Katiba mpya

George Jinasa

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
395
225
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na hoja toka miongoni mwa watanzania kwamba kutokana na mabadiliko mengi ya msingi yaliyotokea toka mwaka 1977 Katiba ya sasa ilipotungwa hadi leo kuna haja ya kuwa na Katiba mpya ambayo uundwaji wake utawashilikisha watanzania wote. Baadhi ya mabadiliko ya msingi wanayoyazungumzia ni pamoja na mabadiliko ya mfumo mzima wa kisiasa na uchumi kutoka ule wa Ujamaa na Kujitegemea uliokuwa umejengwa katika msingi wa Azimio la Arusha na na mfumo wa chama kimoja kwenda katika mfumo wa soko huria ulio na muelekeo wa kibepari chini ya mfumo wa vyama vingi.

Kwa kuwa katiba kama ilivyo sheria zingine ni zao la jamii, mfumo wa ujamaa na kujitegemea chini ya chama kimoja ulikuwa na mchango mkubwa katika uundwaji wa katiba ya mwaka 1977. Wakati tunaingia katika mfumo wa vyama vingi Tume ya Nyalali ililiona hili na kupendekeza mabadiliko makubwa katika Katiba. Suala kubwa lililoibuka wakati huo (nadhani hadi sasa bado lipo) ni namna gani katiba mpya itapatikana. Itakuwa ni kwa kufuta katiba iliyopo na kuunda katiba mpya kama Waganda na Wakenya walivyofanya au kufanya marekebisho ya msingi ya Katiba na kuundoa mapungufu yaliyomo kama tulivyojaribu kufanya katika Marekebisho ya 8 ya Katiba na hatimaye ya 9 hadi kumi na mbili?

Kwa utangulizi huu nilioutoa ningeomba wananchi tujadili kwa kuongozwa na dondoo zifuatazo:-

1. Katiba mpya ije kwa kufutwa iliyopo na kutungwa nyingine au kuifanyia katiba iliyopo marekebisho ya msingi kuondoa dosari zote. ( Kadili jibu litakavyokuwa sababu ni mhimu)

2. Ni mapungufu gani ya msingi kwa sasa yaliyomo katika katiba na tungependa yarekebishwe vipi?

3. Katika mabadiliko ya katiba tunayoyataka kuna mafundisho yoyote tunayoweza kuyapata kutokana na uzoefu wa jirani zetu wa Kenya na Uganda?

4. Ni njia zipi na kwanini tuzitumie kupata katiba mpya.

NB Ningewaomba wachangia tujenge hoja kwa lugha ya kistaarabu na kuvumiliana. Lengo la majadiliano yetu iwe na kujenga zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom