Katiba ya Tanzania kuruhusu mikusanyiko Vs Polisi kuwa na uwezo kuzuia mikusanyiko Kisheria

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,012
2,000
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 20, Ibara ndogo ya Kwanza inasema

“Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.”

Kwa maana hiyo Ibara hii ya Katiba inawapa uhuru wananchi kukusanyika kwa Amani, bila kuvunja sheria wala kutukana mtu au watu.

Lakini uhuru huu wa kukusanyika kwa amani unafinywa hapa nchini, hususani baada ya kuwepo kwa sheria kali kama vile inayowataka watu kuchukua kibali Polisi saa 48 kabla ya kukusanyika. Wakati huo huo Polisi hawa kupitia sheria ya polisi ya mwaka 2002 (The Police Force and Auxiliary Services Act 200) inawapa Polisi uwezo wa kukataa makusanyiko hayo.

Sheria hii imeonekana kufanya kazi mara kwa mara ambapo watu wananyimwa uhuru wao wa kukusanyika kwa amani.

Je, nini kifanyike ili watu wawe na uwezo wa kukusanyika kwa amani nakutoa maoni yao bila kumkwaza wala kumtukana mtu yeyote wakati tunasubiri kubadili Katiba yetu?
 

w0rM

Member
May 3, 2011
44
150
Mkuu hawa Polisi wapo chini ya Serikali lazima watafanya yale serikali inataka, hivyo lazima watakuwa na utendaji wa kuegemea upande mmoja kwa namna moja au nyingine!

Ila nadhani kuna haa kuna haja ya kubadili hicho kifungu cha sheria cha Polisi kinachikipa mamlaka hayo.
 

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
759
1,000
kwa kuwepo na mamlaka ya namna hiyo kwa Polisi ni dhahiri kuwa mkutano au maandamano yoyote ambayo yanaonesha kuwa hasi kwa serikali yatazuiwa.

Solution: Maybe ni wakati njia nyingine ziangaliwe. Dunia imebadilika kuna mitandao n.k, si lazima sana watu kukutana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom