Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977 Inayopendwa na Wana Ccm

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
INAMFANYA RAIS KUWA MUNGU NA CCM KUWA CHAMA PEKEE NCHINI



Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.


Ibara ya 46 (1) inasema "Wakati wote Rais atakapokuwa ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashitaka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.


Ibara ya 46 (2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au ametumiwa taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai, yenyewe, jina lake, na anwani ya mahali anapoishi huyi mdai na jambo hasa analodai.


Ibara ya 46 (3) Isipokuwa kama ataacha madaraka ya Rais kutokana na masharti ya 46(10), itakuwa marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilolifanys yeye kama Rais wakati alipokuwa anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.
..................................

Tafsiri yake:

Hakuna anayeweza kumshitaki Rais hata:

*Akiamua kuua mtu au watu bila hatia.

*Kuuza miradi au kujimirikisha mali za umma.

*Kugawa mali ya umma kwa watu anaowapenda kinyume na utashi wa umma.

*Kuanzisha vyeo na kuwapa wapenzi na marafiki zake.

*Kufukuza mfanyakazi au wafanyakazi wasioendana na utashi wake bila kujali kuwa wanatekereza sheria.


*Lakini pia inamwezesha Rais kumpandisha au kumshusha cheo afisa yeyote wa serikali hata akiwa ametukanwa tu na mpenzi wa kigogo wa serikali Rais akifurahi anampandisha cheo.


*Lakini pia, Rais anaweza kufuta au kuanzisha wizara anavyotaka.


*Rais anaweza kuanzisha au kufuta taasisi yoyote ya umma bila kumshirikisha yeyote.


*Katiba inampa madaraka Rais hata akigawa eneo la nchi au kuingia mikataba ya kufilisi nchi hakuna wa kuhoji au kumshitaki na hakuna mahakama inayoweza kumtia hatiani maana wote ni wateule wake na anawateua yeye kama yeye, au vyovyote aonavyo inampendeza.


*Hakuna kifungu cha katiba au sheria inayomwajibisha kufanya chochote. Katiba imempa madaeaka yote kama Mungu.

* Kwa mwamvuli huo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanasimamisha wafanyakazi watakavyo bila kufuata utaratibu na hakuna sheria inayosema mkuu wa mkoa au wilaya anaweza kumsimamisha mfanyakazi au uzalishaji wa taasisi.

*******///********

Huo ndio msingi/chimbuko la umasikini, ukosefu wa ajira na uongozi mbovu nchini kutokana na katiba mbovu sana iliyoundwa na CCM mwaka 1977.


Katiba inayopendekezwa haina tofauti yoyote ya maana na katiba ya mwaka 1977. Tena bora ya 1977.


Je, hii katiba inayopendwa na wana CCM inakubariki? Unaiunga mkono?


Toa maoni yako na unavyofikiri nini kifanyike.
 
Huo ndio msingi/chimbuko la umasikini, ukosefu wa ajira na uongozi mbovu nchini kutokana na katiba mbovu sana iliyoundwa na CCM mwaka 1977
husipotoshe umma, ndani ya TZ kuna watu ni matajiri na ndani ya TZ kuna watu ni masikini. unapofanya uchanganuzi inabidi ufanye uchanganuzi yakinifu. potosha ukawa ambao hawafikiriii sawa sawa
 
CHADEMA wenyewe wakiingia ikulu wataitaka katiba hii hivyo waongeze ujasiri kushika dola
 
Kweli Raisi analindwa na katiba kiasi hichi! Kumbe Raisi anamiliki Tz na kila kilichomo ndani yake. Inasikitisha sana.
 
husipotoshe umma, ndani ya TZ kuna watu ni matajiri na ndani ya TZ kuna watu ni masikini. unapofanya uchanganuzi inabidi ufanye uchanganuzi yakinifu. potosha ukawa ambao hawafikiriii sawa sawa
Yao matajiri ni akina nani?
Si ndio hao wanaonufaika kupitia milango dhaifu ya kikatiba?hivi kabisa kwa akili yako (kama iko timamu) unaona katiba hii iko sawa sawa!!!!?
 
Back
Top Bottom