KATIBA MPYA: WAKRISTO wataka MCHINJIO YAO... Hawataki Kukamatwa wakichinja Mifugo yao...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
kijamii kama za afya(mawasiliano mazuri) picha na Dinna Maningo
Na Fredy Azzah

Posted Alhamisi,Novemba22 2012 saa 8:28 AM

Kwa ufupi

"Katiba ikubali kuwa waumini wachinje wanyama wao, tofauti na kuwa kwamba machinjio yote yameshikwa na watu wa dini moja tu," alisema Iswambula Kiswaga mkazi wa kata ya Kalemela

Simiyu

BAADHI ya wananchi wa Wilaya ya Busega wametaka kuwepo na machinjio ya Wakristo peke yao kwani hivi sasa wanapa shida wanapochinja mifugo yao ambayo wakati mwingine hukamatwa.

Wakitoa maoni kwenye kata mbalimbali juu ya uandikwaji wa Katiba mpya, walisema kutoka na kutokuwepo kwa machinjio ya Wakristo, baadhi ya maduka ya nyama yamekuwa yakichomwa kutokana na kudhaniwa yanauza nyama ambazo mifugo yake ilichichwa na Wakristo.

"Katiba ikubali kuwa waumini wachinje wanyama wao, tofauti na kuwa kwamba machinjio yote yameshikwa na watu wa dini moja tu," alisema Iswambula Kiswaga mkazi wa kata ya Kalemela

Pia alisema kuwa, katiba hiyo ianishe siku ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali ambapo siku hizo zisiwe zile za kuabudu.

"Uchaguzi uwe unafanyika kati ya siku ya Jumatatu, Jumanne, Jumatano au Alhamisi jambo analosema litaongeza idadi ya watu wanaopiga kura, tofauti na sasa ambapo maelfu wanajitokeza kujiandikisha lakini siku ya kupiga kura ya wanajitokeza wachache.

Naye Enock Kindika, alisema kuwa Rais apunguziwe muda wa kutawala, awe na vipindi viwili vya miaka miwili na siyo vipindi viwili vya miaka mitano.

Anasema kuwa, kwa muda uliopo sasa unawafanya wananchi wateseke kama walifanya makosa katika kumchagua kiongozi huyo wa nchi.

Kwa upande wa Musa Simba (18), mkazi wa Kalemela, alisema kuwa idadi ya wabunge ipunguzwe, na pia kuwafuta wabunge wa kuteuliwa na Viti Maalumu kwa kile alichosema kazi yao haionekani.

"Hata vyama vipunguzwe, tuwe na vyama viwili tu vitakavyoshindana kwenye uchaguzi," alisema.

Haya... Sasa KILA kitu KITAOMBWA kubaguliwa... SUBIRINI ITAKUJA kuwa MIKAHAWA...

Walimuona NYERERE MPUMBAVU... MWINYI akaja na UHURU KUPITA Kiasi wa DINI... MWINYI Kazipa NGUVU DINI NDANI ya SERIKALI na NJE>>>

Tusubiri Tutaanza kulia NGONJA hao VIJANA waliozaliwa Baada ya UTAWALA wa MWINYI wakue
Waliishi kwa RUKSA...
 
wabongo kweli tuna akili.yaani tulichoona cha kuandika kwenye katiba ni machinjio! kweli sisi ni kiboko yao!
 
wabongo kweli tuna akili.yaani tulichoona cha kuandika kwenye katiba ni machinjio! kweli sisi ni kiboko yao!

Waandishi NI HURU na Haujui Wanachokiandika LEO ... KESHO MATOKEO YAKE Yatakuwa NINI...

Tulikuwa hatuna MACHINJIO ya WAKRISTO - Mpaka UTAWALA wa MZEE MWINYI; Kubaguana kukaanza... NGUO za kuficha SURA
 
Waandishi NI HURU na Haujui Wanachokiandika LEO ... KESHO MATOKEO YAKE Yatakuwa NINI...

Tulikuwa hatuna MACHINJIO ya WAKRISTO - Mpaka UTAWALA wa MZEE MWINYI; Kubaguana kukaanza... NGUO za kuficha SURA
ujue tatizo ni kufanya mambo kwa kuongozwa na ntimanyongo badala ya nia njema na sababu za msingi zenye malengo chanya.halafu pia kutotumia akili katika kuyafikia tunayoyataka.hivi hata kama tunataka machinjio ya wakristo,hivi hilo ni suala la kikatiba kweli?
 
Katiba NI CHOMBO cha HAKI kwa Wananchi bila DINI; UKABILA sasa Kama Huyo MTOA MAONI kanona hilo ni KERO? Katiba lazima isema kuhusu MACHINJIO sababu ya NCHI yetu kuwa na DINI MBALIMBALI na kuondoa UGOMVI KATIBA NDIO CHOMBO PEKEE CHA KULITATUA...

Mfano Rais MWNYI Kuruhusu USAWA wa KUABUDU na watanzani kwakaanza kuvaa Nguo za KUJIFICHA...
 
KATIBA MPYA!;

Waislam waachiwe kufuata baraza, taasisi, mfuasi yoyote wanaemtaka, sio lazima BAKWATA
 
jamani machinjio tena, 2tasema na barabara sasa. Ndo maana kuna sheria nyingi nyuma ya katiba. Ilo c jambo la kuwekwa ktk katiba. Kama lawezekana wabunge waliweke ktk sheria ihusianayo na mambo ya mifugo au machinjio.
 
lini tanzania itatumia nembo ya HALAL FOOD kama ile ya TBS?wenzetu kenya huweka ktk packed food.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom