Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
- Thread starter
- #101
Kwa muelekeo huu, niwaombe tume ya katiba wachukulie zoezi lao kama project ili waweze kujipanga vizuri. naona kiza huko mbeleni.
Ni kweli asilimia kubwa hatuijui Tanganyika na hatukuiona,naunga mkono wazo la kufanyia mabadiliko makubwa sana muundo wa Muungano wa sasa ili twende sawa na kupunguza kelele zisizo na maana kwa kila upande na kusawazisha mawazo mgando!
Yaani bado wapo tuu? Aaargh, wataondoka lini hawa wapemba, mie kuna duka nalitamani pale kariakoo
Ni kweli mie siwapendi
Mbona wazenji ni watu wakarimu sana. Sisi watanganyika nafikiri tuna matatizo, tunawachokoza sana. Aina ya muungano sio uaduiTatizo moja nililogundua toka kwa ndugu zenu kutoka tanganyika ni ile kujiona wamesoma sana lakin hawajatambua kuwa KUSOMA SI MALI KAMA HUJAELIMIKA.
Wanahitaji darsa kubwa sana la kuwaelimisha na sio kumalizo vyumba vyote vya madarasa kwa kukariri na kujiita msomi.
Msomi mzuri ni yule aliyeelimika
Hana nguvu kama mwanasheria wa SMZ na BLW. Umemsikia alivyoboronga kuhusu hoja za Lissu! hakuna lolote la maana au la kisheria alilojibu. Mwansheria ambaye ndugu yangu Baru baru kasema amesoma ametia aibu. Kama ule ndio usomi anaoupigia upata Baru baru basi ipo kazi.Mwambieni Mh. Tundu Lissu apeleke mswada wa kuvunja muungano bungeni tutafanya kampeni kabambe tuhakikishe amepata 2/3 ya wabunge wa zanzibar.
Najua kwamba pamoja na kwamba napenda serikali moja, wazenji hawatakubali, basi iwe serikali tatu. Na suala hili lirudishwe bungeni ili hadidu za rejea za tume zirekebishwe. Hii itawezasha upatikanaji wa rasimu ya katiba ya Tanganyika pia.
Muungano wa serikali tatu ni njia pekee ya kuimarisha muungano na vilevile ni njia yakuvutia nchi zingine kuona faida ya muungano. Tusiwe wanafiki, hakuna nchi inayotamani muundo wa sasa maana unalalamikiwa na watu wote hata viongozi wenyewe (wakiwa pembeni). Mchakato wa sasa umejaa hadaa. Wanchi waulizwe kwanza wanataka muungano wa serikali ngapi. Ninavyoamini mimi wananchi wengi kwa asilimia kubwa, wanataka serikali tatu. Asilimia inayofuatia kwa ile ya serikali tatu ni wale ambao hawataki muungano kabisa. Wanaotaka serikali mbili ni wachache sana hasa viongozi tu na wale wanaofaidi muungano huu kwa ufisadi. Hivyo ninawaomba wabunge wasome hisia za watu wasiendeleze matakwa ya serikali katika hili. Wabunge waazimie na kubadilisha sheria ya mchakato ili kuwepo na umuhimu wa kupiga kura ya maoni kuhusu muungano wananchi wautao kwanza. Kama ni serikali tatu, basi mchakato wa kutenegeneza katiba ya kila nchi ifanyike kwanza ikifuatiwa na mchakato wa katiba ya muungano. Hii ndio sawa yake. Kama serikali haitasikia hili, mimi ninadhani wananchi (WaTanganyika) wanapoenda kwenye mikutano ya maoni, wasichangie mengine zaidi ya kutaka Tanganyika izaliwe na tuunde katiba yake ndipo tuanze kujadili namna ya kuungana. Kwa maneno mengine muungano uvunjwe kwanza ili tuifufue Tanganyika. Baada ya hapo tujadili muungano tuutao. Mimi kama mimi na familia yangu tumesimamia hili. Je wewe?
Vote kwenye serikali moja kama unataka option ya pili basi unaweza kuvote kwamba 1 au hutaki, inaeleweka.Mi nina options mbili.
Serikali moja au hakuna muungano. Vote yangu ikaeje?
Analyse kwanza faida ya muungano wa serikali tatu ueleweke kwani kwa sasa bado hatujui tukiwa na aina hiyo utasaidiaje katika kukuza uchumi wa nchi zaidi ya kuongeza gharama za kuendesha serikali na mwananchi wa kawaida ndiye atakayezidi kuumia kura yangu kwa sasa kama ni muungano ni wa serikali moja ili kupunguza gharama za uendeshaji .From what I think kwa sasa tungejadili kwa hoja zenye mashiko namna ya kwaconvince wazenji wakafiki muungano wa serikali moja.That`s is my opinion
Kweli dokta Barubaru.Tatizo moja nililogundua toka kwa ndugu zenu kutoka tanganyika ni ile kujiona wamesoma sana lakin hawajatambua kuwa KUSOMA SI MALI KAMA HUJAELIMIKA.
Wanahitaji darsa kubwa sana la kuwaelimisha na sio kumalizo vyumba vyote vya madarasa kwa kukariri na kujiita msomi.
Msomi mzuri ni yule aliyeelimika