Katiba mpya

Tunko

Senior Member
Dec 24, 2013
181
41
Tayari rasimu ya pili ya katiba imesha toka na Rais amesha kabidhiwa tayari,kwa ajili ya kuandaa bunge la katiba mapema katikati ya mwezi huu lakini tayari vyama vya siasa vimeshaanza kuuteka mchakato mzima wa katiba .Kwa upande wa CCM tayari wameshatoa tamko kwamba watuludia tena kuangalia kipengele kwa kipengele mapendekezo ya rasimu ya katiba yaliotoka hata hivyo kwa upande wa Zanzibar CCM wamesema hawakubaliani na mfumo wa serikali tatu kama rasimu ilivyopendekezwa na wamesema wanandaa mandamano makubwa kupinga kipengele hicho, Na vyama vingine navyo vimeshaanza kupinga mambo yaliyomo kwenye katiba na bado vitapingana vyenyewe kwa vyenyewe sasa huo si ndio mwanzo wa kuharibu mchakato wa katiba?,na katiba ambayo itapatikana si itakuwa kwa maslahi ya vyama kuliko wananchi?.JE,ni nini kifanyike ili wanasiasa wasituharibie katiba yetu.Nawasilisha
 
Back
Top Bottom