Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Mabadiliko ya Katiba yafanyike ili yamnufaishe nani? Je mabadiliko mnayopendekeza kufanyika, nani atanufaika zaidi CCM au Wapinzani? Utaona kuwa hakuna mtu ambaye atafanya mabadiliko ambayo yatamwondolea ulaji, kumpunguzia ujiko, na kumfanya akose nafasi fulani za kutanua!! Ni kwa sababu hiyo, basi ombi la kufanya mabadiliko ya Katiba litaendelea kuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa, kwani hata iwe ni Pase posa.. mbuzi hachezi!!! Ataendelea kula majani, na kuendelea kunya!!!

Ninachotaka kusema ni kuwa, kutegemea na kuombea kuwa serikali ya CCM italeta mabadiliko Bungeni ili kuweka mazingira ambayo Wapinzani watanufaika ni kujidanganya!!! Haitatokea, na itabakia kuwa ni ndoto ya Alinacha!! Sasa sizungumzii kama ipo haya ya kufanya mabadiliko ya Katiba, kwani najua ipo, na mapendekezo mnayoyasema ni miongoni mwa mambo muhimu. Binafsi, sioni haja ya kufanyika kwa mabadiliko viraka ya Katiba, haja iliyopo ni ya kuandika Katiba mpya kabisa, ambayo itaondoa utata, mgongano, na kutokueleweka kwa namna yoyote ile. Katiba hiyo itazingitai historia yetu, baada ya karibu miaka 50 ya uhuru na mang'amuzi ya nchi nyingine juu ya masuala mbalimbali ya kisheria. Katiba tuliyo nayo sasa imetufaa kwa muda huu tangu uhuru (na muungano) lakini ilikuwa iwe ya mpito, na wakati umefika kwa Taifa kuwa na Katiba mpya. Hata hivyo, mabadiliko tunayoyazungumzia au hata uandikaji mpya wa Katiba unakosa nguvu ukizingatia kuwa hivi karibuni tutaingia kwenye Shirikisho la Afriya ya Mashariki.

Kwa sababu hiyo, nguvu zote zielekezwe kwenye Katiba ya Shirikisho hilo kwani kwa huko tunakokwenda hiyo ndiyo itakuwa na nguvu zaidi na matokeo zaidi katika maisha ya watu wa Afrika ya Mashariki.

Hata hivyo, kama kuna kitu wapinzani wanaweza kufanya ili angalau sheria kadhaa zibadilishwe ni kwa wao kuungana na kuwa chama kimoja chenye nguvu, na kwa kufanya hivyo wanaweza kupata viti vingi Bungeni na kusababisha mabadiliko ya kisheria wanayolalamikia!!! Hiyo ndiyo njia nyepesi zaidi.

Kutegemea wema na huruma ya CCM katika kuwaletea mabadiliko, wapinzani wanajidanganya (Sikiliza mada niliyozungumzia hilo kwenye archives za KLH News)!!!
 
Mjadala wa Katiba ni mzuri na mgumu na mpana...
Ili uwe wa manufaa inabidi kwanza wadau na hasa wananchi wengi kadri inavyowezekana wahusishwe; awali ya yote wajadili au waelimishwe kama inaonekana hawajui, umuhimu wa katiba, ili waweze kutoa maoni yao kuhusu nini wanakitaka. Na hapa ndio umuhimu wa Elimu ya Uraia unapokuja. Watu wengi hawaoni uhusiano wa moja kwa moja kati ya maisha yao ya kila siku na katiba. Sana sana Katiba inachukuliwa kama kitu au suala la vyama vya siasa na wanasiasa peke yao.

Wakati huo huo, binafsi ningependa kuona mabadiliko ya dhati lakini kupitia mchakato wa taratibu katika kupata Katiba inayokubaliwa na wengi.

Inawezekana ilikuwa "rahisi" kwa nchi kama Afrika Kusini (sina hakika na Rwanda) kupata katiba yao mpya inayoonekana kuwa bora kwa vile walipitia kwenye mchakato mgumu wa maridhiano, na pia vita/mapambano ya muda mrefu dhidi ya ubaguzi wa rangi kiasi kwamba "watu wenyewe wakawa wastaarabu". Nafikiri hata kwa Liberia ya sasa. Kwa nchi zetu ambazo tumepata uhuru zamani na tumekuwa na "amani" (whatever that means!) wengi wetu ni waoga wa mabadiliko na hivyo utakuta wote watawala na watawaliwa kwa kiasi kikubwa wanaona "bora tuendelee hivyo hivyo" (unaweza kuhusisha hili na suala la Muungano: tuwe na serikali moja, mbili au tatu? wengi wanaona bora tuendelee na mbili japo hawaridhiki, lakini hawako tayari kusema tuwe na serikali moja kama kweli tunazungumzia muungano wa "two parts making a one complete whole").

Hata kama tuna miaka 40 ya uhuru wa bendera bado tu wachanga sana kama taifa ukilinganisha na wakoloni wetu ambao tunajaribu kuiga kutoka kwao mifumo mbalimbali ya siasa na maisha kwa ujumla. Ni uchanga huu ndiyo unafanya viongozi, kwa mfano, wasiwe tayari kujiuzulu pale kunapokuwa na tuhuma au kashfa dhidi yao (Msabaha?), au kutaka madaraka kama vile ubunge kwa ajili ya manufaa binafsi na si suala la sera ya chama (Kaborou?), au kukataa matokeo ya uchaguzi (Maalim Seif?), au kubadili katiba ili kuendelea kuwa madarakani (Ndolanga? Museveni?). Pia tusisahau suala la mapinduzi.

Kutokana na uchanga huo wa mataifa yetu na demokrasia, na mifano niliyoitaja hapo juu, ukiwa na katiba ambayo inasema rais ataapishwa mwezi mmoja baada ya kutangazwa matokeo basi unaweza kupata vita vya wenyewe kwa wenyewe kama siyo jeshi kutwaa madaraka katika hicho kipindi. Angalia tu idadi ya kesi za Ubunge kila baada ya uchaguzi kuthibitisha hili.
 
Hili nalo linahitaji mabadiliko ya Katiba au laweza kufanyiwa kazi bila kubadili katiba? Naona itakuwa hatua nzuri...

Mameya sasa kuchaguliwa kwa kupigiwa kura na wananchi

2006-10-23 17:24:17
Na Abdul Mitumba, Mbezi

Halmashauri za Manispaa na majiji barani Afrika, zimekubaliana kubadili mfumo wa sasa wa kuwapata wastahiki mameya kutoka kuchaguliwa na madiwani hadi kupigiwa kura na wananchi.

Kwa sasa mameya wa manispaa na majiji katika nchi nyingi za Afrika wanapatikana kwa kuchaguliwa na madiwani kutoka eneo husika.

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bwana Julian Bujugo, amesema kuwa makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa mameya, wakurugenzi na watendaji wengine wa serikali za mitaa, uliomalizika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
Ilionekana hakuna ugumu kwa wananchi kutoka eneo husika kuwapigia tena kura wagombea wa umeya.

Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa baadhi ya wagombea kutumia fursa ya uchache wa madiwani kunyakua kiti hicho kwa ulaini, alisema.

Amesema hatua hiyo pia itaongeza heshima ya Meya katika eneo lake kwani ataongoza kwa baraka za walio wengi, tofauti na mfumo wa sasa wa kuwatumia madiwani wachache kupiga kura.

Bwana Bujugo amesema tayari Uganda wameanza kufuata utaratibu huo unaoaminika kuwa ni bora zaidi katika kufikia malengo ya demokrasia ya kweli na utawala bora.

Hata hivyo, Bwana Bujugo amesema ili nchi za Afrika zifikie hatua hiyo, zinahitaji muda wa kujipanga upya kwa faida ya nchi zao na bara zima la Afrika.

Katika mkutano huo wa wiki moja ambao ulihutubiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Edward Lowassa, Bwana Bujugo alimwakilisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bwana Salum Londa.

SOURCE: Alasiri 23 Oktoba 2006
 
Turudishe kwenye katiba pia kipengele kinachomtaka mshindi wa urais awe na walau nusu ya kura zote zilizopigwa. Sijui kipengele hiki kilibadilishwa kwa manufaa ya nani. Kuna siku tutaongozwa na Rais aliyechaguliwa kwa chini ya asilimia 20. Hata DRC wanatushinda katika hili!
 
Mwanasiasa,
Yote haya aliyafanya bwana BMW!

Ukiona hata DRC wanatuzidi kwenye demokrasia ujue nchi yetu hasa chama cha chukua chako mapema kimeja matapeli, wezi na wahuni na makonono wasioitakia mema nchi yetu bali kujitajirisha tu.

Ni wachache sana wenye nia ya kuleta demokrasia ya kweli. ila kukicha wanaweka viraka katika katiba kwa maslahi ya nanI?

Katiba ya nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa sana.
 
Ndio hapo Mkira mimi nasema tutalilia mpaka lini? Kwa nini tusichukue hatua ya kujipanga kitaasisi kwa kuanzisha chama cha siasa au kujiunga na chama kimojawapo ili tuanze mchakato. My warry ni kwamba outside political cycles in TZ, we just cry kilio cha mamba. And by political cycles in TZ it means being in the mainstream of political parties.

Watu kama Mwanakijiji wanaonekana wana uwezo mkubwa wa kioganizesheni, wanaweza wakatoa mawazo ya namna sisi kuwa proactive. Sasa hivi naona tupo reactive, tunasubiri jambo litokee ndo tulalamike. Swali ni kuwa, is it possible to play a more active role in trying to define the future of nation? Au tumeamini kuwa bila CCM haiwezekeni? Mimi nasema mambo yote yanawezekana hata bila ya ccm.
 
wazo zuri sana lakini nashauri sana kwamba kama ni Vyama vya Siasa vipo na vichache ni makini tunaweza kuingia huko ila kitaasisi ni super zaidi then tuanze habari ya Katiba .Tutasalimika ? Maana Malecela , Rostam , Kinana , Kingunge wako tayari kufa kuliko kuona Tanzania ya Usawa .
 
mwanasiasa, kuna wazo nimepolipokea jinsi gani sisi tulioko nje ya nchi tunaweza kushiriki katika ujenzi wa Taifa letu bila kuumizana kichwa na CCM.. bado nalifikiri kichwani, likifikia mahali muafaka nitawaambia ili nisikie michango yenu..
 
Mwanakijiji hilo unalolifikiria ndio ile tunayosema kuwa middleclass inaweza kuleta mabadiliko makubwa! bravo fanyia kazi hilo wazo halafu utuhabarishe
 
Mwanagenzi said:
Hili nalo linahitaji mabadiliko ya Katiba au laweza kufanyiwa kazi bila kubadili katiba? Naona itakuwa hatua nzuri...

Mameya sasa kuchaguliwa kwa kupigiwa kura na wananchi

2006-10-23 17:24:17
Na Abdul Mitumba, Mbezi

Halmashauri za Manispaa na majiji barani Afrika, zimekubaliana kubadili mfumo wa sasa wa kuwapata wastahiki mameya kutoka kuchaguliwa na madiwani hadi kupigiwa kura na wananchi.

Kwa sasa mameya wa manispaa na majiji katika nchi nyingi za Afrika wanapatikana kwa kuchaguliwa na madiwani kutoka eneo husika.

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bwana Julian Bujugo, amesema kuwa makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano wa mameya, wakurugenzi na watendaji wengine wa serikali za mitaa, uliomalizika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
"Ilionekana hakuna ugumu kwa wananchi kutoka eneo husika kuwapigia tena kura wagombea wa umeya.

Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa baadhi ya wagombea kutumia fursa ya uchache wa madiwani kunyakua kiti hicho kwa 'ulaini,' alisema.

Amesema hatua hiyo pia itaongeza heshima ya Meya katika eneo lake kwani ataongoza kwa baraka za walio wengi, tofauti na mfumo wa sasa wa kuwatumia madiwani wachache kupiga kura.

Bwana Bujugo amesema tayari Uganda wameanza kufuata utaratibu huo unaoaminika kuwa ni bora zaidi katika kufikia malengo ya demokrasia ya kweli na utawala bora.

Hata hivyo, Bwana Bujugo amesema ili nchi za Afrika zifikie hatua hiyo, zinahitaji muda wa kujipanga upya kwa faida ya nchi zao na bara zima la Afrika.

Katika mkutano huo wa wiki moja ambao ulihutubiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Edward Lowassa, Bwana Bujugo alimwakilisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bwana Salum Londa.

SOURCE: Alasiri 23 Oktoba 2006
Mawazo haya yanaungana kabisa na ushauri aliotoa mzee Mtei kwamba rais na wagombea urais waruhusiwe kwenda bungeni. Naomba nifafanue:

1. Hoja ya mzee Mtei ni kuwa ni vyema kwa sasa tanzania viongozi wanaoomba urais waruhusiwe kugombea ubunge sambamba na urais ili wale ambao hawatopata wawe ni wasemaji bungeni na pia itawezesha kujenga imani kwa wananchi. Hii ndio process nchini Kenya.

2. Wazo la Mzee Mtei limereflect mawazo ya hao madiwani waliokutana Nairobi. Manake hili kwa sasa ndio gumzo uingereza kwamba mameya nao waruhusiwe kuchaguliwa na wananchi ili wawe na meno ya kuongoza vizuri.

Hili ni wazo ambali linatokana na nchi ambazo kuna secondary legislation yaani baada ya zile sheria za zilizotungwa na serikali kuu basi manispaa au city council nayo inaruhusiwa kutunga sheria zake za mapato, adhabu na sheria nyingine kwa manufaa ya eneo husika mfano jimbo la richmond katika eneo mojawapo la London wameamua kwamba ili kukabiliana na CO2 emmissions basi magari yote ambayo ni 4*4 yaliyosajiliwa katika eneo hilo yatatozwa kodi ya paundi mia tatu ya kupark gari hilo katika jimbo hilo kwa mwaka wakati magari mengine kodi ni paundi 70.

Hii ina maana wilaya kama Tanga mjini inaweza kuwa na sheria zake tofauti kwa vile ipo chini ya CCM na Mainly CHADEMA/CUF constituencies kama vile Karatu na Pemba wanaweza kuwa na taratibu zao tofauti.

Ukiangalia hili ni jambo ambalo litachochea sana maendeleo katika manispaa zinazohusika na pia demokrasia at local level itaimarika sana.Kutakuwa na mashindano so to speak. Na wananchi wataweza kumuondoa meya wakiwa hawana imani nae. Ila tufikirie gharama involved manake itabidi meya huyo azunguke kila kata kuomba

Lakini wasi wasi wangu ni kwamba utaratibu huu hutumika sana katika nchi ambazo zina waziri mkuu mtendaji kama Uingereza au Rais Mtendaji kama vile Kenya lakini kwetu sisi Tanzania ambapo Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli za serikali bungeni na Rais mwenye mamlaka kiutawala inakuwa taabu hususan ukizingatia ukweli kuwa Waziri Mkuu anatoka katika chama chenye wabunge wengi bungeni, jaalia itafikia mwaka wapinzania wakawa na viti vingi kuliko ccm au itokee kwamba Rais kwa vile anachaguliwa ''kivyake'' akatoka chama tofauti na CCM na hivyo ccm kuwa na wabunge wengi katika chombo cha kutunga sheria lakini hawana mwakilishi katika taasisi ya urais basi itakuwa kazi kubwa sana, chaos so to speak...ingawa tunajivunia demokrasia kwa wingi lakini hizi ni sababu ambazo zinatuongezea nguvu katika hoja kwamba tunahitaji katiba mpya.
 
Mbowe au washauri wako mpo na kusoma hapa??? Tunategemea katika topiki kama hii kusikia your views maana wananchi wanategemea sana nguvu yenu kuleta mabadiliko ya kweli.

Mfano katika matatizo yaliyopo sasa tulitegemea CHADEMA muandae maandamano na mkutano Jangwani kutoa tamko la chama kuhusu mwelekeo wa taifa.

P
 
Freemind
Hapa umekosea kwa mawazo yangu. Mbowe na Chadema they have tried hard to tell about CCM na siasa za uongo kwa gharama kubwa sana lakini wananchi walimkataa Mbowe na kuukataa upinzani kisa JK na CCM were good .

Kumbuka wame jaribu tangia mwaka 1995 but we wananchi we gave them shit na kuwaita majina , mara wana njaa , mara waroho wa madaraka nk , leo hii wao wakikaa kimya na kuwaachia wananchi sisi wenye maamuzi ya mwisho ni sawa na wakija kusema next time tutaelewa . Maana kuuliwa Nchi hawafi wao watu bali na sisi.

Kuwategemea bila sisi kujua what we want ni kuwalaumu bure na kuwapotezea muda maana wakati wanatupa issues tuliwasikiliza na kuwapuuza kwenye hili si mpinzani pekee tunatakiwa kujipanga na kusema no to CCM .
 
Mzee Mwanakijiji tunasubiri sana wazo hilo.

freemind: CHADEMA na CUF wameshaimba sana kuhusu mustakabali wa Taifa. Fuatilia habari utapata. Kuhusu maandamano, waliandaa juzijuzi lakini yalipigwa marufuku na Alfred Tibaigana.
 
Kitila Mkumbo habari ya kupigwa marufuku sijaipata popote hebu nihabarishe ilikuwa hadi maandamano yamekataliwa na Tibaigana ?
 
MZEE WA SHUGHULI: Siasa ni process na hasa inapogusa kubadili mind set ya watu waliozoea kwa muda mrefu. Mbona Zambia, Malawi na Kenya wameweza???. Ofcourse inahitaji huge sacrifice na commitment ya mtu wa aina hiyo. Mtu jasiri kama Mchungaji Mtikila kama angekuwa na akili iliyotulia angefaa.

Hivyo viongozi msikate tamaa. Muwe creative kutokana na mazingira yaliyopo. Mfano uovu ulio wazi kabisa ni mitaji ya wapinzani palepale. Msisubiri hadi uchaguzi. Tumieni udhaifu uliopo kwa faida yenu na hiyo ndio siasa. CCM wanatumia udhaifu wa upinzani mara kwa mara kuwasambaratisha.
 
Hapa ndugu said yakubu umeongea mambo ya msingi sana.

Kwakweli kuna mantiki ya kurekebisha katiba ili iweze kwenda sambamba na mfumo huu wa vyama vingi, mafano mambo waliyoyazungumzia jamaa humu kama ile ya vyombo vya usalama wa taifa kuegemea upande wa CCM au ile ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM ambaye ndio rais nk.

Lakini kama tunavyofahamu hawa ndugu zetu CCM wanayaona mambo katika mtazamo wao, madai yoyote ya katiba kwa sasa bado hayatapokelewa kwa mikonmo miwili na serikali inayoongozwa na CCM.

Mimi nafikiri jambo la msingi kwa sasa ni kuimarisha vyama vya upinzani. Na huu ni wajibu kwakweli wa kila mtanzania kuona umuhimu huu wa kuendelea kuviimarisha vyama hivi.

Watanzania tunahitaji chama mbadala kwakweli, na watu kama hawalioni hili basi tutaendelea kulia na kupiga kwata mpaka lihamba lakini hakuna chochote kitakachobadilika.

Hebu tujaribu kuwapa nafasi hawa CHADEMA, mimi naona kama hiki chama tukikiimarisha vizuri, tukawavutia watu kwenye chama hiki na kuongeza idadi ya wabunge ndani bunge basi hapo tutaweza kufanya mengi.

Tunaweza kuwa na serikali ambayo ni responsible kwa wanachi.
 
Tanzania tuna tatizo kuwa la kupungukiwa ma ari ya uwajibikaji na uaminifu kazini. Nina hakika kwa bunge letu tena hata kama mkataba ungekuwa na mapungufu mengi ungeweza kupitishwa tu ukizingatia wengi ni wana ccm. Kujadili bungeni labda kungesaidia isiwe siri tena lakini sio kukwamisha mkataba.

Kitu muhimu ni kwa viongozi wetu kuwa na mioyo yakizarendo hasa na dhamira ya kweli ktk kuwatumikia watu. Kama viongozi wengekuwa hivyo hata mkataba ukiishia wizarani kusingekuwa na mashaka kwa sababu tunaiamini serikali yetu. I wish to replace the officials with robots.... !!!!
 
Tufu na Mwl Moshi,

Maneno MURUA KABISA!!!

Tufu, unafikiri tufanye nini ili hawa wenye dhamana wawe na Uzalendo, Jibu Moja ni kuwa inabidi siku zote tuwaweke kwenye "Offensive side" na tuwaache wajitetee "wa-account matendo yao" and therefore..............

Wacha mikataba iwe wazi bungeni, ili wananchi tujue, hata kama CCM watapitisha mikataba bomu pale bungeni, sisi tutaendelea kuwapigia makelele na ipo siku wananchi tutazinduka na kuchagua wawakilishi watakao tetea maslahi yetu.
 
Haiwezekani mikataba bomu ikapitishwa bungeni, ndio maana hata EL alianza kuwanyamazisha wabunge kuhusu kuanzisha tatizo la umeme.

Utendaji wa kazi bungeni ni kupitia kamati za bunge. Kamati hizi ndizo zinakuwa na uwezo wa kuiangalia mikataba na kuichambua kwa kina, vilevile wabunge wenye interest watayaona haya hivyo ubabaishaji unakuwa haupo kwa sababu muda unakuwepo wa kutosha na wananchi wenye interest kupitia kwa wabunge watajua nini kinaendelea.

Sasa hivi ni wabunge wangapi wanafahamu mikataba mabomu ambayo inaendelea? Hawajui hata ilikoanzia - very interesting. Maana yake kuna makundi fulani fulani tu ndiyo yanayofaidika kupitia kwa marafiki zao wa nje.

Pesa wanazopata wana-invest nje ambako tunaenda kukopa kwa bei ya juu zaidi. wapi na wapi?
 
Kutokana na mawazo ya ndugu yetu J.J.Mnyika ambaye kaniomba nianzishe mada hii kuhusu KATIBA, nadhani huu ni wakati muafaka kujadili mambo yaliyokuwa MUHIMU kwa wananchi wenyewe kuliko mapendekezo ya vyama vya Upinzani na baadhi viongozi wetu.

Nina imani kubwa kuwa mapendekezo mengi yatakayo pendekezwa na viongozi wetu yatahusu zaidi nafasi ya vyama ktk chaguzi na labda Muungano wetu bila kuzingatia maoni ya wananchi ktk swala zima la marekebisho ya katiba.

Binafsi naamini kabisa kuwa KATIBA haiwezi kufanya kazi vizuri ikiwa mfumo wa KIUTAWALA bado utabaki kama ulivyo, hatukubadilisha pia mfumo mzima wa Kiutawala kati ya BUNGE na serikali kama alivyotushauri Mwenyekiti wa GOPAC, nd. Williams alipotembelea Tanzania.

Wana JF, tuweke michango yetu hapa ktk swala hili la marekebisho ya KATIBA ili kuboresha wajibu wa sheria zetu.

Labda kwa kupitia baadhi ya wana JF, wanasheria na wabunge watarajiwa tunaweza kuweka michango yetu hapa ili wao wapate kuiwakilisha huko kunatakiwa.
 

Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom