KATIBA: Salim, Warioba wakutana na Dr. Slaa

Hahahah... Nimependa hiyo.. Itakuwa bomba sana tuje tujue walimaliza huo mjadala kivipi.
 
sidhani kama salim na warioba wana influence kwenye ccm ya sasa yenye historical politicians kama stella manyanya, pindi chana, william ngejela, anne killango, john komba, mwigulu, rosemary kirigini, shyrose bhanji, chenge, dewji, na nape
Mkuu MTM nimelilia hili muda mrefu kuwa tunao wazee wanaoheshimika sana,hata kama Ccm hawawaheshimu wengine bado tunawaheshimu lakini tunawataka wasiishi historia bali kwavile wapo hai lazima waendelee na mapambano bila upendeleo! hawa wakisema watasikilizwa! Tatizo ni waoga sana wanauma na kupuliza!
 
Hao ni CCM kwa jina! Hawa ni watu wenye akili zao timamu na wana busara; lakini ma CCM yenyewe yenye kufuata bendera kama upepo hayako tayari kuweka mjadala mezani ili ukweli ujulikane.
 
Ikifika wakati licha ya uduni wetu ndani ya chama, maisha ya kawaida ya wajuva jasho, na nitakuwa bado kijana wa makamo by then inshaalah tutajitokeza hapa ndani kwa majina yetu, barabarani kumsihi na kumuomba dkt. Salim atusaidie japo kwa 5yrs kisha atuache salama...... Naamini ndie mbadala sahihi wa jakaya.

Akiwa nje ya ccm sawa, lakini ndani ya ccm no, ccm ni tatizo number moja hata kama aje nani kwa ticket ya ccm ni janga la kitaifa tusifanye makosa hayo.
 
huyu kombani apelekwe wizara ya masoko na mbogamboga wakati huu wa mchakato wa katika...hawezi kujibu hoja hata kidogo..anaongea huku anatetemeka anaogopa maswali kama mtoto bwana....atupishe hapa
 
Maskini wale wacheza mduara kule bungeni wanatoa vijembe hawajui huku wazee wanatafuta suluhu! wangejua ingewasaidia kuwa si mepesi kama taarab wanayocheza mjengoni na Dj Ann
 
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki hawa wenye uzalendo na tanzania na vitu vyote vilivyomo na wazalendo wote.walaani wote wanao kwenda kinyume na mapenzi ya hawa watatu, kwani wanamapenzi na nchi hii.

Mbariki Dr Slaa kwani tunaamini amesimama kwa niaba ya watanzania wote wapenda haki.
 
hapo sasa utawasikia sijui wataendelea na kushabikia pumba zao! hapa leo angekuwepo Nyerere nahisi wabunge wote leo wa ccm wangekosa ajira kwa muda. yaani wapo kama watoto vile
 
Si walikuwa wanajidai wababe? Ngoja tuwakomeshe maanda hayati Prof. Mushi alisema duniani Ccm tu ndio chama cha kisiasa kinachotegemea nguvu ya dola badala ya sera! Mfa maji haachi kutapatapa. Tusubirie tujue Dr wa ukweli kawambia nini
 
Nilishangaa sana kuwa CCM ni chama kikongwe jee kinakosa watu wachache wenye uelewa wa mambo?kumbe bado wapo ila wamekaa pembeni hawajishughulishi na ujinga ufanywao kila siku na watendaji
Kuna mambo huwa wana ambiwa ni ya binafsi ndiyo maana wako pembeni....
 
Back
Top Bottom