Ukombozi Sasa
Member
- Nov 5, 2010
- 17
- 10
Katika Mchakato wa katiba mpya mimi moja kwa moja naunga mkono uwepo wa serikali za majimbo. Tunaweza kugawanya Tanganyika katika majimbo matano au sita ya kiuchumi, na jamaa wa visiwani hatuwahitaji, lakini kama watatungangania basi wakubali kutokuwa nchi bali kuwa eneo la Federal Government na hivyo kuongeza idadi ya majimbo Unguja ikawa jimbo moja na Pemba la pili, kitu kinachoitwa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kikabakia kwenye vitabu vya historia......Kwanza wabaki kivyao hawatusaidii chochote ...............
Kwa kuwepo na serikali ya majimbo ni dhahiri kuwa tutakuwa na maendeleo ya haraka kwa maana majimbo yatakuwa na madaraka zaidi katika maamuzi ya kiuchumi, pili serikali ya kitaifa yaani Federal itakuwa na majukumu machache katika kuleta maendeleo na hivyo kuwa na ufanisi zaidi. Si hili tu bali pia kutadumisha demokrasia zaidi na kuboresha usalama wa nchi zaidi kwa kuwa na vyombo vya usalama vyenye mwiinglio mdogo wa kisiasa. Uchumi utapanuka kwa kasi kwa kinachopatikana katika jimbo kitabaki katika maendelea ya jimbo husika, na asilimia fualni itakwenda kwenye serekali kuu ili kusaidia kuboresha usalama wa nchi nzima na kuboresha miundo mbinu ya kitaifa...
Natoa Hoja