KATIBA: Salim, Warioba wakutana na Dr. Slaa

Nadhani Mungu kawaongoza hawa wazee,ili wapate kuongea Na dr ili awezekueleza ni nini wanataka,maana kwa sasa naamini dr slaa na dr kikwete mwenye ushawishi mkubwa au mwenye kuongea yalio mioyoni mwa watanzania wengi ni Dr slaa,ndio maana wakamwita ili akawaeleze wanachotaka kwa niaba ya watanzania walio wengi.
 
Ni jambo la kutia moyo kuona wenye hekima wakiwa wanaongea juuya mustakabali wa nchi acha mavuvuzela waendele kudhalilisha jengo la bunge.
 
Brother Nape i know wewe ni mdau mzuri wa JF (though you may have several identities) but say a word and i shall be happy to know where you stand on this issue.... beba jambo hili kama mtanzania na si kama a leader of certain political party...please

achana na habari za nape..usituharibie mood..nyie ndo mnamfanya ajione mwenye tanzania..
 
Hawa ndiyo wazee wa busara utoto wa kikwete unajidhihilisha tumkumbuke NYERERE aliposema huyu ni mtoto wa akili
 
bora iwe ivyo maana patachimbika! Labda watupe sumu wote kama Mwakyembe maana picha ya mwakyembe ktk gazeti la mwananchi la leo inaogopesha na binafsi nimeamini maneno ya Joson Bourne!!
 
Duh Tanzania ilikosa bahati kubwa laiti mizengwe ya CCM ingewekwa kando Salim A Salim angetusaidia waTanzania. Leo tunalialia kama watoto wadogo Kikwete nchi imemshinda.
yeah..na ni mbinu hizo hizo zitatupa mgombea EL 2015! Tutaendelea kulialia hivihivi humu ndani
 
Dr Please waambie hao wanasiasa wa CCm wananchi wanataka katiba, na si uozo ule ulioletwa bungeni, waambie people's power si utani ni nguvu ya uMMA ambayo mabomu yao ya machozi hayatuzuii chochote kudai haki yetu

kumbuka nguvu ya umma ilimuondoa mubaraka pale misri ikafanya hivyo kwa gadafi, na ninvyoona kwa jinsi hawa mapoyoyo wanavyotufanyia cheusi chekundu kwenye katiba si muda mrefu peoples power itakomboa taifa hili
 
Duh Tanzania ilikosa bahati kubwa laiti mizengwe ya CCM ingewekwa kando Salim A Salim angetusaidia waTanzania. Leo tunalialia kama watoto wadogo Kikwete nchi imemshinda.

Kosa ni kurudia kosa, CCM walimpitisha JK kwa fitina zao wakamwacha Salim! Watanzania tusimamie katiba mpya kwa usahihi ili tulete mabadiliko ya ukweli. Ili hata mgombea binafsi ikiwezekana awepoo. Nguvu ya Umma oyee.................
 
Ushabiki wa kipumbavu wa wabunge wa CCM kuhusu suala hili la katiba na katika mambo mengine mengi yenye manufaa kwa taifa ni hatari kubwa sana. Ni bora kutokuwa na mbunge kuliko kuwa na mbunge aliyetayari kuliona taifa likiangamia na akijari tumbo lake. Huu ni upuuzi uliopitiliza.
 
Thursday, 17 November 2011 21:36
ANONYA BILA MARIDHIANO NCHI ITAELEKEA KUBAYA, KITINE ADAI SERIKALI 'INATUPELEKAPEKA'

Boniface Meena

MJADALA wa Muswada wa Katiba Mpya umechukua sura mpya baada ya viongozi waandamizi wa Serikali wakiwamo wastaafu, kutaka upatikane mwafaka wa kitaifa kuhusu suala hilo vinginevyo taifa litaelekea kubaya.Onyo la viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa , Dk Hassy Kitine, linakuja ikiwa ni siku chache baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutaka mwafaka huo wa kitaifa.

Jana, viongozi wakichangia maoni yao katika mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF), kuhusu nafasi na umuhimu wa katiba katika maisha ya Watanzania, kwa sehemu kubwa walipaza sauti kutaka mwafaka huo ili kunusuru taifa.

Kauli ya Dk Salim
Dk Salim ambaye ni mwenyekiti wa MNH, alisema ni muhimu kuwe na makubaliano na maafikiano katika suala la Katiba Mpya kwa CCM na Chadema.

Alisema, "Chama tawala na chama kikuu cha upinzani vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo".

Dk Salim alisema kwamba malumbano si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe yakasababisha nchi ikafika pabaya.

"Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifa,"alisema Dk Salim ambaye ana uzoefu na utatuzi wa migogoro ya kimataifa.

Alisema zoezi la Katiba ni zito na linatakiwa kufanyika kwa busara na kuwahusisha Watanzania wote.

"Kwa hali ya kisiasa hivi sasa ni lazima mjadala uwe wa nia njema lengo ni kuendeleza makubaliano na si kuhitilafiana. Tujenge na kuimarisha undugu na mishikamano wetu na kuonyesha uzalendo na uongozi madhubuti wa taifa letu,"alisema Dk Salim.

Kitine aionya Serikali
Kwa upande wake, Dk Kitine, alisema ni vizuri Serikali ikasoma alama za nyakati kutokana na hoja iliyoko bungeni kwa kuangalia suala hilo la katiba.

Dk Kitine alisema Serikali haitakiwi kuruhusu Muswada huo wa Marekebisho ya Katiba ukasomwa kwa mara ya pili, kwani tayari upinzani bungeni umekwishapinga.

"Serikali iutoe na kusoma upya, nchi haiko tayari kuona Serikali inavyotupeleka. Sasa ndiyo maana kuna matatizo kila sehemu,"alisema Dk Kitine.

Jaji Samatta
Kwa upande wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta alisema kuna baadhi ya wanasiasa hawaelewi maana ya katiba na kupotosha kuwa ni mapatano kati ya wananchi na viongozi."Katiba ikifutwa viongozi hakuna, hivyo Katiba ni moyo wa taifa,"alisema.

Jaji Samatta alisema kutunga Katiba ni kazi nzito na haiwezekani kila kitu anachokihitaji au kitu kinachohitajiwa na kundi fulani, kiwepo katika Katiba."Katiba ni makubaliano, lakini muda uliowekewa suala hili ni mchache,"alisema.

Alisema Katiba ya mwaka 1977 imefanya kazi nzuri, lakini ina matatizo mengi ndani yake, moja ikiwa ni dhana ya mfumo wa chama kimoja.

"Mfano Spika wa Bunge kuwa sehemu ya Halmashauri Kuu ya chama tawala, hapa atasababisha mgongano wa maslahi kwa kutetea chama chake,"alitoa kasoro hiyo.

Alisema kutokana na hali hiyo, Katiba Mpya ni lazima iwe na chachu ya upanuzi wa demokrasia na uboreshaji wa utawala wa sheria."Iwe ya mfumo wa vyama vingi na kuondokana na mfumo wa chama kimoja na iwe, inayoongozwa na wananchi,"alisema Jaji Samatta.

Dk Slaa atabiri Katiba mbovu
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema mchakato wa Katiba uikiwa mbovu Katiba yenyewe itakuwa mbovu.

"Wenzetu kule Dodoma wanapotosha kwamba kilichopo ni mchakato wanafikiri mchakato ni kitu kidogo, katiba ndiyo mzazi wa kila kitu hivyo kwa hali ilivyo katiba hii haiwezi kuwa ni ya wananchi badala yake Rais anajitengenezea Katiba yake,"alisema Dk Slaa.

Dk Bilal
Awali, akifungua mdahalo huo baada ya wachangiaji hao kutoa maoni yao, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal alisema nchi haiwezi kuwa na katiba nzuri ambayo itapatikana kwa kuliacha taifa likiwa vipande.

Alisema, ni muhimu kuhakikisha kunakuwepo majadiliano kuhusu kupata Katiba kukiwa na dhamira ya pekee ya kuhakikisha umoja, mshikamano na muunganmo vinabakia na kuimarika zaidi.

Dk Bilal alisema Serikali imejipanga vizuri na itahakikisha zoezi hilo linafanyika vema bila bughudha yoyote na kila mwananchi anapata haki ya kutoa maoni yake, kwa uwazi bila vizingiti vyovyote.

"Tunataka kubakia taifa ambalo linasimamia uhuru, haki na misingi ya kutafuta usawa kwa kila mwananchi. Tunataka kubakia taifa linaloheshimu utu, kuenzi ubinadamu na kuthamini ujenzi wa taifa lisilofungamana na matabaka,"alisema Dk Bilal.

Makamu wa Rais alisema kazi ya kuandika Katiba mpya ni lazima ifanyike kwa umakini, kwa uangalifu na kwa weledi mkubwa kwa kuwa taifa linapaswa kubaki linalokuwa kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Tangu kuanza kwa mjadala kuhusu muswada huo, wabunge wote wa Chadema akiungwa mkono na baadhi ya wabunge wa NCCR- Mageuizi hawakuwahi kushiriki kutokana na kile wanachodai kwamba kuingizwa kwake bungeni kulikiuka kanuni za Bunge na Sheria za nchi.

9.jpg
 
Hicho kinachojadiriwa DDM ni katiba ya Chama Cha Mapinduzi na sio Katiba ya WAtanganyika hata kidogo. Huwezi kusanya maoni ya Watanganyika mikoa mitatu halafu ukasema hayo ndo maoni ya Watanganyika juu wa muswada. CCM wanatupotezea wakati tu.
 
Kuanzia leo nimemdharau sana Dr Salim na Warioba yani wanajadiliana na mtu mhuni Dr Slaa ambae ana amini kupitia fujo na vurugu! Such a hopeless retired and an adultery Bishop!
 
Bilal anaongea tu ili aonekane hapingani na wataalamu. Lakini kiukweli hakuna kitu hapo.
 
Thursday, 17 November 2011 21:36

AONYA BILA MARIDHIANO NCHI ITAELEKEA KUBAYA, KITINE ADAI SERIKALI 'INATUPELEKAPEKA'

Boniface Meena

MJADALA wa Muswada wa Katiba Mpya umechukua sura mpya baada ya viongozi waandamizi wa Serikali wakiwamo wastaafu, kutaka upatikane mwafaka wa kitaifa kuhusu suala hilo vinginevyo taifa litaelekea kubaya.

Onyo la viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa , Dk Hassy Kitine, linakuja ikiwa ni siku chache baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutaka mwafaka huo wa kitaifa.

Jana, viongozi wakichangia maoni yao katika mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF), kuhusu nafasi na umuhimu wa katiba katika maisha ya Watanzania, kwa sehemu kubwa walipaza sauti kutaka mwafaka huo ili kunusuru taifa.

Kauli ya Dk Salim
Dk Salim ambaye ni mwenyekiti wa MNH, alisema ni muhimu kuwe na makubaliano na maafikiano katika suala la Katiba Mpya kwa CCM na Chadema.

Alisema, "Chama tawala na chama kikuu cha upinzani vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo".

Dk Salim alisema kwamba malumbano si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe yakasababisha nchi ikafika pabaya.

"Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifa,"alisema Dk Salim ambaye ana uzoefu na utatuzi wa migogoro ya kimataifa.

Alisema zoezi la Katiba ni zito na linatakiwa kufanyika kwa busara na kuwahusisha Watanzania wote.

"Kwa hali ya kisiasa hivi sasa ni lazima mjadala uwe wa nia njema lengo ni kuendeleza makubaliano na si kuhitilafiana. Tujenge na kuimarisha undugu na mishikamano wetu na kuonyesha uzalendo na uongozi madhubuti wa taifa letu,"alisema Dk Salim.

Kitine aionya Serikali
Kwa upande wake, Dk Kitine, alisema ni vizuri Serikali ikasoma alama za nyakati kutokana na hoja iliyoko bungeni kwa kuangalia suala hilo la katiba.

Dk Kitine alisema Serikali haitakiwi kuruhusu Muswada huo wa Marekebisho ya Katiba ukasomwa kwa mara ya pili, kwani tayari upinzani bungeni umekwishapinga.

"Serikali iutoe na kusoma upya, nchi haiko tayari kuona Serikali inavyotupeleka. Sasa ndiyo maana kuna matatizo kila sehemu,"alisema Dk Kitine.

Jaji Samatta
Kwa upande wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta alisema kuna baadhi ya wanasiasa hawaelewi maana ya katiba na kupotosha kuwa ni mapatano kati ya wananchi na viongozi."Katiba ikifutwa viongozi hakuna, hivyo Katiba ni moyo wa taifa,"alisema.

Jaji Samatta alisema kutunga Katiba ni kazi nzito na haiwezekani kila kitu anachokihitaji au kitu kinachohitajiwa na kundi fulani, kiwepo katika Katiba."Katiba ni makubaliano, lakini muda uliowekewa suala hili ni mchache,"alisema.

Alisema Katiba ya mwaka 1977 imefanya kazi nzuri, lakini ina matatizo mengi ndani yake, moja ikiwa ni dhana ya mfumo wa chama kimoja.

"Mfano Spika wa Bunge kuwa sehemu ya Halmashauri Kuu ya chama tawala, hapa atasababisha mgongano wa maslahi kwa kutetea chama chake,"alitoa kasoro hiyo.

Alisema kutokana na hali hiyo, Katiba Mpya ni lazima iwe na chachu ya upanuzi wa demokrasia na uboreshaji wa utawala wa sheria."Iwe ya mfumo wa vyama vingi na kuondokana na mfumo wa chama kimoja na iwe, inayoongozwa na wananchi,"alisema Jaji Samatta.

Dk Slaa atabiri Katiba mbovu
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema mchakato wa Katiba uikiwa mbovu Katiba yenyewe itakuwa mbovu.

"Wenzetu kule Dodoma wanapotosha kwamba kilichopo ni mchakato wanafikiri mchakato ni kitu kidogo, katiba ndiyo mzazi wa kila kitu hivyo kwa hali ilivyo katiba hii haiwezi kuwa ni ya wananchi badala yake Rais anajitengenezea Katiba yake,"alisema Dk Slaa.

Dk Bilal
Awali, akifungua mdahalo huo baada ya wachangiaji hao kutoa maoni yao, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal alisema nchi haiwezi kuwa na katiba nzuri ambayo itapatikana kwa kuliacha taifa likiwa vipande.

Alisema, ni muhimu kuhakikisha kunakuwepo majadiliano kuhusu kupata Katiba kukiwa na dhamira ya pekee ya kuhakikisha umoja, mshikamano na muunganmo vinabakia na kuimarika zaidi.

Dk Bilal alisema Serikali imejipanga vizuri na itahakikisha zoezi hilo linafanyika vema bila bughudha yoyote na kila mwananchi anapata haki ya kutoa maoni yake, kwa uwazi bila vizingiti vyovyote.

"Tunataka kubakia taifa ambalo linasimamia uhuru, haki na misingi ya kutafuta usawa kwa kila mwananchi. Tunataka kubakia taifa linaloheshimu utu, kuenzi ubinadamu na kuthamini ujenzi wa taifa lisilofungamana na matabaka,"alisema Dk Bilal.

Makamu wa Rais alisema kazi ya kuandika Katiba mpya ni lazima ifanyike kwa umakini, kwa uangalifu na kwa weledi mkubwa kwa kuwa taifa linapaswa kubaki linalokuwa kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Tangu kuanza kwa mjadala kuhusu muswada huo, wabunge wote wa Chadema akiungwa mkono na baadhi ya wabunge wa NCCR- Mageuizi hawakuwahi kushiriki kutokana na kile wanachodai kwamba kuingizwa kwake bungeni kulikiuka kanuni za Bunge na Sheria za nchi.

SOURCE: Mwananchi
 
CHADEMA sijui kama wamesoma na kuelewa maneno yayo ya watu wenye busara zao, wasomi na wenye uzoefu wa uongozi wa kitaifa na kimataifa. Nadhani CHADEMA wanaviongozi wanaopungukiwa kitu fulani. Uwezo wao unakosa ladha fulani ya maadili na uzoefu. Nawaona kama wanasiasa za KISHAMBA SHAMBA vile. Yaani , sijui nifafanue vipi hapa. Unajua hata mtu anapotoka kijijni na kuingia mjini anavyojifanya kujua mambo, wakati wanaomzunguka wanabaki kuaibika badala ya yeye kuaibika.

KATIBA NI YA WATANZANIA SI YA CHADEMA na CCM. Kamwe hatuwezi kuwa na Katika ambayo mwisho wa siku itabatizwa jina la KATIBA YA CHADEMA YA MWAKA FULANI. Huu utakuwa ni upuuzi hasa kwa kizazi ambacho tumeshuhudia mbinu wanazotumia CHADEMA za kuwapotosha wananchi kwamba Musuada ukishapita bungeni basi itakuwa ndiyo mwisho wake na kitakachofuata ni kuandikwa kwa katiba hiyo. BINAFSI nisingependa kuishi katika nchi inayoongozwa na katiba ya aina hiyo.
 
wana ccm wanajaribu kufanya marekebisho ya watanzania katika kufikiri. Sijui kama elimu inafaa kutolewa kwa nguvu kiasi hicho na kwa ushabiki usiona tija kwa mwananchi wa kawaida.
Kipindi hiki mpaka wataachia tu.
 
HAHAHAHAHAH UMEnikumbusha pale lowassa alipoenda kuwasihi chadema wasitoke nje wakati mshikaji wake jk akizindua bunge.....mh mbowe alimsikiliza weeee baadae akamuuliza "mheshimiwa lowasa, umetumwa au umekuja wewe kama wewe?"
..Baada ya Mh. Lowassa kuulizwa hivyo, akajibu Nini?
 
04.jpg

Dr. Slaa, Dr. Salim na Warioba wakijadilliana matatizo ya
kisiasa kwa pamoja siku za karibuni

Tofauti za kiitikadi hazisuluhishwi kwa nguvu ya mabomu na mitutu ya bunduki, kukaa pamoja na kufikia muafaka kwa manufaa ya Taifa letu ndio dawa pekee.

Katika kikao hiki cha Dr. Slaa, Dr. Salim na Waziri Mstaafu Warioba walitafakari na kukubaliana na hoja za msingi katika uundwaji wa katiba mpya, baada ya kikao hicho kwa nafasi tofauti walitoa matamko yenye kutoegemea upande wo wote, ila ushauri kwa serikali na CCM kukaa pamoja na wapinzani kupata suluhisho la matatizo.

Serikali inachukuliaje ushauri na uzoefu wa hawa watu mahiri katika mambo ya kitaifa na kimataifa?
 
Back
Top Bottom