Katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by C.T.U, Nov 30, 2011.

 1. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  wakuu habari zenu
  mimi sio mfuatiliaji sana na masuala ya siasa ila nimekuwa ni mfuatiliaji wa vyombo vya habari ni muda sasa nimekuwa nikisikia haya mambo ya katiba well am sure yeyote ambaye amependekeza masuala ya katiba ana malengo mema na nchi yetu fine...
  katika utawala bora ila sasa tatizo linakuja hapa...
  wengi wetu katiba hatuijui kwanini nasema wengi wetu?
  tunaofanya nao kazi hapa asilmia 95 hawajawahi kuisoma katiba (kwa kuwa mimi sio mtaalamu wa mambo ya siasa nikasema labda hatujafuatilia)
  nikafanya kiji research kwa majirani zangu wakasema hawaijui , siku moja nimekaa na marafiki tunapata moja moto moja baridi nilizungumzia suala la katika wakaniambia katiba hii ya sasa hivi hawaijui hata ikiandikwa mpya hawajui imebadilishwa wapi?? n.k
  picha hiyo inanionyesha kuna kundi la mamilioni ya watanzania hawaijui katiba ya nchi yao mimi nilipata kusoma nchi fulani ya Asia hiyo nchi lazima ufundishwe katiba ya nchi yao kama somo la darasani
  sasa swali langu ni hivi ni mimi tu ambaye niko nyuma ya watanzania kuwa sijui katiba ya nchi yangu (sijawahi hata isoma ) ila najua baadhi ya vipengele katika katiba kiubishi bishi (vinavyohusiana na kazi yangu coz tunakutana nayo kwenye mikataba yetu ya kazi)
  au kuna wanaojua??
  mimi nimesikia malalamiko kwa watu wengi kuwa hawajui katiba yao , hawajawahi hata kuiona wengine hawajui inafananaje n.k
  sasa mimi hapa nazidi kupata wasi wasi wa kwetu kwamba kuna kundi kubwa la watanzania hawaijui katiba ya nchi yao je serikali imefanya hatua gani katika kuhakikisha angalau tunaijua katiba yetu ...
  labda sisi sio wapembuzi na wachambuzi wa mambo, labda sisi sio werevu wa kuchangamsha bongo lala zetu
  swali langu je serikali imeweka hatua gani katika kuhakikisha watu kama sisi ambao hatuna hata na habari ya katiba angalau tujue ni nini kinaendelea katika katiba inawezekana kabisa mimi ni Sungura mjanja nimepata fikra na kujitambua so nitatumia akili yangu katika kuijua katiba ya nchi yangu kwa kuumiza ubongo katika kuijua hii kitu ila kuna kundi la watu liko nyuma yangu mbele yao wanaona kiza hawajitambui na wala hawana mpango wa kuijua katiba yao sio leo wala kesho
  NAWASILISHA
   
Loading...