Katiba mpya: Wafanyabiashara / wajasiriamali kuwakilishwa bungeni

Silicon Valley

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
1,092
1,116
Kwa kuwa dunia ya leo uchumi unategemea sector binafsi, km wasemavyo "Private sector is the Engine of Economy" inashaangaza sana sector hiyo kutoshilikishwa au kutopewa nafasi bungeni ili kutatua matatizo yanayo wasibu ili kuboresha na kuchochea ukuaji wa huo uchumi kwa faida ya wananchi wote na taifa kwa ujumla, inakuwa kero kubwa sheria za kibiashara/ kijasiriamali kutungwa na mfanyakazi na kuidhiniswa na mwanasiasa ambao hawajui hata kidogo uhalisia wa mazingira yenyewe,,,, matokeo yake ni ugonvi mkubwa kati ya wadau husika na serikali au pia TRA n.k.

Ushauri wangu katiba mpya iwatambue hao wajasiliamali na wafanyabiashara kama sehemu ya jamii ya watanzania tena wenye jukumu kubwa la kiuchumi linalotegemewa na watu wote ili waweze kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayo wahusu hasa bungeni wapewe angaalau wabunge mmoja mmoja toka kila kanda za nchi. NAOMBA MASWWALI AU MAONI ILI KULIWEKA VIZURI HII HOJA MUHIMU....
 
Ni wazo zuri sana tatizo watanzania bado wana ndoto za kijamaa na domo kaya la siasa hawajajua kuwa uchumi unajengwa na hasa kwa mikakati yenye malenngo ya muda mrefu na yenye tija, wanajua ni kufisadi maliasili na uvivu mwingi, siasa ya ushabiki isiyo na mipango wala malengo yenye kulenga hujuma za mali asili tu...
 
Back
Top Bottom