Katiba Mpya Uchaguzi Ujao na Hali ya Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba Mpya Uchaguzi Ujao na Hali ya Muungano

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Profesa, Jul 3, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  1. Raisi aliyepita ni wa Bara, na wa sasa ni Bara, atakaekuja atatoka Bara au Visiwani?
  2. Raisi wa sasa ni Muislamu, na ajaye atakuwa Muislamu kwa kuwa awamu ya tatu itakuwa ngumu kuacha kuwapa nafasi Wazanzibari ambao wengi ni waislamu? kulinda muungano?
  3. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni ya mseto, ya bara ni ya chama kimoja, iwapo mseto utapatikana bara kwa chama tofauti na mseto wa Zanzibar hii itamaanisha nini?

  Napendekeza yafuatayo ili kunusuru mgogoro mgumu utakao tokana na hojaji hizo hapo juu:

  1. Serikali ya Muungano iwe ya serikali tatu,
  a. Revolutionary state of Zanzibar, and
  b. the State of Tanganyika,
  c. United Republic of Tanzania

  Ambazo zote ziko semi autonomous isipokuwa tu kwa maswala ya ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji (isipokuwa polisi), Afya, Revenues, Bank and monetary (kama kuna kitengo kingine muhimu mtaniongezea). Kutakuwa na bunge mojala Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, na mabaraza mawilii, Baraza la wawakilishi la Tanganyika na baraza la wawakilishi wa Zanzibar.

  2. Kuwe na Mgombea binafsi ili watu kama Mheshimiwa Augustine Ramadhani ambaye ni Mkristo, akiridhia anaweza kugombea Uraisi na kunusuru mgogoro wa sasa.

  3. Madaraka ya raisi yatenganishwe na madaraka ya chama, na Rais asisimamie shughuli za chama iwapo atachaguliwa, ili awajibike kwa utendaji wake. Pia itasaidia raisi kuhangaika kutumia muda mwingi kusimamia interest za chama badala ya interest za Kitaifa. Na hii itasaidia sana kupunguza mgogoro pale ambapo serikali inabidi kuwa ya mseto, ukizaingatia nguvu ya upinzani inaongezeka.

  4. Wajumbe wa tume ya uchaguzi wa serikali ya Muungano wawe wa kuomba nafasi hiyo na kupitishwa na Bunge, na Bunge linaweza kupendekeza majina yao iwapo hawatajitokeza na kupitishwa na Bunge.

  5. Nafasi ya Uwaziri na Ukatibu Mkuu zote ziwe za kuomba na ziwe proffessional post na sio political. Ila bado Waziri apewe nafasi ya kuingia Bungeni.

  6. Nafasi za Wakuu wa Mkoa na Wilaya wabaki ili kulinda interest za Raisi, na Raisi apewe mamlaka ya kuwateua, hawa ndio watakaokuwa administrative officers na wanatoa balanmced supervissions na kusimamia presindents orders and wishes in respective jurisdictions.

  Tutaendelea....
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 3. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimepiga kura tayari Communist. Inapendeza hakikisha unatuandalia kareport ka matokeo na pia kuona uwezekano wa kukasambaza karipoti hako. Shukrani.
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  6. Wajumbe wa tume ya uchaguzi wa serikali ya Muungano wawe wa kuomba nafasi hiyo na kupitishwa na Bunge, na Bunge linaweza kupendekeza majina yao iwapo hawatajitokeza na kupitishwa na Bunge. This is good

  5. Nafasi ya Uwaziri na Ukatibu Mkuu zote ziwe za kuomba na ziwe proffessional post na sio political. Ila bado Waziri apewe nafasi ya kuingia Bungeni. That is good, ila wakubalike na bunge na bunge liwe na veto ya kuwatoa, Hawa jamaa wana viburi sana.

  6. Nafasi za Wakuu wa Mkoa na Wilaya wabaki ili kulinda interest za Raisi, na Raisi apewe mamlaka ya kuwateua, hawa ndio watakaokuwa administrative officers na wanatoa balanmced supervissions na kusimamia presindents orders and wishes in respective jurisdictions
  . Hapana, Hapana. Wachaguliwe na wananchi wakati wa uchaguzi mkuu, na wawe wenyiviti wa hamashauri na mikoa. Pia bunge na wananchi wawe na veto ya kuwaondoa.

  "If a leader is not coming from the people he is leading, he has already lost the legitimacy of being a leader (e.g. kwa kanga na kofia na fulana na rushuwa). The same applies to when a leader has seized to stand for the right of the people he is leading, he has lost the righteousness of becoming a leader" (Haki na watu; by JK Senior)
   
 5. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Sikatai kabisa Bwana Fredrick Sanga, changamoto ya Democrasia inayoanza kukomaa ni pale ambapo, kama atatokea mtu mzuri wa kueneza propaganda nzuri kuliko wewe Raisi, basi hakuna maagizo wala vission utakayo ipresent na ikatekelezwa kwa urahisi, kwa kuwa hakuna mahali ambapo una meno.

  Role ya Hawa wakuu wa Mikoa na Wilaya ni muhimu sana kupunguza viburi vya wakurugenzi. Je unajua kwa mfumo ulivyo, Mkuu wa Wilaya ndiye anayeweza kutoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na si vinginevyo? na ndani ya Wilaya Moja kunaweza kuwa na halmashauri moja?

  Huwezi kuwa raisi halafu usiwe na some levels of power, otherwise uongozi wako utakuwa na mapengo. Kwa kawaida, Nchi inatakiwa iwe na mfumo ambao hata kama Raisi ni Dhaifu, isiyumbe, bado natafakari njia bora zaidi iwapo kama tuatmpigia mkuu wa wilaya kura, itakuwaje? majukumu yake yatakuwa ni yapi?

  Nahisi atakuwa hana wadhifa, labda tuje na utaratibu wa Majimbo ambao binafsi ninaukubali, wasioukubali ni wale wanaohofia kuwa watu wa maeneo fulani watarudi nyumba kimaendeleo!!??? Ni arrangements tu na kuwepo kwa subsdising grants kwa halmashauri kama za Mikindani na kwengineko ambazo revenue collection iko chini. Majombo ni sawa na kuwekza ushindani katika biashara ya kisiasa. Jimbo gani zuri? Linazalisha mali kwa wingi?

  Lina watu wenye uwezo mkubwa? Muhimu nji kuto limit movement order ya watu ambao ni raia au wana permit nchini. Nitafurahi kwa mfano Wamasai wakipata Jimbo lao wakasimamia vema kwa sheria zao utaratibu wa Malisho kwa mila zao bila kubughudhiwa na waroho wa Ardhi wanaotaka kuwagawia Waarabu wakati wao hawagain wala haieleweki nchi inagain kiasi gani!!Mfano: Kama ni kwagawa eneo wamasai waamue sio Mzanzibar aje awaamulie wamasai.

  Hapo ndipo mipaka inapokuwa. Nikimaanisha aidea ya Ardhi kuwa ya serikali iwe na categories, na process ambazo zinailipa baraza la eneo husika la ardhi mamlaka makubwa kabisa, wakikataa kusiwe na power nyingine ya kuamua matumizi ya ardhi yao, ila kwa sasa kuna mwanya ndio maana wanakuja tuuu bila mpangilio, wanamaniputale mambo na madocument yao complicated masikini wazee wale achilia mbali hicho kiingereza, mkataba hawaujui na hata kama kama wana nahati ya kuuona na wanochanganyikiwa ale wanapoondolewa.

  Unadhani kwanini kuna migogoro, wenye kuitaka ardhi huhakikisha interest zao zinalindwa zaidi za yule mwenye nayo, na mwenye dhamana ambaye ni kiongozi anakiuka miiko na kumpa favour mwekezaji...

  TUNAHITAJI KATIBA MPYA KWAKWELI
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kabisa.
  Lakini angalia sana hoja ya madaraka ya raisi, kila mtu anateuliwa (Sanga is right in a way, you are talking the same thing)

  Tunataka Job Description za wafuatao:
  Mameya
  Wabunge
  Wenyeviti wa halmashauri
  Wenyeviti wa mikoa
  Wakuu wa mikoa
  Wakuuwa wilaya
  RAS
  DAR
  Wakurugenzi NK

  1. Pale umeshasema kuna wakurugenzi, kuna DAD, kuna RAS Nk haw wote wanatoka upande wa muhimili wa serikali
  2. Umesema vission, mtazamo wa dunia ya leo ni kwamba vision inajengwa kuanzia chini kwenda juu, na inamilikiwa na wananchi, Hawa wa serikalini wanatengeneza strategy, na zinapitishwa na wakilishi wa wananchi.
  3. Mkuu wa mkuo basically ni meya wa mkoa, kwanini achaguliwe na rais. Tumwachie hao wakurugenzi, DAD, na MA RAS. Sisi tuje tuwakomoli. wafanye kazi.

  Nitachangia zaidi, nime banwa na shughuli.
   
 7. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Wabunge waliochaguliwa majimboni wanaweza kuvuliwa Ubunge iwapo atashtakiwa na kuhukumiwa na mahakama, au kama itathibitika na kamati husika baada ya uchunguzi, amehusika na kuihujumu nchi kiuchumi na kisiasa, na au uchunguzi wowote uwe wa kamati halali au wa chombo cha dola umemtia hatiani kuhusika na kashfa yeyote inayohusiana na ukiukwaji wa maadili yawe ywa kijamii au ya kikazi, au kwa sababu zozote zile, wananchi wamewasilisha malalamiko rasmi ya kutomtaka mbunge wao. Mbunge huyo anaweza kundolewa kwa njia kuu mbili, kwa kura ya maoni ya chama chake (iwapo tuhuma ni za kukiuka misingi na maadili halali ya chama), kwa kura ya maoni ya wananchi, au kwa kura ya maoni ya bunge zima kutegemeana na tuhuma husika. Kura ya maoni inaweza kupigwa kwa kutumia namba ya simu ya wahusika na kwa mfumo ambao utaweza kuitambua simu hiyo (kwa kulingana na register) na namba ya uchaguzi ya muhusika na kumbukumbu zake zilizopo kwenye orodha ya kudumu ya daftari la mpiga kura. Ukokotoaji wa takwimu za kura utakuwa wa wazi na matokeo yatatangazwa wazi.
   
 8. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Wana Jamvi mwenye nakala ya Job Description za hawa hapo juu waliotajwa na Communist waturushie hapa tafadhali
   
Loading...