Katiba mpya tanzania mpya kwa kizazi cha sasa na miaka zaidi ya 50 ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya tanzania mpya kwa kizazi cha sasa na miaka zaidi ya 50 ijayo

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mtu wa Mungu, Jan 13, 2011.

 1. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Katiba Mpya siyo mali ya chama cho chote cha siasa,wala serikali iliyoko madarakani, HAPANA!!!!!!- ni mali na msitakabali wa Watanzania wote, kwa pamoja wapatao miliono 40 waliopo sasa; kwa faida yao sasa, na ya milioni wasiopungua 100 miaka 50 ijayo; (wakati tunapata uhuru tulikuwa milioni 9!!!!!!!; tunaposherehekea miaka 50 mwaka kesho tuko takriban miliono 40-nilikuwemo katika mil 9 mwaka 1961, na nimo katika mil 40 mwaka 2011- kwa hiyo naelewa ninachozungumza)!!!!!!!
  Kwa hiyo suala la kuandika katiba mpya si suala la chama cho chote wala serikali iliyoko madarakani- hawa ni vichocheo tu vya mchakato wa kuandika katiba hiyo!!!!!!!!!!!.
  Watanznia tumeshuhudia madhara ya katiba mbovu-uwezekano wa haya tuliyoshuhudia kutokea tena ni mkubwa zaidi ya sasa hivi-aliyepata 27% ya kura ndiye anakuwa rais, na chaguo la wananchi kwa kura 64% anawekwa kuwa namba 2??????????????-dhana yote ya demokrasia inazikwa. Katiba ya sasa ni ya 1977, wakati wa chama kimoja-misingi yake bado ni ya chama kimoja, ndiyo maana akishatajwa na tume yake dhalimu hakuna ruhusa kuhoji po pote ndani ya nchi hii-hata kama upo ushahidi kuwa ni muuaji wa watu, au ni mwizi wa kura!!!!!!!!!!!!??????????
  Kwa sababu hiyo ni muhimu sana watanzania tuelewe tunachosimamia, na kisha kusimama kidete!!!!!!!!!!!
  Kwa sasa tunahitaji kama kipaumbele (top priority) nguvu ya sheria kuhalalisha kitaifa uamuzi huu wa rais Kikwete-zikiwemo taratibu za kufuatwa, msitakabali mzima kitaifa jinsi zoezi zima litakavyoendeshwa kwa haki na uwazi ili kila raia katika hatua ya mwisho ya kura ya maoni kila mmoja ridhaa yake na haki yake kikatiba iwe imeheshimiwa! Kwa vile bunge ndiye mtunga sheria, suala la katiba mpya kuwasilishwa bungeni ni a must .Tusiruhusu makundi yenye agenda zenye maslahi binafsi kuteka nyara kijanja mchakato-bila ulinzi wa sheria watajitokeza muda mfupi ujao-mtawaona tu!!!; na hii itakuwa salama tu kama ipo sheria inayolinda mchakato huu- KWA SASA HAKUNA sheria hiyo!!!!!!!!!!!! Kitaifa hatujawa na zoezi la aina hii, hivyo hatuna sheria hiyo, mtu asitudanganye!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Sote kwa pamoja tupiganie zoezi hili liingie katika mkondo wa sheria, vinginevyo hapo mbeleni tutegemee vurugu nyingi sana!!!-wanaopokonywa maslahi (mafisadi wenye mapesa mengi-hamuoni wanavyojipanga sasa kwa kuanzia kwa mbali kwa kudai pesa za Dowans?????) dhidi ya wenye haki masikini wakijaribu kutumia nguvu ya umma, lakini wakizimwa kila wakati kwa mitutu ya bunduki kwa kutumia hawa polisi , wasiokuwa na akili hata kidogo, wala macho ya kuona upepo wa nguvu ya umma unavyoongezeka kwa kasi ya ajabu; wanasahau kwamba wengi wao wanaishi uraiani katikati ya hawa ambao wanawaua kwa risasi za moto!!!!!!-wanaodhani mafisadi watawagawia mamilioni haya!!!!!!
   
Loading...