Katiba: Wananchi Waliwakilishwa-Dr. Kashilila Live on TBC!

Hawa jamaa bwana walikuwa watatu lakin hawaelez kitu kinachoeleweka......mswada uliandikwa kingreza hao wananchi walijadili vipi?,,wananchi waliomba uandikw kiswahili ili waweze kuchangia,,,vilaza wamefanya hivyo na kuendelea hatua nyingine....
Chempo hili la lugha nalo neno!. Sheria zetu zote bado zinatungwa Kiibgereza!. Wakoloni wametufanya vibaya sana kwenye mental slavery!.

Wanaambiwa watafasiri ili wananchi waweze kuujadili, wanautafasiri kwa ajili ya wabunge kuhadili!.

Wanabodi, nawashauri tuachane na hii biashara ya nini kilitakiwa kufanyika lakini hakikufanyika tuipe tume ushirikiano tupate katiba bora na sio bora katiba!.
 
Ndani ya nafsi yake Dr Kashilila anaamini kweli watanzania wamepata fursa ya kutoa maoni? Kwa nini huyu bwana anadharua wananchi kiasi hiki? Wananchi wanasema hawakupata fursa ya kutoa maoni yeye anasema walipata, hivi kama mtu umetoa maoni utasahau au inakuwaje?

1. Kwenye research yoyote ni lazima uchukue 'appropriate' sample ndio utoe majibu/conclusion juu ya jambo unalofanyia kazi. Tanzania ina zaidi ya mikoa 27 (Tanganyika & Zanzibar) iweje mikoa mitatu itumike kuchukuwa maoni? Mkoa wa Dar es Salaam una zaidi ya watu milioni nne, siku tatu zinatosha kuchukuwa maoni (hata kwa representation style) kwa siku tatu? Tena jambo lenyewe ni nyeti kama katiba ya nchi? Nani asiyekumbuka kuona picha za watoto wadogo waliosombwa naTambwe Hiza kujaza viti ili watu wenye uwezo wa kuchangia wasipate fursa?

2. Kwenye hiyo mikoa mitatu muswada uliojadiliwa ni ule wa zamani ambao ni tafauti kabisa na huu wa sasa! Na ulikuwa umeandikwa kwa kiingereza hivyo watanzania wengi wasingeweza kuelewa nini kimeandikwa. Hata hivyo huu muswada wa November umeandikwa kwa lugha ya kiswahili na ni toafuti na ule wa mwanzo. Haujawahi kujadiliwa na wananchi maana wameandika upya na kupeleka moja kwa moja bungeni.

3. Ki-utaratibu muswada unatangazwa kwenye national gazzette, wananchi wanatoa maoni yao, ndio wabunge wajadili. Yes, mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake lakini haimanishi kuwa baada ya kuchaguliwa mbunge hatochukua maoni ya wapiga kura wake (from time to time) juu ya nini au kwa vipi awawakilishe bungeni. Kumbe shida za wananchi wanazijua miaka 5 kabla? Busara ya kawaida tu inatosha kuongoza kuwa kwenye jambo nyeti kama katiba (sheria mama ya nchi) kila mbunge alitakiwa arudi jimboni kwake apate maoni ya wapiga kura ndio wakikutana Dodoma wakao pamoja na kujadili watanzania wanataka nini.

Na mtu asilete hoja hakuna muda wala fedha kugharamia wabunge ili waende kwenye majimbo yao. Juzi wabunge wamejiongezea posho - Tsh 24 billion! Muswada uliondolewa February. Hivyo muda na pesa vyote vipo.

Kama kweli watanzania wametoa maoni yao Dr Kashilila anaweza kusema ni kwa nini watanzania hao hao wanalalamika? tena wanasema hawapewa nafasi yao (kikatiba) kutoa maoni yao? Watanzania hawana kumbukumbu? Ana majibu gani huyu baba kama sio madharau kwa watanzania wenzake?

4. Kwa nini Spika Makinda hajitokezi kueleza watanzania kwa vipi huu muswada umesomwa kwa mara ya pili? Why is she alwayes sending this pen-pusher who has absolutely no sense of what is right or wrong? Dr Kashilila ana utaalam gani kwenye mambo ya katiba hadi akazanie kuja kwenye television?

5. Hoja ya wabunge wawakilisha wapiga kura wao kwenye huu muswada does not hold water. Ni wananchi gani au jimbo gani lilimtuma mbunge wao akaporomoshe matusi bungeni? Wabunge wa CCM na CUF badala ya kujadili muswada pamoja na kwamba haukupitia kwa wapiga kura wao, waliamua kwa makusudi kutumia kodi za wananchi kwa kutoa matusi! Watanzania wamebaki kama yatima, wenye hoja za kuwatetea hawasikilizwi, na wale wanaosikilizwa wanatumia fursa iliyopo kutoa matusi!

Nimalizie, kufanya kosa sio kosa ila kurudia! 2015 ni vizuri wananchi wahakikishe wanabalisha sura ya bunge. Ukishakosa bunge linalojadili matatizo ya wananchi usitegemee chochote cha maana toka serikalini. Haiwezekani kila siku tunarudia mambo yale yale. Wabunge wa CCM na CUF wameonesha madharau ya kutisha kwa wananchi wanyonge wa nchi hii. Lazima mambo yabadilike kwa mustakabali wa taifa hili. 2015 -Yes we can!
 
Katibu wa Bunge ameponda kwamba waliotoka nje bungeni walipoteza fursa ya kuwakilisha maoni ya wananchi.Hivi wale waliobaki ndio waliwakilisha maoni sahihi ya wananchi?Hivi mipasho na vijembe vile ndio yalikuwa maoni ya wananchi?Hivi alichosema Lusinde ndiyo yalikuwa maoni ya wana Mtera?Huyu katibu wa bunge nae sifuri brain!


Kama CHADEMA hawakutoka nje huyo katibu asingeenda kwenye televiosion.Miswada mingapi imepita bungeni lakini hakwenda kwenye vyombo vya habari? Na hapo alipo huyo katibu anaongea kama nani?
 
Pasco,

..yaani Kashilila,Ndugai,na Makinda, wana tabia za ajabu sijapata kuona.

..hawa ni sawa na waamuzi ktk mechi ya mpira. sasa wanapojitokeza kuanza kuwasakama makocha na wachezaji wa timu moja nadhani wanakiuka maadili ya kazi yao ya uamuzi.

..kwa kweli sijui nchi hii inaelekea wapi.
 


Hivi wewe ulikuwa hujuwi kuwa wabunge wanawawakilisha wananchi? na muswada umepitishwa Bungeni? Na sasa si muswada tena ni sheria, au ulikuwa hujuwi hilo?


Kama ni hivyo kwa nini tunahitaji maoni ya wananchi, si wangekaa tu hao wabunge wakaandika katiba mpya - si wanatuwakilisha ?
Kwa nini tunapoteza hela na muda kuunda mara kamati mara tume - si wawakilishi (wabunge) tayari tunao ?
 
Me ndio maaana siishi kupigwa ban kwa mambo kama haya,huwa najikuta nimetukana kwa sababu ya hasira,hasa hawa magamba wananikera sana kwa mamboa yao kipuuzi,sasa ni mwananchi gani alieshirikishwa?labda wale wnanchi wa Msoga ndio walioshirikishwa.

Si unapigwa Ban kwa sababu ya malezi yako yaliyozoea mitusi pasipo na sababu? Ningeshangaa sana kama Rais angekataa kusaini Muswada kwa sababu wa presha ya wahuni wachache waliokimbia mchakato wa kidemokrasia. Rais angekuwa anavunja katiba kwa shinikizo tu la watu wakati Bunge limefata taratibu zote ma muswada umepigiwa kura. Mwandishi Mkuu wa Sheria amesema wazi kwamba, tena kwa kunukuu Hansard juu ya namna wabunge wa magwanda walivyoshiriki katika mchakato wa kuutendea haki muswada huu.

Kwa ujumla Chadema wamefundisha adabu na zaidi ya ile chai ya Ikulu, hakuna walichokipata kutokana na ukaidi wao!
 
Mbona TBC1 wanawahoji watu wa magamba peke yao kwenye issue za katiba ina maana Television ya Taifa inahusu CCM peke yao?
 
Kama mbunge wako hakukushirisha uende ukamkoromee mbunge wako huko, sheria imeshasainiwa, mtaifata mkitaka msitake, isuseni kama mnaweza, wewe unafikiri vibunge vyenu 23 ndio vinawakilisha wananchi wangapi wa Tanzania hii, msituchafuwe.
Huwa ninakutamani kweli, ila naogopa ban. Nitamwomba Mod atoe siku moja ya ban-free ili watu tutoe yaliyopo moyoni kwa madodoki.Kama walijua kuwa Wabunge ndio wawakilishi wetu na wao pekee wangetosha kutuwakilisha, Walikuja na Mitakataka yao mingine ikachanwa kule Zanzibar na Mabomu yakapigwa pale Dodoma, walidhani wale wote waliowaita kuchangia mawazo yao ni Wabunge! Kwa hiyo tuseme kwamba waliochana ule muswaada mbofu mbofu pale Zanzibar ni Wabunge! Kama walijua wabunge wanatosha kuwawakilisha wananchi, sasa waliuleta Mswaada wa kwanza kwetu tuuchangie kama sisi ni kina nani!
 
Tunao wabunge na kazi yao ni kutunga sheria hy ndo moja ya kazi yao, sasa wanapotutupia mpira wananchi cjwi wamesahau majukumu yao,. Kwani sheria ngapi zimetungwa kwa kushirikisha wananchi moja kwa moja?

Wabunge wa Tanzania hawatungi sheria bali wanapitisha sheria zilizotungwa na serikali. Sijui sana uataratibu lakini sijasikia bunge limeanzisha hoja ambayo imekuwa sheria! nisaidieni hapa!
 
Katibu wa Bunge anaingilia uhuru wa Bunge kwa kujichukulia mamlaka ya kuwa msemaji wa Bunge.

I hope CHADEMA comes down on him like a ton of bricks.
 
Wanabodi, wale wenye access na TBC, watch TBC -1 now, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila yuko live akiongelea mchakato wa katiba.

Dr. Kashilila amesisitiza kuwa sii kweli wananchi hawakushirikishwa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Wananchi wameshirikishwa kikamilifu kabisa kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Kama kuna wabunge ambao walipaswa kuchangia lakini hawakuchangia, hao sasa ndio waliowakosesha haki wananchi wao na katiba ijayo itaweka kifungu cha kuwawajibisha wabunge wasio wawakilisha wananchi wao ipasavyo!.

Dr. Kashilila ameandamana na Mwandishi Mkuu wa Sheria ambaye amethibitisha wamepokea mapendekezo ya Jukwaa la Katiba kwa mara tatu tofauti na mawazo yao yamejumuishwa kwenye muswada huo!.

Endeleeni kufuatilia...
naona alipokea mawazo toka kwa mama yake, mkewe na wakwezake, basi nadhani ndio watanzania wote?
 
Si unapigwa Ban kwa sababu ya malezi yako yaliyozoea mitusi pasipo na sababu? Ningeshangaa sana kama Rais angekataa kusaini Muswada kwa sababu wa presha ya wahuni wachache waliokimbia mchakato wa kidemokrasia. Rais angekuwa anavunja katiba kwa shinikizo tu la watu wakati Bunge limefata taratibu zote ma muswada umepigiwa kura. Mwandishi Mkuu wa Sheria amesema wazi kwamba, tena kwa kunukuu Hansard juu ya namna wabunge wa magwanda walivyoshiriki katika mchakato wa kuutendea haki muswada huu.

Kwa ujumla Chadema wamefundisha adabu na zaidi ya ile chai ya Ikulu, hakuna walichokipata kutokana na ukaidi wao!

We unaitwa mbopo!!
 
Wanabodi, wale wenye access na TBC, watch TBC -1 now, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila yuko live akiongelea mchakato wa katiba.

Dr. Kashilila amesisitiza kuwa sii kweli wananchi hawakushirikishwa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Wananchi wameshirikishwa kikamilifu kabisa kupitia wawakilishi wao ambao ni wabunge. Kama kuna wabunge ambao walipaswa kuchangia lakini hawakuchangia, hao sasa ndio waliowakosesha haki wananchi wao na katiba ijayo itaweka kifungu cha kuwawajibisha wabunge wasio wawakilisha wananchi wao ipasavyo!.

Dr. Kashilila ameandamana na Mwandishi Mkuu wa Sheria ambaye amethibitisha wamepokea mapendekezo ya Jukwaa la Katiba kwa mara tatu tofauti na mawazo yao yamejumuishwa kwenye muswada huo!.

Endeleeni kufuatilia...


Kwenye red


Maana ya hiyo sentensi kuna kundi la watu tayari limeshaanda katiba kinachofanyika ni "formalities" tu
 
Kichomiz, wale jamaa kule mjengoni ni wawakilishi wa nani?. Ukiondoa wale 'kula kulala, wa sadaka, wa sadakakawe na mapoozeo kibao, waliochaguliwa na wananchi ni wawakilishi wetu!. Chochote wachofanya mle ndani, wanafanya kwa niaba yetu!.
sio kweli kama unavyofikiria ,ingekuwa hivyo wasingekuwa wanjiongezea posho wenyewe wangedai na wafanyakazi wengine,we angalia tra walivyo badilisha system ya kuingiza magari,wote wabunge walilalamka kwa vile inawahusu lakini dawa hospital hawana mpango
halafo sijawahi kusikia mbunge yeyote akiita mkutano kukusanya maoni ya wananchi

 
Pasco,

..huyu Dr.Kashilila ni Katibu wa Bunge wa ajabu kidogo.

..yaani ni tofauti kabisa na wale waliomtangulia kama Pius Msekwa, Mahamoud Mwindadi, na wengine.

..sikuwahi kusikia makatibu hao wakienda kwenye vyombo vya habari na kulumbana na wabunge.

..iliamuliwa kwamba mswada ukajadiliwe na wananchi na ziliteuliwa kanda 10. mswada ilikuwa upelekwe hata Unguja na Pemba ili wananchi waelezwe kilichomo, na waweze kutoa mawazo yao.

..sasa kwanini mswada haukupelekwa huko mikoani kwenye hizo kanda 10 zilizoteuliwa?

..wananchi walipaswa KUSHIRIKISHWA, siyo "kuwakilishwa" kama wanavyosema Dr.Kashilila na mwenzake.

Mkuu (Joka Kuu) sipendi hiyo ID yako kwa sababu kwa wakristo ni mbaya, lakini napenda kufuatilia michango yako kwa sababu huwa napata cha kujifunza. Tunatarajia unapokuwa "The so called Great Thinker" uwe na kitu ambacho mtu/watu watajifunza au kupata habari ambayo hawakuipata kabla na sio ushabiki tu. Hawa jamaa ( Dr. Kashilila na wenzake) walikuwa wanapiga siasa pale TBC1 lkn nilimsikia Dr. (sijui ana PhD ya nini) akisema watu (waliokuwa wakipiga simu) wanaingiza siasa. Hivi mchakato wa kukusanya maoni umeshaanza au hiyo sheria inatanguliwa na kupigiwa kampeni kwenye vyombo vya habari? Tunataka katiba ya wananchi, siyo ya wawakilishi wa wananchi.
 
Kinachonipa faraja ni muda "TIME WILL TELL" mfano Nani alijua raisi anyewaita wenzi mende, panya siku moja yeye mwenyewe atajificha kwenye shimo na kuadhibiwa kama mende na panya !!! Naomba Mola anipe uwezo wa kutojisahau, kulewa madaraka na kusoma alama za nyakati ili niweze kuchukua maamuzi sahihi kwa mstakabala wa watu ninaowaongoza.
 
Sina shaka kwamba hizi nguvu nyingi zinazotumika na katibu wa bunge pamoja na serikali kuwaaminisha watu kwamba wananchi walishirikishwa kikamilifu na maoni ya makundi mengine yalizingatiwa ni kwakuwa wamebaini kwamba wananchi wengi wanaelewa haki yao ya kushiriki katika kutunga katiba mpya, na wameelewa ni kwa kiasi gani bunge limekiuka utaratibu wa kuchukua maoni ya wananchi katika muswada huu.
Kuna baadhi ya maswali ambayo katibu wa bunge na mwandishi mkuu wa sheria walishindwa kuyajibu jana, ama waliyajibu ndivyo sivyo ama waliingiza siasa uchwara. Mojawapo ya swali ambalo walilijibu kisanii, ni kama maelekezo ya spika wakati muswada ulipoondolewa bungeni mwezi april, pamoja na mambo mengine, iliagizwa baada ya kuandikwa kwa kiswahili upelekwe kwa wananchi watoe maoni yao, kwa mujibu wa hansard lakini halikufanyika.

Halafu wanaposema maoni ya wadau wengine kama jukwaa la katiba, Tanganyika lawa society na majaji wastaafu yalizingatiwa, hawakutaja hata jambo moja lililozingatiwa na kuingizwa kwenye muswada, waliishia kusema tu kwamba muda hautoshi kuonyesha nani alichangiua nini! huo ulikuwa ni usanii wa hali ya juu.

Namuona kashilila akijaribu kugeuza ofisi yake kutoka kufanya kazi kitaaluma na kuingia kwenye siasa za chadema na ccm. Na bila aibu kabisa ameamua kuchukua upande ule wa waliomteua kuwatetea kwa muswada mbovu na kukiuka kanuni ili kutekeleza matakwa ya ccm. Katika watu wasiojua sheria, kanuni na uendeshaji wa bunge miongoni mwa makatibu wa bunge niliopata kuwafahamu, huyu kashilila ni hovyo kabisa.
 
Mkuu (Joka Kuu) sipendi hiyo ID yako kwa sababu kwa wakristo ni mbaya, lakini napenda kufuatilia michango yako kwa sababu huwa napata cha kujifunza. Tunatarajia unapokuwa "The so called Great Thinker" uwe na kitu ambacho mtu/watu watajifunza au kupata habari ambayo hawakuipata kabla na sio ushabiki tu. Hawa jamaa ( Dr. Kashilila na wenzake) walikuwa wanapiga siasa pale TBC1 lkn nilimsikia Dr. (sijui ana PhD ya nini) akisema watu (waliokuwa wakipiga simu) wanaingiza siasa. Hivi mchakato wa kukusanya maoni umeshaanza au hiyo sheria inatanguliwa na kupigiwa kampeni kwenye vyombo vya habari? Tunataka katiba ya wananchi, siyo ya wawakilishi wa wananchi.

Thanks for good observation,

Na kwa kuongezea, mimi nadhani ni vizuri sana kwa watanzanbia wengi kujua na kufuatilia siasa za nchi hii. Kwakuwa viongozi wetu-kuanzia wa kitaaluma hadi wa kisiasa wamekuwa wakifanya mambo ya uendeshaji na utawala wa nchi kwa mtazamo wa siasa za simba na yanga, nadhani itakuwa vizuri wananchi nao twende nao hivyo hivyo kisiasa, kwani hapo hawataweza kutudanganya na watagundua kwamba hatudanganyiki tena.

Ni ajabu kwamba yeye anawaona wananchi kuingiza siasa huku akisahau kwamba the whole process imekuwa handled politically! Na yeye mwenyewe amekuwa mpiga siasa mzuri katika jambo hili badala ya kutumia taaluma. Na kama wangeifanya kazi hii kwa weledi sidhani kama leo hii tungekuwa hapa tulipo.
 
Back
Top Bottom