Elections 2010 Katiba nzuri Kuandikwa ni baada ya CCM kutoka madarakani?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Celina%20Kombani(3).jpg

- Wasomi wataka maelezo ya serikali
- Wapinga masharti ya baadhi ya vifungu

Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, amepatwa na wakati mgumu kujibu maswali ya wasomi na wanazuoni wa chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) kilichopo mkoani Iringa baada ya kutakiwa kuweka wazi ni kwa nini serikali ilizuia masuala muhimu kutojadiliwa wakati wa mchakato wa Katiba Mpya.​

Wasomi hao wanapinga makatazo yaliyomo katika kifungu cha 9 (2) ya sheria ya marejeo ya katiba ya mwaka 2011; kifungu ambacho kinakataza kutojadiliwa masuala yanayohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mamlaka ya ya urais na mapinduzi ya Zanzibar. Mambo mengine yanayokatazwa ni pamoja na masuala yanayohusiana na chaguzi za kidemokrasia, haki za binadamu na uhuru wa mahakama.

Wasomi hao walikuwa wakichangia mada katika kongamano la katiba lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria wa chuo Kikuu kishiriki cha mtakatifu Augustino mkoani Iringa (Ruco)................

Kwa mujibu wa Waziri Kombani, tume itakayoundwa kukusanya maoni ya wananchi itakuwa na wajumbe 30 lakini haitajumuisha wanasiasa kutoka vyama mbalimbali kama ambavyo umma umekuwa ukijaribu kupendekeza.

“Wasomi wangu nawaombeni sana mbadili mindset (fikra zenu) kuhusu utaratibu unaotumika, tayari tumeshaandika sheria hiyo ya muswada wa marejeo ya katiba kwa version mbili, moja ni ya Kiswahili na nyingine ni ya Kiingereza…lakini pia Rais amepewa mamlaka ya kuunda tume hiyo katika sura ya 32 ya katiba yetu ya Jamhuri tunayoitumia sasa,” alisema.

Source: Nipashe Jumapili
 
Serikali ya CCM imeshupalia suala la katiba kubaki mikononi mwao, na katu kutowahusisha wanasiasa wengine. Pia watakaoshughulikia Katiba ni wale watakaochaguliwa na Rais wa CCM, hapo tutazamie katiba tunayoitaka au ni usanii wa kubaki na katiba hii hii kwa sura mpya?
 
..CCM hawataki katiba mpya wanajua kabisa itawaondoa madarakani. Ni juu yetu sisi wananchi kuidai kwa NGUVU MOJA!
 
Celina%20Kombani(3).jpg

Kwa mujibu wa Waziri Kombani, tume itakayoundwa kukusanya maoni ya wananchi itakuwa na wajumbe 30 lakini haitajumuisha wanasiasa kutoka vyama mbalimbali kama ambavyo umma umekuwa ukijaribu kupendekeza.

"Wasomi wangu nawaombeni sana mbadili mindset (fikra zenu) kuhusu utaratibu unaotumika, tayari tumeshaandika sheria hiyo ya muswada wa marejeo ya katiba kwa version mbili, moja ni ya Kiswahili na nyingine ni ya Kiingereza…lakini pia Rais amepewa mamlaka ya kuunda tume hiyo katika sura ya 32 ya katiba yetu ya Jamhuri tunayoitumia sasa," alisema.

Source: Nipashe Jumapili

Kwa hoja hiyo ya waziri wa Katiba, serikali inaendelea na jitihada za kuteka hoja ya wananchi kujiamulia juu ya utaratibu wa kutunga katiba yao.
 
Back
Top Bottom