Katiba Mpya, Tume huru chini ya CCM ni ndoto ya mchana! Upinzani chukueni hatua

Siwamilele

JF-Expert Member
Oct 22, 2019
274
1,000
Ndugu zangu, hizi kelele zisizokoma kila siku za kwamba, tume ya taifa ya uchaguzi haiko huru, katiba tuliyo nayo ni mbovu na kwamba imepitwa na wakati, ni madai ya msingi kabisa.

Tumeona uchaguzi ulivyo vurugwa, katiba yenyewe tuliyo nayo inavyo siginwa na watawala, wenye mawazo na mtazamo tofauti wanavyo tendewa, kundi la watu wachache linavyo jiona lina haki kuliko watanzania wengine wote!

Kinacho sikitisha ni kwamba, viongozi wa upinzani wamebaki kulalamika tu bila kuchukua hatua kali kukabiliana na hujuma hizi.

Wananchi mtaani wamechoka, lakini hamuwaambii nini cha kufanya?

2015 CUF Zanzibar mlishinda, mkanyang'anywa ushindi mchana kweupe. Wananchi wakasubiri muwaambie chakufanya mkaishia matamko na kutalii duniani, haki ikapotea!

Chaguzi ndogo za marudio mmefanyiwa hujuma za wazi, mmeishia matamko, haki inanyongwa siku zinaenda!
Haya, uchaguzi s/mitaa umekwisha, mmehujumiwa kweli kweli mpaka huruma, ajabu mmerudia yale yale ya kususia/kujitoa kushiriki na sasa mnaenda kuishia matamko!

Jafo (msimamizi wa uchaguzi huo) alijimwambafy hadharani kwamba wapinzani kufanyiwa hujuma kwenye uchaguzi ni jambo la kawaida, mkachukulia poa? Hivi, aliposema wapinzani mkomae kisiasa, mlimuelewaje?

Tuseme nini basi? Kwamba 2020 mnakwenda kwenye uchaguzi kufanya mlicho kifanya kwenye uchaguzi huu?
Mnatashiriki mchakato mzima halafu dakika za mwisho mtajitoa? Halafu?

Kwamba, serikali hii hii ya CCM kuna siku itaamka asubuhi na kuwaambieni kwamba, njooni tuunde tume huru?
Kwamba itasema tu, sasa tubadilishe katiba?

Au mnasubiri tu iseme "sasa kwa hiari yetu tumeamua kufuta uchaguzi uliofanyika kwakuwa haukuwa huru na haki, na sasa tunauandaa upya?"

Au mnasubiri nini hasa!!
Je, mtaishi matamko yenu mpaka lini?
Je, wananchi (nguvu ya umma) wataendelea kuwaamini, kuwavumilia na kusubiri maamzi yenu magumu hata lini?
Siku wakigundua hamna lolote zaidi ya kulialia na kutoa matamko na kuamua kuachana na ninyi itakuwaje?
Mtatumia hekima na busara katikati ya watawala wapumbavu mpaka lini?

Maswali ni mengi mno wacha niishie hapa, lakini niseme tu;
KAMA MNASUBIRI CCM IWAPE KATIBA MPYA NA TUME HURU, NAWASHAURI MUACHE SIASA. MNACHOSHA INGAWA MNAPENDWA.
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
10,417
2,000
Sasa Kabisa. Tuache kumtegemea shetani ajifitini mwenyewe ili kupata ukombozi.
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,804
2,000
Nilitamani sana watanzania kuweka mijadala muhimu kwa taifa kama huu ndio iwe ajenda Kuu kwetu sote ili kulisaidia taifa letu kufanya mageuzi bora yakutusaidia huko tuendako.

1. Katiba mpya ya Jaji warioba ili vifuavyo vizaliwe

A) Tume huru ya uchaguzi

B) Uhuru wa mahakama uliokamili

C) Uhuru wa Bunge uliokamili

D) kupunguza madaraka ya rais, ilikuona watakao kuja wanatenda kwa mujibu wa katiba na kuruhusu kushitakiwa wanapoharibu au kuvunja katiba

2. -Haki ya kukusanyika na kupeana taarifa
-Haki ya kufanya siasa bora iliyosawa kwa vyama na wanasiasa wote.

3. Haki sahihi ya kupata
Elimu bora sio bora Elimu

Afya bora sio bora afya

Nk

Cha ajabu watanzania wenzangu hata wale tunaowaheshimu hawawezi kupambana na hili. Vita yao ni Chadema. Ukiwauliza kwa nini Chadema hawana hoja za msingi Sanasana njaa na ulafi wa madaraka kuvizia uteuzi. Watanzania tunatia aibu sana
 

Siwamilele

JF-Expert Member
Oct 22, 2019
274
1,000
Hapo kwenye 1.(D) ni mhimu sana mkuu, maana ndipo ilipojeuri ya mtawala/watawala wetu kufanya wanavyotaka na mwisho kutuharibia nchi.
 

JOESKY

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
785
1,000
Kabisa mkuu akina mbowe zitto na wote hawabebeki kiukweli wanachisha
 

Ukugigwa

Member
Jan 23, 2020
15
75
Kumbe zile mbwembwe zote za jpm kuwa ameanzisha miradi wananchi wameona upumbavu tu!
Nakuhakishieni the moment ccm wakikubali tume huru ya u haguzi ndo kifo chake jpm hataambuli hata 20 percent ya kura zote.
Labda atapata singida tu ambapo no jamii ya wajinga( hawana elimu)
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,806
2,000
Aksante kwa kuonyesha kiwango chako cha ujinga!

Naomba uelewe kuwa ujinga sio sifa kama ilivyo upumbavu. Mtu mjinga akielimishwa huondoa ujinga lakini mtu mpumbavu huwezi kumrekebisha kwa sababu upumbavu ni sawa na ufupi au urefu.

Andiko lako limebainisha kuwa unachotakiwa ni kuelimishwa ili uondokane na ujinga ulioonyesha kwenye mada yako!
 

Ukugigwa

Member
Jan 23, 2020
15
75
Kama sijaandika chochote unadhani ulicho quote na kuuliza ni hewa?

Unazidi kuonyesha kuwa unahitaji sana msaada wa kuondolewa ujinga!
Jibu swali acha kurukaruka swali! Kwa nini mnaogopa tume huru ya uchaguzi Kama mnapendwa na mna uhakika wa kuchaguliwa kwa kura mbali na kuiba?
 

Mudi_kidato

Member
Sep 6, 2019
65
95
Aksante kwa kuonyesha kiwango chako cha ujinga!

Naomba uelewe kuwa ujinga sio sifa kama ilivyo upumbavu. Mtu mjinga akielimishwa huondoa ujinga lakini mtu mpumbavu huwezi kumrekebisha kwa sababu upumbavu ni sawa na ufupi au urefu.

Andiko lako limebainisha kuwa unachotakiwa ni kuelimishwa ili uondokane na ujinga ulioonyesha kwenye mada yako!
Point yako ipi sasa mbona huelewek...au wote ni wajinga

from mudi kidato
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,867
2,000
Jibu swali acha kurukaruka swali! Kwa nini mnaogopa tume huru ya uchaguzi Kama mnapendwa na mna uhakika wa kuchaguliwa kwa kura mbali na kuiba?
Akikujibu hilo swali kwa ukweli kazi anafutwa na ataitwa kamati ya maadili
Hawakubali kuwe na Tume Huru hawa,hiyo itakuwa sawa na kujivisha kitanzi.Kura halali hawajazoea,wanapenda vya kubyonga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom