Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Kaka Mkandara:

Kama nilivyosema, huu mjadala ni muhimu sana. Nimekuwa kimya kwa kutokuwa na nakala ya katiba yenye mabadiliko yote(ingawa ninayo orodha ya marekebisho yote).

Wajumbe wengine wamependekeza njia ya kutokea, nitazingatia ushauri wao na kuanza kuchangia.

Kwa upande mwingine, nipo kwenye kamati ya vyama na AZISE chache ya kuandaa Mpango Mkakati wa Kudai katiba Mpya. Hii ni nyaraka itakayoelekeza mchakato(process) wa kudai katiba mpya. Hapa naona tunajadili content!

Hivyo nisingependa kuchanganya 'madawa' hapa! Kwa hiyo kama kuna mtu ana maoni yoyote kuhusu nini vyama na AZISE vifanye kudai katiba mpya naomba anitumie kwenye mnyika@yahoo.com ndani ya wiki moja.

Nitarejea kuchangia huu mjadala wa nini kiwemo ndani ya katiba yetu mpya.

JJ
 
nipende kuwashukuru tena wana bodi wote.
ila ni vizuri kijana JJ akatupatia maeneo ambayo yanapendekezwa ili tuweze wote kukumbushia na kuifanya katiba hiyo mali ya wananchi na sio kukaa kikundi cha watu wachache dhen waje waseme hayo ni maoni ya wadau na hili ni jambo la hatari sana kwenye jamii hii ya leo.

Ndugu wanabodi ni lazima tuliangalie hili kwa undani wake kwani siku zote tumekuwa tukisema ya kuwa katiba ni mali ya wananchi na sisi pia ni sehemu ya wananchi hawa wana AZINZE na wanasiasa nadhani watakuwa wanaangalia tuu matakwa yao ya kisiasa na kuwaacha wanavijiji kama sisi tukiwa hatuna jinsi ya kuweza kufikisha maoni yetu na pia hilo ni jambo la hatari sana .

nikumbushe katiba ni document ya wananchi na mnjika acha woga tupe ili tuweze na sisi kuiboresha na kuangalia kama mawazo yetu yamezingatiwa humo ndani jamani isije ikawa katiba yote inahusu jinsi ambavyo tume ya taifa na uchaguzi zikiwa zinalalamikiwa zaidi.
 
Mpaka Kieleweke,

Nakubaliana nawe. Katiba ni ya watu. Ndio maana nikasema tuendelee na mjadala huu hapa wa watu! Mjadala wa yaliyomo kwenye kamati(content).

kamati imeundwa kujadili mchakato(process) ya kuhakikisha serikali inakubaliana na dhana ya kuanzisha mchakato wa kuwa na katiba mpya. Kwa hiyo nimeomba mapendekezo ya mchakato(process). Sio yanayopaswa kuwemo(content). Mathalani ukishauri kwamba zitolewe elimu kwa umma, mikutano ya katiba ngazi ya chini nk.!! kwa maneno mengine, naomba kuhusu oganizesheni ya harakati za kudai katiba mpya.

Kuhusu uchambuzi wa yaliyomo kwenye katiba ya sasa, nitachangia mawazo yangu binafsi hapa.

JJ
 
Mpaka Kieleweke,

Kwahiyo hamna katiba ambayo imekwisha kuandaliwa. Tunataka kuandaa njia ya kupitia kuelekea huko.

Tuendelee kuichambua katiba iliyopo na kutoa hoja zinazopaswa kuwemo kwenye katiba mpya.

JJ
 
J.J Mnyika,

Katika ushauri wa haraka haraka nakumbuka kuna sehemu niliweka hoja kuhusu responsibility na jinsi bunge la wenzetu (nchi za magharibi) linavyofanya kazi zake tofauti na nchi za kiafrika. Nilimnukuu William.

Mkitumia vigezo vilivyoambatanishwa nadhani kuna sehemu nyingi ktk katiba zitaboreshwa zaidi. Ikiwa utahitaji maelezo yote ya mwenyekiti huyo nitakutumia ktk PM yako.
 
Thanks Mwanakijiji

well well, guys lets set a kick off date tuanze uchambuzi wa katiba kwa
1.kutoa mwongozo wa uchambuzi
2.kutoa mwongozo wa majumuisho ya vipengele

ni maoni tu wengine mwaweza liweka hilo sawia
 
Naona mjadala huu ulilala kwa kuisubiria nakala ya katiba yenye marekebisho yote. Naamini Bwana JF ataiweka kama alivyoahidi.

Ogah:

Nashukuru kwa hoja yako kwamba tujadili kipengele kwa kipengele. Lakini mimi naona tukifanya hivyo tutakuwa tunatafuta kuweka viraka vingine katika katiba yetu ya sasa.

Invisible atuwekee katiba. tuipitie na hatimaye tuone kwa ujumla-je tunahitaji katiba mpya?

Kama hoja nyingi zikionyesha ndio then tuongozwe kujadiliana kuandaa katiba mpya mpaka hatimaye tuwe na katiba mpya.

Kwa mtazamo wangu tunahitaji katiba mpya kutokana na sababu zifuatazo:

1. Katiba ya sasa ilipendekezwa na kuasisiwa kwa muda mfupi na kamati kuu ya chama tawala. Mchakato wote ulifinywa kwa takribani mwezi mmoja bila kuhusisha maoni ya wananchi. kwa hiyo hii tuliyonayo sio katiba ya Umma.

2. Mamlaka ya umma yaliyowekwa kwenye ibara ya 8 yako kama pambo, hayawezi kuhojiwa kikamilifu mahakamani. Ndio maana huwezi kwenda kumwondoa mbunge mahakamani hata kama hawatumikii(there is no power of reccall)

3.Suala umiliki wa ardhi halijafafanuliwa vizuri kikatiba. Ndio maana tunaswagwa kupisha migodi na mashamba ya wawekezaji wa kigeni.

4.Kuna utata kuhusu Muungano. Kwa mfano ardhi sio suala la Muungano wakati ambapo Muungano ni kuunganisha ardhi!

5. Haki ya kupiga kura haiko kwenye haki za msingi za kikatiba badala yake imetajwa kwenye ibara ya 5 ambayo si sehemu ya haki za msingi. Katika Muktadha huu mamlaka ya kuhoji haki ya kupiga kura mahakamani yanakuwa katika mtanziko(tutaona kwenye Kesi ya Mtikila kama suala hili likiibuka)

6. Hakuna suala la uraia. Je, watanzania ni wakimbizi? Kwa mujibu wa katiba ya sasa je, raia wa tanzania ni nani?

7. Haijatamkwa wazi katika katiba kwamba ndio sheria mama.

8. Rais amepewa mamlaka ya kuteua tume huru ya uchaguzi bila checks and balance hatimaye kuharibu haki na uhuru wa mfumo wa kuingia madarakani ambao ni mhimili muhimu wa katiba

9. Rais amepewa madaraka makubwa tena ya mwisho. Kichekesho ni kuwa rais ana mamlaka hata ya kulivunja Bunge kama litakataa kupitisha bajeti ya serikali yake!


10.Katiba hii haitambui na kuzilinda haki nyingi za msingi mathalani za vijana, mazingira,utamaduni nk. Orodha ni ndefu

11. Haifafanunui haki na wajibu wa vyama vya siasa nchini. Je kiongozi wa upinzani ana hadhi gani katika katiba ya sasa? Upinzani una umuhimu gani kwa taifa?

12. Haki ya elimu haimo kwenye katiba, kinachotajwa ni haki ya kujielimisha tena haiko katika orodha ya haki za binadamu zilizotajwa kwenye katiba

13. Mambo nyeti kama vita dhidi ya rushwa, umiliki wa uchumi nk hayajafafanuliwa na yale yaliyodokezwa katika ibara ya 9 hayawezi kuhojiwa mahakamani.

14. Serikali kuu inaingilia serikali za mitaa. Kadhalika pana mwingiliano baina ya wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge , madiwani. Mfumo mzima wa utawala ni mkorogo wenye utata

15. Rais anateua viongozi wakubwa wa nchi kama mwanasheria mkuu, Jaji Mkuu, Mkurugenzi wa mashtaka bila kushauriana na mtu yoyote wala kuthibitishwa na chombo chochote

16. Bunge haliruhusiwi kupendekeza muswada unaoweza kuigharimu pesa serilai bila muswada huo kupitia serikalini. Bunge limewekwa kuwa mpagazi/kuli wa serikali

17. Hakuna mahakama ya Katiba. Mahakama kuu imepewa mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba wakati mahakama kuu sio suala la muungano hivyo maamuzi yake hayana nguvu ZNZ

18.Hakuna mamlaka ya kuwalinda wananchi wasitonewe na vitendo vya watawala

19. Tume za serikali yenyewe mathalani ya Nyalali, kisanga nk zimesema katiba hii haifai!!!!!

20. Hakuna kifungu cha wazi kufafanua namna ya kurekebishwa kwa katiba. Hivyo kuna mwanya wa hata Bunge kurekebisha katiba yote!!!!

21. Ibara ya 152 inayotoa ufafanuzi haijitoshelezi kabisaaaaaaaaaa. Kwa mfano neno ambalo viongozi wanalitumia mara kwa mara kuhalalisha maamuzi yao guesss whaat "MASLAHI YA UMMA" halijafafanuliwa ni nini hasa!

22. Katiba imeeleza bayana namna ya kulipa deni la nje, ingawa iko kimya kuhusu madeni ya ndani.

23. hakuna kifungu cha kuilazimisha serikali kulipa fidia wananchi wake inapodhirika kimahakama kuwa ilivunja haki

24. Tumeshaweka viraka vingi sana mpaka sasa nguo katiba haijulikani ina rangi gani-tununue nguo mpya!!!!

Sababu ni nyingi zinakaribia umri wangu...labda watueleze-ni kwa nini hawataki KATIBA MPYA?
 
J.J. Mnyika,

Duuuuh! hivi kweli tuna Katiba jamani?
J.J sikutegemea kabisa kuwepo kwa mapungufu haya MUHIMU sana yaani haya ndio katiba yenyewe!...Mtumeee imekuwa kama vile katiba yetu imeundwa na Mkoloni?.
 
Mkandara,

Heshima yako mzee. Katiba ninayo hapa na ndo naendelea na scanning. I admit inachukua muda kuimaliza bro!

Naomba uvumilivu kidogo tu kuna mtu ananisaidia kui-scan in PDF format. Hope it wont take long.

Thanks
 
Nianze kwa kuweka hapa habari ya Mwandishi wa Gazeti la "Familia" kuhusu hili tukio na kama kuna masuala mahususi yatahitajika nitaongezea:


Tanzania sasa kupata katiba Mpya

  • Kongamano la pili lapitisha mpango mkakati
  • Timu ya wataalam yaundwa
  • Vyama vya siasa kuchangishana fedha
Umma wa Watanzania umeanza mchakato wa kuunda katiba mpya na kudai tume huru ya uchaguzi. Hilo limejidhihirisha hivi karibuni baada ya mpangomkakati kuwasilishwa mbele ya kongangamano la wawakilishi wa vyama vyote vya siasa visivyoshika dola, asasi za kiraia, wawakilishi wa makundi ya wazee, vijana na wanawake, taasisi za kidini na wanahabari, lililofanyika siku ya Jumanne tarehe 24 Mwezi Machi mwaka huu katika hoteli ya Peackock jijini Dar es salaam. Katika kongamano hilo lililokusanya watu wa kada mbalimbali toka Tanzania bara na visiwani kamati ya kudumu ya watu 20 iliundwa, ikiwajumuisha Maalim Seif Shariff Hamad ( Mwenyekiti wa kamati), Mh. Zitto Kabwe, Bw. Anthony Komu, Bw. Benedicto Mtungirehi, Bi. Ndelakindo Kessy, Bi Riziki Shahari Ngwali na Prof. Abdallah Jumbe Safari miongoni mwa wengine.

Aidha Dr. Sengondo Mvungi alikabidhiwa na kongamano jukumu la kuongoza jopo la wataalam katika mchakato mzima wa kuandika katiba mpya na kudai tume huru ya uchaguzi.

Akifungua kongamano hilo mgeni rasmi Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) aliainisha kuwa kongamano hilo, lisilofungwa na imani wala itikadi ya chama, ni la kuandika na kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi na kusema, Uchaguzi wa Tunduru umethibitisha kwa mara nyingine tena haja ya kudai katiba mpya. Aliendelea kueleza kuwa matumizi ya dola yaliyojitokeza katika uchaguzi wa Tunduru umethibisha kwa kiwango gani wateuliwa wa Rais wanavyoweza kupoteza uhuru wao wa kuongoza na kutoa haki kwa Watanzania wote linapokuja suala la uchaguzi huru ambamo chama cha Rais kinashiriki pamoja na vyama vingine vya kizalendo.

Prof. Lipumba aliendelea kusema kuwa ni udhalimu mkubwa kuutumia umaskini wa Watanzania kuuendeleza umaskini wenyewe kwa kununua hati zao za kupigia kura na hivyo kuwanyima haki ya kufanya mabadiliko ili kujiletea ustawi wa maisha yao.

Akikumbushia maneno ya Baba wa Taifa Prof. Lipumba alisema, Baba wa Taifa aliwahi kutoa kauli ambayo Mheshimiwa Mbatia hupenda kuirudia, ikiwa wakoloni hawatotupa uhuru tutamwomba Mwenyezi Mungu, lakini kama Mwenyezi Mungu hatatusikia katika hili basi tutamwomba shetani. Lakini aliendelea, Hatutaki kufikia kumwomba shetani kutusikia katika hili.

Katika kongamano hilo mpango mkakati wa kuandika na kudai katiba mpya pamoja na tume huru uliwasilishwa na kamati maalum iliyoundwa na Mwenyekiti wa kongamano la kwanza lililofanyika katika hoteli hiyohiyo Januari 29 na 30 mwaka huu, Maalim Seif Shariff Hamad kwa mamlaka aliyokabidhiwa na azimio namba tisa la kongamano hilo. Kamati hiyo iliundwa na Stephen Chonya (National Productivity Institute) ambae alikuwa ni Mwenyekiti, Julius Miselya ( Taasisi ya Ford), Yahya Hamad (Zanzibar Law Society), Elias Michael (Rugazia Advocates), John Mnyika (CHADEMA) na Hussein Mmasi (CUF) ambae alikuwa katibu wa kamati hiyo.

Mkakati huo uliopitishwa na kongamano la pili lililokuwa na wenyeviti wawili, Mhe Augustine Lyatonga Mrema mwenyekiti wa Taifa TLP na Prof. Lipumba, na unaokadiriwa kutumia kiasi cha fedha kisichopungua bilioni 2.68 shilingi za kitanzania, unatarajiwa kuhusisha wilaya 126 za Tanzania bara na wilaya 10 za Tanzania visiwani, tarafa 140 na kata 2553. Katika hatua hizo za awali, mchakato huo umewezeshwa kifedha toka ruzuku za Chama cha Wananchi, imefahamika.

Akiwasilisha kwa kina mkakati huo Bw. John Myika ambae ni mkurugenzi wa vijana wa CHADEMA alisema, Suala la kudai katiba mpya ni kama vita na ushindi ni lazima.

Mpango mkakati huo umeainisha sababu 25 zakudai katiba mpya. Zifuatazo ni sababu hizo:

Uundaji wa katiba iliyopo haukuwashirikisha wananchi. Rasimu ya katiba iliyopo ilipendekezwa na kuasisiwa na kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) Mchakato wote wa kupata katiba hii ulifanywa kwa muda wa mwezi mmoja tu. Hivyo, hakukuwa na muda wa kukusanya maoni ya wananchi. Ndio maana katiba hii sasa ina uhalali wa kisheria tu lakini haikubaliki kwa watu.

Ndani ya katiba iliyopo ibara ya 8 inayotamka kuwa mamlaka ya umma yamo mikononi mwa wananchi yamewekwa kama pambo tu. Mtu hawezi kwenda kuyadai mahakamani. Ndio maana hivi sasa wananchi hawana sauti wala mamlaka kwa viongozi waliowachagua wenyewe. Kwa mfano, hata mbunge akiwasaliti wananchi wake hawawezi kumuondoa madarakani. Lakini mbunge huyohuyo akikisaliti chama basi kinamuondoa madarakani mara moja.

Katiba iliyopo inautata mkubwa kuhusu suala la Muungano. Kwa kuwa katiba hii ni ya muungano, ifafanue wazi mambo yanayohusu Muungano. Hakuna haja ya katiba ya Zanzibar kuwemo ndani ya katiba ya Jamhuri. Kwa mfano, katika katiba haijulikani tunaungana nini? Kwani Ingawa ibara ya kwanza ya katiba inatamka kuwa Jamhuri ya Muungano ni nchi moja, ukiangalia orodha ya mambo ya muuungano; ardhi sio suala la muungano. Sasa hiyo nchi moja iko vipi kama Zanzibar wana ardhi yao.

Katiba yetu haina kabisa suala la umiliki wa ardhi, Ingawa ardhi ndio msingi wa maisha na suala la uchumi. Dosari hii ndio imekuwa chanzo cha watu kunyanganywa ardhi zao bila huruma au kusikilizwa. Mfano, wananchi kufukuzwa kwenye maeneo yao ili kupisha migodi au mashamba yao kuuzwa kwa wawekezaji wengine.

Katiba iliyopo sasa haina kabisa suala la uraia. Wananchi wote tumekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yetu. Hata suala la uzalendo wa dhati limefifia miongoni mwa wa Watanzania. Wasomi na wasiosoma mathalan, wamekuwa na mawazo ya kwenda kuishi Ulaya.

Katika katiba hii, haki ya kupiga kura ambayo ndio msingi na kielelezo cha mamlaka ya umma katika uongozi wa nchi, sio sehemu ya haki za msingi za binadamu ( imewekwa ibara ya tano ambapo sio sehemu ya haki za bianadamu). Hivyo hata mtu akinyimwa kupiga kura hawezi kudai mahakamani. Ndio maana nyakati za uchaguzi watu wamekuwa wakipanga mistari, karatasi za kupigia kura zikiisha, hawawezi kwenda mahakamani kudai haki yake ya kupiga kura.

Ingawa katiba ndio sheria mama, hakuna kifungu cha wazi ndani ya katiba kinachotamka hivyo. Iwekwe wazi ndani ya katiba kuwa ndio inayoshika hatamu. Hakuna mtu yeyote, sheria yoyote au chombo chochote kitakachokuwa juu ya katiba kwa sababu imekuwa ni kawaida kwa watawala na Bunge kutunga sheria zinazo pingana na katiba ilimradi tu zinakidhi haja zao.

Katiba inaweka madaraka makubwa sana tena ya mwisho kwa Rais. Ni hatari sana kuweka hatma ya nchi mikononi mwa mtu mmoja na sio Bunge ambalo ndilo wawakilishi wa wananchi. Cha ajabu, Rais anaweza kuvunja Bunge kama litakataa kupitisha bajeti yake.

Rais ndie anamamlaka ya kuteua na kufukuza wajumbe wa tume ya uchaguzi. Hali hii inaifanya tume kutokuwa huru. Kila wakati inajitahidi kumpendezesha Rais (Chama Tawala) ambaye ndio bosi wao.

Katiba Ingawa inaanzisha mfumo wa vyama vingi, haifafanui wajibu na haki za vyama vingi. Kwa mfano, haitamki kama kiongozi wa upinzani ni kiongozi wa Kitaifa kama alivyo spika.

Katiba hii haitambui wala kuzilinda haki nyingi za msingi. Kwa mfano, haki za elimu, vijana , walemavu, wazee, familia, hifadhi ya wakimbizi, vyombo vya habari, kuandamana, kiuchumi, biashara, taaluma, kutendewa haki na watawala, huduma ya afya, chakula bora, hifadhi ya mazingira, utamaduni, nk.

Katiba hairuhusu wagombea binafsi kwenye nafasi mabalimbali za uongozi wa nchi. Hivi sasa mtu akitaka kushiriki uongozi wa nchi lazima awe mwanachama wa chama cha siasa. Hali hii inawanyima nafasi ya uongozi Watanzania walio wengi ambao si wanachama wa vyama vya siasa. Hata Mahakama kuu imepitisha uamuzi kuwa ruksa mgombea binafsi (Kesi ya Mhe. Mtikila).

Katiba haifafanui mambo mengi ya msingi kama vile vita dhidi ya rushwa, umiliki wa uchumu na mwelekeo wa sera za nchi. Sehemu ya maelezo yaliyopo kwenye ibara ya tisa ni pambo tu kwani hayahojiwi mahakamani.

Haki ya elimu haimo kwenye kwenye katiba. Kilichoandikwa ni kwamba, kila mtu ana haki ya kujielimisha. Tena nayo si sehemu ya haki za msingi za binadamu.

Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye katiba baina ya mamlaka ya serikali za mitaa na serikali kuu. Kwa mfano, katiba haifafanui nafasi ya wakuu wa mikoa na wilaya katika katiba. Aidha, haikuweka wazi kati ya viongozi hao, madiwani na wabunge yupi ana nguvu. Imekuwa kawaida wakuu wa mikoa na wilaya kuwanyanyasa madiwani ambao ndio waliochaguiwa kwa kura na wananchi. Hata hivyo wakurugenzi wa wilaya wanaingiliwa na wakuu wa wilaya ambapo wote wameteuliwa na Rais.

Bunge haliruhusiwi kupendekeza na kupitisha muswada wowote unaoweza kuigharimu fedha serikali. Miswada ya aina hii, ni lazima ianzie serikalini. Hali hii imelifanya Bunge la Jamhuri ya muungano, kuwa kama muhuri tu wa serikali bila mamlaka yoyote katika usimamizi wa mambo ya wananchi.

Rais anaweza kulivunja Bunge wakati wowote kama akikataa kusaini Muswada lililopitisha au likikataa bajeti ya serikali.

Rais anateua viongozi wa juu wa nchi bila kushauriana na mtu yeyote. Na anaweza kuwafuta kazi apendavyo. Baadhi ya madaraka ya Rais yanaweza kupewa vyombo vingine vya dola; Kwa mfano, kuteua wakuu wa mikoa, mabalozi, makamanda wa vikosi vya ulinzi na usalama, Jaji Mkuu, mwanasheria mkuu, mkurugenzi wa mashitaka, nk. Wanaweza kuteuliwa na Rais na kuidhinishwa na kamati zinazohusika za Bunge.

Katiba hii haiweki mahakama ya katiba. Ingawa mahakama kuu imepewa mamlaka ya kusikiliza mambo ya kikatiba. Kuna utata. Katiba ni suala la muungano, wakati mahakama kuu sio suala la muungano. Hivyo maamuzi yake hayana nguvu Zanzibar.

Serikali imeshaunda tume mbalimbali. Zote zimeshauri wazi kuwa katiba hii haifai. Mfano tume ya jaji nyanyalali, tume ya jaji kisanga nk. Hivyo katiba mpya inahitajika.

Katiba hii haina kifungu cha mamlaka ya kulinda wananchi wasionewe na serikali au vitendo vya watala ( Public Protector). Hivi sasa wananchi wanapigwa au kukamatwa na polisi na kubambikiziwa kesi halafu mtu akilalamika, polisi walewale ndio wanachunguza. Wananchi wengi wamekuwa wanayimwa haki.

Katiba imeweka namna ya taifa kulipa deni la nchi, lakini haifafanui namna ya kushughulikia madeni ya serikali ndani ya nchi. Aidha, hakuna kifungu kinacholazimisha serikali kuwalipa fidia wananchi inapodhihirika serikali haikuwatendea haki. Hali hii imesababisha watu wengi kutolipwa na serikali Ingawa mahakama imeamua walipwe. Serikali imekuwa ikilipa fidia kwa watu inaopenda yenyewe kama hisani.

Hakuna kifungu cha wazi kuelezea namna ya kurekebisha katiba. Kifungu kilichopo kinaruhusu katiba kurekebishwa tu kama sheria nyingine. Hivyo, kama Bunge linaweza kurekebisha katiba yote.

Hivi sasa kunamchakato wakuharakisha ushirikiano wa kisiasa (Shirikisho) kwa nchi za Afrika ya Mashariki, itakuwa vigumu kwa Tanzania kuingia kama katiba mpya haijatungwa; kwa sababu katiba iliyopo inamapungufu mengi sana.

Katiba hii haina kifungu cha tafsiri/ ufafanuzi kinachojitosheleza. Ibara ya 152 inayotoa ufufanuzi haitoshi kabisa. Kuna mambo mengi hayaelezwi maana yake. Kwa mfano hakuna tafsiri ya neno maslahi ya umma. Hii imesababisha watu wengi kunyimwa haki kwa madai ya maslahi ya umma kumbe ni maslahi ya viongozi wachache wenye maslahi binafsi.

Akifunga Mkutano huo Mhe James Mbatia mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kuwa na Uzalendo wa kweli kwa nchi yao.
 
Hivi ndivyo vipengele vilivyochakaa katika katiba

NI vigumu kwa nchi yoyote duniani kuwa na uongozi unaoheshimu utawala wa kidemokrasia iwapo katiba yake ina upungufu katika demokrasia kwa kuwanyima uhuru wanamageuzi.

Katiba ndiyo muongozo wa kiongozi wa serikali yoyote duniani, ili aongoze kwa matakwa ya katiba hiyo na si kinyume chake. Endapo katiba itakuwa inamuongoza kukukandamiza ndivyo kiongozi huyo atakvyotakiwa kufanya bila kuivunja katiba yenyewe.

Si kwamba viongozi kama Adolf Hitler, Idi Amin, Saddam Hussein, Mullah Omar, Robert Mugabe na wengine walituhumiwa kuwanyanyasa wananchi katika tawala zao. Mimi naamini kwamba viongozi hao si kwamba walikuwa wanawafanyia hivyo makusudi, bali kosa lilitoka ndani ya katiba wananchi wao waliyokubaliana nayo iwe ndiyo muongozo wa viongozi wao na wao kwa ujumla.

Ni dhambi kubwa kwa kiongozi au mtu yeyote kuikana katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea, halafu akaenda kinyume na matakwa yake - dhambi hiyo itamtafuna.

Hivyo basi, kama tunawatakia viongozi wetu na wananchi kwa ujumla kufanya marekebisho ya katiba hii, ili iwe ni kinga kwao kwa baadaye baasi waepuke kile kitakachotokea siku za usoni kwa kuonekana madikteta kwa kupewa madaraka makubwa na katiba hii.

Kwa wale waliobahatika kusoma mtazamo wa wiki iliyopita, waliweza kuona mfumo mzima uliotumiwa na Serikali ya Tanzania katika uundaji wa katiba inayotumika hivi sasa. Katika mtazamo huo, nilielezea marekebisho yaliyofanywa hadi sasa ndani ya katiba hiyo ya 14.

Katika mtazamo huu wa leo nitaonyesha baadhi ya vipengele vinavyoonekana kuwa viraka vinavyoonyesha dhahiri kwamba ni muhimu kufanya marekebisho kwa kuwa imepita miaka mingi tangu katiba kwa ujumla iundwe mwaka 1977.

Katiba ya mwaka 1977 iliundwa kwa kufumbwa sana kwa baadhi ya vipengele, kwani haikuwa wazi kwa vile imekuwa ikiandikwa kwa ujumla jumla na haina ufafanuzi unaokidhi kifungu husika.

Kwa mfano, Ibara 7 (2) inaeleza bayana kuwa mamlaka ya nchi yapo chini ya wananchi, lakini kifungu hiki hakijitoshelezi kudai haki katika mahakama yoyote na ukashinda, kwani hakielezi bayana haki hiyo unaidai vipi.

Mfano mwingine ni ibara 9 inayozungumzia kuhusu haki za binadamu. Ibara hii inasema Kila mtu anastahili kuheshimiwa na anayo haki mbele ya sheria, haki sawa ya kula keki ya uhuru. Na inakwenda mbele zaidi kuwa hastahili kupewa haki kwa mkondo wa rushwa.

Kwa hili la sheria za rushwa naweza kusema ni sawa na kiinimacho, kwani hadi sasa hakuna sheria iliyo wazi inayoonyesha jinsi ya kuwashughulikia walaji na watoaji zaidi ya kuwabana wanaowataja walaji rushwa.

Sisemi kwa nia mbaya, ila kutokana na jinsi sheria hiyo inavyopelekwa, naweza kushawishika kusema kuwa haya mambo ya kutoa uthibitisho ni wazi kuwa sheria zilizopo za rushwa zimewekwa kwa madhumuni ya kuwalinda wala rushwa.

Utawala uliopo madarakani si utawala wa kisheria. Umeingia madarakani kwa kuvunja sheria hasa kwa kutoa rushwa zilizopewa majina kama takrima, shukurani na mengineyo.

Viongozi hao watakuwa wanaendelea kutesa uraiani kwani hakuna sheria inayoonyesha haki ya kushitaki zaidi ya ile ya kuwakinga ya kutoa uthibitisho ambao ni ushahidi mgumu, na wao kuifumbia macho kwa kuwa wanajua hata wao wameingia kwa misingi hiyo hiyo ya rushwa.

Kwa mfano, tukiliangalia suala la elimu ndani ya katiba, inaonyesha wazi wazi kuwa suala hilo si jambo la lazima kwa mwananchi, ila ni hisani ya serikali inayokuwa madarakani.

Suala la elimu na haki ya ulinzi yanazungumziwa katika maelezo na si ibara kwani ipo chini ya ibara ya 11 ambayo nayo huwezi kwenda mahakamani kwa sababu madai hayo hayana kifungu katika katiba, ila ni maelezo yanayosema kila mtu anayo haki ya kujielimisha.

Kutokana na katiba yetu kukosa kifungu cha haki ya elimu na kuichukulia kama hisani, hii ndiyo sababu utakuta viongozi wetu wanaamua kuwasaidia kwa kuwachagua wanafunzi wanaosomea masomo fulani na wengine kuwaacha wajilipie.

Hata hao wanaowapa hisani ya msaada hawasaidiwi kwa asilimia 100, wanasaidiwa kwa asilimia 60, na asilimia 40 inayobaki huwaachia wajitumikie wao wenyewe hata kama hawana uwezo huo.

Iwapo elimu ingekuwa imeandikwa kikatiba kuwa ni haki ya lazima kwa kila mwananchi, sidhani kama wanafunzi kutoka katika familia maskini wangekuwa wanapata mazoezi ya kila mwaka kwa kuacha masomo na kuanzisha maandamano ya kudai mikopo. Badala yake katiba ingekuwa wazi wangekuwa wanaelekea mahakamani kudai haki hiyo.

Katika masuala ya upigaji kura, katiba haina ibara inayoelezea haki ya upigaji kura na badala yake inaelezwa katika maelezo yaliyopo katika ibara ya 5.

Vifungu vinavyoelezea haki za binadamu hazipo wazi. Mara nyingi zimekuwa zikielezea kiujumlajumla pasipo ufafanuzi unaojitoshereza.

Kwa mfano, ibala ya 25 inasema mwananchi anayo haki ya kufanya kazi, huku ibara ya 12 inazungumzia haki ya usawa, na ibara ya 15 inazungumzia uhuru wa kuzungumza na wakati ibara ya 18 inazungumzia uhuru wa kuabudu katika imani. Zote hizi hazijielezi zinatendeka kwa namna gani ila inazungumziwa kijumlajumla.

Hakuna kipengele chochote katika Katiba ya Jamhuri kinachoonyesha kutoa haki kwa waandishi wa habari inayowaruhusu kutoa habari bila kuingiliwa uhuru wao.

Pia katika sheria za Umoja wa Mataifa zinazozingatia haki za binadamu, maandamano huhesabiwa kama moja ya haki za binadamu kwa wananchi wanapoona wamenyimwa haki zao za kimsingi, lakini kwa Tanzania si hivyo. Maandamano huhesabika kama hisani.

kwa sababu ni hisani ndiyo maana Watanzania wanapotaka kufanya maandamano kwa kupinga jambo fulani, ni lazima waende wakaombe hisani kwa kamanda wa polisi wa sehemu husika, atakapokataa kuwapa hisani hiyo atawazuia kuandamana.

Watawala wanapewa nafasi kubwa ya kiutawala ndani ya katiba hii. Kwa mfano Rais anapewa nafasi kubwa kupita kiasi, kitendo ambacho ni hatari kwa nchi yoyote na inaweza ikamsababisha kuwa dikteta.

Katika mada hii vile vile nitazungumzia kuhusu nafasi ya Rais kikatiba kwa kupitia ibara ya 33 hadi 46. Kifungu hicho kinamtambua Rais kama Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa dola na muajiri mkuu wa wafanyakazi.

Katiba inampa uhuru Rais kuteuwa majaji na mwanasheria mkuu, nafasi 10 za upendeleo kwa wabunge na nguvu ya kuvunja Bunge.

Pia kila muswada unaoingia bungeni ni lazima upitie kwake, kwani ni vigumu kwa wabunge kuanzisha muswada pasipo yeye kujua ni mada ipi inayozungumziwa bungeni.

Mamlaka haya ni makubwa sana yanayoweza kumshawishi Rais kujikuta akiwa mmoja wa washirika wa viongozi wanaotumia mfumo wa utawala wa kiimla (kidikteta)
 
Hoja hii ya Kayombo ni ya kijinga na inahamasisha Serikali kuendelea kujifanyia mambo "kitemi" bil akujali kuwa Mahakama na Bunge vina Nguvu za kulichunguza. Ni kwa misingi hii hii, inabidi Mawaziri wasiwe Wabunge wawe ni watu huru na Bunge!

Govt denies MPs access to contracts with investors
2007-04-20 08:46:01
By Juma Thomas, Dodoma

The government has stated categorically that it will not present to parliamentary committees contracts it enters into with investors because doing so would contravene the principle of separation of powers.

Planning, Economy and Empowerment deputy minister Gaudence Kayombo told the national Assembly here yesterday that, according to the country`s Constitution, the powers of the State authority are separately exercised and controlled by three pillars - the executive, the judiciary and the legislature.

The Constitution stipulates that each of the three arms shall discharge its functions according to the law and none shall usurp functions or authority not falling under its jurisdiction, he explained.

He added that the issue of contracts involves the government, by virtue of its being the organ vested with executive powers, and the respective investors.

According to Kayombo, the principle of best practices worldwide requires that such contracts be kept away from the public domain ? which rules out the possibility of taking the contracts to Parliament.

The deputy minister was responding to a question by Bububu legislator Cosmas Masolwa, who had wanted to know whether the government had any plans to present to parliamentary committees the contracts its enters into with investors for verification before they are sealed.

There have long-running appeals nationwide that all agreements pass through the Parliament for verification, especially after some of those the government had entered into with foreign investors were found to be questionable and going against the nation?s interests.

But Kayombo explained that Parliament was an organ vested with supervisory powers over public affairs and had full powers to question the conduct of the Executive arm of the state, including entry into and execution of contracts.

?When Members of Parliament ask the government about the validity or otherwise of agreements entered into with investors they are supposed to get correct answers on the implementation of such contracts,? he said.

However, he warned that MPs should not use that right to usurp the role of the Executive with regard to the contracts.

He said the most that legislators could do is to advise the government on how best to go about executing the contracts ?but without going to the extent of verifying them?.

The deputy minister noted that whenever MPs suspect that there is corruption in the contracts, they have powers under the 1998 Parliamentary Immunities, Powers and Privileges Act and Parliamentary Standing Orders to direct that legal measures be taken against the people involved.

Asking a supplementary question, Karatu legislator Wilbroad Slaa wondered how MPs could advise the government on contracts that they had not seen.

"Mr Speaker, we are told that we can advise the government on how best to go about the agreements. I wonder what advice we can give while the government keeps treating the issue of contracts as top secret," he observed.
 
tatizo ni kuwa inaonekana Wabunge hawaelewi wajibu wao. Kama wanataka jambo wanalitungia sheria, siyo wanaomba hisani na huruma ya serikali. Kama kweli wanataka kuangalia mikataba, waandike sheria na kusema ni mikataba gani na katika mazingira gani wanaweza kuangalia mikataba ya serikali.

Inasikitisha kuwa wabunge wanaambiwa kile kile walichoambia na mama Rita karibu mwaka mmoja uliopita na wanakaa kimya!

Ibara 63(2) Katiba inasema hivi:
Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
Madai ya kuwa kile ambacho wabunge wanachoweza kufanza zaidi ni "kuishauri" serikali ni uongo wa mchana. Bunge lina jukumu la kusimamia serikali.

Na katika kufanya hivyo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (e) cha Ibara hiyo Bunge linaweza:
"kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa."
Sasa mikataba ya serikali ni ipi basi? Kwa kutumia mwanga wa Ibara ya 67(8)
Mikataba ya Serikali ni "mapatano yoyote ya mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Idara yoyote ya Serikali hiyo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki kwa niaba ya Serikali."
Sasa, Wabunge wasitishwe na maneno matupu watumie uwezo wao wa kutunga sheria na kulazimisha mikataba mikubwa iangaliwe na wawakilishi wa watu siyo kuitolea mamuzi
 
tatizo ni kuwa inaonekana Wabunge hawaelewi wajibu wao. Kama wanataka jambo wanalitungia sheria, siyo wanaomba hisani na huruma ya serikali. Kama kweli wanataka kuangalia mikataba, waandike sheria na kusema ni mikataba gani na katika mazingira gani wanaweza kuangalia mikataba ya serikali.

Inasikitisha kuwa wabunge wanaambiwa kile kile walichoambia na mama Rita karibu mwaka mmoja uliopita na wanakaa kimya!

Ibara 63(2) Katiba inasema hivi:
Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
Madai ya kuwa kile ambacho wabunge wanachoweza kufanza zaidi ni "kuishauri" serikali ni uongo wa mchana. Bunge lina jukumu la kusimamia serikali.

Na katika kufanya hivyo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (e) cha Ibara hiyo Bunge linaweza:
"kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa."
Sasa mikataba ya serikali ni ipi basi? Kwa kutumia mwanga wa Ibara ya 67(8)
Mikataba ya Serikali ni "mapatano yoyote ya mkataba ambayo mmojawapo wa walioshiriki ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Idara yoyote ya Serikali hiyo au mtumishi yeyote wa Serikali aliyeshiriki kwa niaba ya Serikali."
Sasa, Wabunge wasitishwe na maneno matupu watumie uwezo wao wa kutunga sheria na kulazimisha mikataba mikubwa iangaliwe na wawakilishi wa watu siyo kuitolea mamuzi
Kazi NZURI... Tunahitaji wabunge wa aina yako ambao angalau wanapata muda wa kuipitia katiba na kuwazidi serikali pale wanapotoa majibu yasiyokuwa na ukweli. Sasa ni Lini utarudi kuwekeza Bungeni?
 
"wanao Musa na Manabii, maana hata akiwajia mtu toka peponi hawatamsikiliza"!

Mimi nawaunga mkono wale wote wanaotaka kuliamsha Taifa letu!! Hii weekend nitatuma "sms" kwa viongozi mbalimbali nyumbani kuwadokezea kuhusu Jambo Forums... any suggestion ya message fupi!!?
 
Mwanakijiji... unaonaje urudi home kugombea ubunge?
Nitakuwa volunteer kwenye campaign!
 

Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom