Katiba ya Kenya iliandaliwa na vyama vya siasa kwanini CCM inaandaa katiba ya Tanzania?

kimarabucha

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
791
621
Wadau nimekuwa nafuatilia namna jirani zetu Wa Kenya walivyofanikiwa kupata Katiba yao.Wakenya Katiba yao imeandaliwa na wasomi , Taasisi na mashirika mbalimbali ila VYAMA vya Siasa havikushirikishwa.Kinyume na hapa kwetu Mchakato Wa Katiba unaandaliwa na CCM na wajumbe wake wanateuliwa na CCM na Bunge la Katiba Wabunge wake ni Wa CCM je katiba itakayopatikana ni Lazima iwe ya Kichama zaidi.Nashauri ili kumwacha Rais wetu kazi ya kupambana na MAFISADI na maovu mbalimbali pekee yake ni vema tukawa na katiba itakayoandaliwa na Wasomi mashirika na Asasi mbalimbali badala ya VYAMA vya Siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila katiba mpya tena ile ya warioba ambayo haijachakachuliwa sintapiga kura
 
CCM NI LAANA TANZANIA

Imeajiri wajingawajinga kwa kupinga mambo yamsingi kwenye mitandao kishenzishenzi...

.katiba mpya hayataki

.. Mahakama huru hayataki

..Tume huru ya uchaguzi hayataki

.. Mizizi mirefu asivunje katiba hayataki avunje tu

...Bunge live hayataki

...Siasa nimchakato wa kila siku hayataki

Huwa nawashangaa sana hilikundi lakipropaganda mitandaoni la ccm utadhani mapunguani vile,

Wanaoteseka nisisi wote pamoja nawao....ndugu zao, rafiki zao, watoto wao, nk kwanini wanapinga mambo yamsingi?....ujinga na upumbavu waliojazwa na ccm kwa vihera vichache kilofalofa tuu.
 
Ni kosa kuwashirikisha wanasiasa kwenye kuandaa Katiba mpya, wanasiasa wanawaza kutawala tu.

Vv
 
Nchi hii kupata katiba mpya ni lazima kwanza kuiondoa ccm kwa sababu ccm hawataki tupate katiba mpya hivyo ni muhimu kuwaondoa wao kwanza
 
Back
Top Bottom