Katiba: Wananchi Waliwakilishwa-Dr. Kashilila Live on TBC!

Huwa ninakutamani kweli, ila naogopa ban. Nitamwomba Mod atoe siku moja ya ban-free ili watu tutoe yaliyopo moyoni kwa madodoki.Kama walijua kuwa Wabunge ndio wawakilishi wetu na wao pekee wangetosha kutuwakilisha, Walikuja na Mitakataka yao mingine ikachanwa kule Zanzibar na Mabomu yakapigwa pale Dodoma, walidhani wale wote waliowaita kuchangia mawazo yao ni Wabunge! Kwa hiyo tuseme kwamba waliochana ule muswaada mbofu mbofu pale Zanzibar ni Wabunge! Kama walijua wabunge wanatosha kuwawakilisha wananchi, sasa waliuleta Mswaada wa kwanza kwetu tuuchangie kama sisi ni kina nani!

Watu wengine wapo kiutumwa (kikazi zaidi), wanalipwa na nape kwa kuhesabiwa post walizoandika hapa JF, kwahiyo usihangaike nao.
 
Suala la Katiba ni la wananchi,huyu Katibu wa Bunge kweli haelewi,kwa maana mimi ninavyoelewa suala la uwakilishi au Representative Democracy"Kwa kweli wabunge wetu hawalifanyi wao wako Bungeni kwa maslahi binafsi,maana wangekuwa wanatuwakilisha wangeongelea wagonjwa kulala chini kwenye hospitali zetu,lakini wao wanajiongezea posho zao kwa maslahi binafsi,ndio maana wao kwa kufuata formality za Bunge anayohaki ya kusema wananchi waliwakilishwa,lakini kwa hali halisi na ukweli wananchi hatukuwakilishwa,wanafunzi wanagoma kudai haki zao, lakini wabunge wanawakandamiza badala ya kuwa tetea,Hatuna imani na Wabunge wetu,na BUNGE lenyewe linalopitisha/kuongeza posho za wabunge,ambao wengi wao ni kulala tu,bungeni,hizo posho zingepelekwa kusaidia wagonjwa hospitalini,kuongeza mishahara midogo ya waalimu,mikopo kwa wanafunzi na kero nyingi za wananchi kama vile mgao wa umeme,maji na bara bara mbovu za vijiji.Tutawasubiria kwenye kura za maoni.
 
Zanzibar is a semi autonomous entity! Hiyo kuita nchi ni misguidance!

Unakumbuka yaliyomkuta Pinda bungeni aliposema zanzibar si nchi????
Je wapemba na waunguja wanajua hilo?
Je na Tanganyika ni nin?

Katiba mbovu,viongozi wabovu na muungano mbovu ndani ya miaka hamsini.
 
Ndg wanaJF,

Inasikitisha sana kuona kuwa mawazo ya wachangiaji wengi ni kama ya watumwa wanaosifia mabwana zao, wako tayari hata kupigana kwa ajili hiyo.
Tuache ushabiki wa kipuuzi kwa jambo muhimu kama katiba yetu. UCHADEMA, UCCM, UCUF etc. uwekwe kando, tujadili kama watu wamoja, wenye lengo na nia moja ya USAWA na USTAWI wa wote.
 
Kichomiz, wale jamaa kule mjengoni ni wawakilishi wa nani?. Ukiondoa wale 'kula kulala, wa sadaka, wa sadakakawe na mapoozeo kibao, waliochaguliwa na wananchi ni wawakilishi wetu!. Chochote wachofanya mle ndani, wanafanya kwa niaba yetu!.


Kwenye blue hapo umenifurahisha wanasema kwa niaba yetu, wanakula kwa niaba yetu ndiyo maana hawataki kuiwajibisha serikali iwahudumie wananchi bali iwahudumie wao kwa kupandisha maposho na mishahara yao, wanafikili kwa niaba yetu maana yeyote nje yao yao hawamtambui kama vile Jukwaa la Katiba, wanatibiwa kwa niaba yetu, wanasoma kwa niaba yetu huo diyo uwakilishi wetu pale mjengoni. Afrika naipenda lakini Tanzania naipenda sana, maana siasa ni mtaji kuelekea neema, nilikuwa najiuliza kwa nini walimu wadai stahiki zao kwa muda mrefu mpaka watishie kugoma! lakini leo nimepata jibu wapo wanaotuwakilisha katika kufikiri, kula, kuvaa, kutibiwa, kulipwa mishahara, UHURU bado haujapatikana hapa. Tuliowanyonge tunahitajika kupigania uhuru maana tulifikili wanashiriki katika kugawa keki ya taifa ile iwafaidishe watanzania waliowengi kumbe tunawakilishwa katika yote!? Hima waTanzania tulionyonywa kwa muda mrefu tuelewe hivyo na tuchukue hatua.

 
Wanabodi, wale wenye access na TBC, watch TBC -1 now, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila yuko live akiongelea mchakato wa katiba.

Dr. Kashilila amesisitiza kuwa sii kweli wananchi hawakushirikishwa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Wananchi wameshirikishwa kikamilifu kabisa kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Kama kuna wabunge ambao walipaswa kuchangia lakini hawakuchangia, hao sasa ndio waliowakosesha haki wananchi wao na katiba ijayo itaweka kifungu cha kuwawajibisha wabunge wasio wawakilisha wananchi wao ipasavyo!.

Dr. Kashilila ameandamana na Mwandishi Mkuu wa Sheria ambaye amethibitisha wamepokea mapendekezo ya Jukwaa la Katiba kwa mara tatu tofauti na mawazo yao yamejumuishwa kwenye muswada huo!.

Endeleeni kufuatilia...
Mkuu umeamua kufukua mazikio
 
Back
Top Bottom