Katiba nzuri katika nchi za Afrika haina au ina msaada mdogo sana wa kuleta ustawi wa wananchi

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,495
2,043
Kwa yaliyotokea Africa Kusini wananchi kutoka barabarani na kuzua vurugu kubwa dhidi ya uamuzi wa kisheria na kikatiba wa kumuweka ndani Rais Mstaafu, ni dhahiri kwamba bado hatujakomaa kidemokrasia.

Jambo lingine limetokea kule Kenya siku chache zilizopita ambapo Rais wa nchi hiyo aliongoza kampeni ambayo inaenda kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Haya mataifa mawili yanatajwa kama vinara wa katiba Bora Afrika. Ikiwa hakuna utashi wa kuiheshimu katiba kwa haya mataifa yetu bado katiba nzuri haina msaada wowote wa maana.

Binafsi naamini mambo yatabadilika lakini lazima kizazi hiki cha miungu watu wanaoweza kuingilia mhimili wowote bila haya wala bila kujali kifutike kije kizazi cha wastaaraba walio radhi kuheshim mipaka ya mamlaka yao.

Jambo lingine linalonivunja moyo ni kwamba uandishi wa katiba kwa sehemu kubwa unahusiaha utashi wa kisiasa, kwa jinsi hali ilivyo sasa hatuwezi kupata katiba bora kwa kua kati ya wajumbe watakaoteuliwa kuunda bunge la katiba bado ccm watatoa namba inayozidi makundi mengine hivyo kunufaika na kura ya kupitisha vifungu inavyovitaka.
 
Kwa maelezo ya Diallo muhimu ni kufanya vetting Ili kuepuka kuongozwa na vichaa au madikteta Afrika. Katiba yaweza kuwa nzuri shida ni mtu.
Watu ndilo tatizo kuu.
Ni lazima kujenga uelewa wa wananchi kwanza.
Raia wenye tabia kama za mbwa, kujipendekeza na kusifia watawala hata kama wamefanya maamuzi ya hovyo hawafai.
Lazima kuwe na raia wanaojielewa.
Wakati mwingine elimu ya kufanya genetic upgrade ya jamii ifanyike.
Watu waambiwe waoe na kuolewa na wenye fikra chanya badala ya majuha kwa majuha.
Pili, wasichaguliwe wale wanaojipendekeza.
 
Back
Top Bottom