Katiba ya CHADEMA kuhusu chama Kuingia Mseto na Vyama Vingine

Mtamile

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
2,829
1,750
9.3 Chama Kuingia Mseto na Vyama Vingine

9.3.1 Chama kinaweza kuunda mseto na Chama au vyama vingine vyenye madhumuni na
malengo yanayofanana na Chama ili kuimarisha uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au
wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja.

9.3.2 Chama kinaweza kuunda ubia na vyama vingine katika kuendesha miradi ya kiuchumi
ama huduma.

9.3.3 Chama kinaweza kuungana na Chama ama vyama vingine kuunda Chama kipya.

9.3.4 Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1 na 9.3.3 utafanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa na
kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza Kuu.
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,657
2,000
Uchaguzi Mkuu bado kufanyika so kipengele kipi hapo kimevunjwa kwa akili yako ya.kufikiri kwa A55 ?
Back Tanganyika
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
9.3 Chama Kuingia Mseto na Vyama Vingine
9.3.1 Chama kinaweza kuunda mseto na Chama au vyama vingine vyenye madhumuni na
malengo yanayofanana na Chama ili kuimarisha uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au
wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja.
9.3.2 Chama kinaweza kuunda ubia na vyama vingine katika kuendesha miradi ya kiuchumi
ama huduma.
9.3.3 Chama kinaweza kuungana na Chama ama vyama vingine kuunda Chama kipya.
9.3.4 Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1 na 9.3.3 utafanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa na
kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza Kuu.

CC: Ben Saanane , Yericko Nyerere , .....
 
Last edited by a moderator:

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,657
2,000
Mkutano Mkuu ulishakaa na kuamua, CHADEMA kuungana na CCM B?

Mkutano utakaa kuidhinisha Muungano pale uchaguzi utakapokuwepo.
Ni uchaguzi gani CHADEMA weungana na vyama vingine.
A55
 

respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,537
2,000
Uchaguzi Mkuu bado kufanyika so kipengele kipi hapo kimevunjwa kwa akili yako ya.kufikiri kwa A55 ?
Back Tanganyika

Mkuu hawa misukule muda wa kufungiwa umefika sasa ni kawaida kuja na mada kama hizi hapa lazima tuwaeleweshe hivyohivyo wakati tukiendelea kutafuta usingizi.

Nyie Gambaz tambueni kuwa mpaka sasa hakuna mahali Chadema ilipoungaa na vyama vingine kisheria,kilichopo ni makubaliano ya awali yaliyo waunganisha wapinzani kupitia mchakato wa Katiba mpya hivyo baada ya kutathimini faida zilizopatikana baada ya muungano huo ndipo wote kwa ujumla wakatambua kuwa adui yao ni mmoja hivyo waunganishe nguvu ili kumwangamiza kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka kesho na hili halipo kisheria bali ni MoU mean makubaliano ya awali kupitia viongozi.

Ikionekana jambo hili linamaslahi kwa wote na wote wanakubaliana ndipo,sa hatua ya msingi itafuata kuputia vikao na mikutano kikatiba Hii ndiomaana ya kutoa nafasi kwa baadhi ya watu kuongoza yaani kuonyesha njia. Sasa ninyi mnavo panua midomo kupayuka juu ya jambo hili mnafanya kazi msioujua maana huwezi jua kwamba maybe wapinzani wako kwenye utafiti juu ya hili kwamba je ccm wanalipokea vipi sasa nyie kwakupiga mayowe kuanzia kwa viongozi wenu majukwaani mpaka misukule yao hapa jamvini kunaonyesha wazi kuwa hili ni jambo la heri kwa upinzani na kifo kwa maccm maana ni jambo lililiwazi kuw huwezi kumwombea heri adui yako sasa Nyinyi endeleeni kupayuka hapa mkifikiri mnaudhoofisha upinzani kumbe ni kinyume chake.

BACK TANGANYIKA
 

tanganyikakwanza

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
495
0
Watu wengine viazi kweli kwa hiyo mahali pakiandikwa usikae hapa wewe hupiti? kipengele cha kwanza kinaongelea uchaguzi mkuu,cha pili miradi ya uchumi na kingine kuanzisha chama kipya.hapo ya katiba umeipata wapi? na jk katiba ya ccm imemruhusu wapi kukubali katiba mpya? au ni kikao gani kiliamua?
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,869
2,000
Maccm ama mnajikanya! Yamewakuta yamewakuta tu,mmewaibia wananchi vya kutosha,tuachie nchi zamu yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom