Katiba ya nchi ifundishwe kuanzia Shule ya Msingi na kuendelea

CHESEA INGINE

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
200
46
Hoja yangu hapa ni kwa uelewa wa katiba utaanzia chini kabisa katika shule na italeta tija kwenye yafuatayo:

1. Uzalendo wa nchi ya hicho kizazi utakuwa wa hali ya juu kwa kuifahamu katiba ya nchi yao.

2. Huu mtindo wa kufungua vilabu vya kuchukia rushwa havitakuwa na tija nzuri kama mwanafunzi angaielewa katiba ya nchi yake.

3. Somo la Katiba liwe na umuhimu wake na kwamba kama mwanafunzi hakupata alama nzuri wataalamu wetu waje na suluhisho nini kifanyike asipewe cheti au iweje.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri, ila sio hii katiba outdated. Kuliko kuwafundisha katiba hii ni bora wafundishwe matumizi ya kondomu kuepukana na ukimwi. Ikipatikana katiba mpya itakuwa ni sawa kabisa.

..ndugu yangu tindo vijana wakifundishwa katiba hii, na wakaielewa, watakuwa ktk nafasi nzuri zaidi ya kuyaenzi mazuri yake, na kuboresha pale palipopungua.

..pia itawajengea vijana wetu utamaduni wa kuiheshimu na kuienzi katiba yetu.

..sisi tuliokulia ktk mfumo wa chama kimoja tulifundishwa zaidi imani za Tanu na CCM kuliko katiba ya nchi. Matokeo yake ndiyo haya unayoyaona ya baadhi ya viongozi wako more loyal kwa CCM kuliko taifa.
 
Mimi huwa naona Bora concepts za uchumi zingefundishwa kuanzia std 3
Tungepata watu wanaojua resources are scarce
Yaani hii concept ukiielewa utaishi kwa nidhamu ya hali ya juu
 
Katiba hii hii viongozi wameifanya jiwe la kujisugulia baada ya kutoka kufagia mbolea au nyingine?? Sidhani ka ndiyo hii waliapa kwa kuitumia
 
Tutafute Katiba nyingine ya kuwafundisha watoto wetu na vizazi vijavyo... Hakika siyo hii iliyogeuzwa mkeka wa bibi!!
 
Mleta mada itakuwa wewe sio mzazi. jaribu kupata mtoto umugharamukie halafu mtu akuletee stori hizi, unaweza kuondoka na kichwa
 
Hoja yangu hapa ni kwa uelewa wa katiba utaanzia chini kabisa katika shule na italeta tija kwenye yafuatayo:

1. Uzalendo wa nchi ya hicho kizazi utakuwa wa hali ya juu kwa kuifahamu katiba ya nchi yao.

2. Huu mtindo wa kufungua vilabu vya kuchukia rushwa havitakuwa na tija nzuri kama mwanafunzi angaielewa katiba ya nchi yake.

3. Somo la Katiba liwe na umuhimu wake na kwamba kama mwanafunzi hakupata alama nzuri wataalamu wetu waje na suluhisho nini kifanyike asipewe cheti au iweje.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba hihi mbovu ?Acha hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom