Katiba ya JMT inasema juu ya Mgawanyo wa Madaraka kwa mihimili 3 lakini hakuna sehemu inayosema Mihimili hiyo iko sawa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Ni kweli kuna mihimili mitatu kwa mujibu wa katiba ya JMT ambayo ni Executive au Serikali, Bunge na Mahakama.

Katiba imetoa mgawanyo wa majukumu kwa mihimili hii lakini sijaona ibara inayosema kuwa Mihimili hii 3 iko SAWA.

Ukisoma katiba kwa makini utagundua Bunge na Mahakama ziko chini ya serikali.

Rais wa JMT ana kila kitu, NI KWELI!
 
Ni kweli kuna mihimili mitatu kwa mujibu wa katiba ya JMT ambayo ni Executive au Serikali, Bunge na Mahakama. Katiba imetoa mgawanyo wa majukumu kwa mihimili hii lakini sijaona ibara inayosema kuwa Mihimili hii 3 iko SAW...
Kivipi? Kuna mahala imesema mmoja umejichimbia.
 
Kutokea huko nyuma kwa akili za kawaida watawala ninyi mnawaita executive ndio mpango mzima.Watu wanapodai katiba wamechoka na maigizo yaliyo kwenye katiba ya sasa.

Kwa mfano:-
Raisi anaweza akavunja bunge na akajiongeza akatangaza hali ya hatari.Lakini bwana majoho mekundu yaani Chief Justice licha ya kuwa na uwezo kuhukumu mtu kifo, hawezi akaamka akatangaza hali ya hatari .Pammoja Jaji huyu kuhukumu mtu kifo Raisi ana uwezo wa kutengua hiyo hukumu na kumsamehe hata kumwachia huru.

Vivyo hivyo eti bunge laweza kumpigia kura Raisi vote of no confidence huku majority wapo CCM,na mwenyekiti wa chama ndio Raisi wa nchi!!
Hii katiba ya sasa imetengenezwa kuwapa Free way watawala ni antidote.
 
Ukisoma katiba kwa makini utagundua Bunge na Mahakama ziko chini ya serikali.

Rais wa JMT ana kila kitu, NI KWELI!
naunga mkono hoja
P
 
Ni kweli kuna mihimili mitatu kwa mujibu wa katiba ya JMT ambayo ni Executive au Serikali, Bunge na Mahakama. Katiba imetoa mgawanyo wa majukumu kwa mihimili hii lakini sijaona ibara inayosema kuwa Mihimili hii 3 iko SAWA...
Ni kwa ajili ya check and balance, siyo ya nani mkubwa nani mdogo....!!
 
naunga mkono hoja
P
Kama ndio iko hivi..... basi ni haki kabisa kwa muhimili mkubwa (serikali) kuingilia hii mingine na wanaopinga hili hawajaisoma katiba kwa makini.
 
Ni kweli kuna mihimili mitatu kwa mujibu wa katiba ya JMT ambayo ni Executive au Serikali, Bunge na Mahakama...
... na ndio maana ni Katiba ya hovyo! A lot of contradictions! Kwa mfano, Katiba inasema miongoni mwa majukumu ya Bunge ni "kuisimamia serikali"; pia "Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi"; further, "madaraka ya serikali yatatoka kwa wananchi". Logically, kwa Katiba hiyo, who is superior?

Mkiambiwa inahitajika Katiba Mpya itakayoondoa mikanganyiko hamtaki; mkigeuka mnadai "hamuoni ibara"! Zipo ila kwa kuwa mmeamua kujifanya vipofu mnajifanya hazipo.
 
Ni kwa ajili ya check and balance, siyo ya nani mkubwa nani mdogo....!!
... kwenye hilo hilo la check and balance kuna mmoja hautambui majukumu yake ipasavyo na mwingine unajitahidi iwezakanavyo kumdhoofisha mwenzake kwa kila hali ili asitambue na/au kutekeleza majukumu yake. Njia mojawapo ni kuweka vibaraka.
 
Nyerere ndiye alitaka absolute power na CCM wakampa. Hakutaka kusumbuliwa akiwa anaitengeneza Tanzania kuwa nchi ya kijamaa. Mwishowe ujamaa wa Nyerere ulifeli, nchi ilifilisika lakini zile nguvu walizompa Nyerere kama kiongozi wa nchi bado zimebaki.
 
... na ndio maana ni Katiba ya hovyo! A lot of contradictions! Kwa mfano, Katiba inasema miongoni mwa majukumu ya Bunge ni "kuisimamia serikali"; pia "Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi"; further, "madaraka ya serikali yatatoka kwa wananchi"...
Mkuu dudus, naunga mkono hoja yako, japo katiba ni Supreme, na hakuna aliye juu ya katiba, ila hiyo katiba ina mmiliki, the owner.

Mmiliki wa katiba, the owner, ni wananchi, "we the people", hivyo kama Bunge ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi, then muundo wa serikali yetu ulipaswa uwe wa "perliamentary supremacy" na sio "presidential supremacy".

Rais awe anateua baadhi wa viongozi, wakiwemo wakuu wa mihimili, na wakuu wa vyombo vya dola halafu Bunge ndio liwaidhinishe.

P
 
Tunataka katiba yenye nguvu kama hii.
NMj.jpg
 
... na ndio maana ni Katiba ya hovyo! A lot of contradictions! Kwa mfano, Katiba inasema miongoni mwa majukumu ya Bunge ni "kuisimamia serikali"; pia "Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi"...

Heshima yangu kwa hao wanachama, wasomi, wanasiasa na wavaa suti na vibaraka wote wa ccm imeshuka sana!
Nimewaweka kundi moja na vinyonga!

Kama nimekosa mimi na nimekosa sana naombeni mnisamehe na Watanzania wote wanisamehe.
 
naunga mkono hoja
P
Kama unaunga mkono hoja ubadilishe kauli yako hadharani tena hapa JF kuwa Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli alijibu swali lako wakati wa press conference kwa majibu mepesi. Rais wakati huo alikuwa anakueleza maana halisi aliyoizungumzia mleta mada tena kwakutumia mifano.

Kwa kifupi you have to apologise to our beloved late President Magufuli kwa kukejeli majibu yake kwa swali lako. Atasikia msamaha wako na kukusamehe, kwa sababu umetufundisha humu jukwaani kuwa roho yake bado ipo nasi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni kweli kuna mihimili mitatu kwa mujibu wa katiba ya JMT ambayo ni Executive au Serikali, Bunge na Mahakama...
Watu hawajui umuhimu wa Katiba yetu inampa Raisi nguvu kuliko mihimili mingine kitu ambacho sio sahihi.. yani viongizi wote wa mihimili iliyo Baki ukiachana na Executive committee inayoongizwa na Raisi nao wanateuliwa na Raisi

Mpaka hapo lazima watakuwa ma loyal kama vile Dog anavyo muheshimu mmiliki wake.

This is the right time kubadilisha hii Katiba yetu.. bado tunahitaji pia kusolve changamoto za Muungani kupitia Katiba mpya
 
Mfumo wa kiutawala tunaoutumia hapa nchinu Rais ni Mkuu wa Serikali na Nchi.

Hivyo mihimili yote mitatu yaani Executive (serikali kuu) Legislative (Bunge) na Judiciary (Mahakama) vipo chini yake.

Nchi nyingine kwa mfano. Uingereza Malkia ni Mkuu wa Nchi ila Serikali inaongozwa na Waziri Mkuu.
 
Back
Top Bottom