Katiba mpya: Wabunge ni bora kwa Kikwete kuliko wananchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya: Wabunge ni bora kwa Kikwete kuliko wananchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Father of All, Mar 2, 2012.

 1. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ... ambao waliujadili muswada huo na kuupitisha. Wangeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani.” Jakaya Kikwete.
  Hii maana yake ni kwamba wabunge ni bora kuliko wananchi ambao ni wenye nchi? Wanaomshauri mwanangu Kikwete mbona wanazidi kumjengea historia chafu baadaye?
  Angalia kituo kingine cha mwanangu Kikwete.

  Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania, kwa ndugu wa marehemu wetu hao,”
  Je wananchi wanahitaji rambi rambi au huduma? Je haya ndiyo maisha bora kwa watanzania wote aliyoahidi Kikwete?
  “Nashukuru kwamba amani na utulivu vimerejea katika Manispaa ya Songea, nawapongeza viongozi wa ngazi zote na wananchi kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuwezesha amani kupatikana,”
  Kwa Kikwete waliokufa hawana thamani kwa vile walikuwa wakiandamana. Je hii ndiyo amani na mshikamano tunavyosikia Kikwete na wenzake wakiimba kila uchao?
  Mnaipeleka wapi nchi yetu? Je mnajua kuna kesho na mambo hubadilika?
   
Loading...