Watanzania tumekuwa chini ya serikali yetu ambayo kila mtu anaifahamu. Kila awamu imekuwa ikiingia madarakani kwa ushawishi na mikakati mbalimbali na kila awamu imekuwa na aina yake ya utandaji. Awamu iliyopita tuliona ikija kwa mambo mengi yakiwemo "nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya kabila haijabadirika na kuwa 'Nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi". Bila shaka tuliona sote namna ambavyo ufisadi, ubabe na hujuma kwa taifa nguvu zaidi, kasi zaidi na ari zaidi.
Awamu hii imekuja kwa "hapa kazi tu" ambacho kinaonekana ki nadharia zaidi, kikisukumwa na uigizaji wa watendaji na kuimarishwa na nguvu ya vyombo vya habari. Ni nini kimeboreka tangu hapa kazi na utumbuaji wa majipu umeanza zaidi ya propaganda tu? Kila siku watu wanakufa hospitalini kwa kukosa huduma za afya, hakuna ajira vijana wanateseka mitaani bila kujua wafanya nini kila kitu wanachokifikiria hakiko supported kiasi wanajiona ni yatima. maisha magumu, uchumi mbaya makampuni yanapunguza wafanyakazi; majipu mengine yanajisifu kwamba hayatumbuliki na ukweli unabakia kuwa pale pale kwamba majipu halisi yatatumbulika tu pale ambapo serikali itajibainisha na kujipambanua kuwa ni kitu tofauti na ccm ambayo ndiyo majipu yenyewe.
Ninaomba sasa Watanzania, tuachane na episode ya majipu ambayo bila shaka imethibiha kwau haina tija yoyote zaidi ya ku divert attentions za watu kutoka kwenye machungu ya ccm ya miaka 50+, na kuwapeleka cinema hall wakabadilishe mawazo. Cinema hall unaona jamaa kapiga deal, kafanikiwa na kuwa millionaire, anaona wake wazuri, anajenga nyumba safi na anamiliki kisiwa chake na ndege za kisasa, anamiliki jeshi lake, anaoa mke mzuri nk. Ukirudi nyumbani, unakuta bado kitanda chako cha teremka tukaze, maharage chukuchuku, kodi ya nyumba unadaiwa na bill ya maji iko mlangoni, hujui kesho itakuwaje.
Hii ya majipu ni sawa na wale wanaokula msoto jeshini halfu jioni wanapelekwe disco kuimba nyimbo ili angalau wasahau karinyekarinye za mchana tayari kwa fatiki za RSM na Ma Buriji ya dharura usiku kibao. Hii majipu episode kila mwenye ufahamu ameona namna ambavyo hayatransform chochote na hata kama kuna impact ni ya juu juu tu, kwa watu aina fulani na haina mzizi wowote wa kuleta sustainable changes zaidi ya show.
Ninaomba Watanzania wachache (ninajua ni wachache) watakaonielewa waniunge mkono kwa kutumia chochote Mungu alichowapa kama ni intellectual ability, influence, n.k tuanze seriously mkakati wa kudai katiba mpya. Katiba mpya ndiyo kitu pekee kitamkomboa Mtanzania. Katiba ya Wananchi na tuanzie pale tume ya warioba ilipoishia. Tusimame imara katika muundo wa bunge la maalumu la katiba ili lisitengenezwe na wabunge wa bunge la JmT.
Bila katiba mpya, ndugu zangu tutaendelea kuishi utumwani mwa ujanja wa watu wachache na hatutakuwa n ahatima yoyte sisi ni uzao wetu. Mwenye ufahamu bila shaka anaelewa kinachoendelea na malengo yake ni nini. Suala la katiba tulianze sasa tusisubiri dkaika za majeruhi ili kuwe na sababu zingine za muda hautoshi, tume iko busy, budget hatuna, tupige kura ya jumla n.k.
Mpumbavu hujifunza kwa maumivu ya makosa yake ambayo bila shaka tumeyaona na ninaomba tusirudie. Mwerevu hujifunza kwa makosa ya wenzake wala hakubali kufanya walipokosea wengine.
Mchana mwema.