Katiba mpya sawa, watekelezaji je

Wakuletwa

Senior Member
Oct 31, 2010
134
9
Heshima kwenu wana JF.
Katiba mpya ndio habari iliyopo mjini sasa, ni kweli hata mimi naihitaji sana ila hofu yangu ni kuwa katiba ni maandishi tu hayatendi chochote pasi na matakwa ya walioitunga. Hii mbovu tulionayo ina mazuri yake lakini hakuna wa kuyatekeleza tena machache.
Wakati tunahangaika na katiba hiyo mpya pia tuhangaike na watu tutakaowakabidhi maana tunaweza tukawa na katiba safiiii lakini tunaowapa wachafuuuu hapo sijui itakuwaje?

Nasikia kuna nchi katiba zao hata sio za maandishi lakini watu wa huko wastaarabu na wanatekeleza matakwa ya raia zao. Wakati tunatafakari kuhusu katiba pia tutafakari na uadilifu wetu.

Asanteni sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom