Katiba Mpya Rais wa Muungano atakuwa na nguvu - Tujifunze Marekani, Urusi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
images



images
images
images

Kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mfumo wa nchi kuwa serikali za zenye mamlaka ya ndani na serikali ya Muungayo yenye mamlaka ya juu na kimataifa, pamoja na shaka la namna yakupata nguvu za kiuchumi kwa serikali ya Muungano, kuna haja ya kujifunza mataifa ambayo yamefanikiwa katika uendeshaji wa mfumo huo ikiwa ni Marekani na Urusi.

Nguvu na mipaka Marais wa Visiwani na Tanganyika
Pamoja na kuwa na hadhi ya rais kwa marais wa Tanzania visiwani na Tanganyika, kwa mtazamo wangu ni sawa tu na hadhi ya Gavana wa State nchini Marekani, pamoja na kwamba ana senator na congress inayoongoza state, katiba ya state na sheria za state, hali kadhalika mamlaka mbalimbali kama usafiri, biashara, leseni, lakini hayo ni mambo yanayoweza kufanyika ndani ya Federal si kimataifa. Inapokuja shughuli za kimataifa ni shughuli ya Rais wa Muungano, ingawa Jamhuri ya Tanzania tumekiuka mara kadhaa jambo hilo kwa kutoa mwanya kwa Rais wa Zanzibar kupenya kimataifa labda kwa ajili ya kuwaridhisha wa visiwani malalamiko yao.

Kiuchumi Jamhuri ya Muungano mapato yafafanuliwe
Mapato ya serikali ya Muungano ni yale yale ambayo yamezoeleka miaka yote, isipokuwa mkorogo ambayo haukuwa wasi kimantiki ndio uliofanya kisieleweke nini ni kwa pato la Muungano ni kipi ni kwa pato la Tanganyika au Zanzibar.

Marekani kodi inapotozwa, iwe katika bidhaa, payroll na mengineyo, kuna utaratibu kama ifuatavyo:
% Federal Tax
% State Tax
% Local government Tax
Kwa makampuni makubwa na wenye mishahara mikubwa Federal Tax ni kubwa zaidi na kwa wale wa kipato cha chini Federal Tax imekuwa reduced na pengine kwa wanaofanya kazi part time federal Tax wanasamehewa kwa sababu ya kipato cha chini.

Dr. Hadji Semboja chuo kikuu Dar ameteleza kwa utetezi wake
Kulinganisha mfumo wa kifalme wa Uingereza na serikali za kidemokrasia ameteleza, maana mfumo na utendaji ni tofauti mno. Kama msomi alitakiwa kuwa mpana na mchambuzi wa kuangalia mifumo ile ambayo sisi tunaiga katika uendeshaji wa serikali, maama taifa la Tanzania si la kifalme kama Uingereza.

Tuondoe shaka na kujifunza kwa wenzetu
Kwa utaratibu huu sioni tatizo la kuhofia mapato ya Serikali ya Muungano kama tutajifunza hawa wenzetu walivyofanikiwa. Sikubaliani na shaka la baadhi ya watu kufikiria mamlaka na nguvu ya serikali ya Muungano kudhoofu kwa sababu ya serikali ya Tanganyika na Zanzibar, kama ingekuwa hivyo kwa nini serikali ya Mapinduzi haikudhoofika kwa miaka karibu hamsini?

Iwapo rasimu hii itakukubalika mfumo wa serikali Tatu, basi mipaka ya utendaji iwekwe wazi na iheshimiwe, hali hiyo itaoondoa mwingiliano wa mamlaka na utendaji katika serikali za shirikisho na serikali ya Muungano. Pia serikali za shirikisho zitategemea nguvu za serikali ya Muungano kwa vile kimataifa hazina nafasi ya kupenya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom