Katiba Mpya sawa, lakini unadhani watu wengi wana weledi wa kutosha: Case Study South Africa

MbantuOG

Member
Mar 7, 2021
30
95
Naitazama katiba mpya kama swala lenye ulazima na tija sana katika uendeshaji wa nchi: Sababu kuu ni moja sheria zetu nyingi zinapwaya na kuhitaji marekebisho kila mara ila sidhani kama kuna mambo muhimu matatu ya kushughulikia nchi hii Katiba itaingia katika miaka mitatu ijayo.

Nadhani kuwe na marekebisho ya acts muhimu tatu hadi tano lakini katiba kwa ujumla wake twende nayo hii, moja iwe ya elimu, ya pili siasa na nyingine (nitapenda kama watu watashauri katika thread hii).

Nadhani ukiangalia nchi kama South Africa (ambao huenda wakawa na Katiba bora kuliko zote Africa) matumizi ya uhuru kwako yamekua mabaya mfano maandamano yamekua kichaka cha uhalifu na unyang'anyi wa mali za watu. Sababu ikiwa katiba yao ni "copy-paste" ya katiba za nchi zilizoendelea na hivo haiko "suitable" na uhalisia wa watu wa Afrika ya Kusini. Kitakwimu makadirio ya Investec Bank Ltd, ni kwamba uchumi utakua kwa chini ya asilimia 4 sababu ya "vuguvugu la kisiasa". Unategemea kwa urahisi tu nchi yenye katiba nzuri kama Afrika kusini huwezi kuta vitu kama hivi lakini in the African Case vipo ndomana nadhani katiba mpya inahitaji muda.

Rasimu ya warioba ilikua nzuri sana lakini ile recruitment ya wabunge wa katiba ilifanya katiba isipite hadi leo kweli kuna mtu anataka kupoteza pesa tena? Bila kubadili acts hizi io "recruitment" tu ya wabunge wa katiba itatujazia watu wasio elewa mapana ya sheria.

Nakaribisha matusi,kejeli,dharau na majadiliano yenye tija vyote kwa pamoja.
 
Kayamba Moses

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,632
2,000
Haya maelezo ni ya mtu anayekula na kulala sebuleni kwa shemeji yake, hajui uchungu wa UFISADI katika maisha ya kujitafutia.

Zuma alikuwa Rais chini ya ANC, alishinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Hakuna katika katiba ameambiwa afanye ufisadi! Uwepo wa vurugu ni jambo la kawaida katika siasa, anao wafuasi, wafia mtu, anao wafuasi wafia Kabila (Zulu natal Kabila lake ni kubwa), ulitaka katiba izuie vipi vurugu?

Hoja muhimu ni kwamba Rais Zuma ali-resign kwa Ufisadi, shinikizo lilitoka kwa Julius Malema & Co chini ya Economic Freedom Party, katiba imewaruhusu kuandamana, kupinga ndani na nje ya Bunge kwa uhuru (fatilia kashikashi zao Bungeni), katiba imara imewapa Bunge imara. Hapa kwetu Bunge ni mali ya Ndugai na CCM!

Vurugu ni matokeo ya uimara wa Katiba inayoweza kumuwajibisha hata Rais akiwa madarakani. Unashangaa uporaji huu katika vurugu za South Africa wakati hapa kwetu kila taarifa ya CAG kuna uporaji mkubwa kwa karamu!

Zurazura rudi nyumbani kwa shemeji ule ulale.
 
The MaskmaN

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
236
500
Mzee utakuwa umeingia digrii ya sheria mwaka huu ee? Unajaribu kutest mitambo !

Ila ujue katiba ni kama au inamuelekeo wa vitabu vya dini yani kipengele kimoja kinashabiana na kipengele/vipengele vingine...ni ngumu na sio rahisi kusema tu tubadili maeneo au sehemu mbili sijui tatu afu zingine tuache kama ilivyo,

Kwako wewe unaeza kuona sheria/miongozo ya kwenye sekta ya elimu kwenye katiba haiendani na sheria au miongozo ya kwenye sekta ya afya kwenye katiba! Ila wenye uelewa mpana wanajua kuna mshabiiano au muingiliano so sio rahisi kubadili vipengele tu vya afya then useme vya kwenye elimu vipo sawa..!!

Unapoamua kukaa chini kubadili katiba basi jua una jukumu la kupitia kama sio kurekebisha katiba yote na sio vipengele kwenye katiba..
 
petrol

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
378
250
Pamoja na ukabila na baadhi ya watu kuwa na mapenzi makubwa na Zuma suala la ukosefu wa ajira kwa raia wengi wa Afrika Kusini limechochea ghasia hizo. Asilimia kubwa ya vijana wa nchi hiyo hawana ajira. Siasa na hoja zisizotoa jawabu kwa tatizo hili zitaongeza mafuta kwenye moto unaowaka chinichini. Hivyo suala la Zuma ni kiberiti (kisingizio) kilichokuwa kinasubiriwa kwa muda mrefu.
 
Hapana kaka, ila naelewa io dhana kuna concept similar wanaitwa jellyfish situation ou try to solve one problem the other problem arises, which ni ujumla ya marekebisho ya katiba yetu kwa miaka kadhaa toka marekebisho ya kwanza. Nacho shauri mimi ni sheria itungwe kwanza itakayosimamia recruitment ya watu wazuri katika bunge la katiba before kuanza mchakato ili tusipoteze pesa hata kidogo katika hatua hii.
 
MbantuOG

Member
Mar 7, 2021
30
95
Pamoja na ukabila na baadhi ya watu kuwa na mapenzi makubwa na Zuma suala la ukosefu wa ajira kwa raia wengi wa Afrika Kusini limechochea ghasia hizo. Asilimia kubwa ya vijana wa nchi hiyo hawana ajira. Siasa na hoja zisizotoa jawabu kwa tatizo hili zitaongeza mafuta kwenye moto unaowaka chinichini. Hivyo suala la Zuma ni kiberiti (kisingizio) kilichokuwa kinasubiriwa kwa muda mrefu.
Kabisa na swala hili liko predictable sana kwa nchi za Afrika ndomana nasema tuwe na jinsi yetu ya kipekee ya utekelezaji wa na uundwaji wa katiba zisiwe bandika bandua za watu.
 
MbantuOG

Member
Mar 7, 2021
30
95
Ile Katiba kipindi cha JK ilikwama wapi?
Iliishia mitini guess who were most vocal kwenye lile bunge kisha jiulize wako wapi sasa? imagine rasimu mpya inaanza lakini bado tupo na cyber crime act hii ridiculous mchakato hauwezi kuwa engaged vizuri na mbinumbinu zilezile za awali
 
MbantuOG

Member
Mar 7, 2021
30
95
Haya maelezo ni ya mtu anayekula na kulala sebuleni kwa shemeji yake, hajui uchungu wa UFISADI katika maisha ya kujitafutia.

Zuma alikuwa Rais chini ya ANC, alishinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Hakuna katika katiba ameambiwa afanye ufisadi! Uwepo wa vurugu ni jambo la kawaida katika siasa, anao wafuasi, wafia mtu, anao wafuasi wafia Kabila (Zulu natal Kabila lake ni kubwa), ulitaka katiba izuie vipi vurugu?

Hoja muhimu ni kwamba Rais Zuma ali-resign kwa Ufisadi, shinikizo lilitoka kwa Julius Malema & Co chini ya Economic Freedom Party, katiba imewaruhusu kuandamana, kupinga ndani na nje ya Bunge kwa uhuru (fatilia kashikashi zao Bungeni), katiba imara imewapa Bunge imara. Hapa kwetu Bunge ni mali ya Ndugai na CCM!

Vurugu ni matokeo ya uimara wa Katiba inayoweza kumuwajibisha hata Rais akiwa madarakani. Unashangaa uporaji huu katika vurugu za South Africa wakati hapa kwetu kila taarifa ya CAG kuna uporaji mkubwa kwa karamu!

Zurazura rudi nyumbani kwa shemeji ule ulale.
I have chosen to ignore the messenger and the message. I never believed if a man and his ideas are inseparable. Quick to assume something just uncover your idiocy.
 
Evarist Chahali

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
995
1,000
Haya maelezo ni ya mtu anayekula na kulala sebuleni kwa shemeji yake, hajui uchungu wa UFISADI katika maisha ya kujitafutia.

Zuma alikuwa Rais chini ya ANC, alishinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Hakuna katika katiba ameambiwa afanye ufisadi! Uwepo wa vurugu ni jambo la kawaida katika siasa, anao wafuasi, wafia mtu, anao wafuasi wafia Kabila (Zulu natal Kabila lake ni kubwa), ulitaka katiba izuie vipi vurugu?

Hoja muhimu ni kwamba Rais Zuma ali-resign kwa Ufisadi, shinikizo lilitoka kwa Julius Malema & Co chini ya Economic Freedom Party, katiba imewaruhusu kuandamana, kupinga ndani na nje ya Bunge kwa uhuru (fatilia kashikashi zao Bungeni), katiba imara imewapa Bunge imara. Hapa kwetu Bunge ni mali ya Ndugai na CCM!

Vurugu ni matokeo ya uimara wa Katiba inayoweza kumuwajibisha hata Rais akiwa madarakani. Unashangaa uporaji huu katika vurugu za South Africa wakati hapa kwetu kila taarifa ya CAG kuna uporaji mkubwa kwa karamu!

Zurazura rudi nyumbani kwa shemeji ule ulale.
Unaona sasa? Katiba mpya haiwezi kuleta mabadiliko endapo watetezi wenyewe ni watu wa aina hii. Kama huwezi kuheshimu HAKI ya mwenzio kutoa hoja hapa JF na wewe kutimiza WAJIBU wa aidha kuipuuza au kujibu kiungwana, utawezaje kuheshimu Katiba mpya ambayo inahusu HAKI na WAJIBU wa mwananchi?
 
Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
15,909
2,000
Naitazama katiba mpya kama swala lenye ulazima na tija sana katika uendeshaji wa nchi: Sababu kuu ni moja sheria zetu nyingi zinapwaya na kuhitaji marekebisho kila mara ila sidhani kama kuna mambo muhimu matatu ya kushughulikia nchi hii Katiba itaingia katika miaka mitatu ijayo.

Nadhani kuwe na marekebisho ya acts muhimu tatu hadi tano lakini katiba kwa ujumla wake twende nayo hii, moja iwe ya elimu, ya pili siasa na nyingine (nitapenda kama watu watashauri katika thread hii).

Nadhani ukiangalia nchi kama South Africa (ambao huenda wakawa na Katiba bora kuliko zote Africa) matumizi ya uhuru kwako yamekua mabaya mfano maandamano yamekua kichaka cha uhalifu na unyang'anyi wa mali za watu. Sababu ikiwa katiba yao ni "copy-paste" ya katiba za nchi zilizoendelea na hivo haiko "suitable" na uhalisia wa watu wa Afrika ya Kusini. Kitakwimu makadirio ya Investec Bank Ltd, ni kwamba uchumi utakua kwa chini ya asilimia 4 sababu ya "vuguvugu la kisiasa". Unategemea kwa urahisi tu nchi yenye katiba nzuri kama Afrika kusini huwezi kuta vitu kama hivi lakini in the African Case vipo ndomana nadhani katiba mpya inahitaji muda.

Rasimu ya warioba ilikua nzuri sana lakini ile recruitment ya wabunge wa katiba ilifanya katiba isipite hadi leo kweli kuna mtu anataka kupoteza pesa tena? Bila kubadili acts hizi io "recruitment" tu ya wabunge wa katiba itatujazia watu wasio elewa mapana ya sheria.

Nakaribisha matusi,kejeli,dharau na majadiliano yenye tija vyote kwa pamoja.
Kwa hiyo kama watu hawana ufahamu wa makundi ya chakula yatengenezayo chakula bora waachwe tu wapate unyafuzi?Mpuuzi
 
nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,355
2,000
Haya maelezo ni ya mtu anayekula na kulala sebuleni kwa shemeji yake, hajui uchungu wa UFISADI katika maisha ya kujitafutia.

Zuma alikuwa Rais chini ya ANC, alishinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Hakuna katika katiba ameambiwa afanye ufisadi! Uwepo wa vurugu ni jambo la kawaida katika siasa, anao wafuasi, wafia mtu, anao wafuasi wafia Kabila (Zulu natal Kabila lake ni kubwa), ulitaka katiba izuie vipi vurugu?

Hoja muhimu ni kwamba Rais Zuma ali-resign kwa Ufisadi, shinikizo lilitoka kwa Julius Malema & Co chini ya Economic Freedom Party, katiba imewaruhusu kuandamana, kupinga ndani na nje ya Bunge kwa uhuru (fatilia kashikashi zao Bungeni), katiba imara imewapa Bunge imara. Hapa kwetu Bunge ni mali ya Ndugai na CCM!

Vurugu ni matokeo ya uimara wa Katiba inayoweza kumuwajibisha hata Rais akiwa madarakani. Unashangaa uporaji huu katika vurugu za South Africa wakati hapa kwetu kila taarifa ya CAG kuna uporaji mkubwa kwa karamu!

Zurazura rudi nyumbani kwa shemeji ule ulale.
Kwahiyo wewe ndiyo unajiona uko sahihi kwa fikra zako.

Katiba siyo andiko la hadithi lina siga zake acha kujiona unaomba katiba kwaajili ya ufisadi.

Ufisadi na katiba ni vitu viwili tofauti kabisa jifunzeni kwanza kuheshimu katiba na jitambueni
 
KateMiddleton

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,304
2,000
Iliishia mitini guess who were most vocal kwenye lile bunge kisha jiulize wako wapi sasa? imagine rasimu mpya inaanza lakini bado tupo na cyber crime act hii ridiculous mchakato hauwezi kuwa engaged vizuri na mbinumbinu zilezile za awali
Basi CDM mtulie
 
RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
660
1,000
Pamoja na ukabila na baadhi ya watu kuwa na mapenzi makubwa na Zuma suala la ukosefu wa ajira kwa raia wengi wa Afrika Kusini limechochea ghasia hizo. Asilimia kubwa ya vijana wa nchi hiyo hawana ajira. Siasa na hoja zisizotoa jawabu kwa tatizo hili zitaongeza mafuta kwenye moto unaowaka chinichini. Hivyo suala la Zuma ni kiberiti (kisingizio) kilichokuwa kinasubiriwa kwa muda mrefu.
Kwa nini ukosefu wa ajira wakati mnadai katiba ndio muarobaini wa kila kitu?

Yaliyotokea Kenya, Malawi na huko SA ni kielelezo kuwa katiba sio suluhisho kwa ustawi wa nchi.

Kama nchi uzalishaji wa mali ni mdogo na hauna tija kulinganisha na idadi ya watu wake nchi hiyo daima itakuwa kwenye matatizo tu hata Ghana ni suala la nuda tu nao wataslide kuelekea huko huko.

Tazama nchi zenye uchumi imara kama Botswana na Mauritius tangu uhuru zimekuwa na amani ingawa katiba zao ni nzuri.

So long mtu mweusi huwezi kugeuza mchanga/ udongo kuwa mashine bado umaskini utabaki nao tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom