Katiba, Nchi gani Dunia hii iliyowahi kubadilisha kwa hiari?

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,402
8,891
Sijawahi kusikia hata siku moja Katiba ikiombwa, Katiba hushinikizwa au kulazimishwa kama ukipenda na sababu ni moja wale wanaotaka Katiba mpya wana nia ya kuingia madarakani ambapo kwa Katiba iliyopo wanaona hawana chance, wale waliokuwa na power ambao ni wanufaika wa Katiba iliyopo hawawezi kukubali kuibadilisha kwa maana iko upande wao.

Na huo ni ukweli uko Dunia nzima, hivyo mnaoomba Katiba mpya Tanzania mtasubiri mpaka Yesu arudi sana sana CCM watabadilisha hapa na pale kuwafurahisha lakini kiini hawatokigusa.

Chagueni aidha mlazimishe au ingieni tu kundini!
 
Back
Top Bottom