katiba mpya,tunataka kiongozi anayetaka kututawala watoto wake ni lazima wasome shule za serikali.

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
wadau hili mnalionaje kama likiwepo kwenye katiba mpya?

Moja wapo ya matatizo yanayoikumba sekta ya elimu ni kutelekezwa na viongozi,watoto wao wanasoma shule za nje ya nchi au shule binafsi za pesa nyingi jhapa nchini. Nafikiri hili likiingia katika katiba mpya litatusaidia kukuza elimu na kuboresha shule za serikali,mbona kina makongoro walisoma shule hizi?

Mi napendekeza iingie katika katiba ili tuwajue viongozi wenye mapenzi na nchi yetu.
 
Ndugu yanngu hilo ni wazo jema. Lakini hoja yako haina mantiki sana!!! La msingi ni wananchi kuiondoa CCM madarakani na kisha serikali mpya kubadidili mfumo mzima wa elimu, full stop!!! Tofauti na hapo watanzania tutakuwa tunajitumainisha kwa kubahatisha mambo mithili ya mtu anayepiga ramli..
 
wadau hili mnalionaje kama likiwepo kwenye katiba mpya?
moja wapo ya matatizo yanayoikumba sekta ya elimu ni kutelekezwa na viongozi,watoto wao wanasoma shule za nje ya nchi au shule binafsi za pesa nyingi jhapa nchini.
nafikiri hili likiingia katika katiba mpya litatusaidia kukuza elimu na kuboresha shule za serikali,mbona kina makongoro walisoma shule hizi?
mi napendekeza iingie katika katiba ili tuwajue viongozi wenye mapenzi na nchi yetu.
Naunga mkono hoja...
 
Mkuu, hatuna njia mbadala ya kulinusuru taifa hili tofauti na kuing'oa CCM na mizizi yake; Hata tufanyeje chini ya mfumo huu wa maCCM, piga ua galagaza hatutoki ndugu, sana sana tunazidi kujimaliza wenyewe. Hivi Ritzone amesoma wapi vile ...........................
 
Back
Top Bottom