugu kwa mama!
  Na ndio maana wamewaachia fahawisha wanasheria wetu wasasambue Katiba ya Muungano na kasoro zake badala ya kuichukua Katiba ya Zanzibar na kuipa dozi ya msimamo wa kuikomboa Zanzibar ili izidi kupewa nguvu ya “People’s Power” kupitia Kura ya Maoni, na imtishe atakayeijia Zanzibar kwa nia ya kutaka kuendelea kuitawala kikatiba. Badala yake tunasasambua Katiba isiyotuhusu.
  Chengine cha kustaajabisha ni wako wanaofika hadi kulalamika kwanini TVZ na Redio Zanzibar haitangazi mijadala ya makongamano ya Katiba ili wananchi wapate kuilimika? Kuupeleka umma kwenye Katiba ya Muungano badala ya Katiba ya Zanzibar ni kuuilimisha au kuupumbaza?
  Katiba ya Zanzibar ndio iwe mada na dira yetu ya siku na ya kila siku dhidi ya Katiba yao! Tunasema Katiba yao iko tayari na ni Khati za Muungano na Katiba ya Muungano. Hapana! Wao wana mchakato wao wenye mtizamo wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ijayo! Sisi tunatakiwa tushiriki ili papatikane njia ya “mkato” ili tusicheleweshe kuiweka Katiba yao.
  Na mtego wenyewe uko hapa. Kwa kushiriki kwetu katika Katiba ya Muungano tutakuwa tumeivunja Zanzibar kwa mikono yetu wenyewe na kuidhoofisha kikatiba! Kivipi na nani atakayechaguliwa kuifanya kazi hiyo? Atatafutwa mtu au watu ndani ya vyama vya siasa ambao wanaonekana “wanasikilizwa” na ambao wanaonekana ni “moderates” ambao wako tayari kwenda na kujiweka kwenye mapaja ya kundi la wahafidhina linakula kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ambalo haliwezi kuzikosa fadhila zao za kisiasa na za kimali.
  Zanzibar inakabiliwa na hatari kubwa kutokana na wale ambao tunakula nao na tunakunywa nao kumbe wana ajenda ya siri ya kumtumikia Mtawala Mkoloni kutoka Bara ili wajijengee nafasi za baadae za kuunenepesha uroho wao kwa kutarajia kutunzwa madaraka ya “kuiongoza” Zanzibar. Hawa ni viongozi ambao wameweka maslahi yao binafsi ya kisiasa mbele zaidi kuliko kuirudishia Zanzibar haki zake za Kitaifa na za Kimataifa kabla ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1964.
  Wanasheria wetu wako mstari wa mbele wanakimbilia wawemo kugombea uundaji na uandishi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ukitizama wote ni wanasheria.
  Katiba ya Zanzibar ni gari letu la mwisho kabla ya giza kuingia. Tusiwaachie madereva wanasheria wasioona vizuri kuliendesha usiku wakati Zanzibar kumeshakucha.
  Kwa kumalizia, someni haya maneno aliyoniandikia mzalendo wa Kizanzibari asieyumba:
  “Sasa ni kuelezana ukweli machoni na zile haya za wazee wetu zilizotufanyia ugumu wa kujikomboa ziishe!”
   
 2. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utumbo
   
 3. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utumbo ni nyama ya ndani lakini biashara ya ndani siyo utumbo.
   
 4. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Wako? changia mada kwa kutumia kichwa na si masaburi yako!
   
Loading...