Katiba Mpya yaja, somo la awamu ya tano linatosha

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,406
Katiba mpya itaundwa tu.

Utawala wa awamu ya 5 ndiyo umeleta chachu na hamu ya uhitaji wa kuundwa kwa Katiba mpya. Kila kundi katika jamii linahitaji Katiba mpya. Wanaccm, Wapinzani, Wanaharakati, n.k.

Wananchi wa makundi mengi katika jamii hawakufurahishwa na mwenendo wa mwendazake lakini hawakuwa na namna ya kumdhibiti kwasabb Katiba hii mbovu inampa rais umungu Mtu. Ninaamini wasingependa kuona hali hii inajirudia tena. Hivyo hata wao wanataka Katiba mpya.

Katiba mpya yaja bandugu, maana hakuna kundi ambalo halikuonja machungu ya mwendazake.

Hata U-turn ya maamuzi, maoni na mitazamo ya viongozi waandamizi katika Serikali ni ushahidi tosha kuwa kila Mtu alikuwa anaburuzwa na mwendazake.

Nawahakikishia katiba mpya yaja.
 
Katiba mpya itaundwa tu. Utawala wa awamu ya 5 ndiyo umeleta chachu na hamu ya uhitaji wa kuundwa kwa katiba mpya. Kila kundi ktk jamii linahitaji katiba mpya....wanaccm, wapinzani, wanaharakati, n.k...
Uwepo wa Katiba na uzingatiaje wake ni vitu viwili tofauti. Je km katiba mpya itakanyagwa utafanya nini? Kuna haja kwanza kujenga utamaduni wa kuheshimu katiba, sheria na kanuni hata bila ya uwepo wa mapitio ya katiba ya sasa.
 
Katiba mpya itaundwa tu. Utawala wa awamu ya 5 ndiyo umeleta chachu na hamu ya uhitaji wa kuundwa kwa katiba mpya. Kila kundi ktk jamii linahitaji katiba mpya....wanaccm, wapinzani, wanaharakati, n.k...
Hata ikija kama kule mjengoni ataendelea kuwepo empty head ataichambia tu!!
 
Kwani katiba mpya itakuwa ya chadema tu?

Watanzania tuna tatizo gani jamani duuuh!
Mtaka katiba ipi? Ile ya Sita?
Mgedai ile rasimu ya Warioba ninge waelewa maana ilipendekeza ukomo wa wabunge.
Hapo ndo mwisho wa watawala wa milele kama Mbowe.
 
Katiba mpya itaundwa tu.

Utawala wa awamu ya 5 ndiyo umeleta chachu na hamu ya uhitaji wa kuundwa kwa Katiba mpya. Kila kundi katika jamii linahitaji Katiba mpya. Wanaccm, Wapinzani, Wanaharakati, n.k...
Mama akitaka aheshimike na aache legacy basi aendeleze mchakato uliokufa 2014 wa katiba ya wananchi! Tunaweza hata ongeza kipengele kwenye katiba cha kumfanya 'yeye tu' awe kiongozi wa tz wa maisha!

Wananchi tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, akifanya hivyo hata mimi nitaacha kazi yangu nikachukue kadi ya kijani
 
Katiba mpya itaundwa tu.

Utawala wa awamu ya 5 ndiyo umeleta chachu na hamu ya uhitaji wa kuundwa kwa Katiba mpya. Kila kundi katika jamii linahitaji Katiba mpya. Wanaccm, Wapinzani, Wanaharakati, n.k.

Wananchi wa makundi mengi katika jamii hawakufurahishwa na mwenendo wa mwendazake lakini hawakuwa na namna ya kumdhibiti kwasabb Katiba hii mbovu inampa rais umungu Mtu. Ninaamini wasingependa kuona hali hii inajirudia tena. Hivyo hata wao wanataka Katiba mpya.

Katiba mpya yaja bandugu, maana hakuna kundi ambalo halikuonja machungu ya mwendazake.

Hata U-turn ya maamuzi, maoni na mitazamo ya viongozi waandamizi katika Serikali ni ushahidi tosha kuwa kila Mtu alikuwa anaburuzwa na mwendazake.

Nawahakikishia katiba mpya yaja.
Yule alikuwa shetani kabisa
 
Back
Top Bottom