Katiba ya chama cha ACT inayopendekezwa kabla ya kupitishwa na Kamati kuu hii hapa

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
322
255
*Alliance for Change and Transparency-Tanzania*
*(Mabadiliko na Uwazi*

*KATIBA*

*TOLEO LA 2014*

Kama lilivyoidhinishwa na Mkutano Mkuu Maalumu wa ACT Tanzania Uliofanyika
Tarehe…katika Ukumbi wa ….
------------------------------------------------------------------------
*Page 2*

*YALIYOMO*
DIBAJI......................................................................................................................................5

SURA YA KWANZA
..............................................................................................................6

1.1

IBARA 1
.....................................................................................................................................
6

1.1.1

JINA LA CHAMA:
...........................................................................................................
6

1.2

IBARA 2
.....................................................................................................................................
6

1.2.1

MAKAO MAKUU YA CHAMA:
....................................................................................
6

1.3

IBARA 3
.....................................................................................................................................
6

1.3.1

ALAMA ZA CHAMA
......................................................................................................
6

1.4

IBARA YA 4
................................................................................................................................
6

1.4.1

ITIKADI
............................................................................................................................
6

1.5

IBARA YA 5
................................................................................................................................
7

1.4.2

LUGHA RASMI YA CHAMA:
........................................................................................
7

1.6.2

MISINGI YA CHAMA
.....................................................................................................
7

2.1

IBARA YA 7
................................................................................................................................
8

2.1.1

MALENGO YA ACT-TANZANIA
..................................................................................
8

SURA YA
PILI.......................................................................................................................10

3.1

IBARA YA 7
..............................................................................................................................
10

3.1.1

UANACHAMA
...............................................................................................................
10

3.1.2

AINA ZA WANACHAMA
............................................................................................
10

3.1.3

ADA YA UANACHAMA
..............................................................................................
11

3.1.4

HAKI ZA MWANACHAMA
.........................................................................................
11

3.1.5

WAJIBU WA MWANACHAMA
...................................................................................
12

3.1.6

KUKOMA UANACHAMA
............................................................................................
12

3.1.7

KUSIMAMISHWA UANACHAMA:
............................................................................
12

3.1.8

KUFUKUZWA UANACHAMA
....................................................................................
13

------------------------------------------------------------------------
*Page 3*

3
3.1.10

ORODHA YA WANACHAMA
...................................................................................
13

SEHEMU YA
PILI.................................................................................................................14

IBARA 8
............................................................................................................................................
14

I.

SIFA ZA KIONGOZI
...........................................................................................................
14

II.

MUDA WA UONGOZI:
.....................................................................................................
15

III.

MIIKO YA UONGOZI:
.....................................................................................................
15

IV.

HAKI ZA KIONGOZI
.......................................................................................................
16

V. UKOMO WA UONGOZI
.......................................................................................................
16

VI.

KUZIBA NAFASI WAZI ZA UONGOZI
.........................................................................
16

VII.

KUKASIMU MADARAKA
............................................................................................
17

SURA YA TATU
...................................................................................................................17

4.1

IBARA YA 9
..............................................................................................................................
17

4.1.1

NIDHAMU NA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA CHAMA
.............................. 17

SURA
NNE.............................................................................................................................22

5.1

IBARA YA YA 9
.........................................................................................................................
22

5.1.1

MUUNDO WA ACT-TANZANIA
................................................................................
22

5.2

IBARA YA 10
............................................................................................................................
22

5.2.1

ACT-TAWI
.....................................................................................................................
22

5.4

IBARA YA 11
............................................................................................................................
26

5.4.1

ACT-KATA/WADI:
........................................................................................................
26

5.5

IBARA YA 12
............................................................................................................................
31

5.5.1

ACT- JIMBO
...................................................................................................................
31

5.6

IBARA YA 13
............................................................................................................................
37

5.6.1

ACT-MKOA
...................................................................................................................
37

5.7

IBARA YA 14
............................................................................................................................
41

5.7.1

ACT-ZANZIBAR
...........................................................................................................
41

5.8

IBARA 15
.................................................................................................................................
43

------------------------------------------------------------------------
*Page 4*

4
5.8.1

ACT- TAIFA
...................................................................................................................
43

IBARA 16
..........................................................................................................................................
53

I.

NGOME ZA CHAMA:
.........................................................................................................
53

IBARA 17
..........................................................................................................................................
54

JUMUIA YA WABUNGE
..........................................................................................................
54

SURA YA
SITA.....................................................................................................................54

IBARA 18
..........................................................................................................................................
54

MAPATO NA MALI ZA CHAMA:
.........................................................................................
54

IBARA 19
..........................................................................................................................................
55

WADHAMINI WA CHAMA:
....................................................................................................
55

IBARA 20
..........................................................................................................................................
55

UKAGUZI WA MAHESABU YA CHAMA
..............................................................................
55

SURA YA SABA
...................................................................................................................56

IBARA 21
..........................................................................................................................................
56

MAREKEBISHO YA KATIBA
..................................................................................................
56

IBARA 22
..........................................................................................................................................
56

KANUNI ZA UENDESHAJI WA CHAMA
...............................................................................
56

IBARA 23
..........................................................................................................................................
56

KUVUNJWA KWA CHAMA:
...................................................................................................
56

IBARA 24
..........................................................................................................................................
57

------------------------------------------------------------------------

*Page 5*
*DIBAJI*
Kwa kuwa tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, hongo, ufisadi, uzembe na
uvivu;
Kwa kuwa tumeamua kuhakikisha kuwa maliasili ya Nchi yetu Tanzania ni
mali ya wananchi
wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na
kuleta maendeleo
sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa;
Kwa kuwa tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea
ujenzi wa Taifa la
Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila,
jinsia, maumbile, hali
ya kipato na lililo juu ya misingi ya haki kwa watu wake wote;
Kwa kuwa tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili
kuwaenzi waasisi wa
ukombozi wa Mwafrika na kujenga kontinenti lenye sauti yenye nguvu na
ushawishi katika
jamii ya mataifa ulimwenguni;
Kwa kuwa tumeamua kupigania demokrasia, uhuru wa mawazo, umoja, utu,
uadilifu,
uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa;
Kwa kuwa kwa nia moja tumeamua kujenga chama cha mrengo wa kushoto
chenye kufuata
misingi ya Demokrasia ya Kijamii (Social Democracy) na ujamaa wa
kisayansi, na misingi
asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) ikiwemo Azimio la Arusha
1
; na
Kwa mujibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na
utamaduni wa
mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania;
Hivyo basi:
Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wa Chama cha ACT Tanzania
*TUMEIKUBALI na KUIDHINISHA*
*KATIBA HII*

1
Tamko la Azimio la Arusha lililotolewa na Chama cha TANU
mnamo mwezi Februari mwaka 1967 .
Tutazingatia misingi ya Azimio hili na hususani Miiko ya
Uongozi kama itakavyopfanyiwa marejeo mara kwa
mara, pamoja na Maazimio mengine yatakayotangazwa na chama kwa
mujibu wa Katiba hii yatakuwa ni
marejeo halali ili kufikia maamuzi yeyote ya kisera ya Chama
cha ACT – Tanzania.
------------------------------------------------------------------------
*Page 6

6
*SURA YA KWANZA*
*SEHEMU YA KWANZA*
*JINA LA CHAMA, MAKAO MAKUU, ALAMA ZA CHAMA, ITIKADI NA LUGHA*
*YA CHAMA*
*1.1*
*IBARA 1*
*1.1.1 JINA LA CHAMA:*
Jina la Chama ni *ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT -*
*Tanzania), yaani UMOJA WA MABADILIKO NA UWAZI TANZANIA.*
*1.2*
*IBARA 2*
*1.2.1 MAKAO MAKUU YA CHAMA:*
Makao Makuu ya Chama ni /*Mwanza */na ofisi ndogo ya Makao Makuu ni
/*Zanzibar na Dar es*/
/*Salaam.*/
*1.3*
*IBARA 3*
*1.3.1 ALAMA ZA CHAMA*
a) Bendera ya chama yenye rangi ya Zambarau, ambayo ndiyo alama kuu ya
chama. Rangi hii inawakilisha taswira ya mchanganyiko wa wanachama
kutoka kona na pembe zote za nchi; utambuzi wa umuhimu wa wanawake na
familia katika jamii; na alama ya kujali makundi yenye mahitaji ya ziada
katika jamii wakiwemo watu wenye ulemavu, watoto na wazee.
b) Nyota ni alama ya kumulika na kuangaza ikiashiria uwazi, ambao ni msingi
mama wa ACT Tanzania
c) Bendera ya Taifa ikiashiria uzalendo, upendo na utayari wa kulilinda na
kulitumikia Taifa la Tanzania.
d) Nembo ya Chama, ambayo ina mchanhanyiko wa nyota, bendera ya Taifa na
manano ACT-Tanzania.
*1.4*
*IBARA YA 4*
*1.4.1 ITIKADI*
ACT Tanzania inaamini katika misingi ya demokrasia jamii na ujamaa wa
kisayansi
(Scientific socialism). Shabaha kuu ya ACT-Tanzania ni kupigania na
kusimamia mabadiliko
------------------------------------------------------------------------
*Page 7*

7
na uwazi nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Chama kinazingatia elimu,
uadilifu,
kujitegemea na bidii katika kazi kama njia kuu ya kujikomboa dhidi ya
umaskini, ujinga,
maradhi na rushwa, ambao ndio maadui wakuu wa Taifa la Tanzania. Falsafa
ya ACT
Tanzania ni UNYERERE, ikiwa ni dhamira ya kurudisha, kuhuisha na
kupigania misingi
mama iliyoasisi taifa la Tanzania, kama ilivyoanishwa katika Azimio la
Arusha na kwa
mazingira ya Tanzania mpya.
*1.5*
*IBARA YA 5*
*1.4.2 LUGHA RASMI YA CHAMA:*
Lugha rasmi ya Chama ni Kiswahili. Lugha ya kiingereza inaweza kutumika
sambamba na
lugha ya Kiswahili inapobidi. Nyaraka zote muhimu, ikiwemo Katiba hii,
zitaandikwa katika
lugha ya Kiswahili na kutafsiriwe katika lugha ya Kiingereza. Chama
kitaweka mazingira
yatakayowezesha kuwepo kwa mawasiliano mbadala zikiwemo lugha za alama
kwa kadri ya
mahitaji.
*SEHEMU YA PILI*
*MISINGI NA MALENGO YA CHAMA*
*1.6*
*IBARA YA 6*
*1.6.2 MISINGI YA CHAMA*
ACT Tanzania inaongozwa na Misingi Kumi (10) ifuatayo:
a) Uzalendo
b) Usawa
c) Uadilifu
d) Uwazi
e) Uwajibikaji
f) Demokrasia Raslimali
g) Hifadhi ya Jamii
h) Utu
i) Umoja wa Afrika
------------------------------------------------------------------------
*Page 8*

8
j) Kujitegemea, Bidii na Umakini katika Kazi
Misingi hii itafafanuliwa katika maandiko mbalimbali ya chama.
*2.1*
*IBARA YA 7*
*2.1.1 MALENGO YA ACT-TANZANIA*
ACT Tanzania itapambana kuhakikisha kwamba inashinda uchaguzi na kuunda
serikali ili
kutekeleza malengo yafuatayo:
1) Kuhakikisha kwamba serikali inatumia raslimali yote ya nchi kwa ajili
ya kuondosha
umaskini, ujinga, maradhi, rushwa, na kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla.
2) Kupigania na kulinda uongozi bora na utawala wa sheria.
3) Kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia raslimali na serikali
inayowajibika kwa
umma wa watanzania.
4) Kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa raia wote wanaume kwa wanawake bila
kujali kabila, rangi, imani za kidini, itikadi, utamaduni ama hadhi yake
ya kiuchumi
na kijamii.
5) Kuendeleza na kudumisha Demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama
vingi vya
siasa.
6) Kuchochea, kuimarisha na kulinda uzalendo, uadilifu na uwazi kama
misingi mikuu
katika uongozi wa nchi.
7) Kuchochea na kuendeleza mapambano katika kulinda haki za watoto,
wanawake na
watu wenye ulemavu.
8) Kupigania haki na heshima ya wafanyakazi, wakulima, wafugaji na
wajiasiriamali
katika ngazi zote.
9) Kudhibiti soko huria ili kuhakikisha kuwa haliathiri haki za utu za
wafanyakazi na
walaji wenye kipato cha chini.
10)Kulinda na kuendeleza mazingira bora kwa vizazi vya leo na vijavyo.
11)Kuhakikisha kuwa idhini na mikataba ya kikanda barani Afrika ambayo
Tanzania ni
mwanachama kama vile AU, EAC na SADC zinaendana na misingi mikuu ya
kidemokrasia na kuendeleza kuheshimu utawala wa sheria Afrika.
12)Kuhimiza ushirikiano na mahusiano na vyama vingine vinavyoamini katika
demokrasia jamii Afrika na duniani kote.
------------------------------------------------------------------------
*Page 9*

9
13)Kuunga mkono na kusukuma mbele juhudi za kuundwa kwa Shirikisho la
Kisiasa la
Afrika Mashariki na kupigania umoja wa Afrika.
------------------------------------------------------------------------
*Page 10*

10
*SURA YA PILI*
*SEHEMU YA KWANZA*
*UANACHAMA*
*3.1*
*IBARA YA 7*
*3.1.1 UANACHAMA *
a) Uanachama wa ACT-Tanzania utakuwa wazi kwa raia wote wenye umri wa kupiga
kura bila kubagua jinsia, kabila, dini, au hali yeyote.
b) Kila raia atakaye kuwa ameandikishwa kuwa mwanachama wa ACT-Tanzania
atapewa kadi ya uanachama itakayoonyesha jina lake, anuani, sahihi yake
na sahihi ya
afisa wa chama aliyemwandikisha.
c) Asiwe Mwanachama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na ACT-
Tanzania
*3.1.2 SIFA ZA MWANACHAMA*
a) Awe raia wa Tanzania
b) Awe ana umri wa kupiga kura kwa mujibu wa sheria za Tanzania
c) Awe anakubaliana na itikadi, falsafa na misingi ya ACT-Tanzania
d) Awe na akili timamu
e) Awe na moyo na utayari wa kutumikia chama na kueneza itikadi, falsafa
na misingi
yake
*3.1.2 AINA ZA WANACHAMA*
/*a) Wanachama*/
Ni wanachama wote waliojiandikisha na kulipa ada ya ACT-Tanzania na
kuzingatia
masharti ya Katiba hii.
------------------------------------------------------------------------
*Page 11*

11
/*b) Wanachama Vikundi*/
Ni wanachama wanaotokana na jumuiya, taasisi, mashirika au vikundi
mbalimbali
ambavyo vimeamua kujiunga na chama kupitia umoja wao.
/*c) Wanachama wanafunzi*/
Hawa ni wanachama ambao hawajatimiza umri wa kupiga kura na ambao
wanajiandaa kujiunga na chama siku za usoni
*3.1.3 ADA YA UANACHAMA*
a) Kila mwanachama atawajibika kulipa ada za uanachama kama
itakavyopangwa na
vikao vya chama
b) Bila kuathiri sheria zinazohusu vyama vya siasa nchini, pamoja na
misingi na
masharti ya Katiba hii, kila mtu, kundi la watu, wanaokubaliana na
misingi, malengo,
sera na mipango ya chama wanaweza kutoa ada ya kundi la uanachama
c) Kutakuwa na kiingilio kwa kila mwanachama na kundi lolote litakalo
taka kujiunga
na chama kama itakavyopangwa na vikao mbalimbali vya maamuzi katika chama
d) Utaratibu wa ulipaji wa kiingilio na ada vitafafanuliwa katika kanuni
za chama
*3.1.4 HAKI ZA MWANACHAMA*
a) Kushiriki shughuli zote za chama kwa mujibu wa kanuni na taratibu
zilizowekwa
b) Kuwa na haki ya kusikilizwa na kuuliza swali kuhusu maendeleo na
mwenendo wa
chama
c) Kuchagua na kuchagliwa kuwa kiongozi ndani ya chama
d) Kuwasilisha pendekezo au maelezo kwenye kikao chochote cha chama,
hadi katika
ngazi ya Halmashauri Kuu
e) Kukosoa kiongozi yeyote ndani ya vikao vya chama
f) Wanachama wanaweza kuitisha kikao chochote endapo tu asilimia sabini
na tano ya
wanachama wote au wajumbe wa kikao hicho watatia sahihi kuhitaji kikao
hicho
kiitishwe. Bila kuathiri maneno haya tangulizi wajumbe wanao hitaji
kikao hicho
lazima waonyeshe kuwa viongozi katika ngazi husika wameshindwa kuitisha
vikao
hivyo zaidi ya mara tatu kwa mujibu wa katiba na utaratibu wa kuitisha
vikao vya
namna hiyo utafafanuliwa kwenye kanuni za chama.
------------------------------------------------------------------------
*Page 12*

12
*3.1.5 WAJIBU WA MWANACHAMA*
a) Kujifunza na kupanua uelewa kuhusu itikadi, falsafa na misingi ya
ACT-Tanzania
b) Kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kwamba ACT-Tanzania inashinda
katika
chaguzi mbalimbali zitakazoitishwa nchini kwa mujibu wa Katiba na sheria
za nchi
c) Kuzingatia nidhamu ya ACT-Tanzania, kushiriki kikamilifu katika
shughuli za chama
na kutekeleza kwa vitendo sera na maamuzi ya chama, na kushiriki
kikamilifu katika
kukomoesha vitendo vyovyote ndani na nje ya chama vinavyoweza
kuhatarisha uhai
na maslahi ya chama
d) Kueneza itikadi, falsafa na misingi ya ACT-Tanzania kwa umma, na
kujifunza
mahitaji ya umma kwa wakati na kuhakikisha kwamba yanazingatiwa katika
sera za
chama
e) Kuwa mfano na sura ya ACT-Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na
umakini
f) Kulipa ada na kuchagia mchango wowote kwa mipango maalumu na shughuli za
ACT-Tanzania kama itakavyokuwa imeamuliwa mara kwa mara na vikao vya chama.
*3.1.6 KUKOMA UANACHAMA*
A:
Mwanachama atakoma kuwa mwanachama ikiwa:
a) Atajiuzulu mwenyewe kwa hiari yake kwa kuandika barua kwa katibu wa
jimbo au
katibu mkuu kwa kueleza kusudio la kuacha kuwa mwanachama na kurudisha
kadi ya
uanachama.
b) Kujiunga na chama kingine cha siasa.
c) Kufukuzwa uanachama kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa katika Katiba hii.
d) Atapoteza sifa za uanachama kama zilivyoanishwa katika Katiba hii.
B: Kila mtu ambaye amekoma kuwa mwanachama atalazimika kurudisha mali za
chama
zilizo chini yake. Hata hivyo ada, michango na mali zingine ambazo
atakuwa amechangia
alipokuwa mwanachama hazitarudishwa.
*3.1.7 KUSIMAMISHWA UANACHAMA:*
a) Mwanachama anaweza kusimamishwa uanachama au nafasi ya ofisi
anayoishikilia ili
kupisha uchunguzi kuhusu mwenendo wake utakaofanywa na Kamati ya Uadilifu
------------------------------------------------------------------------
*Page 13*

13
katika ngazi husika.
b) Uamuzi wa kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote hautakuwa na nguvu
hadi pale uamuzi huo utakapokuwa umewasilishwa kwa mwanachama kwa maandishi
na shauri lake limeanza kushughulikiwa na Kamati ya Uadilifu.
*3.1.8 KUFUKUZWA UANACHAMA*
a) Mwanachama anaweza kufukuzwa kwenye chama kwa sababu zinazotokana na
mwenendo usiofaa kwa mujibu wa masharti na Kanuni za Katiba hii, na mara
baada
ya kufukuzwa uanachama wake utakoma.
b) Hakuna mwanachama atakaye fukuzwa uanachama hadi pale ambapo masharti na
kanuni zilizoanishwa katika Ibara ya Nne (4) ya Katiba hii zitakuwa
zimefuatwa.
c) Mwanachama yeyote ambaye atasaidia, kushawishi, kujiunga, kutoa tamko
la kuunga
mkono chama kingine au mgombea wakati chama kimeweka mgombea kwenye
uchaguzi wowote kwa mujibu wa sheria ya nchi atakuwa amepoteza uanachama wa
ACT-Tanzania
d) Pale mwanachama atakapokuwa amepoteza uanachama wake kwa njia yoyote ile
anaweza kuomba tena uanachama wa ACT-Tanzania na anaweza kukubaliwa kuwa
mwanachama tena kwa mujibu wa Katiba hii, labda tu pale ambapo
Halmashauri Kuu
ya ACT-Tanzania itakuwa imeamue vinginevyo.
*3.1.10 ORODHA YA WANACHAMA*
*a) *Kutakuwa na rejesta ya orodha ya wanachama wote katika kila Tawi,
Kata na katika
kila Jimbo la Uchaguzi, na rejesta hii itahuishwa kila baada ya miezi
sita. Makatibu
wa chama katika ngazi husika watatuma orodha ya wanachama kwa ngazi
inayofuata
kwa ajili ya kumbukumbu za chama katika kila ngazi.
*b) *Katibu wa chama mkoa atatunza orodha ya wanachama wote kwenye mkoa
wake na
atapokea orodha ya wanachama wote walioandikishwa kila jimbo katika mkoa
wake.
*c) *Sekretariati ya Chama makao makuu itatunza rejesta ya wanachama
wote nchi nzima.
*3.1.11 AHADI TANO (5) ZA MWANACHAMA WA ACT-TANZANIA*
*Kila mwanachama wa ACT-Tanzania atatoa ahadi zifuatazo:*
i) Nitapambana dhidi ya dhuluma, fitina, unafiki uwongo, rushwa na
ufisadi kwa uwezo
wangu wote
------------------------------------------------------------------------
*Page 14*

14
ii) Nitapambana dhidi ya Umasikini na nitasimamia utajiri wa nchi yangu
kwa faida ya
wote
iii) Nitashiriki kujenga Taifa lenye kujitegemea, lisilo na unyonyaji,
ubaguzi na lenye
misingi ya Haki
iv) Nitashiriki kujenga Umoja wa Afrika
v) Nitapigania uwepo wa demokrasia ndani na nje ya Chama changu.
*SEHEMU YA PILI*
*UONGOZI*
*IBARA 8*
*I.*
*SIFA ZA KIONGOZI*
i) Awe mwaminifu kunakothibistishwa na historia yake ya kuwa mkweli katika
maisha binafsi na umma
ii) Awe ni mtu anayeheshimu na kuzingatia misingi ya demokrasia
iii) Awe ni mtu aliyethibitika kutoa na/au kutokuminya haki za wengine
iv) Awe ni mtu mwenye kuheshimu, kulinda na kuendeleza utawala wa sheria
kunakothibitishwa na yeye mwenyewe kufuata na kuzingatia sheria katika
maisha
yake binafsi na utumishi wa umma
v) Awe muwazi katika mambo ya umma na atakayehakikisha kwamba wanachama
na wananchi kwa ujumla wanapata taarifa muhimu kuhusu mambo ya chama na
nchi yaliyo chini ya himaya yake
vi) Awe na kiwango cha uadilifu kisichotilika shaka katika maisha yake
binafsi na
umma
vii)Awe ni mtu anayeonyesha kwa vitendo bidii na umakini katika kazi
viii)
Awe ni mtu aliyedhihirika kuzingatia na kuishi misingi mama ya ACT-
Tanzania
*II.*
*AINA ZA VIONGOZI*
a) Viongozi wa kuchaguliwa na mikutano mikuu ya kila ngazi
b) Viongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa na vikao vya uongozi katika ngazi
mbalimbali za chama
------------------------------------------------------------------------
*Page 15*

15
c) Watendaji waajiriwa/watumishi katika chama
d) Viongozi wa ngome za chama watakao chaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa
katiba hii na kanuni za ngome zao
e) Viongozi wanaotokana na nafasi zao kama zilivyoanishwa na Katiba ya
Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania kama vile diwani, mbunge, Waziri, Waziri Mkuu,
Rais, n.k.
*II.*
*MUDA WA UONGOZI:*
i) Kila uongozi uliochaguliwa au kuteuliwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Chama
utashika wadhifa wake kwa kipindi cha miaka tano.
ii) Kiongozi aliyechaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, atashika
wadhifa wake hadi kipindi cha Uchaguzi Mkuu alichochaguliwa/teuliwa
kuisha na
anaweza kugombea au kuteuliwa kwa kipindi kingine cha miaka mitano ambacho
kitakuwa ndio ukomo wake wa kugombea au kuteuliwa kushika nafasi hiyo.
iii) Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na
kuchaguliwa
tena, mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi. Isipokuwa
mwanachama yeyote wa ACT-Tanzania atakuwa kiongozi kwa vipindi visivyozidi
viwili katika nafasi moja ya uongozi katika ngazi husika.
iv) Ibara hii itahusu pia viongozi wa NGOME za ACT-Vijana, Walezi na
Wanawake
*III.*
*MIIKO YA UONGOZI:*
i) Ni mwiko kwa kiongozi kutumia madaraka aliyopewa kwa ajili ya manufaa
yake
binafsi, au kwa upendeleo au kwa namna yoyote ambavyo ni kinyume cha lengo
lililokusudiwa madaraka hayo.
ii) Ni mwiko kwa kiongozi kupokea mapato ya kificho, kutoa au kupokea
rushwa au
kushiriki mambo yoyote yale ya magendo au mambo mengine ambayo ni
kinyume cha lengo lililokusudiwa kwa madaraka hayo.
iii) Ni mwiko kwa kiongozi yoyote wa chama kufitinisha/kuchonganisha au
kutoa
tuhuma zisizo kuwa na ukweli kwa wanachama, viongozi wa chama au kwa
chama bila kufuata utaratibu wa katiba au kanuni za chama
iv) Ni mwiko kwa kiongozi kufanya, kuchochea au kushabikia aina yeyote ya
ubaguzi kama vole wa kidini, ukabila, jinsia, n.k
------------------------------------------------------------------------
*Page 16*

16
v) Kiongozi yeyote wa ACT-Tanzania lazima aweke wazi ndani ya chama mali
alizonazo na namna alivyozipata, na taarifa ya mali za kiongozi
zitatolewa katika
kila baada ya miaka mitano.
*IV.*
*HAKI ZA KIONGOZI*
Pamoja na haki za uanachama zilizoanishwa katika Katiba hii, Kiongozi wa
ACT-Tanzania
pia ana haki zifuatazo:
i) Haki ya kukiwakilisha Chama katika shughuli mbalimbali za kijamii na
kiserikali.
ii) Kuandaa na kupendekeza programu mbalimbali za Chama ili kuleta
ustawi katika
Chama.
iii) Haki ya kujitetea au kutoa taarifa juu ya jambo au mashtaka yoyote
juu yake na ana
haki ya kukata rufaa kwenye vikao vya juu iwapo hajaridhika na uamuzi
uliotolewa
na kikao cha chini.
iv) Haki ya kupata habari au taarifa zote zilizojadiliwa na kutolewa
uamuzi na
wanachama au uongozi wa juu katika kumbukumbu za vikao vinavyomhusu.
*V. UKOMO WA UONGOZI*
Mwanachama wa ACT-Tanzania atakoma kuwa Kiongozi wa Chama:-
i) Kwa kujiuzulu kwa hiari yake;
ii) Kwa kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama;
iii) Kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya Katiba,
Kanuni au maadili ya Chama;
iv) Kwa kufariki;
v) Kupatwa na matatizo ya akili;
vi) Muda wa uongozi kumalizika;
vii)Kupatikana na hatia Mahakamani kwa kosa la jinai ambalo Chama kitaona
kinakifedhehesha na kukiingiza katika mkanganyiko wa kisiasa.
*VI.*
*KUZIBA NAFASI WAZI ZA UONGOZI*
i) Kamati ya Uongozi katika ngazi za Jimbo au chini yake na/au
Halmashauri Kuu
------------------------------------------------------------------------
*Page 17*

17
itaziba kwa muda nafasi yoyote ya kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu wa
ngazi husika.
ii) Nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa na vikao husika kwa
kufanya
uteuzi mpya katika muda usiozidi miezi sita tangu nafasi kuwa wazi.
iii) Muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu (b) hapo juu
hautazidi miezi
kumi na miwili (12).
iv) Bila kuathiri sharti la kifungu (iii) hapo juu, hakutafanyika
uchaguzi rasmi wa
kuziba nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini ya hapo kabla ya
Uchaguzi
Mkuu wa kawaida wa Chama unaofuata kufanyika.
*VII. KUKASIMU MADARAKA*
i)Kamati ya Uongozi wa Jimbo au Kamati Kuu Taifa zinaweza kukasimia
baadhi ya
madaraka kwa Sekretarieti yake kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe wa
kikao
ii) Halmashauri Kuu inaweza kukasimu baadhi ya madaraka yake kwa Kamati Kuu
kwa azimio la wingi wa kura za wajumbe
iii) Mkutano Mkuu unaweza kukasimu kwa Halmashauri Kuu baadhi ya madaraka
yake, lakini kwa azimio maalumu kwa ajili hiyo.
*SURA YA TATU*
*4.1*
*IBARA YA 9*
*4.1.1 NIDHAMU NA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA CHAMA*
*I: Kuteuliwa kwa Kamati ya Uadilifu*
a) Kila jimbo litakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itakayoteuliwa na
Halamashauri
ya Jimbo. Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itaundwa na wajumbe wasiopungua
watatu
(3) na wasiozidi watano (5), kwa kuzingatia kuwa kutakuwa na angalau mjumbe
mmoja (1) mwanamke kama Kamati itakuwa na wajumbe watatu (3), au angalau
wajumbe wawili (2) wa kike kama Kamati itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna
afisa au kiongozi wa chama katika ngazi ya Jimbo atakayeruhusiwa kuwa
mjumbe wa
Kamati ya Uadilifu wa Jimbo.
------------------------------------------------------------------------
*Page 18*

18
b) Kila mkoa utakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itakayoteuliwa na
Halmashauri
ya Mkoa. Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itaundwa na wajumbe wasiopungua
watatu (3)
na wasiozidi watano (5), kwa kuzingatia kuwa kutakuwa na angalau mjumbe
mmoja
(1) mwanamke kama Kamati itakuwa na wajumbe watatu (3) au angalau wajumbe
wawili (2) wa kike kama Kamati itakuwa na wajumbe watano (5). Hakuna
afisa au
kiongozi wa chama katika ngazi ya Mkoa atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati
ya Uadilifu wa Mkoa.
c) Kutakuwa na Kamati ya Uadilifu ya Taifa, ambayo itakuwa ni moja kati
ya Kamati za
Kudumu za Chama, na itaundwa na wajumbe watakaochaguliwa na Baraza Kuu la
Taifa la ACT Tanzania kwa mapendekezo ya Kamati Kuu.
i) Kamati ya Uadilifu ya Taifa itakuwa na wajumbe wasiopungua watano (5)
na wasiozidi tisa (9).
ii)
Mwanachama yeyote mwaminifu na mwenye uelewa wa chama na
siasa za nchi na dunia anaweza kuomba ujumbe wa Kamati ya Uadilifu
iii)
Kamati Kuu itayachuja majina ya waombaji wote wa ujumbe wa
Kamati ya Uadilifu na kupendekeza majina yasiyopungua matano (5)
na yasiyozidi tisa (9) kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa uwiano wa
kijinsia
iv)
Halmashauri Kuu ya Taifa itateua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu
wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa (9), kwa kuzingatia kuwa
kutakuwa na angalau wajumbe wawili (2) wanawake kama Kamati
itakuwa na wajumbe watano (5), au angalau wajumbe watatu (3)
wanawake kama Kamati itakuwa na wajumbe wanaozidi watano (5).
Hakuna afisa au kiongozi wa chama katika ngazi ya Taifa
atakayeruhusiwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Uadilifu wa Mkoa
v)
Baraza Kuu litachagua Mwenyekiti wa Kamati ya Uadilifu ya Taifa
kwa mapendekezo ya Kamati Kuu kwa kuzingatia kuwa mwenyekiti
atakuwa mtu mwenye shahada ya sheria ya chuo kikuu
kinachotambulika na mamlaka husika nchini.
d) Hakuna chombo kitakachokuwa na mamlaka ya kuivunja Kamati ya Uadilifu ya
Taifa, isipokuwa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa idadi isiyopungua nusu ya
kura zote
za wajumbe waliohudhuria.
------------------------------------------------------------------------
*Page 19*

19
*II: Muda wa Wajumbe wa Kamati ya Uadilifu*
Muda wa wajumbe wa Kamati ya Uadilifu utakuwa miaka minne, lakini
wanaweza kuteuliwa
tena baada ya muda wao kwisha na uwepo wake utazingatia masharti mengine
ya Katiba hii.
*III: Mamlaka ya Kamati za Uadilifu*
a) Kamati ya Uadilifu ya Jimbo itakuwa na mamlaka kuhusu masuala yote ya
kinidhamu
katika ngazi ya Jimbo na ngazi za chini yake
b) Kamati ya Uadilifu ya Mkoa itakuwa na mamlaka ya masuala yote ya
kinidhamu
yanayohusu ngazi ya Mkoa, yaani kuhusu maafisa, viongozi wa ngazi ya
Mkoa. Pia
kitakuwa chombo cha rufaa na mapitio kwa masuala ya kinidhamu katika
ngazi ya
Jimbo na uamuzi wake utakuwa wa Mwisho.
c) Kamati ya Uadilifu ya Taifa itakuwa na mamlaka ya kinidhamu kuhusu
maafisa na
viongozi katika ngazi ya Taifa, pamoja na viongozi na wanachama wengine
waandamizi wakiwemo wabunge, Walezi, wajumbe wa Kamati za Kudumu na
wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, pamoja na masuala yote ya
kinidhamu yatakayoelekezwa kwake na vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri
Kuu.
d) Kamati ya Uadilifu Taifa ndicho kitakachokuwa chombo cha Rufaa kwa
masuala ya
kinidhamu katika ngazi ya Mkoa.
e) Halmashauri Kuu itakuwa ndiyo ngazi ya rufaa ya kitaifa.
f) Mwanachama yeyote asiyeridhishwa na uamuzi katika ngazi ya jimbo anaweza
kukata rufaa au kuomba mapitio ya shauri hilo kwa kupeleka rufaa au ombi
la pitio
kwa maandishi kwa katibu wa ACT-Mkoa ambaye atawasilisha rufaa au ombi
la pitio
kwa Kamati ya Uadilifu Mkoa. Shauri kuhusu kiongozi au mjumbe katika
ngazi ya
Mkoa au Taifa litaelekezwa kwa Katibu Mkuu ambaye atapeleka katika kamati ya
uadilifu ngazi ya Taifa.
*IV: Kazi za Kamati za Uadilifu*
i) Kufanya uchunguzi kamili, kwa imani na weledi na bila upendeleo,
kuhusu tuhuma
zilizowasilishwa dhidi ya mwanachama, mjumbe, afisa au kiongozi wa chama
katika
ngazi husika
------------------------------------------------------------------------
*Page 20*

20
ii)
Kutoa taarifa kwa maandishi kuhusu matokeo ya uchunguzi na sababu na
mazingira
yaliyosababisha kufikia hitimisho
iii)
Kutoa adhabu yeyote kwa mujibu wa Katiba hii isipokuwa kusimamisha au
kufukuza
uanachama au uongozi
iv)
Kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa au Kamati ya Uongozi kwa
ngazi ya Mkoa na Jimbo kwa adhabu ambayo haina mamlaka nazo
v)
Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa au kamati ya Uongozi kwa ngazi ya Mkoa na
Jimbo
itayapitia mapendekezo ya Kamati ya Uadilifu na kutoa mapendekezo yake kwa
Halmashauri Kuu kwa ngazi ya Taifa au Halmashauri ya Mkoa au Jimbo kwa ngazi
hizo kwa maamuzi ya mwisho
vi)
Kikao katika ngazi husika kitapokea na kutoa maamuzi ndani ya siku kumi
na nne
(14) kuhusu mapendekezo ya Kamati ya Uadilifu kwa kukubali mapendekezo
yote,
kurekebisha au kukataa na itatoa maamuzi yake na sababu za maamuzi hayo kwa
wote walioathirika
vii)
Kikao katika ngazi husika kitatoa maelekezo na maamuzi yanayolenga
kuimarisha
nidhamu ndani ya chama, ikiwemo kusimamisha au kufukuza uanachama. Uamuzi wa
kikao husika utaanza kutekelezwa mara moja kama hapatakuwa na rufaa ndani ya
siku 14 tangu maamuzi yatolewe.
*V: Namna ya Kushughulikia Mashauri ya Nidhamu*
a) Shauri la kinidhamu au lalamiko lolote dhidi ya mwanachama, mjumbe au
kiongozi wa chama linaweza kupelekwa kwa maandishi na mlalamikaji kwa
Kamati ya Uadilifu katika ngazi husika
b) Mashtaka yataendeshwa kwa uwazi kwa mujibu wa kanuni za haki ya asili ya
mtuhumiwa (natutal justice)
c) Kamati ya Uadilifu itamaliza kushughulikia shitaka/lalamiko ndani ya
siku ishirini
na moja (21) tangu ipokee shitaka/lalamiko husika. Hata hivyo, Kamati
Kuu kwa
ngazi ya Taifa, Kamati ya Uongozi kwa ngazi ya Mkoa au Jimbo inaweza
ikaongeza muda wa kushughulikia shauri kadri itakavyoona inafaa
d) Maamuzi ya mwisho katika Kamati ya Uadilifu yatafikiwa kwa mujibu wa
maridhiano au idadi ya watu walio wengi katika kikao cha Kamati hiyo
------------------------------------------------------------------------
*Page 21*

21
e) Kamati ya Uadilifu haitaingiliwa wala kuulizwa maswali na mtu yeyote
wakati
ikiendelea kushughulikia shauri husika.
f) Bila kuathiri masharti ya ibara hii viongozi wa ngazi husika
watashughulikiwa na
kamati ya uadilifu ya ngazi hiyo na kutoa mapendekezo kwenye kamati ya
uadilifu ya ngazi ya juu yake kwa maamuzi
*VI: Rufaa*
Mwanachama, mjumbe au kiongozi yeyote ambaye hakuridhishwa na maamuzi ya
kikao
kilichotoa maamuzi ya kinidhamu atakata rufaa kwa mamlaka ya rufaa ndani
ya siku kumi na
nne (14) tangu maamuzi yatolewe. Mamlaka ya Rufaa itatoa maamuzi ya
Rufaa ndani ya
siku ishirini na moja (21) tangu kupokea rufaa husika, na maamuzi yake
yatakuwa ya
mwisho.
*VII: Makosa Yanayoweza Kusababisha Hatua za Kinidhamu*
a) Makosa yafuatayo yanaweza kusababisha hatua za kinidhamu kwa mwanachama,
afisa, mjumbe au kiongozi wa chama
i) Kukataa kutekeleza wajibu na/au majukumu ya kikatiba
ii) Kufanya fujo au kutoa vitisho dhidi ya mwanachama mwingine
iii) Kughushi au kutoa taarifa za uwongo kuhusu mahesabu au madai ya uwongo
kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali
iv) Kuharibu mali ya chama kwa makusudi
v) Kupinga sera za chama katika majukwaa ya kisiasa
vi) Kusababisha mgawanyiko ndani ya chama
vii)Kufanya kitendo chochote ambacho kinagharimu na/au kuharibu taswira ya
chama katika umma
b) Kuthibitika kutenda kosa lolote hapo juu au linalofanana na hilo
kutahesabiwa kuwa
ni utovu wa nidhamu na litasababisha kutolewa adhabu sitahiki ikiwemo:
i) Karipio kali
ii) Onyo
iii) Onyo kali
iv) Faini
------------------------------------------------------------------------
*Page 22*

22
v) Kusimamishwa kugombea nafasi ya uongozi kwa kipindi kisichopungua
mwaka mmoja au
vi) Kusimamishwa uanachama
vii)Kufukuzwa uanachama.
*SURA NNE*
*5.1*
*IBARA YA YA 9*
*5.1.1 MUUNDO WA ACT-TANZANIA*
I.
ACT-Tanzania ni chama cha kitaifa, na kitakuwa na uwakilishi katika kila
ngazi
katika muundo wa uchaguzi wa nchi kama ifuatavyo
a) ACT Tawi
b) ACT Kata
c) ACT Jimbo
d) ACT Mkoa
e) ACT Taifa
II.
Uundaji wa ngazi moja ya chama utafanyika tu baada ya kuwa na muundo na
uongozi katika ngazi za chini kwa angalau theluthi moja. Mfano, ili
kuunda ngazi ya
Kata ni lazima kuwe na angalau theluthi (1/3) ya matawi katika kata husika
III.
Kwa kuzingatia Ibara ndogo ya 5.1.1. (I) hapo juu, ngazi ya juu ya Chama
itateua
Kamati ya muda itakayokuwa na wajibu wa kuratibu shughuli za chama na
kuwaunganisha wanachama katika eneo lisilo na uongozi wa kikatiba mpaka
wanapofikia uwezo wa kuwa na uongozi wa kikatiba.
*5.2*
*IBARA YA 10*
*5.2.1 ACT-TAWI*
II.
Ngazi ya ACT-Tawi itaundwa katika eneo la kijiji, Mtaa, na/au Sheia kwa
Tanzania
Zanzibar
a) *Idadi ya wanachama*
Idadi ya Wanachama wa ACT-Tawi itakuwa ni watu ishirini (20) na kuendelea.
------------------------------------------------------------------------
*Page 23*

23
b) *Viongozi wa ACT-Tawi*:
(i.) Mwenyekiti wa ACT- Tawi
(ii.) Katibu wa ACT-Tawi
(iii.) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Tawi
(iv.) Wenyeviti wa NGOME za ACT-Vijana na Wanawake katika Tawi
(v.) Makatibu wa NGOME za ACT-Vijana na Wanawake katika Tawi
II.
Viongozi wa ACT Tawi watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa ngazi ya ACT Tawi
kwa kuzingati Kanuni zilizotungwa na Halmashauri Kuu ya Chama.
c) *Vikao vya ACT-Tawi*
*i)*
*Mkutano Mkuu*.
Mkutano Mkuu ndiyo Kikao Kikuu kupita vyote na wajumbe wake watakuwa
wanachama wote katika ngazi ya ACT-
Tawi ambayo akidi yake ni 1/2 ya wanachama wote. Mkutano wake utafanyika
mara 4 kwa mwaka na unaweza kuitishwa kwa dharura
*ii)*
*Kamati ya Uongozi*.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi katika ngazi ya ACT Tawi ni mwenyekiti wa
kijiji,
mtaa au shehia anaye tokana na ACT-Tanzania na wajumbe wengine ni kama
walivyoanishwa katika ibara ya 5.2.1 (Ib)
d) *Kazi za Mkutano wa Ngazi ya ACT-Tawi*
i) Kuchagua viongozi wa ngazi ya ACT-Tawi.
ii) Kupendekeza wagombea katika uchaguzi wa kiserikali wa Vitongoji na
Mitaa na kuwasilisha kwa Kamati ya Utendaji ya kijiji/mtaa kwa taarifa.
iii) Kuunda timu ya kampeni katika ngazi ya Tawi
iv) Kujadili taarifa za Kamati ya Uongozi na kutoa uamuzi au
maelekezo/mwongozo wa utekelezaji.
v) Kujadili hali ya uhai wa chama.
vi) Kujadili masuala ya kijamii katika eneo lao
e) *Kazi za Mwenyekiti wa ACT-Tawi*
------------------------------------------------------------------------
*Page 24*

24
i)Atakuwa Mwenyekiti wa mikutano na vikao vyote vya ACT-Tawi.
ii) Atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za Chama katika ACT-
Tawi.
iii) Atakuwa ndiye mwenezi na mhamasishaji mkuu wa siasa ya Chama katika
eneo lake.
iv) Katika mikutano anayoongoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida,
atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na
wasiofiki zitalingana
v) Kuhakikisha kuwa Chama kinashinda ngazi ya Tawi katika uchaguzi wa
serikali za mitaa
f)*Kazi za Katibu wa ACT-Tawi*
i) Atakuwa Katibu wa mikutano na vikao vyote vya ACT-Tawi.
ii) Atawajibika na kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu utendaji wa
shughuli za
Chama katika ACT-Tawi kwa ngazi ya kijiji/mtaa.
iii) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa ACT-Tawi
iv) Atakuwa Mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika ACT-Tawi.
v) Atatunza daftari la wanachama wote waliopo katika eneo lake.
vi) Atakuwa ndiye mwajibikaji mkuu wa masuala yote yahusuyo fedha na mali za
Chama katika eneo lake.
vii) Kuhakikisha kuwa Chama kinashinda ngazi ya Tawi katika uchaguzi wa
kiserikali.
g) *Kazi za Kamati ya Uongozi ACT-Tawi*
i)
Kuendesha shughuli za kila siku za Chama katika eneo lake.
ii)
Kuandaa Mikutano Mikuu ya ngazi ya ACT-Tawi.
iii)
Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa,
sera na madhumuni ya Chama.
iv)
Kuendesha na kusimamia Kampeni za Uchaguzi wa wagombea wa Chama
katika Uchaguzi wa Kiserikali.
v)
Kusimamia nidhamu ya wanachama katika ngazi ya ACT-Tawi na
kuchukua hatua kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama.
------------------------------------------------------------------------
*Page 25*

25
vi)
Kusimamia na kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya
ngazi husika.
vii)
Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
viii)
Kuhakikisha chama kinashika hatamu kwenye uchaguzi wa Tawi na
kinapata kura nyingi za mwenyekiti wa kijiji/mtaa,ubunge na uraisi katika
ngazi ya Tawi
h) *Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Tawi*
i)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Tawi watakuwa ni viongozi wote
wa chama ACT-Tawi na kijiji/mtaa/shehia.
ii)
Mkutano Mkuu wa ACT-Tawi utakutana mara mbili kwa mwaka.
Mkutano Mkuu maalum/dharura inaweza kuitishwa wakati wowote na
Kamati ya Utendaji kadri itakavyolazimu.
i)*Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT-Tawi*
i) Kuchagua viongozi wa ACT-Tawi
ii) Kuchagua wawakilishi wawili wa ACT-Tawi kuingia katika Mkutano
Mkuu wa ACT-Kata/Wadi.
iii) Kuchagua wagombea katika uchaguzi wa serikali za kijiji na mtaa
iv) Kujadili taarifa ya Kamati ya Utendaji ya ACT-Tawi na kutoa maamuzi au
maelekezo/mwongozo wa utekelezaji.
v) Kupokea maamuzi na maagizo ya vikao vya juu vya Chama na kutoa
maelekezo kwa Kamati ya Utendaji ya ACT-Tawi.
vi) Kujadili utekelezaji wa itikadi, falsafa, sera na mipango ya Chama
inayohusu masuala ya jamii katika eneo la kijiji, mtaa ama Sheia.
vii)Kutoa mwongozo na maelekezo kwa wawakilishi wa Chama walio kwenye
Serikali ya Kijiji au Kamati ya Mtaa au katika Shehia.
viii)
Kujadili na kuzingatia taarifa za utendaji wa NGOME za ACT-Vijana
na ACT Wanawake katika Tawi na kutoa maelekezo.
ix) Kuidhinisha programu za chama katika eneo lao.
------------------------------------------------------------------------
*Page 26*

26
*5.4*
*IBARA YA 11*
*5.4.1 ACT-KATA/WADI:*
Ngazi ya ACT-kata/Wadi itaundwa katika eneo la kiutawala la Kata/Wadi
katika Serikali
za Mitaa, yaani za Vijijini na za Mijini.
a) *Vikao vya Chama vya ACT- Kata/Wadi*:
i) Mkutano Mkuu wa ACT-Kata.
ii) Kamati ya Uongozi yaACT- Kata.
b) *Viongozi wa Chama ngazi ya ACT- Kata/Wadi*
i) Mwenyekiti wa Chama Kata/Wadi;
ii) Katibu wa Chama Kata/Wadi;
iii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama wa Kata/Wadi;
iv) Wenyekiti NGOME ya ACT-Vijana, na ACT Wanawake ngazi ya Kata;
v) Makatibu NGOME ya ACT-Vijana na ACT wanawake ya Kata.
c) *Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Kata/Wadi*:
i)
Wajumbe wote wa kamati ya uongozi ya ACT-Kata
ii)
Wenyeviti wote wa ACT-Kijiji/mtaa
iii)
Makatibu wote wa ACT-Kijiji/mtaa
iv)
Makatibu wote wa NGOME za ACT-Vijana na ACT- Wanawake katika Kata,
Diwani, Viti Maalum, Mbunge/Mwakilishi anayeishi katika Kata
v)
Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Wenyeviti wa Kamati za Mitaa au Shehia
wanaotokana na Chama katika Kata
vi)
Wawakilishi wawili wa kila ACT-Kijiji/mtaa waliochaguliwa na Mkutano
Mkuu.
d) Mkutano Mkuu wa ACT-Kata utakutana mara mbili (2) kwa mwaka. Mikutano
maalum/dharura inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya Utendaji kadri
itakavyolazimu.
e) *Kazi za Mkutano Mkuu wa Kata/Wadi*
------------------------------------------------------------------------
*Page 27*

27
i)
Kuchagua viongozi wa ACT-Kata na kuchagua mgombea udiwani katika
kata husika kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Katiba na Kanuni ya
ACT-Tanzania.
ii)
Kuchagua mwakilishi wa Kata katika Mkutano Mkuu wa Jimbo.
iii)
Kujadili taarifa za Kamati ya Uongozi ya Kata na kutoa maamuzi au
maelekezo kwa utekelezaji.
iv)
Kupokea maamuzi na maagizo ya vikao vya juu na kutoa maelekezo ya
utekelezaji kwa Kamati ya Utendaji.
v)
Kuzingatia, kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa falsafa na sera
za Chama katika Kata.
vi)
Kujadili na kutoa mapendekezo kwa ngazi za juu, kuhusu masuala ya
kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojitokeza katika Kata, ambayo
yanahitaji hatua za kichama ngazi za juu.
vii)
Kusikiliza na kutoa uamuzi au mapendekezo kwa ngazi ya juu, kuhusu
masuala ya kinidhamu kwa wanachama au viongozi wa Chama kwa
kuzingatia masharti ya Katiba na kanuni za Chama.
viii)
Kuidhinisha Programu ya Chama katika Kata.
ix)
Kujadili taarifa za utendaji wa NGOME za ACT-Vijana na ACT
Wanawake katika Kata.
x)
Kuchagua wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo.
f) *Kazi za Mwenyekiti wa Kata/Wadi*:
i)
Atakuwa na madaraka ya kuangalia mambo yote ya Chama katika
Kata/Wadi yake.
ii)
Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama wa Kata au
Wadi/Mkutano wa Baraza Kuu ya Chama ya Kata/Wadi na Kamati ya
Utendaji ya Kata au Wadi.
iii)
Katika Mikutano anayoiongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya
kawaida, Mwenyekiti wa Chama wa Kata/Wadi pia atakuwa na kura
ya uamuzi endapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki
zitalingana.
iv)
Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa Chama katika
Kata/Wadi.
------------------------------------------------------------------------
*Page 28*

28
v)
Atahakikisha chama kinashinda uchaguzi wa udiwani na kupata kura
nyingi za uraisi na ubunge katika eneo lake
g) *Kazi za Katibu wa Kata/Wadi*:
i)
Atakuwa Katibu wa vikao vyote vya kikatiba vya Chama katika
Kata/Wadi.
ii)
Atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama katika Kata/Wadi.
iii)
Atakuwa ndiye Mkuu wa mipango ya Chama katika Kata /Wadi..
iv)
Atatunza orodha ya ACT-Vijiji/mtaa, idadi ya ACT-Vitongoji na
wanachama waliopo wa kila ACT-kijiji lililoko katika Kata/Wadi
yake.
v)
Atatunza
kumbukumbu za mali za Chama zisizoondosheka na
zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya
Kata/Wadi hiyo.
vi)
Atawajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa
shughuli za Chama katika Kata/Wadi kwa ngazi ya Jimbo.
vii)
Atakuwa ndiye mdhibiti Mkuu wa mali za Chama katika Kata/Wadi.
viii)
Atawajibika kuandaa na kuitisha mikutano yote ya vikao halali vya
Chama vya Kata/Wadi akishirikiana na Mwenyekiti wake wa
Kata/Wadi.
ix)
Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wa Chama katika
Kata/Wadi yake.
x)
Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa pengine na Katiba hii.
xi)
Atahakikishs chama kinashinda ngazi zote za udiwani na kupata kura
nyingi za uraisi na ubunge
h) *Wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa Kata/Wadi*:
i)
Mwenyekiti wa ACT-Kata/Wadi.
ii)
Katibu wa ACT-Kata/Wadi.
iii)
Katibu Mwenezi wa ACT-Kata/Wadi.
iv)
Wenyeviti wa NGOME ya ACT- Vijana na ACT-Wanawake ngazi
Kata/Wadi
v)
Mwakilishi mmoja aliyechaguliwa na Kamati ya Uongozi ya ACT-
------------------------------------------------------------------------
*Page 29*

29
Kijiji/mtaa.
vi)
Diwani anaye tokana na ACT-Tanzania
i) Kamati ya Uongozi ya ACT-Kata itakutana mara nne kwa mwaka yaani kila
baada ya
miezi mitatu. Vikao maalum/dharura vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu.
j) *Kazi za Kamati ya Uongozi ya Kata/Wadi*.
i) Kupokea na kujadili majina ya wagombea wa Chama katika uchaguzi wa
Madiwani na kupeleka kwa wanachama wote wa ACT-Kata kwa kupingiwa
kura;
ii)
Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Kata;
iii)
Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji washughuli za Chama katika
Kata;
iv)
Kusimamia na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama na viongozi
wa Kata kwa mujibu wa masharti ya Katiba na Kanuni za Chama.
v)
Kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Chama katika Mitaa, Vijiji na Vitongoji;
vi)
Kuandaa mikakati na kusimamia kampeni za wagombea wa Chama katika
chaguzi za kiserikali;
vii)
Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa, sera
na madhumuni ya Chama;
viii)
Kutekeleza maamuzi ya vikao vya juu vya Chama;
ix)
Kuweka kumbukumbu sahihi za uanachama na ufuasi wa Chama katika
madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa mujibu wa kanuni
za Chama;
x)
Kuandaa taarifa mbali mbali za Chama Kata/Wadi na kuziwasilisha kwenye
ngazi ya Jimbo kwa mujibu wa Kanuni za Chama;
xi)
Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu za vikao na nyaraka nyingine
za mawasiliano katika Chama;
xii)
Kufuatilia utendaji kazi wa viongozi wa kiserikali katika Kata/Wadi
waliotokana na Chama na kutoa ushauri kwa kadri inavyowezekana;
xiii)
Kusimamia na kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya Kata
husika.
xiv)
Kufuatilia utendaji na utekelezaji wa maelekezo ya Chama kwa viongozi
------------------------------------------------------------------------
*Page 30*

30
wawakilishi wa Chama katika Baraza za Serikali za Mitaa.
xv)
Kutoa msaada kila inapobidi kwa viongozi wawakilishi wa Chama katika
Baraza za Serikali za Mitaa.
xvi)
Kutayarisha na kusimamia programu za Chama katika ngazi husika.
xvii)
Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama.
xviii)
Kusimamia utendaji wa NGOME za ACT-Vijana na ACT- Wanawake katika
Kata.
------------------------------------------------------------------------
*Page 31*

31
*5.5*
*IBARA YA 12*
*5.5.1 ACT- JIMBO*
ACT Jimbo ni eneo la Uchaguzi wa Ubunge katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na
litaundwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama
a) *Vikao vya Chama vya ACT-Jimbo*:
i)
Mkutano Mkuu wa ACT-Jimbo;
ii)
Halmashauri kuu ya ACT-Jimbo; na
iii)
Sekretarieti ya ACT- Jimbo.
*b) Viongozi wa ACT-Jimbo*
i)Mwenyekiti wa ACT-Jimbo
ii)Katibu wa ACT-Jimbo;
iii)Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Jimbo;
iv)Mweka Hazina wa ACT-Jimbo;
v)Wenyeviti wa NGOME katika Jimbo
vi)Makatibu wa NGOME katika Jimbo
vii)Katibu wa Uchaguzi na Mipango wa Jimbo
*c) Wajumbe wa Sekretariati ya ACT-Jimbo*
i) Katibu wa ACT Jimbo (Mwenyekiti)
ii)Makatibu wa NGOME katika Jimbo
iii) Mweka Hazina wa ACT Jimbo
iv) Makatibu wa Kamati mbalimbali katika Jimbo
v)Katibu wa Uchaguzi na Mipango wa Jimbo
d) *Wajumbe wa Halmashauri ya ACT-Jimbo*
i)
Mwenyekiti wa ACT Jimbo;
------------------------------------------------------------------------
*Page 32*

32
ii)
Wajumbe wa Sekretariati ya ACT Jimbo;
iii)
Wenyeviti wote wa Kata katika jimbo husika;
iv)
Makatibu wote wa Kata katika jimbo husika;
v)
Wenyeviti wa NGOME wa ACT-Jimbo;
vi)
Mbunge na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi katika jimbo husika
vii)
Madiwani wanaotokana na ACT-Tanzania katika jimbo husika
viii)
Makatibu wa Kamati mbalimbali zilizoundwa katika ngazi ya jimbo
ix)
Wajumbe watatu waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Jimbo; angalau mjumbe
mmoja atakuwa mwanamke
x)
Wajumbe wote wa Kamati Kuu wanaoishi katika Jimbo watakaoingia kama
waalikwa lakini watakuwa hawana haki ya kupiga kura
*e) Kazi za Halmashauri ya ACT-Jimbo*
i) Kuchagua Katibu wa ACT-Jimbo
ii) Kuthibitisha uteuzi wa Mweka Hazina wa Jimbo
iii) Kusimamia misingi mikuu ya ACT-Tanzania katika jimbo husika
iv) Kuchagua makatibu wa kamati za chama katika jimbo
v) Kupanga mipango ya kampeni za uchaguzi katika jimbo
vi) Kuhakikisha chama kinaenea kwenye jimbo lote
vii)Kufukuza au kusimamisha kiongozi ambaye uteuzi umefanywa na
halmashauri ya jimbo kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na Katiba
hii
viii)
Kuteua wajumbe wa kamati ya uadilifu ya jimbo kwa utaratibu
zilivyoanishwa katika Katiba hii na/au Kanuni zitakazotungwa na vyombo
husika vya maamuzi katika chama
ix) Kupanga na kuandaa mkutano mkuu wa chama jimbo
x) Kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi mbalimbali katika ngazi
ya Kata
xi) Kutoa maoni kuhusu wagombea wa nafasi za ubunge, wawakilishi na
madiwani katika jimbo husika
xii)Kuunda Kamti ndogo kadri itakavyoona inafaa
xiii)
Kujaza nafasi za uongozi zilizowazi katika jimbo isipokuwa nafasi ya
Mwenyekiti
------------------------------------------------------------------------
*Page 33*

33
Vikao vya halmashauri ya jimbo vitakutana angalau mara tatu (3) kwa
mwaka na vinaweza
kuitishwa kwa dharula pale panapokuwa na uhitaji kufanya hivyo.
f) *Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ACT-Jimbo*
i) Wajumbe wote wa Halmashauri ya ACT- Jimbo;
ii) Wenyeviti wote wa matawi wa ACT-Tanzania katika jimbo
iii) Makatibu wote wa matawi wa ACT-Tanzania katika jimbo
iv) Wajumbe watatu wanaowakilisha kila kata katika Jimbo, ambapo angalau
mjumbe
mmoja atakuwa mwanamke.
g) Mkutano Mkuu wa ACT-Jimbo utafanyika mara moja kwa mwaka na akidi itakuwa
nusu (½) ya wajumbe wote na ndicho kitakuwa kikao cha juu kabisa katika
Jimbo.
Mikutano maalum/dharura inaweza kuitishwa wakati wowote na Kamati ya
Uongozi
ya Jimbo kadri itakavyolazimu.

h) *Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT-Jimbo*
i)Kuchagua mwenyekiti wa ACT Jimbo
ii)Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utendaji na mapato na
matumizi ya Jimbo
iii) Kupokea na kuzingatia mikakati ya ushindi wa ACT Tanzania katika
chaguzi za
kiserikali ndani ya Jimbo
iv) Kuzingatia na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Halmashauri ya
Jimbo juu ya
maamuzi na maagizo ya vikao vya juu.
v) Kujadili taarifa za Halmashauri ya Jimbo na kutoa maamuzi au
maelekezo kwa
utekelezaji.
vi) Kujadili na kuweka miongozo ya utekelezaji wa falsafa na sera za
Chama katika
Jimbo.
vii) Kutoa mwongozo na maelekezo kwa wawakilishi wa Chama katika vyombo vya
maamuzi vya kiserikali.
viii) Kuzingatia na kutoa mapendekezo kwa ngazi za juu, juu ya masuala
ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii yanayojitokeza katika Jimbo na yanayohitaji hatua za
kichama
------------------------------------------------------------------------
*Page 34*

34
ngazi za juu.
ix) Kusikiliza na kutoa uamuzi au mapendekezo kwa ngazi ya juu, kuhusu
masuala ya
kinidhamu kwa wanachama au viongozi wa Chama kwa kuzingatia masharti ya
Katiba na Kanuni za Chama.
x) Kuidhinisha Programu ya Chama katika Jimbo
xi) Kupiga kura ya mapendekezo ya wagombea wa ubunge katika Jimbo husika
xii) Kuchagua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Jimbo
i) *Kazi za Mwenyekiti wa ACT-Jimbo*
i)
Atakuwa na wajibu wa kusimamia mambo yote ya Chama katika Jimbo;
ii)
Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mikakati ya ushindi wa chama katika
chaguzi za serikali ndani ya Jimbo, na utendaji wake utapimwa kutokana na,
pamoja na mambo mengine, ufanisi wa chama katika chaguzi za kiserikali ndani
ya Jimbo
iii)
Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu na Halmashauri ya Jimbo;
iv)
Katika mikutano anayoingoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida,
Mwenyekiti wa Chama wa Jimbo atakuwa na kura ya uamuzi endapo kura za
wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana; na
v)
Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa shughuli za kila siku za Chama
katika Jimbo.
vi)
Atahakikisha chama kinashinda uchaguzi wa ubunge na kupata kura nyingi za
uraisi
j) *Kazi za Katibu wa Jimbo*
i)
Atakuwa Katibu wa mikutano na vikao vyote vya Kikatiba vya Chama katika
Jimbo;
ii)
Atakuwa mwenyekiti wa vikao vya Sekretarieti ya Jimbo
iii)
Atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama katika Jimbo na atafanya kazi chini
ya Hamashauri Kuu ya uongozi wa Jimbo;
iv)
Atakuwa ndiye Mkuu wa mipango ya Chama katika Jimbo;
v)
Ataitisha na kuongoza vikao vya viongozi watendaji wakuu wa Chama katika
Jimbo kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda ya vikao vya Jimbo na
kuchukua hatua za utekelezaji wa maamuzi ya Chama;
------------------------------------------------------------------------
*Page 35*

35
vi)
Atatunza orodha ya Kata/Wadi, vijiji/mtaa na wanachama wa Jimbo lake;
vii)
Atatunza kumbukumbu za mali za chama zisizoondosheka na
zinazoondosheka zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya Jimbo
lake;
viii) Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama za Jimbo;
ix) Atawajibika kutoa taarifa za utendaji wa shughuli za Chama katika
Jimbo kila
mwezi kwa ngazi ya Mkoa;
x)
Atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano yote ya vikao vya
Chama Jimbo kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Jimbo;
xi)
Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wa Chama katika Jimbo
lake; na
xii)
Kufanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba hii.
j)*Kazi za Sekretarieti ya Jimbo*
i) Kupokea taarifa ya majina ya wagombea udiwani katika Kata zilizo ndani ya
Jimbo;
ii)
Kuandaa agenda za Mkutano Mkuu wa Jimbo;
iii)
Kuandaa mikakati na kusimamia uendeshaji wa shughuli za kila siku za
Chama katika Jimbo;
iv)
Kusimamia na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama na viongozi
wa Kata kwa mujibu wa masharti ya Katiba na Kanuni za Chama;
v)
Kusimamia Uchaguzi wa viongozi wa Chama katika Kata;
vi)
Kuandaa mikakati na kusimamia kampeni za wagombea wa Chama katika
chaguzi za kiserikali;
vii)
Kuhamasisha wananchi kujiunga na Chama kwa kueneza itikadi, falsafa, sera
na madhumuni ya Chama;
viii)
Kutekeleza maamuzi ya vikao vya juu vya Chama;
ix)
Kuweka kumbukumbu sahihi za wanachama na wafuasi wa Chama katika
madaftari ya wanachama na wafuasi vijana wa Chama kwa mujibu wa
Kanuni za Chama;
x)
Kuandaa taarifa mbali mbali za Chama katika Jimbo na kuziwasilisha kwenye
ngazi ya Taifa kwa mujibu wa Kanuni za Chama;
xi)
Kuweka katika majalada maalum kumbukumbu za vikao na nyaraka nyingine
------------------------------------------------------------------------
*Page 36*

36
za mawasiliano katika Chama;
xii)
Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Jimbo na kutoa maamuzi au maelekezo ya
utekelezaji;
xiii)
Kusimamia na kuweka kumbukumbu za mali, mapato na matumizi ya Jimbo;
xiv)
Kufuatilia utendaji na utekelezaji wa maelekezo ya Chama kwa viongozi
wawakilishi wa Chama katika Baraza za Serikali za Mitaa na inapobidi kutoa
ushauri na msaada pindi unapohitajika;
xv)
Kutayarisha na kusimamia programu za Chama katika ngazi husika;
xvi)
Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi wa Chama katika ngazi
ya Kata;
xvii)
Kufanya utafiti na kupendekeza majina ya wagombea Ubunge na Baraza la
Uwakilishi (Zanzibar) kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi;
xviii)
Kusimamia utekelezaji na uzingatiaji wa maadili ya Chama; na
xix)
Kusimamia utendaji wa NGOME za chama katika Jimbo.
k)
Viongozi wa jimbo ambalo ndio makao makuu ya wilaya watakuwa ndio
wawakilishi
wa chama wilaya kwa mambo yote ya kiserikali yanayo husu chama katika wilaya
husika.
------------------------------------------------------------------------
*Page 37*

37
*5.6*
*IBARA YA 13*
*5.6.1 ACT-MKOA*
Ngazi ya ACT Mkoa itaundwa katika kila eneo la nchi la kiutawala la Mkoa.
k) *Vikao vya ACT-Mkoa*
i)
Sekretariati ya Mkoa
ii)
Halmashauri ya ACT Mkoa
iii)
Mkutano Mkuu wa Mkoa
l)Viongozi wa ACT-mkoa
a) Mwenyekiti wa ACT-Mkoa
b) Katibu wa ACT-Mkoa
c) Muweka hazina wa ACT-Mkoa
d) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi wa ACT-mkoa
e) Katibu wa Mipango na Uchaguzi wa Mkoa
m) Wajumbe wa Sekretariati ya Mkoa
i)
Katibu wa Mkoa (Mwenyekiti)
ii)
Makatibu wa NGOME za ACT Mkoa
iii) Katibu wa Mawasiliano na Uenezi Mkoa
iv)
Mtunza Hazina wa ACT Mkoa
v)
Katibu wa mipango na uchaguzi
n) *Kazi za Sekretariati ya Mkoa*
i)
Kuratibu shughuli za chama katika Mkoa;
ii)
Kutoa ushauri na misaada ya kiutendaji kwa uongozi wa ACT-Jimbo katika
Mkoa;
iii)
Kuratibu shughuli za kampeni za wagombea urais na ubunge katika mikoa na
mgawanyo wa majukumu kijimbo;
iv)
Kuratibu na kuunganisha shughuli za NGOME za Chama katika Mkoa;
------------------------------------------------------------------------
*Page 38*

38
v)
Kuwa kiunganishi cha chama na shughuli za kiserikali katika Mkoa;
vi)
Kuratibu na kutoa taarifa kwa chama ngazi ya Taifa juu ya hali ya kisiasa,
kijamii na kiutawala ndani ya Mkoa;
vii)
Kupendekeza majina ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wa ndani ya Chama
katika ngazi ya Mkoa
viii)
Kupendekeza majina ya Wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Mkoa kwa
mujibu wa masharti na Kanuni za Katiba hii
ix)
Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote katika ngazi ya Jimbo ambaye
imeona kwamba mwenendo wake hauendani na itikadi na misingi ya ACT
Tanzania kwa kanuni na utaratibu uliowekwa na Katiba hii, isipokuwa tu
haitakuwa na uwezo wa kumsimamisha uongozi kiongozi ambaye uteuzi wake
wa mwisho haukufanywa na Halmashauri kuu ya Mkoa
o) Sekretariati ya Mkoa itakutana mara moja kila baada ya miezi mitatu
na inaweza
kukutana kwa dharura au vikao maalum kadri itakavyoona inafaa au kwa
maagizo
ya vikao vya juu.
p) *Wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa*
i)
Wajumbe wote wa Sekretariati ya ACT Mkoa.
ii)
Wenyeviti na Makatibu wa ACT Jimbo katika Mkoa.
iii)
Wenyeviti na Makatibu wa NGOME za ACT katika ngazi ya Jimbo.
iv)
Meya/Wenyeviti wa Baraza za Jiji/Miji/Wilaya katika Mkoa wanaotokana na
ACT Tanzania
v)
Wabunge/Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotokana na ACT Tanzania
katika Mkoa
vi)
Mjumbe mmoja (1) anayewakilisha kila Jimbo katika Mkoa aliyechaguliwa na
Mikutano Mikuu ya ACT ya majimbo
q) *Kazi za Halmashauri ya Mkoa*
i)
Kuongoza, kueneza na kusimamia itikadi, misingi na sera za ACT katika ngazi
ya Mkoa;
ii) Kueleza mipango ya ACT Tanzania kwa majimbo katika mkoa husika;
------------------------------------------------------------------------
*Page 39*

39
iii) Kupanga mikakati ya kampeni za kitaifa za uchaguzi katika Mkoa;
iv) Kuidhinisha uteuzi wa Mweka Hazina wa Mkoa atakayependekezwa na
Sekretariati ya Mkoa
v) Kupokea, kuzingatia na kuamua juu ya mapendekezo ya vikao vya ACT majimbo
vi) Inapofika wakati wa uchaguzi, Halmashauri ya Mkoa itashughulikia mambo
yafuatayo:
a. Kuchagua Katibu wa Mkoa
b. Kufanya uteuzi wa mwisho wa majina ya wanachama wanaoomba
kugombea nafasi za uenyekiti wa ACT Tanzania katika ngazi ya Jimbo
katika mkoa husika
c. Kujaza kwa niaba ya Mkutano Mkuu wa Mkoa nafasi zilizoachwa wazi,
isipokuwa nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa
d. Kuchagua makatibu wa Kamati mbalimbali katika ngazi ya mkoa
e. Kuunda Kamati ndogo kwa kadri itakavyoona inafaa kwa ajili ya
kufanikisha shughuli za chama katika Mkoa
f. Kuunda Kamati ya Uadilifu katika ngazi ya Mkoa kwa mujibu wa
masharti na Kanuni za Katiba hii
g. Kumwachisha au kumfukuza kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa
mwisho unafanywa na Baraza la Mkoa .
r) Vikao vya Halmashauri ya Mkoa vitafanyika mara tatu (3) kwa mwaka,
lakini vikao
vya dharura na maaulum vinaweza kufanyika wakati wowote na/au kwa maagizo ya
vikao vya juu vya ACT.
s) Halmashauri ya Mkoa inaweza kukasimu madaraka yake kwa Sekretariati
ya Mkoa
kwa ajili ya utekelezaji wa kazi zake kadri itakavyoona inafaa.
t)*Kazi za Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa*.
i)
Atashughulikia au atakuwa na madaraka ya kuangalia mambo yote ya Chama
katika Mkoa.
ii)
Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Chama wa Mkoa, Halamshauri
ya Chama Mkoa, na vikao vyote vya mashauriano katika mkoa wake.
------------------------------------------------------------------------
*Page 40*

40
iii)
Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida,
Mwenyekiti wa Chama wa mkoa atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura
za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana.
iv)
Atakuwa msemaji na mhamasishaji mkuu wa Chama wa Mkoa.
u) *Kazi za Katibu wa Chama wa Mkoa*:
i)
Atakuwa mtendaji mkuu wa shughuli zote za Chama katika mkoa na atafanya
kazi chini ya uongozi wa Halmashauri ya Chama mkoa.
ii)
Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa mipango ya Chama katika Mkoa.
iii)
Ataitisha na kuongoza vikao vya viongozi watendaji wakuu wa Chama katika
mkoa kwa madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda za Halmashauti Kuu
ya Chama Mkoa na kuchukua hatua za utekelezaji wa maamuzi ya Chama.
iv)
Kutunza orodha ya majimbo, Kata/Wadi, vijiji, idadi ya vitongoji na
wanachama wa mkoa wake.
v)
Kutunza kumbukumbu za mali za Chama zisizo hamishika na
zinazohamishika zilizopo katika au chini ya ofisi ya Chama ya mkoa huo.
vi)
Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama wa mkoa.
vii)
Atawajibika kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu utendaji wa shughuli za
Chama katika mkoa kwa ngazi ya Kamati kuu ACT-Taifa.
viii)
Atakuwa na wajibu wa kuanda ana kuitisha mikutano yote ya vikao vya
Chama mkoa akishirikiana na Mwenyekiti wake.
(a)Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama wea Chama katika
mkoa
wake.
(b) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo kartika Katiba hii.
v) *Wajumbe wa mkutano mkuu wa ACT-Mkoa*
Mkutano Mkuu wa Mkoa utaundwa na Wajumbe wote wa Halmashauri ya Mkoa,
pamoja na:
*a) *Wajumbe watatu waliochaguliwa kutoka katika kila jimbo angalau
mmoja (1)
atakuwa mwanamke
*b) *Mjumbe mmoja kutoka kila kata kwa Tanzania Bara au wajumbe wawili
kutoka kila wadi kwa upande wa Zanzibar
------------------------------------------------------------------------
*Page 41*

41
*c) *Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa waliopo katika Mkoa
w) Mkutano mkuu wa ACT-mkoa utafanyika mara mbili (2) katika kipindi cha
miaka
mitano. Mkutano Mkuu Maalumu au wa dharura unaweza kutishwa wakati wowote
kwa mahitaji maalumu na/au ya dharura.
x) *Kazi za Mkutano Mkuu wa ACT-Mkoa*
i) Kuchagua mwenyekiti wa ACT-Mkoa
ii) Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa mipango ya chama katika
majimbo
iii) Kupokea, kujadili na kuidhinisha taarifa ya fedha ya Mkoa
iv) Kujadili na kupanga kampeni za mgombea urais katika mkoa
v) Kuhakikisha chama kinashinda chaguzi zote ndani ya mkoa
vi) Kuchagua wajumbe wa Kamati ya Uadilifu ya Mkoa
vii)Kufanya kazi ingine kwa mujibu wa katiba hii.
*5.7*
*IBARA YA 14*
*5.7.1 ACT-ZANZIBAR*
*a) Kamati Maalum ya Chama Zanzibar*:
Kutakuwa na Kamati Maalum ya Kamati Kuu kwa upande wa Zanzibar.
a) *Wajumbe wa Kamati Maalum ya Chama Zanzibar*:
Wajumbe wa Kamati Maalum Zanzibar watakuwa:
i) Makamu Mwenyekiti Zanzibar (Mwenyekiti wa Kamati).
ii) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
iii) Wajumbe wa Kamati Kuu watokao Zanzibar.
iv) Wenyeviti wa Mikoa Zanzibar.
v) Wajumbe wa Sekretarieti ndogo ya Zanzibar watakuwa wajumbe wasio na
kura.
------------------------------------------------------------------------
*Page 42*

42
b) *Kazi za Kamati Maalumu Zanzibar*:
i) Kutoa mapendekezo kwa Sekretarieti ya Kamati Kuu itakayo wasilisha mambo
yote ya Kamati Kuu;
ii) Kusimamia utendaji wa Sekretarieti ya ofisi ya Makao Makuu Zanzibar;
iii) Kupendekeza mambo ya kisera yahusuyo Zanzibar; na
iv) Kupendekeza majina ya wagombea ngazi mbalimbali ya kitaifa.
c) *Sekretarieti ya Ofisi ya Makao Makuu ya Zanzibar*:
Kwa shughuli za kiutendaji Zanzibar, patakuwa na Sekretarieti ya ofisi
ya Makao
Makuu yenye wajumbe wafuatao:
i)
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
ii) Wakuu wa idara zilizopo Zanzibar.
iii) Katibu/Naibu Katibu wa NGOME za Chama Zanzibar.
d) *Kazi za Sekretarieti ndogo Zanzibar*:
i)
Utekelezaji wa kazi za kila siku za chama Zanzibar
ii)
Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu yanayohusu Zanzibar
iii)
Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya Kamati maalum
Zanzibar.
------------------------------------------------------------------------
*Page 43*

43
*5.8*
*IBARA 15*
*5.8.1 ACT- TAIFA*
ACT-Taifa ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwa
kwa kuzingatia
masharti ya Kanuni za Chama zilizotungwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
/*a) Viongozi Wakuu wa Chama Taifa */
i)
Kiongozi Mkuu wa ACT- Tanzania
ii)
Mwenyekiti wa ACT-Taifa
iii)
Makamu Mwenyekiti ACT-Zanzibar
iv)
Makamu mwenyekiti ACT-Bara
v)
Katibu Mkuu ACT-Taifa
vi)
Naibu Katibu Mkuu ACT-Zanzibar
vii)
Naibu Katibu Mkuu ACT-Bara
/*b) Vikao vya Chama Taifa:*/
i) Mkutano Mkuu Taifa
ii) Mkutano Mkuu wa Wanachama
iii) Halmashauri Kuu ya Taifa
iv) Kamati Kuu
v) Sekretarieti ya Kamati Kuu.
/*c) Wajumbe wa Mkutano Mkuu ACT- Taifa:*/
I.
Mkutano Mkuu wa Chama Taifa ndicho kikao cha juu katika ACT Tanzania na
ndicho chenye maamuzi ya mwisho kuhusu jambo lolote ndani ya chama, na
utaundwa na wajumbe wafuatao:
i)
Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa
ii)
Wenyeviti wote wa NGOME wa Majimbo na Mikoa
------------------------------------------------------------------------
*Page 44*

44
iii)
Wawakilishi 30 wa wanafunzi wa vyuo vikuu waliochaguliwa na umoja wao
kwa mujibu wa Kanuni zitakazowekwa na Ngome ya Vijana, kwa masharti kwamba
angalau theluthi moja wa wajumbe hawa watakuwa wanawake
iv)
Wajumbe wanne waliochaguliwa na Mikutano Mikuu ya kila Jimbo ambapo
angalau nusu ya wajumbe katika kila Jimbo watakuwa wanawake
II.
Mkutano Mkuu Taifa utakutana mara moja katika kipindi cha miaka mitano.
Mkutano
Mkuu maalum/dharura unaweza kuitishwa wakati wowote ikiwepo ulazima kwa
utaratibu utakaowekwa na Kanuni. Akidi ya mkutano mkuu itakuwa ni 1/2 ya
wajumbe wote.
/*d) Kazi za Mkutano Mkuu wa Chama Taifa:*/
i) Kuchagua Kiongozi Mkuu wa Chama Taifa
ii) Kuchagua Mwenyekiti wa ACT-Taifa
iii) Kuchagua Makamu Mwenyekiti wa ACT-Taifa (Tanzania Bara)
iv) Kuchagua Makamu Mwenyekiti wa ACT-Taifa (Zanzibar)
v) Kujadili taarifa za Halmashauri Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa
utekelezaji
vi) Kuteua mgombea wa Urais na mgombea mwenza wake kwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na mgombea Urais wa Zanzibar.
vii) Kujadili na kuridhia Itikadi, Falsafa na Sera za Chama kisha kuweka
mikakati
na miongozo ya utekelezaji
viii) Kujadili na kuridhia programu ya Chama kwa kuzingatia mapendekezo ya
Halmashauri Kuu.
ix) Kupokea na kujadili taarifa ya Bodi ya wadhamini wa Chama juu ya mali na
rasilimali za Chama
x) Kuidhinisha Ilani (Manifesto) ya Chama kwa Uchaguzi Mkuu.
xi) Kujadili na kufanyia maamuzi agenda nyingine yeyote iliyoletwa kwake na
Halmashauri Kuu au Kiongozi Mkuu wa chama.
xii) Kujadili na kuthibitisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Chama.
III
*Mkutano Mkuu wa Wanachama wa ACT-Tanzania*
------------------------------------------------------------------------
*Page 45*

45
a) Mkutano Mkuu wa Wanachama utafanyika mara moja kwa mwaka na unaweza
kuitishwa mara nyingi zaidi kama kuna hitaji la kufanya hivyo
b) Wajumbe wa mkutano huu ni wanachama wote wa ACT-Tanzania, wadau,
wafadhili
na wananchi wote kwa ujumla watakaopenda kuhudhuria
c) Mkutano Mkuu wa Wanachama utakuwa ndiyo jukwaa la Kiongozi Mkuu wa Chama
kutoa mwelekeo wa kisera wa chama na jukwaa la wanachama wote kuhoji
utendaji
wake
d) Mkutano Mkuu wa wanachama utajadili hali ya siasa na uchumi ya nchi,
Afrika na
dunia kwa kila mwaka
e) Mkutano Mkuu wa Wanachama litakuwa jukwaa la majadiliano lakini
hautakuwa na
maamuzi yoyote
f) Mambo yote yaliyojitokeza na kupendekezwa katika majadiliano ya
Mkutano Mkuu
wa Wanachama yatawasilishwa katika Kamati Kuu na vikao vingine vya chama kwa
maamuzi na utekelezaji
/*e) Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya a Taifa:*/
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa watakuwa:
i) Wajumbe wote wa Kamati Kuu
ii) Wenyeviti wote wa Mikoa
iii) Makatibu wote wa Mikoa
iv) Wenyeviti wa Kamati za Kudumu
v) Wawakilishi kumi wa wabunge na wawakilishi wanaotokana na ACT
Tanzania
vi) Wajumbe kumi na tano (15), ambapo angalau wajumbe watano (5)
watakuwa wanawake, waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa
III.
Halmashauri Kuu ya Taifa itakutana angalau mara mbili kila mwaka. Vikao
maalum/dharura vinaweza kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa
kanuni za
Chama.
------------------------------------------------------------------------
*Page 46*

46
/*f) Kazi za Halmashauri Kuu ya Chama ya Taifa:*/
i) Kupendekeza wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuwasilisha mapendekezo
yake katika Mkutano Mkuu wa Taifa;
ii) Kuchagua Katibu Mkuu wa Chama
iii) Kuidhinisha uteuzi wa Makatibu wa Kamati za Chama Makao Makuu
iv) Kuchagua wajumbe nane kuingia kwenye Kamati Kuu
v) Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na za kinidhamu kwa
mujibu wa Katiba hii
vi) Kujadili mikakati ya uendeshaji wa shughuli za Chama kwa kipindi kati ya
Mkutano Mkuu na kuifanyia maamuzi panapostahili;
vii)Kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa
Chama katika chaguzi za Serikali hususani Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa;
viii)
Kuandaa ratiba na maelekezo ya Uchaguzi wa kichama kwa mujibu wa
Katiba na Kanuni za Chama;
ix) Kutunga na kuzifanyia marekebisho Kanuni za kuendesha shughuli za Chama;
x) Kujadili taarifa za Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwa
utekelezaji
xi) Kusimamia utendaji kazi wa Kamati Kuu
xii)Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu masuala yote ya Katiba ya Chama na
mabadiliko yake;
xiii)
Kujadili rasimu ya Ilani (Manifesto) ya uchaguzi kwa Uchaguzi Mkuu
na uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwasilisha mapendekezo yake kwa
mkutano Mkuu kwa maamuzi;
xiv)
Kuteua wadhamini wa Chama;
xv)Kuthibitisha kanuni za uendeshaji Chama na miongozo ya NGOME za Vijana,
Wanawake na Wazee;
xvi)
Kujadili na kuidhinisha majina ya wagombea wa nafasi za Kiongozi
Mkuu, Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti
/*g) Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa:*/
IV.
Wajumbe wa Kamati Kuu watakuwa:
------------------------------------------------------------------------
*Page 47*

47
i)
Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania
ii)
Mwenyekiti wa Chama Taifa
iii)
Makamu wenyeviti Taifa
iv)
Katibu Mkuu
v)
Manaibu Katibu wakuu Taifa
vi)
Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Chama Taifa
vii)
Wajumbe nane waliochaguliwa na Halmashauri Kuu kuingia Kamati
Kuu kwa kuzingatia kuwa wajumbe sita watatoka bara na ambao angalau
wawili (2) watakuwa wanawake, na wajumbe wawili (2) watatoka
Tanzania Zanzibar na ambao angalau mjumbe mmoja (1) atakuwa
mwanamke.
viii)
Wenyeviti wa NGOME za Vijana na Wanawake Taifa
ix)
Mwenyekiti wa Baraza la Walezi
x)
Wajumbe watano walioteuliwa na Kiongozi Mkuu wa Chama na
kuidhinishwa na Halmashauri Kuu au Kamati Kuu kwa idhini ya
Halmashauri Kuu
xi)
Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar au Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar aliyetokana na ACT-Tanzania.
xii)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Spika wa Baraza la
wawakilishi.
xiii)
Waziri Mkuu au Kiongozi wa Kambi ya Upinzani katika Bunge la
Jamhuri ya Muungano na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar au
Kiongozi wa Kambi ya upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi
Zanzibar
xiv)
Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini
V.
Kamati Kuu itakutana mara nne (4) kwa mwaka. Vikao maalum/dharura vinaweza
kuitishwa kadri itakavyolazimu kwa mujibu wa kanuni za Chama.
/*h) Kazi za Kamati Kuu ya Chama Taifa:*/
VI.
Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:
i)
Kuteua Wenyeviti na Makatibu wa kamati za kudumu za Chama
Makao Makuu.
------------------------------------------------------------------------
*Page 48*

48
ii)
Kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na
kinidhamu.
iii)
Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Halmshauri Kuu, Mikakati ya
kuendesha shughuli za Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha
miaka mitano.
iv)
Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu, Mikakati ya
kupata mahitaji ya rasilimali za kuendesha kampeni za wagombea wa
Chama katika chaguzi za kiserikali.
v)
Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ratiba na
maelekezo ya uchaguzi wa kichama.
vi)
Kupitia na kutoa kwa Halmashauri Kuu mapendekezo ya haja ya
kuzifanyia marekebisho au maboresho Kanuni za chama ama Katiba ya
chama
vii)
Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na
maelekezo kwa utekelezaji.
viii)
Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu.
ix)
Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa
Halmashauri Kuu kwa kuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na
Sekretarieti ya Kamati Kuu.
x)
Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Halmashauri Kuu
na Mkutano Mkuu.
xi)
Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama
vingine vya siasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine.
xii)
Kuthibitisha ajira za watumishi wakuu wa Chama ngazi ya Taifa.
xiii)
Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama
kwa muda maalumu.
xiv)
Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka.
xv)
Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Baraza la
wawakilishi Zanzibar
xvi)
Kuandaa agenda za Halmashauri Kuu na Mapendekezo ya agenda za
Mkutano Mkuu.
xvii)
Kufanya uamuzi juu ya mapendekezo ya kufukuza Mwanachama.
xviii)
Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama
------------------------------------------------------------------------
*Page 49*

49
xix)
Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.
xx)
Kusimamia utendaji kazi wa NGOME za Vijana, Wanawake na Walezi
xxi)
Kuchagua manaibu katibu wakuu wa Tanzania bara na visiwani
VII. Kutakuwa na kamati za za kudumu za Utendaji Makao Makuu ya Chama
zitakazoundwa na Kamati Kuu.
i) Kamati ya Raslimali na Fedha
v)
Kamati ya Mawasiliano na Uenezi
v)
Kamati ya Mipango na Chaguzi
iv)
Kamati ya Katiba na Sheria
v)
Kamati ya Utafiti na Sera
vi)
Kamati ya Uadilifu ya Taifa
vii)
Kamati ya Mambo ya Nje
VIII. Kamati Kuu inaweza kuunda Kamati zingine kama itakavyoona inafaa kwa
ufanisi wa chama
IX.
Kutakuwa na Kikosi cha Amani cha Chama kitakachoitwa /*ACT-Rugaruga*/
kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa. Kazi ya kikosi itakuwa ni kuhakikisha
ulinzi na
usalama wa wanachama, viongozi na mali za chama.
X. Muundo na kazi za Kamati zitaanishwa katika Kanuni za uendeshaji
zitazotungwa na
Halmashauri Kuu.
/*i) Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama Taifa:*/
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Kuu:
i)
Katibu Mkuu – Mwenyekiti wa Sekretarieti
ii) Naibu Katibu Mkuu Bara
iii) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
iv) Makatibu wa Kamati zote Makao Makuu
v) Makatibu wa NGOME zote za chama Taifa
X
Katibu wa Mawasiliano na Uenezi atakuwa ndiye msemaji wa chama na ndiye
Katibu
wa secretariet ya Kamati Kuu.
------------------------------------------------------------------------
*Page 50*

50
/*j) Kazi za Sekretariati ya Kamati Kuu ya Chama Taifa*/
i) Utekelezaji wa kazi za kila siku za uendeshaji shughuli za chama;
ii) Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Kamati Kuu; na
iii) Uandaaji wa agenda na nyaraka kwa ajili ya vikao vya Kamati Kuu,
Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.
/*k) Kazi za Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania*/
i) Atakuwa kiongozi mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama Taifa,
mkutano mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.
ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na
maafisa wa ACT-Tanzania
iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii
iv) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa
chama
v) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, Halmashauri Kuu
na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa
na kimataifa.
vi) Atasimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT-
Tanzania
vii) Iwapo kiongozi wa ACT-Tanzania hayupo kwa sababu yoyote ile basi
Mwenyekiti wa chama Taifa atakuwa Kaimu kiongozi mkuu wa Chama.
viii) Iwapo kiti cha kiongozi mkuu wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya
kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama,
maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, utaratibu
ulioelezwa katika (vi) ya ibara ndogo hii utatumika kwa sharti kwamba
Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi
sita tangu kuwa wazi kwa kiti hicho kwa ajili ya kuchagua Kiongozi Mkuu
wa Chama mwingine.
ix) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Taifa
litakaloungwa mkono na theluthi mbili ya kura za wajumbe halali
waliohudhuria na kupiga kura.
x) Atakuwa ni nuru na taswira ya ACT-Tanzania
------------------------------------------------------------------------
*Page 51*

51
/*l) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Taifa :*/
i)Atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa kiongozi mkuu wa ACT-Tanzania
ii) Atakuwa mlinzi mkuu wa sera zilizopendekezwa na kupitishwa au jambo
lolote litakaloamliwa na kupitishwa na vikao cya chama na kuhakikisha
kuwa ngazi zote za chama zinatekeleza maamuzi yaliyotolewa
na
kuhakikisha kuwa ngazi zote zinafanya kazi ndani ya mipaka ya katiba,
kanuni, sera na maamuzi yoyote yaliyoagizwa na vikao vikuu vya chama
iii) Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya chama ya kitaifa isipokuwa
vikao vya utendaji
iv)
Atafanya shughuli nyingine za Chama kama atakavyoelekezwa na
Kiongozi Mkuu wa Chama
v) Katika mikutano anayoiongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida
atakuwa pia na kura ya uamuzi endapo kura ya wajumbe wanaoafiki na
wasioafika zitalingana
vi)
Iwapo Mwenyekiti wa Chama hayupo kwa sababu yoyote ile basi Makamu
Mwenyekiti kutoka Bara atakuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama kama
Mwenyekiti anatoka Zanzibar, au Makamu Mwenyekiti kutoka Bara kama
Mwenyekiti anatoka Bara.
vii) Iwapo kiti cha mwenyekiti wa Chama kitakuwa wazi kwa sababu ya
kujiuzulu, kuondoka katika Chama, kuvuliwa uongozi au uanachama,
maradhi yenye kuondoa uwezo wa kufanya kazi au kifo, Mkutano Mkuu
maalumu wa Taifa utaitishwa katika muda usiozidi miezi sita tangu kuwa
wazi kwa kiti hicho ili kuchagua Mwenyekiti mwingine.
viii) Ataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya mapendekezo ya
Kiongozi Mkuu wa Chama au Halmashauri Kuu ya Taifa, kwa azimio la
Mkutano Mkuu wa Taifa litakaloungwa mkono na nusu ya kura za
wajumbe halali waliohudhuria na kupiga kura
/*m) Kazi za Makamu Wenyeviti wa Chama Taifa */
i) Watakuwa wasaidizi wakuu wa Mwenyekiti wa Chama na watafanya kazi
zozote za Chama watakazopewa na Mwenyekiti wa Chama Taifa
------------------------------------------------------------------------
*Page 52*

52
ii) Watakuwa washauri wakuu wa Ngome za chama katika maeneo yao (Bara
na Zanzibar)
iii) Makamu Mwenyekiti Zanzibar ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati
Maalumu ya Zanzibar
iv) Watamshauri Mwenyekiti katika majukumu yake ya kila siku kwa maeneo
yao
v) Watakuwa wahamasishaji wa chama katika maeneo yao.
/*n) Kazi za Katibu Mkuu wa Chama Taifa */
i) Atakuwa Katibu wa mikutano ya chama katika ngazi ya Taifa
ii) Atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za Chama
iii) Ataitisha na kuongoza vikao vya viongozi watendaji wakuu wa Chama kwa
madhumuni ya kushauriana, kuandaa agenda za Kamati Kuu na kuchukua
hatua za utendaji wa maamuzi ya Chama.
iv) Atakuwa na uwezo wa kuajiri, kufukuza na kusimamia nidhamu ya watumishi
wote wa Chama kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, taratibu za Chama na sheria
za nchi.
v) Atakuwa na wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano yote ya vikao vya
Chama katika ngazi ya Taifa na kuchukua hatua za utekelezaji wa maamuzi ya
Chama
vi) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama katika Chama Taifa.
vii) Atakuwa mdhibiti mkuu wa mali za Chama zinazohamishika na
zisizohamishika.
viii) Atafanya kazi yoyote itakayokuwa imetajwa penginepo katika Katiba
hii na/au
kwa maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Chama.
/*o) Kazi za Manaibu Katibu Wakuu wa Chama Taifa*/
i)
Kutakuwa na Naibu Katibu Mkuu atakayeishi na kufanya kazi zake Zanzibar
na mwingine ataishi na kukaa Tanzania Bara. Isipokuwa kwa kuishi kwao
hivyo hakutapunguza upeo wa madaraka yao ya kushughulikia kazi za Chama
kwa Tanzania nzima.
------------------------------------------------------------------------
*Page 53*

53
ii)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama atakayefanya kazi Zanzibar ndiye atakuwa na
wajibu wa kuandaa na kuitisha mikutano ya Kamati maalumu ya
Halmashauri Kuu ya Chama Taifa Zanzibar.
iii)
Mmoja wao atamsaidia Katibu Mkuu kukaimu kiti chake wakati Katibu Mkuu
hayupo.
iv)
Manaibu Katibu Mkuu wa Chama watakuwa ndio wasaidizi wakuu wa Katibu
Mkuu wa Chama na watafanya kazi zozote za Chama watakazopewa na
Katibu Mkuu wa Chama.
v)
Watakuwa Makatibu wasiadizi wa vikao vyote vya Chama wakimsaidia
Katibu Mkuu.
vi)
Watamsaidia Katibu Mkuu kusimamia shughuli, taratibu na Kanuni zote za
Kiutawala za Chama za kila siku.
vii)
Watakuwa wajumbe wa vikao vyote ambavyo Katibu Mkuu wa Chama Taifa
anashiriki kwa wadhifa wake
viii)
Naibu Katibu Mkuu Bara ndiye atakuwa mkuu wa utawala na itifaki wa
chama
ix)
Watafanya kazi nyingine zozote za Chama zitakazokuwa zimetajwa penginepo
na Katiba hii na/au kwa maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Chama.
*IBARA 16*
*I.*
*NGOME ZA CHAMA:*
1.
NGOME ni vitengo au jumuiya za Chama ambazo zitaundwa na vijana na wanawake
na walezi ambao ni wanachama wa ACT-Tanzania.
2.
Kutakuwa na Ngome za Vijana, Wanawake na Walezi
3.
NGOME za chama zitakuwa na jukumu kuu la kueneza itikadi, falsafa,
misingi na
sera za chama kwa makundi yao husika (Vijana, Wanawake na Walezi)
4. Kanuni za uendeshaji wa Ngome zitatungwa na Ngome husika na
kuidhinishwa na
Halmashauri Kuu kabla ya kuanza kutumika.
------------------------------------------------------------------------
*Page 54*

54
5. Kanuni na miongozo ya Ngome lazima zizingatie misingi ya Katiba hii.
Pale ambapo kuna
mgongano wa kitafsiri kati ya Katiba hii na Kanuni za Ngome, Tafsiri ya
Katiba
ndiyo itakayotamalaki.
* *
*IBARA 17*
*JUMUIA YA WABUNGE*
Kutakuwa na jumuia ya wabunge wa ACT-Tanzania itakayoundwa na wabunge
wote wa
ACT-Tanzania kwa mujibu wa katiba hii na kanuni za chama. Jumuia itaunda
utaratibu wake
wa kuijiendesha bila kuathiri masharti ya Katiba hii.
*SURA YA SITA*
*IBARA 18*
*MAPATO NA MALI ZA CHAMA:*
*1. Mapato ya Chama ni:*
i) Ada na viingilio vya wanachama.
ii)
Michango ya hiari ya wanachama na wafuasi wa Chama.
iii) Michango ya hiari ya watu wa ndani na nje wanaounga mkono Chama.
iv) Misaada kutoka kwa vyama rafiki vya kisiasa vya ndani na nje ya nchi.
v)
Misaada na ruzuku toka ndani na nje ya nchi.
vi) Mapato yanayotokana na hisa na miradi halali ya Chama.
*2. Mali za chama ni:*
Mali za Chama ni pamoja na:
i) Mali zozote zenye kuondosheka na zisizoondosheka
ii) Hisa za Chama katika miradi ya kiuchumi.
iii) Mali za NGOME Taasisi zingine katika chama
------------------------------------------------------------------------
*Page 55*

55
*IBARA 19*
*WADHAMINI WA CHAMA:*
1. Kutakuwa na bodi ya wadhamini wa Chama yenye wajumbe wasiopungua saba
(7) na
wasiozidi tisa (9) itakayoteuliwa na Baraza Kuu.
2. Mali zote za kudumu, vitega uchumi na dhamana zote zitawekwa chini ya
jina
lililosajiliwa la Bodi ya Wadhamini.
3. Bodi ya wadhamini itateuliwa kila baada ya miaka mitano ya Uchaguzi
Mkuu wa
viongozi wa Chama.
4. Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini watateuliwa na Kamati Kuu na kuidhinishwa na
Halmashauri Kuu
5. Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini watachaguliwa kutoka
miongoni mwa
wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
6. Wajumbe wa Kamati Kuu hawatateuliwa katika Bodi ya Wadhamini, isipokuwa
Mwenyekiti na Katibu wa Bodi ya Wadhamini watakaoingia kwa nafasi zao
7. Kanuni za Chama zitaainisha taratibu za mikutano ya Bodi ya wadhamini.
*IBARA 20*
*UKAGUZI WA MAHESABU YA CHAMA*
1.
Kutakuwa na Kanuni za Fedha za chama zitakazoidhinishwa na Halmashauri Kuu.
Kanuni hizi zitaanisha utaratibu wa fedha ndani ya chama
2.
Kutakuwa na idara ya ukaguzi wa mahesabu itakayokaguwa mahesabu ya chama
3.
Mahesabu ya chama yatakagukiwa kila mwaka na Kampuni ya Wakaguzi wa Nje
iyakayoteuliwa na Kamati Kuu na kuidhinishwa na Halmashauri Kuu
4.
Mahesabu ya chama yatawasilishwa katika vikao vya chama na kwa Msajili wa
Vyama na vyombo vingine kwa mujibu wa sheria za nchi
5.
Mweka Hazina atatoa taarifa kwa umma kuhusu taarifa ya fedha ya chama
kila baada
ya muda maalumu kama itakavyoamriwa na Halmashauri Kuu.
------------------------------------------------------------------------
*Page 56*

56
*SURA YA SABA*
*IBARA 21*
*MAREKEBISHO YA KATIBA*
1. Mapendekezo ya mabadiliko yoyote ya Katiba yatafanywa na Hamashauri
Kuu ya
Taifa kabla ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Taifa.
2. Mapendekezo yoyote ya mabadiliko ya Katiba yatajadiliwa katika ngazi
za chini za
chama kabla ya Halmashauri Kuu kuandaa Rasimu ya mapendekezo kwa Mkutano
Mkuu.
3. Mkutano Mkuu ndiyo wenye mamlaka ya juu ya kubadili Katiba.
4. Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba yatafikishwa katika ngazi ya
Jimbo sio chini
ya siku 60 kabla ya tarehe ya Mkutano Mkuu unaohusika kujadili mabadiliko.
5. Kamati za Jimbo zitatakiwa kurejesha maoni yake ndani ya siku 30
tangu tarehe ya
mapendekezo kutumwa.
*IBARA 22*
*KANUNI ZA UENDESHAJI WA CHAMA*
1. Halmashauri Kuu itatunga Kanuni mbalimbali za uendeshaji wa chama kwa
kuzingatia masharti ya Katiba hii.
2. Kukitokea migongano kati ya kipengele cha Katiba na kile cha Kanuni,
kipengele cha
Katiba kitatamalaki.
3. Halmashauri Kuu itakuwa na mamlaka ya kuzifanyia marekebisho Kanuni
za Chama
ili kwenda na mahitaji ya wakati.
4. Kamati Kuu itatunga mwongozo wa uendeshaji wa vikao vya chama.
*IBARA 23*
*KUVUNJWA KWA CHAMA:*
1. Chama kitavunjwa rasmi endapo robo tatu (3/4) ya wajumbe wote
watakaohudhuria
------------------------------------------------------------------------
*Page 57*

57
Mkutano Mkuu wa Chama wa Taifa ulioitishwa kwa madhumuni ya kuvunjwa kwa
Chama watapitisha hoja hiyo. Mkutano huo utatangaza rasmi kuvunjwa kwa Chama
na kusimamishwa kwa shughuli zote za Chama.
2. Katika tukio la kuvunjwa kwa Chama, Bodi ya Wadhamini wa Chama
itahodhi mali
hiyo kulipia madeni yote ya Chama. Endapo kutakuwa na salio lolote la
mali ya
Chama baada ya kulipa madeni yote, salio hilo litawasilishwa au
kukabidhiwa kwa
Taasisi yoyote ambayo shughuli zake zinaakisa misingi iliyoanzisha chama
hiki kama
itakavyoamuliwa na Bodi ya Wadhamini.
3. Katika tukio la kuvunjwa kwa Chama kwa nia ya kuungana na Chama
kingine cha
Siasa Bodi ya Wadhamini wa Chama itahodhi mali yote ya Chama na kuitumia
mali
hiyo kulipia madeni yote ya Chama. Endapo kutakuwa na salio lolote la
mali ya
Chama baada ya kulipa madeni ya Chama salio hilo litatumika kufuatana na
azimio la
kuvunja Chama ili kuungana na Chama kingine.
*IBARA 24*
*MASHARTI YA MPITO*
1. Muda wa mpito utakuwa muda wote kuanzia tarehe ya kuanza kutumika
Katiba hii hadi
uchaguzi mkuu wa kwanza utakapofanyika
2. Kutakuwa na uongozi wa muda utakaodumu tangu chama kiliposajiliwa hadi
utakapofanyika uchaguzi wa mpito
3. Jukumu kuu la uongozi wa muda litakuwa ni kukitaasisha chama kwa
kurasimisha
Katiba ya chama katika vikao husika na kwa mujibu wa sheria za nchi,
kuandaa kanuni
na miongozo ya uendeshaji na kukiandaa chama kwa ajili ya uchaguzi wa
serikali za
mitaa.
4. Uchaguzi wa mpito utafanyika ndani ya mwaka mmoja tangu chama
kilipopata usajili wa
kudumu
5. Kazi ya uongozi wa mpito utakuwa ni kukiandaa chama kwa ajili ya
uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015, na kuandaa uchaguzi mkuu wa kwanza wa chama.
6. Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa chama utafanyika kabla ya mwezi wa sita
mwaka elfu
mbili na kumi na sita.
------------------------------------------------------------------------
*Page 58*

58
7. Baada ya kumalizika kwa Muda wa Mpito, masharti ya Ibara hii yatakoma.
 
Tatizo sio Katiba, mwaweza kuwa na katiba nzuri sana lakini utekelaji wake ni ovyo kabisa! nyie mmekuja na na kitu gani "UNIQUE" ambacho Watanzania wanasema hiki chama ni mkombozi wao? kwanini mnashambulia vyama pinzani?
 
hakuna jipya ni kikundi cha walioshtukiwa kwa hujuma wameunda kijisaccos ili wapate fedha kwa mabwana zao ccm
 
Ccm hiyo imekuja kivingine! Tawi la CCM.
ACT kama tawi la CCM.ZZK akihamia huko ndio mwisho wake kisiasa. Hawezi kupambana na CCM,kama hoja zake zitajikita kuishambuliwa CHADEMA,jamii itashangaa,na watz wa sasa sio wa enzi za miaka ya 90's
 
unazifaham sheria lakini, hebu soma hiyo rasim Kisha Toa mapendekezo kuwa mzalendo mkuu ondoa chuki
Ndio mjue hata hapa jamvini watu walishawadharau, uzi zenu za ACT huwa zinaishia wachangiaji 20 tu.

JF tulishawapuuza.

Chama usajili wa zimamoto? What the motives behind this harakaharaka?
 
Naona ACT wamekuja na kitu kipya kinaitwa "Kiongozi wa chama" safi sana ACT
 
Back
Top Bottom