Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Mwanasiasa,
Unajua toka tupate Uhuru hiyo KATIBA imekwisha andikwa mara tatu?... Kufanyiwa marekebisho hiyo mbali na kila mara wananchi wametupwa nje! Kwa hiyo hata sielewi kifanyike kipi ikiwa kila tunapokuwa na matatizo fulani tunandike katiba mpya...

La msingi hasa nadhani wakati huu ni kuwashirikisha wananchi zaidi kuliko ilivyotokea nyuma. Na hasa jamaa zetu wa Unguja ambao binafsi sina imani na wawakilishi wao.
 
Ukweli ni kuwa hatuhitaji kuandika Katiba Mpya hasa kama tunaelekea kuingia katika Shirikisho la Afrika ya Mashariki. Kama shirikisho hilo litakuwa ni la kisiasa basi mawazo ya Katiba ya Shirikisho hilo ni lazima yaanze kutolewa sasa.

Hata hivyo, kuhusu Katiba yetu tunahitaji kufanyia mabadiliko makubwa ambapo yatatimiza hamu na matarajio ya watu wetu kuliko hivi sasa ambao CCM kutokana na wingi wao wanaweza kupitisha mabadiliko yoyote bila kibali cha wananchi.
 
Hii thread ni bab kubwa!
Hivi nchi zote za Commonwealth zinafuata mfumo wa utawala kama tulionao?
 
Mkandara hongera kwa kuanzisha mjadala chanya kama huu.

Kwa leo yangu mawili matatu ni:

1. Tuondoe cheo ya waziri mkuu, ni anasa isyo ya lazima. Majukumu ya Waziri mkuu yaonganishwe na yale ya makamu wa raisi. Mmoja kati ya wawili hawa anapaswa kuondoka.

2. Viongozi katika ngazi zote za utawala wawe wa kuchaguliwa ili kuendana na mfumo wa vyama vyingi. Si sahihi kuwa na halamashauri iliyo chini ya chama A halafu kukawa na mkuu wa wilaya akisimamia maslahi ya chama B.

3. Nakubaliana na mwanasiasa, katiba isukwe upya na ishirikishe wananchi na si ya kujifungia.

4. Tuwe na kipengele cha "power of Recall". Mwanachi asiwe na nguvu wakati wa uchaguzi tu, kama kiongozi anafanya vibaya awajibishwe hata kabla ya miaka mitano.

Nitaendelea kuchangia.
 
Eric Ongara,

Wakati tukisubiri hiyo katiba mpya ningependa kuuliza kuhusu baadhi ya mapendekezo yako hasa hapo uliposema Cheo cha waziri mkuu kiondolewe!..

Je, nani atakuwa msimamizi wa serikali bungeni?...

Nauliza kwa sababu hata mimi napata utata napomtazama rais wetu (nchi maskini) kutoshiriki moja kwa moja bungeni ambako ataweza kuyasikia malalamiko ya wananchi kupitia wawakilishi wao, pia kuna hatari kubwa sana ya kutofahamu uwezo wa mawaziri fulani ktk nyadhifa walizochaguliwa kwa sababu atakuwa akitegemea sana report zinazotayarishwa na wahusika.

Kuna kila haja ya muundo wa bunge pia kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwa ni pamoja nahao wabunge wa kuteuliwa. Kuwepo na uchaguzi pia ktk kila viti vinavyowakilisha jumuiya husika. Kama ni Jumuiya ya wanawake, basi wanawake watachagua wawakilishi wao.

Pia swala la pili, ambapo umesema mfumo uliopo ni halmashauri zetu kuwa chini ya chama!... nadhani hili ni kosa kubwa kiutendaji! Ningependelea kuona halmashauri huru yenye uwezo na ujuzi bila kuwakilisha chama A, lakini mkuu wa wilaya lazima awe amechaguliwa toka chama.

Hadi hivi sasa pia kupepita ushauri wa kuondoa hawa wakuu wa mikoa yaani RC na DC lakini sijasikia wanabodi wakipendekeza utendaji kazi wa huyu RC ama DC mchaguliwa. Hivi sasa RC na DC ni wawakilishi wa rais wateule ktk mikoa na wilaya husika chini ya wizara ya mambo ya ndani na waziri mkuu (kama sikosei)

Je, ikiwa hawa viongozi watachaguliwa bila shaka watakuwa wawakilishi wa vyama ktk mikoa na wilaya husika chini ya Taasisi gani ya serikali kuu?
 
Na Ndesanjo Macha

ILIKUWAJE hadi wakatokea watu wakatuibia mamilioni ya fedha kupitia ununuzi wa rada? Wakatuleta mikataba ya kiajabu ajabu kama ya Richmond. Ilikuwaje wakaja jamaa na kampuni yao ya magirini wakituahidi kuwa watatatua tatizo letu la umeme?

Hii sio mara ya kwanza kwa mikataba ya mamilioni kupitia kwenye mikono michafu ya baadhi ya Watanzania wenye dhamana ya kulinda maslahi yetu. Wala haitakuwa mara ya mwisho. Usishangae sana unaposikia habari kama hizi. Tena habari unazozipata ni kama asilimia moja ya ulaji unaoendelea kwa kasi mpya.

Mikataba wanasaini ofisini mwao, wananchi hatuonyeshwi. Hatujui inasema nini. Sijui kwa nini huwa hawatuonyeshi hii mikataba tuisome herufi hata herufi. Mikataba hii sio mikataba yao binafsi, ni mikataba inayohusu mali na maslahi ya umma. Katika kusaini mikataba hiyo ofisini mwao, huko huko ndio asilimia kumi zinaingia matumboni. Vitambi vinazidi kuwa vikubwa. Suti zinanunuliwa. Majumba yanajengwa. Biashara zinaanzishwa. Vitega uchumi vinaongezwa. Wananchi tukilia njaa tunalishwa kauli mbiu.

Kama ambavyo imekuwa miaka na miaka, nchi inaongozwa kwa kauli mbiu na ahadi za mara moja kila baada ya miaka mitano. Ahadi ambazo tunapewa kila miaka mitano ingekuwa zinatimizwa, huenda tungekuwa hivi sasa tunashindana na nchi kama Singapore. Huenda tungekuwa tunatoa misaada kwa nchi majirani zetu.

Nchi ya kauli mbiu na mapambio. Mapambio ya chama twawala. Twawala nanyi mwalala. Mapambio: vyombo vya habari ni sauti ya pili, wananchi sauti ya nne. Wakereketwa sauti ya kwanza. Wakoloni wapya kwa jina la washauri, Benki ya Dunia (eti benki ya dunia), shirika la fedha duniani, n.k., ni wapiga ala. Wanatuambia kwenye ripoti zao kuwa serikali yetu inaendesha uchumi kwa ufanisi na imepiga hatua mbele kwenye vita dhidi ya rushwa.

Eti nini? Rushwa? Niambie, toka uzaliwe, umemsikia nani kati ya akina nani hii amefikishwa mahakamani kwa rushwa kisha akaenda jela? Niambie ni kesi ngapi unazifahamu za rushwa ya mamilioni? Ukisikia mtu kakamatwa kwa rushwa, utasikia elfu 50 au laki moja. Wote hawa ni dagaa tu. Samaki wakubwa mahakamani hawafikishwi, jela hawaioni. Kwanza walioko kwenye tume ya rushwa ni dagaa, watathubutu kuwaendea samaki wakubwa? Wamezwe?

Naomba unipe orodha ya Watanzania waliofikishwa mahakamani au walioko jela kwa kula rushwa ya mamilioni. Ni akina nani hao? Hiyo vita tunayoambiwa ya rushwa inapiganiwa kwenye ripoti zinazotumwa kwa wazungu kuwafurahisha na kwenye hotuba za kutupumbaza. Watupe rekodi, takwimu, majina yao, n.k. Tuachilie mbali watu kufikishwa mahakamani, niambie ni akina nani katika kambi ya samaki wakubwa ambao wameshawahi hata kuchunguzwa tu. Sio kushtakiwa, hapana. Kuchunguzwa. Wapi.

Kuuziana maneno tu na tabasamu. Ndio maana Mwalimu Nyerere akatuambia uongozi sio sura. Kama ni sura, basi mkaribishe huyo mwenye sura nzuri mkanywe naye chai. Tunaongelea maslahi ya nchi na watu wake. Sio utani utani na ushabiki wa mtaani. Eti, aah, fulani ana siha njema na ni mzuri na mtanashati. Wanakuonyesha picha zake akiwa anatabasamu.

Tuache utani na masuala ya kuongoza nchi katika kipindi ambacho tuna mtihani mkubwa wa kuamua mwelekeo wa nchi yetu na jinsi ambavyo utajiri wake wa maliasili na akili na ubunifu wa watu wake vitakavyotumiwa ili kutunufaisha sisi na vizazi vijavyo. Narudia, utani utani na ushabiki wa sijui rangi ya kijani, nyeupe, na nyekundu acha nao kabisa. Unajiumiza mwenyewe na wanao na wajukuu zako.

Wakati shule zilizoko kwenye jiji ambalo ndio kitovu cha nchi, Dasalama, hazionyeshi kuwa tayari kuandaa watoto wetu kwa ajili ya dunia mpya ya ushindani wa sayansi na teknolojia, tunaambiwa kuwa Rais wetu anahitaji ndege mpya ya kifahari kwakuwa ana hadhi kubwa. Eti ndege ya hadhi yake.

Hivi nani kasema kuwa Rais ni mtu mwenye hadhi ya juu kuliko Watanzania wote? Ofisi yake ina majukumu makubwa, ndio. Lakini hii hadhi tunayoambiwa ambayo inahitaji dege la kifahari sijui imetoka wapi. Hivi huyu si mtumishi wetu? Watu tuna mawazo tofauti, achilia mbali suala la ndege. Mimi binafsi sioni sababu yoyote ya Rais eti kufunguliwa mlango wa gari. Kama anaumwa, sawa. Mfungulie mlango, na hata mbebeni kabisa.

Kisha mpelekeni hospitali (tena hospitali ambayo wananchi wengine wanakwenda, sio sijui Ulaya, mara Afrika Kusini). Ila kama ni mzima wa afya hakuna sababu yoyote ya kuwapa binadamu wengine kazi za kitumwa na wengine vyeo vya kimungumungu hapa duniani.

Kumfungulia binadamu mwenzako mlango wakati ana afya njema ni aina ya utumwa unaomfanya yule anayefunguliwa mlango kukwezwa kwenye daraja linalokaribia kuabudiwa. Ndio ibada hizo tulizoambiwa na mchora vikaragosi wa Kenya. Ibada za vyombo vya habari Tanzania kumlamba miguu. Kama anashindwa kufungua mlango wa gari, basi hata kuvaa nguo avalishwe, tuajiri mtu wa kumsaidia kupiga mswaki. Mtu wa kumlisha.

Tusimnunulie ndege tu, bali meli na helikopta pia. Tunaweza pia kumnunulia visiwa vyetu vilivyoko bahari ya hindi iwapo Waarabu na Wahindi hawajavinunua vyote.

Kufungua mlango wa gari ni jambo la kawaida. Hakupunguzi heshima aliyonayo rais, hakumfanyi awe nusu mtu, hakumfanyi ashindwe kutekeleza kazi zake. Kunachofanya ni kuondoa kiwingu cha ibada za miungu watu ambazo zinaelekea kutumika kuwaenzi na kuwapamba marais na viongozi wetu. Vitabu wanavyovitumia kuapa vinatuambia kuwa wanaojikweza watashushwa. Ndio, watashushwa na hizo kashfa wanazoshindwa kulieleza taifa undani wake. Kashfa zinabisha hodi kushoto, kulia, juu, chini, wanabaki kurandaranda dunia nzima kama vile mambo ni shwari.

Ni lini utamaduni wa viongozi kukubali makosa na kueleza ukweli utaanza? Yule wa uwazi na ukweli hakufanya hivyo. Alificha kiasi cha kufanya maneno uwazi na ukweli kutokuwa na maana yoyote. Yule wa fagio la chuma hakufagia chochote. Kila kitu kiliruhusiwa ikiwa ni pamoja na fagio la chuma kuruhusiwa lisifagie chochote.

Sasa watu tunatofautiana. Wako wanaolaumu viongozi kwa ulaghai unaoendelea nchini. Wanalaumu kisha wanaendelea na hamsini zao. Wako wanaotoa lawama kisha wanatafuta njia za kuhakikisha kuwa ulaghai na ufidhuli huu mchafu unamalizika na wanaohusika kujibu mbele ya umma.

Njia hii ya pili ni muhimu sana. Ni jinsi gani wananchi wanaweza kuhakikisha kuwa ulaghai hauendelei kutokea au ukitokea wanaohusika wanapelekwa kula ugali mbichi na maji ya maharagwe yaliyochemshwa?

Hapa ndipo penye mchezo. Hapa ndipo penye fainali. Tunaweza kuorodhesha kila aina ya uchafu, uongo, na utumbo wanaotufanyia watawala wetu. Hiyo ni kazi rahisi sana. Shughuli iko kwenye suala la kuhakikisha kuwa sheria inafuata mkondo wake, taratibu za kuchunguza wanaotumuhiwa kuhujumu uchumi zinafuatwa, wenye hatia kufikishwa mahakamani na wala sio kuambiwe eti warudishe fedha walizoiba, na zaidi kuhakikisha kuwa wizi wa mchana mchana kama huu hautokei tena.

Mjadala huu lazima tuuanze hivi sasa. Ni vipi wananchi, ambao ndio wengi kuliko viongozi walaghai, tutakuwa na uwezo, njia, na mfumo imara wa kuhakikisha kuwa hatuibiwi kama watoto wadogo? Kuna wakati niliandika kuhusu mbinu za kuleta mabadiliko kwenye jamii. Nilisema kuwa iwapo hujaweza kumwajibisha mwenyekiti wa serikali za mtaani kwenu, ni vipi utaweza kumwajibisha raisi, mbunge, au waziri? Kama hujaweza kuunda vuguvugu mtaani kwenu kuhakikisha kuwa mnaondoa wezi, mnajenga utamaduni wa kutupa takataka sehemu zinazohusika, mna utaratibu wa kusafisha mtaa wenu, n.k., ni vipi utaweza kuongelea suala la utunzaji wa mazingira kitaifa au kampeni ya kukamata majambazi kitaifa?

Utakapoweza kuleta mabadiliko mtaani kwenu kwa kushirikiana na wenzako, hapo utakuwa umeanza safari ya kuleta mabadiliko kitaifa. Utajifunza mbinu na kanuni muhimu za harakati za kijamii na kisiasa.

Utakuwa na uzoefu ambao utakusaidia kuweza kuleta mabadiliko makubwa ya kitaifa. Anza mtaani kwenu kisha panda juu. Unaweza hata kuanza kwa balozi. Makundi haya madogo madogo yanaendesha vuguvugu la kuleta mabadiliko katika mitaa na vitongoji, ndio haya haya yanakuja kuungana na kutumia mbinu na mshikamano unaotokana na uzoefu wa kuleta mabadiliko madogo madogo ili kuleta mabadiliko makubwa.

Hii ndio changamoto tuliyonayo. Je tunaweza kuhakikisha kuwa wilaya zetu zinatumia fedha zake sawasawa? Je bajeti ya shule anayokwenda mwanao unaijua? Je inatumiwa ipasavyo? Je unajua manispaa yako ina bajeti gani? Inatumia vipi fedha hizo? Je unajua ripoti ya mkaguzi wa mahesabu wa manispaa yako au wilaya yako inasema nini? Je kituo cha polisi unapoishi kina askari wa kutosha? Je ni waadilifu? Kama jibu ni hapana, unafanya nini? Unamsubiri nani?

Ilikuwaje tukafika hatua hii ya kuingizwa mjini na kila kampuni kubwa inayoingia nchini? Iwe ni umeme, madini, mawasiliano, utaliitumeingizwa mjini. Ilikuwaje? Ulikuwa wapi? Anza sasa kujifunza jinsi ya kuleta mabadiliko ya jamii, jinsi ya kulazimisha viongozi kujali kiapo na majukumu yao. Waonyesha kuwa unajua kuwa kuwa wao ni watumishi wako na una uwezo, mbinu, na hata sababu za kuwaondoa kwenye kiti wanachotaka kukifanya cha enzi. Anza mtaani kwenu. Kisha kesho, tukusanyike twende bungeni Dodoma, keshokutwa twende ikulu.

Mwananchi
 
Wakati tukisubiri hiyo katiba mpya ningependa kuuliza kuhusu baadhi ya mapendekezo yako hasa hapo uliposema Cheo cha waziri mkuu kiondolewe!..


Waheshimiwa,

Nimeahidiwa Latest Constitution leo. Let's hope for the best. Samahani kwa kuchukua muda mrefu lakini katiba nyingi zimeonekana kuwa za kabla ya 2005 kwa kila nilikoenda.

Shukrani kwa uvumilivu.
 
Shukrani...

Pia ombi lako nimelifanyia kazi naamini nimefanya kadiri ulivyotaka. Nampigia jamaa alotaka kuniletea nakala hiyo kumwambia asiwe na haraka alete kwa nafasi yake! Thanks in advance mzee
 
Wanabodi

Naona baadhi mtakuwa mmestushwa na heading hapo juu...!!

Nimefikiria nikajiuliza kwa nini umma wa watanzania wenye nia nzuri na mustakabali wa nchi yao wasimpe support Mtikila. Hoja zangu ni hizi:-

Huyu bwana ameonyesha ujasiri wa kutetea mabadiliko ya kweli...amekuwa mvumilivu na kuendelea kutetea hoja zake zile zile alizokuwa anazitetea miaka 90's rushwa, katiba, maonevu ya dola, wagombea binafsi n.k

Hivi majuzi ameshinda baadhi ya kesi kuhusu madai ya msingi ya Katiba yetu. Sasa kama sisi watanzania ambao tuna upeo kidogo japo wa kuja hapa na kuchangia mada mbalimbali tunashindwa kuona kama Mtikila anahitaji kuungwa mkono kwenye vita vya katiba yetu...ni nini basi tunategemea kwa wananchi wenzetu huko vijijini..???

CCM pamoja na baadhi ya media wameweka hadharani sana mbele ya macho ya watanzania maovu ya Mtikila..lakini hebu tujiulize swali huyu Mtikila kweli ni mhuni, muovu, mropokaji, mbinafsi na tapeli kuliko hawa viongozi walioko madarakani...??

Na je hebu tujiulize kama Taifa tutanufaika nini na jitihada hizi za Mtkila katika kupigania katiba mpya?? Pia, tujiulize je hatuta faidika zaidi iwapo kama tukimuunga mkono katika vita vyake dhidi ya mabadiliko ya katiba..??

Mimi nadhani wakati umefika wa kuangalia namna huyu Askofu Mtikila anavyosimamia haki ya kila mtanzania kupitia mapambano yake dhidi ya katiba yetu mbovu. Hivyo tumuunge mkono kwa kadri kila mmoja wetu anavyoweza...wakale walisema Nabii hatambuliki kijijini kwake...pengine huyu bwana ndio Nabii...!!!

Katika kujadili hayo hapo juu itatusaidia sana kama tutamuangalia Mtikila na hoja zake za katiba ya Tanzania na sio jana alikula nini, mkewe alikuwa wapi na udaku mwingine ambao hauna maslahi kwa jamii na Taifa.
Naomba kutoa hoja.
 
ninachoweza kusema ni kwamba ccm ina pesa sana kutokana na ruzuku ya kila mwezi, sasa kama mwenzangu na mie hali yako choka mbaya halafu unataka kushindana na ccm nadhani hiyo itakuwa ngumu kidogo, aidha labda u-blend in na ccm wenyewe then uwageuke na wakikustukia ujue kifo au kifungo cha maisha ! so, kutokana na pesa za ccm wanafanya chochote wanachoweza ili mradi tu wavunje sheria, kitu ambacho hawajakianza jana wala leo. jamani tuna njia ndefu sana ya kwenda na sidhani kama kuna haja ya kukata tamaa mapema, na mfano mzuri ni huyu mzee mtikila.

Lakini yote tisa kumi, je naye akipata position fulani atafanya kama anachosema au nae ndio atalewa madaraka na kujisahau ? itabidi tumuweke kwenye mtihani kidogo huyu mtikila, tuanzisheni chama fulani cha human rights, kuwe na "mlo" ( pesa ) halafu tuone nae kama ataingia kwenye 18 !
 
ninachoweza kusema ni kwamba ccm ina pesa sana kutokana na ruzuku ya kila mwezi, sasa kama mwenzangu na mie hali yako choka mbaya halafu unataka kushindana na ccm nadhani hiyo itakuwa ngumu kidogo, aidha labda u-blend in na ccm wenyewe then uwageuke na wakikustukia ujue kifo au kifungo cha maisha ! so, kutokana na pesa za ccm wanafanya chochote wanachoweza ili mradi tu wavunje sheria, kitu ambacho hawajakianza jana wala leo. jamani tuna njia ndefu sana ya kwenda na sidhani kama kuna haja ya kukata tamaa mapema, na mfano mzuri ni huyu mzee mtikila. lakini yote tisa kumi, je naye akipata position fulani atafanya kama anachosema au nae ndio atalewa madaraka na kujisahau ? itabidi tumuweke kwenye mtihani kidogo huyu mtikila, tuanzisheni chama fulani cha human rights, kuwe na "mlo" ( pesa ) halafu tuone nae kama ataingia kwenye 18 !


Alichokifanya na mpaka sasa bado tunakiona hakitoshi...?? Mimi hapa nazungumzia jitihada zake za kukemea katiba ya Taifa..huo ndio msingi wa kila kitu sasa ninachoshindwa kujua ni nini hapati support kwa wananchi ambao wanajua kuwa katiba ndio inayowaumiza.

Inakuwaje watanzania wanakuwa na ugumu kiasi cha kushindwa kujua pumba na mchele ni upi...huyu Mtikila si yeye ndiye anayefanya jitihada ndani ya system mbovu iliyopo kivitendo katika kudai haki za kikatiba..?
 
Yebo Yebo,
Binafsi nitasema kwamba tatizo sio nani anayewakilisha!.. Ukitazama huko tulikotoka kila kiongozi mpinzani ndani ya CCM ama nje wamepiga kelel sana kuhusu Kubadilishwa kwa katiba, lakini wote wamezimwa!...

Nadhani swala zuri lililobaki ni kutafuta wapi viongozi hawa hukwamishwa. nani mhusika mkubwa ambaye hapendio kabisa mabadiliko ndani ya katiba kisha vita ianze kwa huyo maanake nina hakika wazuiaji ni watu wachache sana wenye nguvu ndani ya uongozi wa CCM.
Tutaweza vipi kubadilisha kitu chochote ikiwa hata dira ya taifa inapangwa na CCM, Katiba lazima ipitishwe na baadhi ya watu ndani ya CCM...

Who are these people?
 
Katiba itabadilishwa kama wananchi wataweka mguuuchini, mshahara na marupu rupu ya wabunge ahaykuongezwa kutokana na wananchi kuweka mguuu chini kwamba hapana!

Ingawa wamejingeza kwa siri anyway!
 
Katiba itabadilishwa kama wananchi wataweka mguuu chini

Wanabodi mmesikia hilo?... Je, kumetokea nini hadi sasa tumekwama hapa wakati sote tulikubaliana kuwa na mwanzo mpya utoka JF ktk hili swala!. J.J Mnyika uko wapi mwanangu?..
 
Mwankijiji,

Salaam Mkuu
Tafadhali tuwekee hiyo latest katiba mkuu.............tuanze kuijadili
 
Mwankijiji,

Salaam Mkuu
Tafadhali tuwekee hiyo latest katiba mkuu.............tuanze kuijadili

Ogah,

Naona Mwanakijiji yuko occupied probably. Nalishughulikia la kuweka KATIBA hiyo hapa na najaribu kui-zip iweze kukaa vema ili kila member mwenye kuihitaji aweze kui-download na kuwa nayo wakti tunaendelea na mjadala huu.

Aidha napendekeza twende kipengele baada ya kipengele. Tukirukaruka mbele na nyuma tutaishia kuulizana tulikoanzia.

Meanwhile, nina ujumbe wako naomba u-drop email yako kwenye PM yangu nikutumie.

Regards
 
Mwaka 2005 Rais Mkapa aliridhia sheria ya mabadiliko ya 14 ya Katiba yetu ya mwaka 1977. Yafuatayo ni mabadiliko hayo ambayo mtayaona kwenye Katiba kama Invisible akiibandika. Kwa wale wenye katiba ya zamani, basi unaweza kusoma sheria hii na kulinganisha na Katiba yako.
 
Eric Ongara,

Wakati tukisubiri hiyo katiba mpya ningependa kuuliza kuhusu baadhi ya mapendekezo yako hasa hapo uliposema Cheo cha waziri mkuu kiondolewe!..
Je, nani atakuwa msimamizi wa serikali bungeni?...
Nauliza kwa sababu hata mimi napata utata napomtazama rais wetu (nchi maskini) kutoshiriki moja kwa moja bungeni ambako ataweza kuyasikia malalamiko ya wananchi kupitia wawakilishi wao, pia kuna hatari kubwa sana ya kutofahamu uwezo wa mawaziri fulani ktk nyadhifa walizochaguliwa kwa sababu atakuwa akitegemea sana report zinazotayarishwa na wahusika.
Kuna kila haja ya muundo wa bunge pia kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwa ni pamoja nahao wabunge wa kuteuliwa. Kuwepo na uchaguzi pia ktk kila viti vinavyowakilisha jumuiya husika. Kama ni Jumuiya ya wanawake, basi wanawake watachagua wawakilishi wao.

Pia swala la pili, ambapo umesema mfumo uliopo ni halmashauri zetu kuwa chini ya chama!... nadhani hili ni kosa kubwa kiutendaji! Ningependelea kuona halmashauri huru yenye uwezo na ujuzi bila kuwakilisha chama A, lakini mkuu wa wilaya lazima awe amechaguliwa toka chama.

Hadi hivi sasa pia kupepita ushauri wa kuondoa hawa wakuu wa mikoa yaani RC na DC lakini sijasikia wanabodi wakipendekeza utendaji kazi wa huyu RC ama DC mchaguliwa. Hivi sasa RC na DC ni wawakilishi wa rais wateule ktk mikoa na wilaya husika chini ya wizara ya mambo ya ndani na waziri mkuu (kama sikosei)
Je, ikiwa hawa viongozi watachaguliwa bila shaka watakuwa wawakilishi wa vyama ktk mikoa na wilaya husika chini ya Taasisi gani ya serikali kuu?

Heshima kwako ndugu Mkandara,

1. Kwa Mtazamo wangu, Makamu wa raisi awe kiongozi wa serekali bungeni, majukumu ya waziri mkuu yaonganishwe na waziri mkuu. Makamu wa raisi kwa utaratibu wa sasa hana majukumu, kazi zake zinategemea maamuzi ya raisi.

2. Nakubaliana na wewe kuna haja ya bunge kupitisha wateule wote wa raisi wakiwemo mawaziri

3. Kwenye ngazi ya wilaya tuchague moja, tusichanganye mambo kuleta utitiri wa vyeo usio na ulazima. Kama tuanataka kumpa mamlaka zaidi raisi, basi tuache andelee kuteuwa viongozi wa wilaya na kuondoa halmashauri kuondoa mgongano au vingivevyo halmashauri zisamame pekee yake zipewe nguvu zaidi za kimaamuzi. Huu ni mjadala mpana. Ninachokioana sasa ni mgongano baina ya waliochaguliwa na wananchi na wateule wa raisi katika ngazi moja, tuondoe mgongano huu. Mimi napendekeza serekali za halmashauri zisimame pekee yake, tuangalie tulianguka wapi wakati tunajaribu madaraka mikoani.

4. Pia kuna haja ya katiba kubainisha kikomo cha ukubwa wa baraza la mawaziri, serekali ya sasa ian baraza kubwa mno , kwa kisingizio cha ajenda nyingi, hofu ni hapo tutakuwa na ajenda mia hali itakuwa mbaya. Tuanishe kwenye katiba idadi ya mawaziri au kikomo cha ukubwa wa baraza la mawaziri kupuka gharama kubwa zisizo za lazima.
 
Lile swala la kubadili kura za ushindi kwa Rais mnalionaje? Zamani ilikuwa lazima upate angalau nusu ya kura (50%) ndio utangazwe mshindi, CCM wakabadili katiba, tena kinyemela wakabdaili. Sasa hivi hata ukipata 15% madamu ndio umeongoza unakabidhiwa nchi! Hii ni sawa kweli?
 
Back
Top Bottom