Katiba mpya ya wananchi ndiyo suluhisho na dawa pekee kwa matatizo yote

bridalmask

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
2,195
1,167
Kwanza kabisa nimshukuru Mwenye Mungu na mwenye wingi wa Rehema kwa kunipa afya njema na uzima katika siku hii tena, na ninawasalimu nyote wana JF pamoja na Watz. Wote kwa Ujumla.

Ndugu zangu kama sote kweli tunaipenda nchi yetu na ni Wazalendo wa kweli pasipo kujadili Itikadi zetu na mengineyo yote, ni kweli na nishairi kuwa PASIPO KATIBA MPYA YA WANANCHI bado tutakuwa tunadanganyana katika masuala YOTE YALE YAWE YA KIUCHUMI,KISIASA,KIJAMII,KIUTAMADUNI N.K.

Hata tumpate kiongozi gani atakaye ingia madarakani awe UKAWA au CCM kwa maoni yangu bado hakuna jipya pasipo katiba MPYA.

Yaani tusipapase chochote kile pasipo kuwa na katiba mpya kwani tutakuwa tunapoteza bure muda na rasilimali zetu.

Na yale matatizo tuliyonayo ya UJINGA,UMASIKINI, MARADHI,UFISDI kamwe hayata kwisha.

Binafsi ningelipenda kuona tunapata KATIBA MPYA itakayo kuwa na mambo yafuatayo;

1. Kuwa na Tume huru ya Uchaguzi.

2. Rais kupunguziwa madaraka ya Uteuzi kama vile: Uteuzi wa Majaji na Majaji Wakuu,Uteuzi wa Tume ya Uchaguzi n.k.

3. Rais kuondolewa Kinga ili tuweze kutathiminiwa na Mahakama amalizapo muda wa Uongozi wake na kuwajibika kisawasawa pale alipoliingiza Taifa au kulisababishia Hasara.Kama hakutimiza na hadi zake alizo zitoa.

4. Kuhojiwa kwa Matokeo ya Urais Mahakamani.

5. Kutenganisha Wanasiasa na Serikali kama Vile Mbunge kutokuwa Waziri ili aweze kuisimamia Serikali vizuri.

6. Kuwa na Kikomo cha Uongozi, na kupeuka Forever Living Leaders.

7. Mbunge Kuwajibika na Kuwajibishwa na Wananchi wake.

8. Kufuta nafasi za ZOTE za Uongozi zisizo na Tija na maslahi kwa Taifa kama vile uDC ambao ni mzigo kwa Taifa kwa kuongeza gharama za uendeshaji wa Serikali na Kuumiza wananchi kwa kodi zao kutumika bure.n.k.

9. Adhabu kwa viongozi ziwe wazi na kubainika pindi kiongozi anapofanya makosa yatakayo ligharimu Taifa afanywe nini, mfano Ufisadi….na ikithibitishwa na Mahakama Afungwe na Kufilisiwa Mali zake zote pamoja na Familia yake yote,Ndugu Jamaa,na Marafiki WOTE kama wamehusika, Kifungo cha gerezani+Viboko na Kufilisiwa au afanywe nini zaidi pasipo kukwepa niliyo yataja..

10. Kufuta nafasi za Uteuzi wa Wabunge ili kuondoa ofa ofa na upendeleo pia..

Wana JF wenzangu ninaomba tutoe mchango juu ya Mada Tajwa pasipo kujali ITIKADI ZETU na tukumbuke kuwa kila mmoja wetu atatoa hesabu yake baadaye hivyo pia tuepuke unafiki,nimeona nitoe yangu ya Moyoni.

Zaidi tuongeze Mengineyo…… kwani iko siku lazima tuipate Katiba MPYA na hata kama si kizazi chetu kitafanya MABADILIKO hata kijacho wasije chapa makaburi yetu kwa kutuona hatukuwa na FAIDA enzi za uhai wetu.

Bora tuseme wajue tulisema ikashindikana, kuliko kukaa kimya tukaja pata adhabu ya Wanadamu naya Mungu pia.
 
Katiba iliyopo waijua? hadi utake mpya?
 
Katiba ilishaharibiwa wataalamu wakaweka vipengele vinavyowalinda ili waendelee kuwakamua wananch wa nchi ya kufikirika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom