Katiba ya CCM inawabeba Lowassa, Rostam, Chenge na kuwatosa Membe na Sitta

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Wakuu nimeipitia kwa umakini katiba ya CCM na nimegundua inamapungufu makubwa na inalinda na kuruhusu wahalifu kushika nyadhifa hata kama walishakwenda jela maisha, ilimradi tu uifurahishe kamati kuu.

Nimejaribu kuchukua sehemu ya Wanachama na viongozi katika katiba hiyo toleo la 2005.

2.1. WANACHAMA NA VIONGOZI

FUNGU LA 1:

6.Kila mtu aliyekuwa mwanachama wa TANU au wa ASP mara kabla ya kuvunjwa kwa Vyama hivyo, na aliyekuwa anatimiza masharti ya Uanachama wake, atakuwa mwanachamaa wa Chama Cha Mapinduzi, isipokuwa kama atakataa mwenyewe.

7.Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, anaweza kuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi iwapo anakubali Imani, Malengo na Madhumuni ya CCM.
8.Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM, au kuendelea kuwa Mwanachama, ni yule anayetimiza Masharti yafuatayo:

(1)Kuwa mtu anayeheshimu watu.
(2)Kuwa mtu anayefanya juhudi ya kuielewa, kuieleza, kuitetea na kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM.
(3)Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha Utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo.
(4)Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake

5)Kuwa mtu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya Umma, kulingana na Miongozo ya CCM.
(6)Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake, kuwa mwaminifu na kutokuwa mlevi au mzururaji.
(7)Kuwa ama Mkulima, Mfanyakazi, au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegemea. Utaratibu wa kuomba Uanachama Utaratibu wa kufikiria maombi ya Uanachama Mafunzo kwa Wanachama Kiingilio na Ada za Uanachama
10. 9.Mtu atakayetaka kuwa Mwanachama atajaza fomu ya maombi na kuipeleka kwa Katibu wa Tawi anapoishi.

10.Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itafikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya Uanachama.

11.CCM itakuwa na Mpango wa kutoa Mafunzo kwa wanachama wake juu ya Imani, Malengo na Madhumuni ya Siasa ya CCM kwa jumla.
12.(1)Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:

(a)Atatoa kiingilio cha Uanachama.
(b)Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c)Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa.
(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

13.(1) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:

(a)Kujiuzulu mwenyewe;
(b)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba. (c)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(e)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

(2)Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.

(3)Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka kuingia tena katika CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama.
(4) Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

14.Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo:-
(1)Haki ya kushiriki katika shughuli zote za CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

(2)Haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya CCM pale ambapo anahusika kwa mujibu wa Katiba.

(3)Haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa CCM na ya kuchagua viongozi wake wa CCM kwa mujibu wa Katiba au Taratibu za CCM.
(4)Haki ya kujitetea au kutoa maelezo yake mbele ya Kikao cha CCM kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake, pamoja na haki ya kukata rufani ya kwenda katika Kikao cha juu zaidi cha CCM kama kipo endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa.

(5)Haki ya kumuona kiongozi yeyote wa CCM maadam awe amefuata utaratibu uliowekwa.
Wajibu wa Mwanachama
15.Kila Mwanachama atakuwa na wajibu ufuatao:

(1)Kujua kwamba Chama Cha Mapinduzi ndicho chenye nguvu, uwezo na kwamba nguvu hizo zinatokana na umoja wa Wanachama, fikira sahihi za CCM na kukubalika kwake na umma. Kwa hiyo kulinda na kuendeleza mambo hayo ni Wajibu wa kwanza wa kila Mwanachama.
(2)Kutumikia nchi yake na watu wake wote kwa kutekeleza wajibu wake bila hofu, chuki wala upendeleo wa nafsi yake, rafiki au jamaa.

(3)Kujitolea nafsi yake kuondosha Umasikini, Ujinga, Maradhi na Dhuluma, na kwa jumla kushirikiana na wenzake wote katika kujenga Nchi yetu.
(4)Kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania.
(5)Kukiri kwa imani na kutekeleza kwa vitendo Siasa ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea

6)Kujielimisha kwa kadiri ya uwezo wake, na kutumia elimu hiyo kwa faida ya wote.
(7)Kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa ili kuweza kuwa na msimamo sahihi wa siasa ya CCM.
(8)Kuwa wakati wowote hadaiwi ada zozote za Uanachama.
(9) Kuhudhuria mikutano ya CCM inayomhusu

FUNGU LA II VIONGOZI

Maana ya Kiongozi Sifa za Kiongozi Miiko ya Kiongozi:

14. 16.Kiongozi wa CCM ni kila Mwanachama mwenye dhamana yoyote katika CCM aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

17.Pamoja na kutimiza masharti ya Uanachama kama yalivyoelezwa katika Katiba, Kiongozi sharti pia awe na sifa zifuatazo:

(1)Awe ni mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.

(2)Awe ni mtu anayependa kueneza matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa jumla.

18.Ni mwiko kwa kiongozi:-

(1)Kutumia madaraka aliyopewa ama kwa ajili ya manufaa yake binafsi au kwa upendeleo, au kwa namna yoyote ambayo ni kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo.

(2)Kupokea mapato ya kificho, kutoa au kupokea rushwa, kushiriki katika mambo yoyote ya magendo au mambo mengine yaliyo kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo

19. (1) Uongozi wa kiongozi utakoma kwa:
(a) Kujiuzulu mwenyewe.
(b)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba. (c) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kung’atuka /kuacha kazi.
(e) Kujiunga na chama kingine cho chote cha siasa.

(2)Kiongozi aliyeachishwa au kufukuzwa uongozi anaweza kuomba tena nafasi ya uongozi wowote na maombi yake yatafikiriwa na kutolewa uamuzi na kikao kilichomwachisha au kumfukuza uongozi.

20.(1) Mwanachama anayeomba nafasi ya uongozi wa aina yoyote katika CCM hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.

(2)Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura hizi zinafikia nusu ya kura zote

Mfano wa madudu katika katiba hiyo ni vifungu hivi hapa chini vinavyompa fursa "mhalifu" kuongoza chama/nchi.

13 (3)Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka kuingia tena katika CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama.
(4) Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

19 (2)Kiongozi aliyeachishwa au kufukuzwa uongozi anaweza kuomba tena nafasi ya uongozi wowote na maombi yake yatafikiriwa na kutolewa uamuzi na kikao kilichomwachisha au kumfukuza uongozi.

Kinyume chake, vifungu hivihivi vinawafinya na kuwatosa wanafiki wa kisiasa, hili litatikea ikiwa wezi watatumia ukwasi walionao kuinunua kamati kuu ya ccm ili iwape ridhaa ya kugombea!

Hiyo ndio katiba ya chama mufilisi kinacholitafuna taifa usiku na mchana

Kwamsaada zaidi wakuijua siasa tembelea https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/640686-darasa-la-siasa-4.html
 
Ndo maana kumbe kila mtu anafanya anachoweza na alichozoea mwenyewe.

Kweli wahalifu ccm kwao
 
Weka na ya chadema tuone inampendelea nani kati ya mbowe na slaa

CHADEMA: KATIBA YA 2006

Sura ya tano (5) ya katiba ya chadema ndio inayohusu mambi ya Uanachama kama nilivyoeleza awali kuwa hayo ndio nitakayofundisha kwa mapana zaidi.

5.0. Uanachama

5.1. Sifa zakuwa mwanachama/mfuasi wa Chama.

5.1.1. Awe raia wa Tanzania
5.1.2. Awe na umri wa miaka 18 au zaidi

5.1.3. Awe na akili timamu
5.1.4. Awe anakubaliana na katiba,sera,kanuni na maadili ya chama.

5.1.5. Awe anakubaliana na itikadi na falsafa ya chama.

5.1.6. Asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa baada yakujiunga na CHADEMA.

5.1.7. Vijana wa umri wa 12-17 ambao wanatimiza sifa ya 5.1.1, 5.1.3, 5.1.4, 5.1.5, na 5.1.6, watajiunga na Chama kama wafuasi wa Chama na watapewa kadi maalumu za Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA).

5.1.8. Kuwa mwanachama wa Chadema itakuwa ndio sifa ya msingi yakujiunga na Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.

5.2. HAKI ZA MWANACHAMA.
Kilawanachama anahaki ya:

5.2.1. Kuchagua viongozi wa Chama wa ngazi anayohusika kwamjibu wa katiba.

5.2.2. Kuchaguliwa kuongoza na kuwakilisha Chama katika ngazi yoyote kwakuzingatia masharti yaliyowekwa ya sifa za uongozi,

5.2.3. Kushiriki vikao vya Chama vinavyomhusu na kutoa mawazo yake kwa uhuru kwamjibu wa taratibu za vikao.

5.2.4. Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za kinidhamu kichama.

Itaendelea.........

5.3. WAJIBU WA MWANACHAMA.

5.3.1. Kushiriki kikamilifu katika vikao vinavyomhusu na katika shughuli nyingine za chama kadri atakavyotakiwa.

5.3.2. Kuchangia gharama za uendeshaji Chama kwa njia ya ada ya uanachama ya kila mwaka na kwamichango mingineyo itakayoamriwa na vikao vya chama.

5.3.3. Kutetea na kueneza itikadi, falsafa na madhumuni ya Chama ndani ya jamii anamoishi.

5.3.4. Kushirikiana na wanachama na viongozi wengine wote katika kutekeleza sera na mipango ya chama.

5.3.5. Kuwa tayari kupambana na namna yoyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi.

5.4. KUKOMA KWA UANACHAMA.

5.4.1. Kwakujiuzulu mwenyewe kwahiari yake.

5.4.2. Kutokana na kufariki.

5.4.3. Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya chama, kwa mujubu katiba kwakukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa kuwa na mwenendo usioendana na itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki yakukata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.

5.4.4. Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, kamati kuu inaweza kumwachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwautaratibu utakao wepangwa na kanuni za chama.

5.4.5. Kukosa sifa za uanachama.

5.4.6. Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu.

5.5 ADA NA KIINGILIO YA UANACHAMA.

5.5.1. Kutakuwa na kiingilio kwa kila mwanachama mpya.

5.5.2. Kutakuwa na ada ya mwaka ya uanachama.

5.5.3. Utaratibu wa ulipaji na viwango vya ada zote utafafanuliwa na kanuni za Chama.
 
Wakuu nimeipitia kwa umakini katiba ya CCM na nimegundua inamapungufu makubwa na inalinda na kuruhusu wahalifu kushika nyadhifa hata kama walishakwenda jela maisha, ilimradi tu uifurahishe kamati kuu.

Nimejaribu kuchukua sehemu ya Wanachama na viongozi katika katiba hiyo toleo la 2005.

2.1. WANACHAMA NA VIONGOZI

FUNGU LA 1:

6.Kila mtu aliyekuwa mwanachama wa TANU au wa ASP mara kabla ya kuvunjwa kwa Vyama hivyo, na aliyekuwa anatimiza masharti ya Uanachama wake, atakuwa mwanachamaa wa Chama Cha Mapinduzi, isipokuwa kama atakataa mwenyewe.
Kwanza unachokiongea ni illogical and outdated.

Tatizo lako unawaza kibavicha bavicha. CCM tunaenda na wakati.

Wewe unatuletea Katiba ya 2005. You're out of this world.

CCM tuna katiba toleo la 2012.
 
Kwanza unachokiongea ni illogical and outdated.

Tatizo lako unawaza kibavicha bavicha. CCM tunaenda na wakati.

Wewe unatuletea Katiba ya 2005. You're out of this world.

CCM tuna katiba toleo la 2012.

Ilete hapa hiyo katiba ya 2012 katika ibara na vifungu hivyo inasemaje?
 
Ilete hapa hiyo katiba ya 2012 katika ibara na vifungu hivyo inasemaje?
Nilichokuwa nafanya ni kukupa somo.

Siyo kazi yangu kukusaidia kujenga hoja ambayo inaendana na wakati katika mantiki ya hoja.

Wagombea wa CCM hawatolewi kutoka ndani ya mifuko ya suruali za viongozi wa chama kama ilivyo CHADEMA.

CCM ina kanuni na taratibu zake zinazoisimamia na kuiongoza katika kufanya shughuli zake mbalimbali zikiwemo za mchakato wa kuwapata wagombea wake katika ngazi mbalimbali kuanzia shina hadi taifa.

CCM ina kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Februari, 2010 na Kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la 2012.

Unazifahamu kanuni za CCM kwenye mchakato wa uchaguzi wa ndani?. Au umekariri kama ilivyo kawaida ya vijana wa BAVICHA.
 
Historia ya chama cha mapinduzi kuanzia 2000, haitoi fursa ya demokrasia kuamua mambo ya kichama,

Soma katiba yako kifungu hadi kifungu, na kila kufungu utakuta kinakinzana na uhalisia wa ccm.
 
Historia ya chama cha mapinduzi kuanzia 2000, haitoi fursa ya demokrasia kuamua mambo ya kichama,

Soma katiba yako kifungu hadi kifungu, na kila kufungu utakuta kinakinzana na uhalisia wa ccm.
Kwanza lazima uelewe neno demokrasia lina maana ndefu ambayo pia huwa ni kinzani kulingana na mazingira.

Unashika bango tu na kupiga kelele ukisema CCM haina demokrasia. Wanaofahamu vizuri neno demokrasia watakuuliza, demokrasia ipi?. Katika kanuni zipi ambazo zinaongozwa na taratibu zipi?.

Ndiyo maana nikakueleza kuwa Katiba ya chama inajenga misingi tu ya uendeshaji lakini huo uendeshaji lazima uwe na taratibu na kanuni ambazo zimekubaliwa na wanachama wengi. Hizo kanuni na taratibu ndiyo demokrasia yenyewe.

Kijana acha kukariri maandiko ambayo hata tafsiri yake hufahamu.

Ya CHADEMA imekushinda, utaiweza ya CCM iliyojengeka katika misingi ya chama endelevu.
 
Nilichokuwa nafanya ni kukupa somo.

Siyo kazi yangu kukusaidia kujenga hoja ambayo inaendana na wakati katika mantiki ya hoja.

Wagombea wa CCM hawatolewi kutoka ndani ya mifuko ya suruali za viongozi wa chama kama ilivyo CHADEMA.

CCM ina kanuni na taratibu zake zinazoisimamia na kuiongoza katika kufanya shughuli zake mbalimbali zikiwemo za mchakato wa kuwapata wagombea wake katika ngazi mbalimbali kuanzia shina hadi taifa.

CCM ina kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Februari, 2010 na Kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la 2012.

Unazifahamu kanuni za CCM kwenye mchakato wa uchaguzi wa ndani?. Au umekariri kama ilivyo kawaida ya vijana wa BAVICHA.

Kumbe ni kanuni sio katiba, mwenzako aliomba hiyo katiba ya 2012, ungemwelewesha kuwa mna kanuni sio katika. hayo ndiyo malumbano ya hoja ya wanazuoni kama haipo sio ugomvi kuwa wazi kuwa haipo ila mna kanuni mbadala na kile kilichopo kwenye katiba yenu ya 2005
 
Kwanza lazima uelewe neno demokrasia lina maana ndefu ambayo pia huwa ni kinzani kulingana na mazingira.

Unashika bango tu na kupiga kelele ukisema CCM haina demokrasia. Wanaofahamu vizuri neno demokrasia watakuuliza, demokrasia ipi?. Katika kanuni zipi ambazo zinaongozwa na taratibu zipi?.

Ndiyo maana nikakueleza kuwa Katiba ya chama inajenga misingi tu ya uendeshaji lakini huo uendeshaji lazima uwe na taratibu na kanuni ambazo zimekubaliwa na wanachama wengi. Hizo kanuni na taratibu ndiyo demokrasia yenyewe.

Kijana acha kukariri maandiko ambayo hata tafsiri yake hufahamu.

Ya CHADEMA imekushinda, utaiweza ya CCM iliyojengeka katika misingi ya chama endelevu.

Mkuu kwanza rejea kwenye majubu yako ya awali kwenye hoja yangu ya msingi,

Ulisema ccm inatumia katiba toleo la 2012, kwabusara kabisa nikaomba uweke hapa vifungu vya katiba hiyo vilivyofanyiwa marekebisho katika fungu la 1 na 2,

Lakini sasa unahamisha mantiki kuwa ni kanuni na sio katiba,

Rejea kwenye msingi wa hoja mkuu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom