Katiba mpya: Waislam watoa madai mazito Mwanza yawekwe kwenye katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya: Waislam watoa madai mazito Mwanza yawekwe kwenye katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Return Of Undertaker, Jul 7, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,367
  Likes Received: 8,369
  Trophy Points: 280
  Source gazeti la mzawa

  Katika kuelekea kupata katiba mpya waumini wa dini ya kiislam jijini mwanza wamesema katika kutoa maoni ya katiba mpya kwa mambo ambayo yanahusu dini ya kiislam mambo yafuatayo lazima yaanguzwe katika katiba ili kulinda na kutetea haki za waislam kwa ujumla;

  1. Mahakama ya kadhi iwe kisheria na serikali igharamie shughuri zote.

  2. Tanzania kujiunga na jumuiya ya kiislam ya OIC

  3. Kuwapo kwa vyama vya kisiasa vya kidini
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  hapo namba tatu, badilisheni katiba,itambue kuwa tanzania nchi ya kidini
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mna matatizo sana na hamuelewi na mnashindwa kujua maana ya maoni ,hivi hamuelewi kuwa mtu au watu kikundi au chama kinaweza kutoa maoni ya aina yeyote kutaka yawemo ndani ya katiba ?

  Hivi wa dini zingine mmekataliwa kutoa maoni ? Msitangulize meno mbele yatang'olewa.
   
 4. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,306
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Wallah waislam wenzangu mnanipa taabu kufikiria mnavyofikiria. Au ndo ukweli kuwa serikali legelege?
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Watu wachache ambao amzidi million 10 hamuwezi kuangaisha serikali kihasi hiki.

  Mwisho mtataka hata mwezi wa ramadhani serikali iwagharamie.
   
 6. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 331
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Nakumbuka niliwah kusoma mahali that watu wameuana sana kwa sababu ya pesa au madaraka, but watu wameuana zaidi because of faith.
  wapendwa tusiache dini, ambazo nying zimekuja na meli zituponze, pia tuheshimu maoni ya watu
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Return Of Undertaker

  Haya ndiyo madai mazito siku yakitolewa madai mazito utaandika nini ?.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bora Wahame nchi tu wafate wenzao wenye akili hizo,
   
 9. knaan

  knaan Senior Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Uislam ndo dini ya haki.na mwenyezi mungu amesema ndani ya qurain kuwa ndiyo dini anayotambua.chonde chonde achane utani na uislam.
   
 10. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  wacha kuweka upuuzi wako..hapa kwa heading kubwa bila ya source ya habari yenyewe.
  kuwangangania kwa chuki waislam ...tutabaki hivyo hivyo mambo muhimu yanayoleta umaskini nchii hayataondoka kwa kushabikia udini.
  waislam kama walivo wakristo na wengineo wanayo haki ya kuchangia upatikanaji wa katiba mpya.

  kila kundi lina mlengo yake lakini mwisho wa yote lengo ni kupatikana katiba ambayo lengo kubwa litakuwa
  • kulinda haki za raia wote bila ya kubagua kwa misingi ya dini,ukabila,ukanda ama rangi au jinsia.na kuwa serikali itakuwa mwajiri wa bila ya ubaguzi
  • haki ya kuabudu italindwa ndani ya katiba na mengineyo
  kuna mengi ambayo waislam wamesema ili katiba ilinde haki za raia wake na kutoa fursa sawa basi yanapaswa kuwemo ndani ya katiba mfano
  • suala la kurejesha mahkama ya kadhi -suala hili linahusu ndoa za waislam inajulikana wazi waislam wana sheria zao za ndoa na ilii mashauri yao ndoa na mirathi yapate uhalali wa kisheria basi ni lazima kuwepo na mahakama inayotambiliwa kisheria sio suala la udini.ni kustahamiliana katika jamii hii ambayo makundi haya mawili yanakurubiana kwa wingi na maingiliano.wengi ya makundi ya wakristo waliobatizwa miaka ya 60 na 70 basi familia zao ni mchanganyiko wa dini hizi..
  • suala la kadhi lina kuzwa sana na viongozi wa makanisa kuliko uhalisia wake..hili kwa vile ni lazima katika maisha ya muislam basi tustahamiliane na hili sio lazima liwemondani ya katiba lakini sheria inaweza kutongwa kuanzisha mahakama hii. na ukweli halihusu watu wengine bali kazi yake ni mashauri ya ndoa ya kiislam.
  • kama katiba lengo lake ni kuleta usawa basi sheria zote kandamizi au zile sheria ambazo zimeletwa kwetu kwa malengo maaulum ya kuwa kandamiza makundi fulani ndani ya nchi..mfano wa hapa ni sheria ya Ugaidi...hii sheria imeletwa kwa lengo la kuwakandamiza waislam.ndani ya katiba mpya hii lazima iondoke
  • japo serikali haina dini lakini itambue raia wake ni waumin wa dini tofauti , hivyo kama serikali inasaidia kwa namna yoyote ile makudi ya dini au taasisi ya dini basi iwekwe fumula maalum ya usawa kabisa kwamba ni kiasi gani.kuliko sasa hivo misaada ya serikali inalenga zaid upande mmoja
  • ama suala lingine ni kutambua kuwa tanzania ni nchi huru hivyo haifungamani na nchi yoyote duniani kiitikadi ama kimsimamo
  • rasilimali zote ni mali ya watanzania hivyo mikataba yote iwe ya uwazi na taifa lifaidi zaidi kwa mkataba wowte wa madini na mafuta
  • kuwe na bunge tafauti la muungano ambalo litajumiasha wawakilishi na wabunge wa Tanganyika (kama ni 100 basi kila upande uwe 50) hili ndio lipitishe sheria za muungano.sio kama sasa hivi wabunge wa znz wanapiga kura kupitisha bajeti ya magufuli ..hhaaaaa mpaka unaona kinyaaa ...watu kama hawaoni ukweli hivi magufuli na wizara yake inahusu nini na mbunge wa michweni pemba? hivyo bunge la muungano liwe tofauti kujadili mambo ya muungano na yale ya kina magufuli basi yajadiliwe na wabunge wa Tanganyika..ima hili nalo litategemea Hali ya mungano baada ya katiba mpya
  ama sula la OIC hili sio suala la katiba ni suala uamuzi tu wa serikali...kama kuna umuhimi wa kujinga ama la..na kama zanzibar wajiunge ama la hili ni suala ambalo pia litaamuliwa na katiba kwani Tanganyika wanakataa kwa mashinikizo lakini katiba hio hio basi itambue imeungana na zanzibar amabyo ina waislam wengi hivyo ina maslahi na jumuia za waislam dunian, hii lazima ndani ya katiba iepo na lazima ipewe haki hii ya kujiunga na jumuiya kama hizi.

  ama kuhusu vyama vya dini sijasikia madai hayo ila hii ni yale matongo tongo aliyonayo mleta mada....
  lakini hapa katiba lazima ikataze na ipige marufuku vyama vyote vya kidini ama kikanda ama kikabila ...na lazima katiba za vyama uongozi wao uwe wa kitaifa usiwe wa kimkoa
  mwisho mleta hoja wacha chuki kwa waislam ....
   
 11. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kama issue ni maamuzi ya mahakama hiyo kutambuliwa kisheria, kwa nini kusiwe na mahakama binafsi ya Kiislamu halafu hukumu zake zikasajiliwe Mahakama Kuu ili ziwe na nguvu ya kisheria kama hukumu ya Richmond na Tanesco ilivyosajiliwa Mahakama Kuu japo mahakama iliyoamua kesi ile, sio tu haipo kisheria Tanzania, bali haipo Afrika!! Na hukumu ikatambuliwa vilevile!

  Kingine, vipi kama mke kaenda kufungua kesi kwa Kadhi Mkuu halafu mume akenda ku counter sue kwa Hakimu Mkazi. Wote tukatumiwa summons kwenda mahakamani, sasa tunakutana mahakama ipi?
   
 12. M

  Morrison Senior Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hoja hizo hazina mashiko kwani hayo ni masuala ya ndani, na jamii ya Waislam wanaozungumziwa hapa ni Watanzania si wageni kama ilivyokuwa kampuni ya kigeni ya Richmond iliyosajiliwa nje ya Tanzania, It's ridiculous!, kusajili hukumu baina ya raia wa nchi moja iliyotokana na Mahakama ilyopo ndani ya nchi hiyohiyo. Acha upuuzi.
  Katiba ni lazima ilinde uhuru wa kuabudu. Mahakama ya kadhi ni hitaji la kisheria katika kutekeleza ibada ya Muislam anapoyaendea masuala ya ndoa, mirathi, na wakfu. Kwa sababu hiyo ni lazima Mahakama hiyo itambuliwe kikatiba ili uhuru huo wa kuabudu ulindwe kikamilifu moja kwa moja kupitia nguvu ya kisheria.
   
 13. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  sijui kwa nini waislamu wako hivi mungu wangu, nawaheshimu sana. Lazima uangalie maslahi ya wenzako. Sasa kila dini/dhehebu likitaka kuwekewa mahakama, kujiunga na makundi wanayotaka yawekwe kwenye ka nchi hii itakuwaje na katiba itakuwa ya namna gani. Ndugu zangu waislamu jalini na maslahi ya watanzania wote wasio dini yenu
   
 14. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Kingine, vipi kama mke kaenda kufungua kesi kwa Kadhi Mkuu halafu mume akenda ku counter sue kwa Hakimu Mkazi. Wote tukatumiwa summons kwenda mahakamani, sasa tunakutana mahakama ipi?[/QUOTE]
  hapa nadhani unamanisha kukazia hukumu..hii ni tofauti ..hapa inayotakiwa kukidhi masuala haya ni mahakama kamili ya kadha...mfano wa hii ni mahakama ya biashara, ama mahakama ya ardhi au mahakama ya kazi...hizi ni mahakama zinajitegemea na zipo kuhukumu masuala yalio kusudiwa..lengo upande mmoja ni kuboresha na kuharakisha uendeshaji kesi hizi .
  na upande wa mahakama ya kadhi ndio hivo hivo ila sheria zake zitakuwa zinafata sheria za kiislam ..
  iwapo mke ama mume ana shauri lolote dhidi ya mwenziwe basi kawaida huwa shauri linapelekwa kwa kadhi kwa suluhu.ima kama suluhu haikupatikana basi shauri ndio linapelekwa kwa mahakama ya kadhi na mahakama inaamua kwa mujibu wa sheria na kama hawakuridhika kunakuwa na rufaa katika mahakama hio hio ila inasikilizwa na jopo la mahakimu.
  hichi kitu si cha kubishana lakini ndugu zetu wakristo wamelishwa sumu ya ubaya basi wana chukulia kama nchi tayari imeshasilimishwa ikiwa mahakama ya kadhi itaanzishwa..
  ni mahakama itayo shughulika tu na masuala ya ndoa na uruthi ya waislam hayahusu watu wengine.
  hii ipo kenya
  ipo uganda
  ipo mozambique
  na sasa hata uingereza ipo
  na zanzibar ipo
  na hapa tanganyika ilikuwepo kabla ya uhuru na waislam wa dar es salaam walimpokea nyerere mkristo wahamvalisha suruali ndefu (alikua anavaa kaptura tu) na kumkabidhi ukuu wa Tanu...uwepo wa mahakama ya kadhi haikuleta ubaguzi wowote ..sheria hii ilikuwepo tangu wakati wa mjerumani na muingereza aliboresha zaidi. ikaendelea mpaka 1972 nyerere aliipiga marufuku kwa nguvu na kwa uonevu...
  hakuwa na sababu ya msingi kufanya hivyo ila alifanya kwa udini na mashinikizo ya mapadre walio kuwa wakimwendesha
  sasa kuwarejeshea waislam haki hii sio favour ni lazima ni jambo la kuonesha kwamba Tanzania hatubaguani kidini kwani tumeweka Jumapili siku ya kwenda kanisani na jumamosi kuwa siku za mapumziko...ilhali inajulikana waislam wanapendelea ijumaa ndio iwe siku ya mapumziko kama zilivo nchi za kiislam..lakini waislam wa nchi wameridhia hili kwani hapo nyuma waingereza na wao walikubali kuwepo na mahakama ya kadhi '

  jamii hizi lazima ziishi kwa kukubaliana baaadhi ya mambo na wakristo wao kama waislam wameweza kukubali jumapili basi nao wakridto wakubali hili
  kuna shauri la gharama....lakini ni ukweli usio pingika kwamba kanisa nchi linapata mabilioni ya misamaha ya kodi na mishahara kulipa madaktari wanao fanya kazi hospitali za kanisa ambazo hazitoi huduma bure ila kwa malipo..na waislam wamekaa kimya na kustahamili...sasa ikiwa kuna haja ya serikali kutokuwa na dini hivyo lazima ije clean iwe safi kabisa isiwe ndumi la kuwili
  lazima serikali iondowe misamaha ya kodi kwa mashirika yote ya dini..iwe ni marufuku kabisa kwa serikali kulipa gharama zozote taasisis za kanisa....serikali iwache kabisa kutoa chochote kwa kanisa....hapa ndio serikali kweli haitakuwa na dini
  vinginevyo ndugu zangu tustahamiliane...kwa lengo moja tu ..nalo ni kuleta mshikamano kama taifa bila ya kujali dini yamtu.
   
 15. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wewe unauelewa mdogo. Nani kakuambia waislamu hawazidi milioni kumi? au umefuata takwimu za uongo zilizotolewa na maajenti wa kanisa? Waislamu ni zaidi ya theluthi moja ya watanzania wote na ni wengi kuliko wakristo. Uzushi huu wa takwimu fake ndio umesababisha waislamu waone kuna umuhimu wa kipengele cha dini kiingizwe kwenye sensa ili kuondoa kitendawili hiki, mkijigamba iwe kiuhalali au muone haya kuongopea umma
   
 16. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  wake wa 4 ni haki kwa mwenye kuelewa...mtu kamaa wewe huwezi kuelewa hata siku moja na haina haja ya kukufahamisha kwa nini wake 4...
  na pia hatusali kwa sababu ya mama na baba walifanya hivyo..lakini tunasali kwa sababu sisi tunamsalia yule aliumba mbingu na ardhi na vyote alivo viumba ndani yake huyu ndio tunamsalia na kumuomba
  sisi hatumsalii na kumuomba yule ambaye hata hakuishi zaidi ya miaka 36, amabye uzawa wake ni kizungu mkuti...haijulikani kama ni mwanaharamu ama na nani..wayahudi walimkataa wakasema huyu ni mwana haramu hawezikuwa masihi ama mtume...walimkataa...ingawa yeye aliletwa kwa ajili ya kwao peke yao
  huyu kutokana na dhambi hii waliyo dhania mayahudi wakamfitini kwa wakuu wa nchi...
  na hukumu ikapitishwa akamatwe auliwe...sasa huyu akakamatwa..huyu munae muomba , huyu muungu wenu, huyu ambaye alikuwa na kunya anakula na akashindwa hata kujificha ama kuleta nguvu yake ya uungu...akakamatwa akauliwa msalabani muungu akauliwa....msalabani na muungu huyu huyu alisema kabla ya kwamba kusulubiwa ni jambo la kikafiri na ukifanywa hivi basi wewe umepotea lakini yeye mwenyewe muungu huyu wako alishindwa na nguvu za viumbe wake hakuwa na nguvu hakuwa na hili wala lile akasulubiwa kishenzi kabisa hata sasa hakuna hukumu kama ile, hata hitler hakuwahi kufanya haya ila muungu wako alifanyiwa

  sasa wewe unaenda kanisani unamuomba huyu ambaye yeye uzawa wake ni wa mashaka , unamuomba na kusali unafikiri ana kusikia ? soma ..soma na fanya utafiti usifate tu kwa sababu kupewa pesa ama nafasi ya kusoma ama mitumba (maana inaelekea hukufata baba na mama)
  soma upate kujua..ama kuhusu Quraan nani kaandika basi imeletwa kwa Mtume wetu na Jibril...sasa ni miaka 1500 na zaidi lakini imebaki kama ilivoteremshwa ...
  na humo sasa ndani yake hii Quraan ndio sasa inamsafisha yule muungu wako ...hii Quraan unayo idhihaki basi hii ndio unamsafisha muungu wako..hii quraan ina wajibu mayahudi ya kwamba huyu alikua ni mtume kama walivo kina daud, yusuf,ibrahim na alizaliwa bila ya baba..kwa uwezo wa MUNGU TUNAYEMSALIE SISI,
  Na pia hii quraaan inaweka wazi kwamba huyu hawaku msulubu..kwani Mungu wake alimlinda ..kwa nini aruhusu mtume wake aburuzwe kama kibaka>? haiwezekani...alimtoa Musaa misri atashindwaje kumlinda mtume wake ambaye wale walio kusudiwa awalinaganie walimkataa?
  hivyo Mungu wetu ali mlinda huyu..hawakumuua...bali ali uliwa mwengine mnamwita Yuda huyu ndio alie uliwa ...Huyu Yesu hakuuliwa....ndio maana Jumapili alijitokeza akiwa hai......na kuchukuliwa na Muumba wake Jumatatu...
  sasa nyie mnasema kafa...halafu kaffuka...hebu weka bong yako sawa wewe ndio muumba halafu ufe..yaaani ufe kabisa ...hiviu utafufuka vipi? wewe umeshakufa ...hebu weka akili yako sawa sawa...itabidi awepo mtu mwengine alie hai akufufue ..hii ndio mantki ati...kilichokufa hakiwezi kurudi kiwenyewe hii ni sayansi ya kawaida, muungu hafi
  sasa uislam unaweka sawa haya na qURAAN ndio unasema huyu hakufa wala hawakumua....
  ukitaka zaidi ndugu yangu tafuta quraan soma surat Maryam..uone vipi muungu wako ali vosafishwa dhidi ya uongo wa mayahudi na paulo...
  usihesabu rozari tu kwa sababu ya mitumba au mikopo..soma uelewe...
   
 17. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145

  mimi sijui nani aliyetuloga waislam!
  yaani hata siku moja hatufikiri mambo ya maendeleo ila chuki tuuuuu
  hata mtu akiambiwa mwanae akajitoe mhanga anakubali harakaharaka ati thawabu.....wakati aliyemtuma wanawe wanakula bata!!
  tuamke jamani na tubadili mitazamo yetu
   
 18. K

  Ken.Rogers2012 Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Takwimu zipi zinazokueleza kwamba Waislamu wako Milioni 10 ndio wanataka sensa hii ianishe kila anaye hesabiwa na ajulikane ni dini gani ili kupata takwimu sahihi kuliko hizo zenu za uongo. Sensa zote zilizopita hakuna mahali wana hesabu wewe ni wa dini gani lakini cha ajabu mmeisha pata hata idadi mwaijua kumi ni milioni 10. Watu wenyewe mnaoa mke mmoja na huku mnajidai wasomi mna zaa kwa mpango kweli mshindane na wanaooa wake zaidi ya mmoja. au na wale mnazaa nje pia mnawahesabu ni wa kwenu sio?
   
 19. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  1. Serikali inagharimia mahakama zake za dola, sasa kwa nini Islam kama dini wasigharimie mahakama zao za kadhi? Kama wanaona ni muhimu kwa ajili yao, si waingie gharama kuziendesha? Kila kizuri kina gharama yake. Sasa wanataka serikali ndio iendeshe mahakama za kidini kwa kutumia fedha ya watu wa dini nyingine au hata wasio na dini? Hili ni suala la dini husika na wanatakiwa wabebe mzigo wao wenyewe kama dini. Vinginevyo waliache hadi watakapokuwa tayari.

  2. Hili la kujiunga na OIC naona inabidi lisubiri hadi pale Katiba Mpya itakapobainisha wazi kwamba Tanzania sasa ni nchi ya Kiislam!

  3. Kwani vyama vilivyopo ambavyo si vya kidini havitoshi au Watanzania wamekuwa wengi sana kiasi kwamba nafasi za uanachama kwenye vyama vya kawaida hazitoshi? La msingi anayetaka aanzishe chama chake, aweke sera zake za kidini kisha atafute wanachama, akipata-mwendo mdundo! Hili nalo inatakiwa lingojee kwanza Tanzania itangazwe rasmi kuwa ni ya kiislamu.

  Asanteni wanaounga mkono na wasiounga mkono pia.
   
 20. s

  seth Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo kubwa la pekee katika mchakato wa marekebisho ya Katiba na utoajiwetu wa maoni si kuleta hisia na imani zetu ndani ya Katiba ya nchi. Kila mtu ana dini yake na dini hiyo ina madai mbalimbali. Madai ya dini yako au yangu hayawezi kuingia kuwa sehemu ya Katiba ambayo ni mwongozo mama wa maisha ya watanzania wote. Ninafurahi sana kuona watu wa dini ya kiislamu wakitoa maoni mazuri sana na kupinga maoni yale ya kiislamu ambayo si tu yanaleta hisia mbaya kwa wengine lakini pia yanaleta sura isiyofaa kwa dini hii ambayo huhusishwa sana na machafuko.

  Naamini kabisa uhuru wa kutoa mawazo lakini wakati huu si wa uhuru tu wa kutoa mawazo bali ni wakati wa kuileta nchi yetu ya Tanzania pamoja. Mimi ninamarafiki zangu wengi ambao si tu ni waislamu lakini ni mashekhe na viongozi wengine wa dini hiyo. Urafiki wetu umejengwa na utazidi kujengwa kwa kuilinda misingi mbalimbali iliyotuweka pamoja bila ya ubaguzi. Matatizo na mapungufu ya dini yako au yangu yatatuliwe kwa njia nyingine ifaayo zaidi.

  Naomba notoe hoja kwamba masuala kama Kadhi na mahakama ya kadhi si tatizo maana yanaimarisha imani na maisha kamili ya kiislamu. Pamoja na umuhimu huo hatuhitaji kuweka mfumo huo kwa njia ya katiba maana tayari katiba hata iliyopo inatoa uhuru wa kuabudu. Serikali imesharidhia kuwa mahakama hizo ziwepo na jana tayari hata kadhi mkuu ametangazwa kwa upande wa tanzania bara. Je, ametangazwa kwa katiba ipi? Hii ni ishara wazi kabisa kuwa mambo yanaweza kwenda vizuri kabisa bila kuleta migongano hii ambayo wengine wanaitaka. Waislamu nawaomba tushikamane wote na tuwe na umoja wa dini zote na hata wasio na dini. maombo ya OIC ni kwa nchi za kiislamu na maana hata katiba ya OIC ipo wazi kabisa kuwa jumuiya hiyo ina malengo yake na moja ya malengo hayo ni kueneza dini ya kiislamu. Ni jambo nzuri kueneza dini hiyo lakini sasa lisiwe na kitaifa. Naomba waislamu tubaki kama tulivyokuwa miaka yote. Chembechembe hizi mnajua zinatoka wapi? Wengi wana hamu sana kuona nchi yetu ikiingia katika mafarakano, wanaingia kwa hoja ambazo kama huna akili nzuri utaona kama ni kutetea dini yako. Tufunguke na tuwe na akili ambayo Rais Kikwete aliisema alipokuwa akielezea juu ya mgomo wa walimu - kuhusu Kong'osi na mbayuwayu. Ebu changanya akili yako na yale unayopewa. Ukifanya hivyo utakuwa mtanzania halisi na si kama tunavyoona baadhi ya mawazo huu eti dini yetu..........eti dini yao.............. Haaaaaaaaaaaaaaaa! Maneno haya ya kutafuta nani ni mchawi yataisha pale tutakapojishughulisha na kazi. Sio kupiga bao chini ya mwembe ahalafu unatafuta mchawi aliekuloga kwa kukosa mlo wa jioni. Umejiloga mwenyewe. Tunataka watu wasemee haya katika katiba na sio umbeya.

  Asanteni.
   
Loading...