Katiba Mpya: Rais mmoja wa Shirikisho,Zanzibar na Tanganyika kuwa chini ya Magavana

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
147
Rasimu sifuri ya Katiba mpya iliyoandaliwa na CUF imeonesha kuvunja muungano wa Tanzania na kuleta msigano kati ya CUF Bara na CUF Zanzibar hasa baada ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuonekana kuwa kuna maslahi ya wachache yatapotea...

Mwaka jana 2010, Zanzibar ilifanya mabadiliko yake ya Kikatiba na iliunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Mbali ya kuendelea kuihifadhi nafasi ya Raisi wa Zanzibar, iliunda nafasi nyengine mbili za Makamo wa Kwanza na Makamo wa Pili wa Rais ambazo zinashikiliwa na Waheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Ali Iddi.

Na hapa ndipo kinapoingiya kidonge cha kwinini kilichovishwa ganda la sukari. Mwanzoni mwa mwaka huu mpya wa 2011 na katika kuitangaza rasimu ya Katiba Mpya iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 130 na iliyochukuwa miaka minne kuitengeneza, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alinukuliwa kusema kuwa ”rasimu hiyo inavunja Muungano wa Tanzania unaoundwa kati ya Tanganyika na Zanzibar na kuunda Serikali ya Shirikisho litakalokuwa chini ya rais mmoja.”

Kwa mujibu wa rasimu hiyo Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, ataitwa GAVANA. Ni kama vile California inatawaliwa na Gavana Arnold Schwarzenegger basi Zanzibar itakuwa na Gavana wake na Tanganyika itakuwa na Gavana wake. Magavana hao watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na Katiba ya Tanganyika.

Rasimu hiyo inatamka kinagaubaga:

”Jamhuri ya shirikisho la Tanzania ni nchi moja yenye dola moja na vyombo mbalimbali vya utekelezaji wa mamlaka ya dola na Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na gavana.”

Kwa maana hiyo Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (BLW) litakuwa linauendesha Mkoa wa Zanzibar. Suala si tena Zanzibar ni nchi au si nchi, au Zanzibar ni nchi huru au si huru. Suala na jawabu yake ni Zanzibar ni Mkoa na ili Wazanzibari tusishituke na tujione kuwa tuko SAWA na wenzetu, basi na Tanganyika pia itakuwa Mkoa na itakuwa na Gavana wake!

Kutakuwa na Raisi wa nchi mpya iitwayo Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania ambayo itakuwa na Raisi wake. Zanzibar Mkoa na Gavana wake na Tanganyika Mkoa na Gavana wake. Nguvu ziko wapi? Kwa Raisi wa Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania ambaye ataitawala nchi moja, dola, moja, na yenye mipaka yake. Na Rasi huyo ataweza: ”kutangaza hali ya hatari katika jamhuri ya shirikisho la Tanzania au katika sehemu yake yoyote, ikiwa nchi iko vitani, hatari ya kuvamiwa, hatari ya kuvurugika kwa amani na usalama wa raia na tukio la balaa la kimazingira.” Maana yake tukija kutanabahi kuwa tumegeuzwa Mkoa na tunatawaliwa na Gavana basi tusije tukalia na mtu!

Mambo yako wazi kama kama mchana na jua lake. Sasa tujiulize.

a. Katiba ya aina hii si inatupeleka kule kwenye Serikali Moja na inazidi kuishindilia Zanzibar ndani ya tumbo jipya la Danganyika?
b. Kweli inaingia akilini Chama cha Wananchi CUF kwa upande wa Zanzibar wataweza kukubaliana na Katika Mpya ya aina hii wakati juzi tu wameunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kuitangaza mipaka ya Zanzibar na kuongeza Mamakamo wake wawili wa Urais mbali ya Rais wa Zanzibar?
c. Katiba hii ni kweli inayawakilisha matakwa ya Zanzibar na ya Wazanzibari au inanukia harufu ya CHADEMA ambayo mkubwa wake amenukuliwa kusema kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika?

Source: Mzalendo
 
Tuache ubinafsi, ni vyema tuwe na shirikisho na rais mmoja tu! ama tuwe na marais watatu (tanganyika, zanzibar na shirikisho).
 
Kwenye muungano hapo ngoma itakuwa nzito!

Viongozi kama sikupenda sana madaraka, tungesema tuwe na nchi moja tu.
 
Back
Top Bottom