Katiba: Tanganyika Irudi Kwanza Ndipo Rasimu ya Katiba Ifuate

Unapenda Muundo Gani wa Muungano


  • Total voters
    210
Hivi tume inaangalia suala la muundo wa muungano? Hasa kwa wale waliokwisha pitiwa na hiyo tume?
 
Jamani tunahaitaji at least kura mia mbili, tupeleka kwa tume. Pigeni kura
 
Naona suala la kutaka kuvunja muungano, linaelekea kushindwa. Hebu tungoje kidogo.
 
Ha haaaaaa ha: naona serikali tatu inaelekea kushinda kura hizi maana inakuja kwa kasi. Nape rafiki yangu hii serikali mbili unasemaje?
 
Kweli swala la Muungano linachanganya, ni bora likazungumzwa na mambo yakawa bayana.

Sasa jamani naombeni mnisaidie hivi Tz mbona wimbo wa taifa siuelewi? sababu uliopo hauna asili ya either Tanganyika or Zanzibar! Ni wimbo wa South Africa uliotungwa na Msauzi. Ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga, „Nkosi Sikelel' iAfrika”.

Jamani mbona Wabunge hawahoji? Hivi sis hatuwezi kuwa na National Anthem ya kikwetu?
 
Kweli swala la Muungano linachanganya, ni bora likazungumzwa na mambo yakawa bayana.

Sasa jamani naombeni mnisaidie hivi Tz mbona wimbo wa taifa siuelewi? sababu uliopo hauna asili ya either Tanganyika or Zanzibar! Ni wimbo wa South Africa uliotungwa na Msauzi. Ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga, „Nkosi Sikelel' iAfrika”.

Jamani mbona Wabunge hawahoji? Hivi sis hatuwezi kuwa na National Anthem ya kikwetu?
Kwa sababu sasa hivi tuna Sugu na Komba bungeni tuwaachie hilo. Wanaweza wakatoa mchakachuo wa bongo flavor na modern Taarab.
 
CCM bado mnang'ang'ania serikali mbili, Mliyakataa ya Kolimba sasa mtayaona ya Nyalali.
 
kwa wabara muungano hauna faida bali hasara tupu kila siku madai kutoka upande mmoja yanatekelezwa na wanasiasa wa ccm kwa kasi ya ajabu! kwa sababu ya malengo ya kisiasa ya wanasiasa wa ccm tumechoka.
 
Serikali Tatu inakwenda juu kwa kasi, ningewashauri wale wanaotaka kuvunja muungano, wapunguze jazba. Tuwe na Tatu, nanihii.
 
kwa wabara muungano hauna faida bali hasara tupu kila siku madai kutoka upande mmoja yanatekelezwa na wanasiasa wa ccm kwa kasi ya ajabu! kwa sababu ya malengo ya kisiasa ya wanasiasa wa ccm tumechoka.
Nakubali. Je hii sio kwa sababu muundo ni mbaya?
 
Ndugu wana JF. Naungana na alichokisema Ndugu yangu Fred. Mzee Warioba alitulpiga changa la macho. Kama tutakuwa na kumbukumbu vizuri, Baba Ridhiwan alikataza watu kuujadili muungano. Baada ya kuona watu wamelalamika sana pamoja na kuonesha nia ya kutaka kususia mchakato wa utoaji maoni, Ndipo akaibuka Mzee Warioba na kusema Muungano ujadiliwe, na maoni yatolewe hata kama ni ya kuuvunja. Haya yote ni ili kuwashawishi Watanzania wajitokeze kwenye kutoa maoni yao. Lakini ukweli ni kwamba, maoni yote yanayohusu kuupangua muungano hayatafanyiwa kazi kabisa. Tukumbuke kuwa mzee Warioba ndiye alikuwa anautetea huu Muungano kwa nguvu zote kabla ya kuteuliwa, na baada ya kuteuliwa amejipangia maeneo yale ambayo Wakazi wake hawaupendi muungano huu. Cha muhimu hapa, ilitakiwa tuujadili Muungano kwanza, ili tukishakubaliana kuhusu hatima ya Muungano, tuweze sasa kujadili Katiba. Kwa njia tunayoitumia sasa, ya kutupiga changa la macho watanzania, najua hata katiba tutakayoiunda, tutaifanyia marekebisho baada ya miaka michache ya uhai wake. KAZI KWETU WATANZANIA.

Natamani kumwona mama yangu TANGANYIKA. Walimpoteza kwa makusudi, na wakajitahidi kufuta kumbukumbu lake, lakini naamini kama siyo leo, ipo siku wanangu au wana wa wana wa wanangu watapigana kufa na kupona kumdai mama yao TANGANYIKA. NAJUA MAMA YANGU TANGANYIKA HAJAFA, ILA AMEFICHWA TUU. Fredrick Sanga
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la WaTanganyika wanaongea saaana vitendo hamna kitu.
Ni kweli, umeona. nafikiri tatizo hatuna mwelekeo, wala hatujui mkakati mzuri wa kupata katiba nzuri. Kukusanya maoni ni kitu kizuri. Likini kuna kitu kinaitwa milestone katika mchakato, hiki kinakosekana. Hii inatokakana na kudhani watanzania wote wameshakubali serikali mbili. Kama itagundulika wanataka serikali tatu 2014, sijui kama hiyo rasimu ya katiba itapatikana. Ni ubishi tu wa wabunge wa CCM.
 
STRATON MZEE Huyu Sanga ana nia nzuri sana, ila kama watu wanamzarau profesa wa Shivji, wantasikia chochote? Sisi tupige kura kupitia JF ili picha halisi ianze kuonekana. Na liwalo na liwe, kura ya maoni kuhusu muundo wa muungano ni kizingiti kikubwa cha upatikanaji wa rasimu ya katiba. Sio upande wa Tanganyika tu hata Zenji. Maana hii katiba lazima itagusa ile ya Zenji. Hiki ni kihindimkuti.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom