Katiba mpya;ni fursa pekee ya kuthibiti safari za raisi na uundwaji wa tume za uchunguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya;ni fursa pekee ya kuthibiti safari za raisi na uundwaji wa tume za uchunguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Oct 14, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,822
  Trophy Points: 280
  Wadau wote hasa sisi wana jf tumelalamika mno kuhusu safari za mara kwa mara za raisi na uundwaji wa tume za uchunguzi ambazo kwa uhalisia tume hizi nyingi zimekuwa ni za kichina tu.

  Kuhusu safari za viongozi na hapa msisitizo ni raisi wa nchi tutumie mikutano ya katiba mpya ktk maeneo yetu na mimi ningependekeza kama ifuatavyo:-
  1.Katiba iweke idadi maalum ya wajumbe wanaopaswa kusafiri na raisi kulingana na shughuli husika ktk ziara hiyo na isiwe ni maamuzi ya raisi na washauri wake kuamua ni nani aende na nani abaki.
  2.Katiba iainishe mambo/shughuli ambazo raisi anakuwa na uhalali wa kuzifanya ktk ziara hizo na kama hazipo basi awakilishwe na wasaidizi wake.
  3.Katiba iweke ukomo wa safari za raisi nje ya nchi ktk kipindi fulani labda kama kuna jambo la dharuru na lenye ulazima kwa yeye kusafiri.Haiwezekani raisi kusafiri zaidi ya mara 3 au hata 4 ndani ya mwezi mmoja wakati anawasaidizi wanaolipwa ili kumsaidia.Tutafafakari athari za kukosekana kwake ofisini mara kwa mara.

  Kuhusu tume za uchunguzi.Hii ni kero nyingine kwa watanzania na ni bora kupitia katiba mpya tukadhibiti utaratibu unaotumika kuunda na kutangaza matokeo ya uchunguzi wa tume hizo.Tume nyingi ni feki,habibu za rejea za kisanii na matokeo/mapendekezo ya tume hizo ni ya kichinachina tu.

  Kwa upande wangu nashauri kama ifuatavyo:-
  1.Iwe ni marufuku kwa mtu/kiongozi yeyote kushiriki ktk uundaji au uteuzi wa wajumbe wa kamati ambayo yeye kama kiongozi ni mtuhumiwa au analalamikiwa kwa namna yoyote ile.
  2.Katiba iweke ukomo ktk utekelezaji wa mapendekezo ya tume yoyote ladda kama kuna sababu maalumu na za msingi za kuongeza au kupunguza muda.
  3.Katiba itamke wazi kuwa ni makosa kwa wanaopaswa kutekeleza mapendekezo ya tume na itamke hatua za kinidhamu zinazopaswa kuchukuliwa kwa kiongozi/mtumishi anaeshindwa kutekeleza mapendekezo ya tume husika.
  4.Katiba itamke wazi kuwa ni lazima ndani ya muda fulani, isipokuwa kama kuna sababu maalumu, taarifa na mapendekezo ya tume shariti yawe yametangazwa hadharani kwa umma na isiwe ni uamuzi wa kiongozi mmoja kuamua kutangaza au kuyaweka kabatini.
  5.Katiba itamke wazi kuwa ni kosa la jinai kwa kiongozi kutotangaza taarifa na mapendekezo ya tume husika.
  6.katiba ipige marufuku uundaji wa tume za uchunguzi wa mambo ambayo ushahidi na taarifa za tukio husika ziko wazi kabisa.

  Wadau mimi haya ni mawazo yangu ila na wewe unaweza kuyaboresha na hata kuongeza yakwako na kuyafikisha yanakohusika.Tusiwe watu wa kulalama tu ila tutimize wajibu wetu kwa kutumia fursa zilizipo na hii katiba mpya ni fursa muhimu sana kwetu.

  Kila mtu ana wajibu ktk viti hii ya ukombozi wa taifa letu pale alipo na kwa nafasi aliyonayo.
   
Loading...