Katiba Mpya: Wabunge na Madiwani wa Viti Maalumu Waondolewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya: Wabunge na Madiwani wa Viti Maalumu Waondolewe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 22, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Wakati Mjadala wa Katiba Mpya unaendelea suala la Wabunge na Madiwani wa Viti Maalumu litajadiliwa.

  Wapo watu ambao wanaona kwamba kundi hili la viongozi ni mzigo kwa nchi ukiangalia hali yetu ya kiuchumi.

  Wapo wanaoamini nafasi hizi ni 'za kupewa' kwa ajili ya kuridhisha makundi husika na sio kwa sababu ya mahitaji wala uwezo.

  Suala kubwa zaidi ambalo linazungumzwa ni 'wabunge na madiwani wa viti maalumu' wanapatikana katika mazingira ya kudhalilisha haswa rushwa ya ngono. Hili ni suala ambalo linazungumzwa kwa vyama vyote, CCM, CDM nk. Wengi wanasemekana ni vimada, mabibi, hawara wa baadhi ya viongozi ambao wapo kwenye nafasi ya kuinfluence maamuzi. Wengine wanasemekana wanapewa nafasi hizo kutokana na ukaribu au undugu na viongozi.

  Sasa kama haya yote ni kweli (inawezekana kabisa si kweli) kwa nini nafasi hizi ziendelee kuwepo? Je Katiba Mpya iondoe nafasi hizi na tuhakikishe Bunge letu halizidi wabunge 200?

  Au ndio itakuwa vita kati ya wanaume na kina mama??

  Angalizo: Hakuna Viti Maalumu wanaowakilisha makundi ya wanaume. Na natambua kwamba sio samaki mmoja akioza wote wameoza.
   
 2. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  And, is our Parliament tailored in such a way it is the quality (the ability to represent) or quantity (number in representation) that matters? food for thought.
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  The means justifies the end result.....namna ya kuwapata hawa wabunge ni tatizo la kwanza.....nakubaliana nawe wengi wao wanapata hizo nafasi kwa kutoa rushwa ya ngono na kujuana sana.....kwa misingi hiyo we have a large quantity of women representatives with less quality compared to their number....wako wachache sana wanaoweza kutushawishi hata sisi wanawake wenzao kwamba vile viti vina umuhimu.....natamani kuwaona wanawake zaidi bungeni kama Regia na Halima au hata Esther...lakini hawa warembo tu wakuuza sura nasema hapana....

  Kwa upande mwingine,nafikiri tunaweza badili namna ya kuwapata hawa wabunge wa viti maalum....kusiwe na mianya ya hizi rushwa za ngono na kujuana sana....nafikiri tunaweza kaa chini tukajadili how? i tell you women who deserve this positions wanakuwa discouraged na tabia kama hizi za rushwa za ajabu ajabu na utumwa....manake ukishavua inakuwa ngumu kuwa against yule uliyomvulia ndo tulivyo....so unabaki kuwa mpiga makofi tu na vigelegele bungeni na kujaza nafasi.....

  naunga mkono mabadiliko ya katiba kupunguza idadi ya wabunge lakini pia kubadili namna ya upatikanaji wa wabunge wachache wa viti maalum....ila kuviondoa kabisa nafikiri haitakuwa vyema katika juhudi zetu za ukombozi wa fikra za mwanamke na jamii ambayo bado kuna wasio amini wanawake wanaweza.
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Michelle, that is such a bold statement. And I agree with you on the need to relook at the way we get these MPs for Special Seat.

  We also have witnessed some women complaining that they hav been in politics for long and therefore 'deserve' to be rewarded by that position.

  It is a pity some very strong women personalities opt to stay out of politics because of the dirtiness in getting to those positions.

  Mfumo dume unaruhusu upatikanaji wa wabunge dhaifu wa viti maalumu ili uendelee kuwepo!
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi kilio changu hata wakibakiza nafasi zote zilivyo, wabakize tume ya uchaguzi kama ilivyo, sina matatizo kabisa hadi hapo maana sihitaji kubebwa na siasa.LAKINI nitaiona katiba mpya ina maana tu kama katiba mpya itafanya mambo yafuatayo.

  1.Mawaziri na makatibu wa kuu iwe nafasi ya kitaaluma yani zitangazwe kama kazi zingine na waziri awe ana qualify kutokana na fani yake inayoendana na wizara yake.Na asiwe mbunge.
  2.jaji mkuu ateuliwe na mahakimu wenzake.
  3.Mkuu wa polisi ateuliwe na polisi wenzake.
  4.Mkuu wa jeshi ateuliwe na wanajeshi wenzake.
  5.Bunge libaki kama lilivyo na shuguri zake.Lakini iundwe jopo nyingine ya wataalamu inayojitegemea inayopanga mishahara na posho za wa bunge.

  Hayo kama wanayajadili nitakuwwa na kiu sana ya katiba mpya , lakini kama msisitizo ni NEC hahaha wala sioni maana yake maana naona manyang'au wengine wanalegeza kamba ili nao wapate kuingia.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuondoa kabisa hapana ila ni vizuri kama mfumo unaotumika kuwatunuku hizo nafasi ukibadilishwa!
  Tutafute njia mbadala ambayo itazuia waliopo juu kutoa hizo nafasi kwa rushwa ya aina yoyote ile ama ukaribu, na nafasi kugawiwa
  wale wasio na uwezo wa kufanikisha kinachowapeleka kule.
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lizzy, ni kweli kabisa. Mfumo au utaratibu wa kuwapata wabunge na madiwani wa viti maalumu lazima uangaliwe upya. Je ni nani wa kusukuma ili hili lifanyike? Si kina mama wenyewe mlivalie njuga? Au ni sisi ndio tulishikie bango?
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wote kwa pamoja.....tusisifanye hili kua swala la kijinsia.Besides nguvu ya watu wawili ni bora zaidi ya mmoja!!
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkama,

  Kuhusu polisi, mahakimu na wanajeshi kuteua kuna walakini. Kwanza, wote hawawezi kuteua labda unamaanisha wachague. Pili, siasa za uchaguzi zitatawala. Tatizo litakuwa lile lile kama kumchagua Raisi.

  Tuangalie tena upatikanaji wa watu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo. Hebu tujaribu kuangalia kwa wenzetu wanafanyaje. Wamefanikiwa wapi na wameshindwa wapi katika utaratibu wanaoutumia.

  Tuendelee kufikiria zaidi.
   
 10. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Tutalivalia njuga kuanzia TGNP na TAMWA+TAWLA na taasisi zote then mapendekezo tutaleta yajadiliwe na different stakeholders na mwishowe yafanyiwe maamuzi,ni lazima sisi kina mama tu-play role kubwa katika hili......!!!
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa,ndo maana hawataki watu tough na wanaoweza enda kinyume au kufanya zaidi yao.....yaani mwanamke hata wakikupa nafasi kubwa unakuwa kama kivuli,wanaoongoza wengine.....i hate when we are used like this.....because in the long run,wale wanaume waliotuweka pale kama kivuli wakiboronga tunaonekana sisi vivuli na si wao walioko nyuma yetu......!!!
   
 12. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lizzy, lakini bado ni suala la wanawake ambao ndio wanaowakilishwa nao. Ni vyema nyie ndio mkawa mstari wa mbele kuleta mabadiliko kwenye uwakilishi wenu. Sisi tutakuwa nyuma yenu.
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilikwazika sana na statement ya kiongozi mmoja wa CCM aliposema 'sasa hivi tumeona ni zamu ya mwanamke kuongoza mojawapo ya mihimili mitatu'. Ina maana it was more of a gift to women sio kwamba alikuwa anaweza au anastahili kuongoza. Ni wanaume wameona ngoja tuwape na wao.

  That mindset ya kwamba sisi ndio tunaamua must change. Lizzy and Michelle and the rest must work towards changing it. You guys are able as of ur own right to stand up and lead!
   
 14. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160

  Yes we can stand up and change this....ilitukera sisi pia ila tukafurahia hiyo zawadi tukiwa na matumaini itajenga taswira mpya ya uwezo wa mwanamke na kuonyesha uwezo wa kuhimili changamoto.....nachokiona kwa mwanzo huu ni tofauti na matarajio ya wengi wetu....tusubiri tu labda zawadi ya mwanamke spika italeta mema zaidi na kutujengea imani kuwa nasi tunaweza kumudu kuongoza mhimili kama bunge.....
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa inabidi sisi ndio tuwe mstari wa mbele kuonyesha tunataka mabadiliko ila tunawahitaji kina baba nyuma yetu kutuunga mkono!
   
 16. R

  Rugemeleza Verified User

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwaka 1998 nilitoa mapendekezo mbele ya Tume ya Jaji Kisanga kuwa Wabunge wa Viti Maalumu wapatikane kwa kuchaguliwa katika majimbo na wapigiwe kura na wanawake na wanaume. Hivyo nao watakuwa wabunge wa kuchaguliwa ila tu viti hivyo vitagombewa na wanawake tu. Kwa hiyo basi mbunge huyo atapatikana kwa misingi ya kimkoa au kwa kuchaguliwa katika majimbo mawili au matatu yaliyounganishwa kwa kumpata mbunge huyo. Hivyo majimbo yao yatakuwa ni makubwa zaidi kushinda yale ya wabunge wa majimbo.
  Cha pili nilipendekeza kuwa kuwe na ukomo wa kugombea majimbo hayo na muda wao uwe ni kipindi kimoja na hawataruhusiwa tena kugombea viti hivyo. Hayo mawazo kwa bahati mbaya hayakukubaliwa na Tume ya Jaji Kisanga na sikushangaa kuona mmojawapo wa wajumbe wa Tume hiyo Dr. Asha Rose-Migiro, miaka miwili baadae alipogombea ubunge wa viti maalumu kupitia CCM, kwani hiyo ndiyo ilikuwa njia nyepesi ya mtu kuukwaa ubunge.

  Wazo jingine ambalo nimekuwa nikilifiria sana ni kuwa ni lazima iandikwe katika katiba ya nchi yetu kuwa viti hivi vitafutwa kabisa baada ya miaka fulani na ninapendekeza miaka 20 ijayo. Hivyo ifikapo mwaka 2030 wabunge wote wa nchi yetu ni lazima wawe wa kuchaguliwa katika ushindani wa wagombea huru na wa vyama bila ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote.

  Ni kweli kabisa viti hivi vinawadhalilisha akina mama na ni lazima mfumo na muundo wa kuwapata wabunge hawa ubadilike. Mfumo mwingine ambao mtu anaweza kuupendekeza ambao utaondoa kabisa dhana ya viti maalumu na upendeleo na ambayo itaheshimu matakwa ya Watanzania wote ni ule mfumo wa uwiano wa uwakilishi (proportional representation). Katika mfumo huu kila chama kitakuwa na orodha ya wagombea na wabunge wake watapatikana kwa kulingana na wastani wa kura kilichopata. Ukiangalia kwa makini mfumo huu unaheshimu kila kura iliyopigwa na hivyo tutaondokana na utaratibu wa sasa wa mshindi-hupata yote. Mtu anaweza kusema kuwa sasa akina mama si watashindwa kuingia katika orodha hiyo? Ni kweli, lakini kinga itawekwa ambayo itataka kuwa katika orodha hiyo lazima iwepo idadi fulani ya wagombea akina mama ambao, kama wagombea wengine, watakuwa wameshinda katika kura huru za mchujo za kila chama. Lakini baada ya miaka ishirini utaratibu huo wa idadi ya akina mama utafutwa.

  Aidha, Katiba lazima idai kuwa jitihada za makusudi za kujenga uwezo wa wanawake kugombea lazima zifanywe na serikali, vyama, taasisi za elimu na vyama vya kiraia. Na jukumu hilo liwe kubwa kwa kila chama na kuwa hakuna chama ambacho kitaruhusiwa kushiriki uchaguzi kama hakitaonyesha jitihada zake za makusudi za kujenga uwezo wa akina mama kushiriki katika uongozi wa nchi na kugombea nafasi za uongozi.

  Naomba kutoa.
   
 17. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kuna Dada mmoja alikuwa mbunge wa viti maalum kutoka mkoani Singida katika bunge lililopita. Sina uhakika kama yupo kwenye bunge la sasa. She was just a STD VII leaver na sikuwahi kumsikia akiongea bungeni. Siku moja nikiwa bungeni nilimwona na kuuliza wenzagu kwamba huyo nae alikuwa mbunge? mbona sura yake ni ngeni kabisa!! Rafiki yangu mmoja alinijiubu kwa mkato na kwa sauti ya kunong'ona na ningependa nimnukuu. Alisema 'hiyo ni chakula ya waziri mkuu, nitakusimulia jioni tukitulia'.

  Ilipofika jioni rafiki yangu huyo ambaye kwa nafasi yake niliamini moja kwa moja maneno yake, alinisimulia namna waziri mkuu alivyofahamiana na huyo dada akiwa kwenye ziara ya mkoa wa singida na namna alivyomwezesha huyo binti kupata hiyo nafasi ya mbunge wa viti maalum. Ni stori ndefu lakini kwa kifupi ni kwamba kwa mara ya kwanza waziri mkuu alimwona huyo binti akicheza ngoma ya utamaduni kwenye hafla ya kumpokea waziri mkuu. Inasemekana uchezaji wake ulimvutia sana waziri mkuu. Na kama unavyojua dada zetu wa singida, huyo binti alikuwa amejaaliwa sana!

  Hao ndiyo wabunge wetu wanaoamua mustakabali wa watanzania takribani milioni 40 wanavyopatikana. Hence, naunga mkono hoja yako. Lazima katiba mpya iondoe upuuzi huu.
   
 18. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwa uchunguzi wa haraka haraka, nafasi hizi hazina faida yoyote kwa taifa. Kwanza wawalikilishi wa viti maalumu wawapo bungeni au kwenye mabaraza ya madiwani kazi yao ni kulinda maslahi ya wale waliowaweka katika nafasi hizo. Pili nafasi hizi zinatolewa kwa mchezo mchafu sana, na ni kwa sababu hiyo wamama wengi wenye heshima zao pamoja na kuwa na uwezo hawaingii katika kinyang'anyiro. Tatu nafasi hizi hutolewa kwa upendeleo na rushwa ya hali ya juu sana. Mfano ukiangalia kwa sasa wengi wa wawakilishi waliopita kwa njia hii ni wake wa mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na kama si wake wa watu hawa basi mara nyingi ni vimada wao. Utaratibu huu ni wa kipuuzi kabisa. Hakuna demokrasia ya kumpa mtu nafasi ya upendeleo ni ujinga na ukosefu wa maarifa kabisa.
  Mimi naona hamna haha kabisa ya kuwa na wabunge wa viti maalumu.
   
 19. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rugemeleza, binafsi nashukuru sana kwa mchango wako na solutions ulizotoa. Tuzijadili kwa kina na naamini muda umefika wa kulisimamia hili. Gharama tunzazoingia kama taifa kubeba mzigo huu ni kubwa sana.

  Badala ya kuwasaidia wanawake tunawagandamiza na kuwadhalilisha. Hili lazima tuhakikishe linaangaliwa upya. Haliwezi kubaki ni suala la vyama vya siasa peke yao kuamua nani awe Mbunge kuwawakilisha wanawake. Kwa utaratibu huo kila mmoja unakuta anawakilisha wanawake wa chama chake. Wenye access naye ni wale wa chama chake tu. Je wakina mama wasiokuwa na vyama au ambao hawako kwenye NGO? Inakuwaje?
   
 20. F

  Felister JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa hiyo ndiyo inayoondoa maana kamili ya uwakilishi wa hili kundi linalopewa upendeleo wa msingi kutokana na historia. Badala ya kuandikia mate wakati wino upo jambo ambalo jeshi letu invisible lingefanya kama kweli kuna utashi waki siasa ni kuchunguza haya si kwaajili ya kuwadhalilisha au hata kuwa disgrace kwajinsi yeyote ile bali kwa faida ya maendeleo ya taifa. Maana kwa jinsi hiyo bado mfumo dume unaendelea ndiyo maana hatuoni tofauti kubwa maana hawa wanawakilisha kundi lile lile la wanaume na wanawake wenye nguvu katika jamii kutekeleza matakwa yao au kufanikisha malengo binafsi.

  Ukichukulia mfano wa spika wa sasa je ni wanawake waliotoa pendekezo na kama ndiyo wanawake gani wa chama chenye nguvu au wanawake watanzania ambao ni walengwa hasa? Je huyo ananafasi gani ya kuwa tetea wanawake wakawaida katika kufanikisha mambo yao? Just being sincere kwa maoni yangu binafsi ni wanawake na wanaume wenye nguvu katika jamii ambayo according to gender huyo ni mwanamke wa mfume dume maana anawakilisha kundi la wenye nguvu maana ndiyo hasa waliofanikisha uwepo wake. Yeye kama individual anaweza asiwe na tatizo ila mfumo uliomweka hapo utamsababisha atende kama watakavyopenda maana nguvu walizonazo katika kumweka ndizo zenye uwezo pia wakumwajibisha.

  Hapa ndipo definition na context ya gender as Tanzania is concerned linapotakiwa liwekwe sawa na ni njia gani itakayo weza kuwa leta hao ambao kwa nafasi zao kijamii si rahisi kufika kwenye nafasi za maamuzi ili mahitaji yao yazingatiwe katika maamuzi mbali mabali ya kisera na sheria.

  Mwanamke aliyekaa kwenye siasa miaka zaidi ya 20 bado anataka kupata nafasi kwa upendeleo? Hiyo ni abuse of that opportunity, maana jamii inamjua vizuri imeona utendaji kazi wake hahitaji tena kupewa nafasi maana alishaipata na kama hawezi basi hatakaa aweze, anachotafuta au wanomweka wanachotafuta ni zaidi ya uwakilishi wake; nawakilisha.
   
Loading...