Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima sii hiyari, tudai vyote

...priority ya kila moja wetu ni kuangamiza ccm kwa vyovyote vile.
 
Kutokana na yaliyojitokeza sehemu mbalimbali hapa nchini kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,ni ukweli usiopingika kwamba pamoja na mambo mengine ya msingi pia inahitajika sana Tume Huru ya Uchaguzi, tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.Ukifuatilia kwa makini sehemu nyingi kulikotokea uvunjifu wa amani ni kwasababu haki uhuru na uwazi vilikosekana.Kama wadau wa amani na utulivu katika nchi yetu ni vizuri sana kwa kila mpenda haki na kila raia mwema, anayeitakia heri nchi hii akapaza sauti kwa njia yoyote iliyo njema ili kuhakikisha inakuwepo tume huru ya uchaguzi itakayoridhiwa na wadau wote,ambayo haitatiliwa mashaka hata kidogo.
Pamoja na kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni vema ikaendana na mchakato wa kuhakikisha usalama wa hizo kura zitakazopigwa kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi.Tunda la amani na utulivu ni haki,ukiiondoa haki na uwazi ulio dhahiri ni vigumu sana amani na utulivu vikaendelea.
Kila mmoja kwa sehemu yake akiweza ashiriki kuchangia ili tume iwe huru na ya haki inatakiwa iweje?.Nawasilisha.​
 
Mpaka sasa nashindwa kuelewa kwanini wapinzani hawalioni hilo, wao wana 'ngangana na serikali tatu !!!!!!
UKAWA
ebu angalieni swala la​ TUME HURU YA UCHAGUZI.
 
Mpaka sasa nashindwa kuelewa kwanini wapinzani hawalioni hilo, wao wana 'ngangana na serikali tatu !!!!!!
UKAWA
ebu angalieni swala la​ TUME HURU YA UCHAGUZI.

Mheshimiwa kwa kupaza sauti kama ulivyoandika hapa ndipo tunaamushana maana hakuna mwanadamu aliyekamilika!TUME HURU YA UCHAGUZI ni muhimu sana kwa majira ya sasa.Watanzania wa miaka ya 1950,siyo watanzania wa leo,wengi wameanza kujitambua sana na ni vigumu kuendelea kuwadanganya!
 
Kutokana na yaliyojitokeza sehemu mbalimbali hapa nchini kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,ni ukweli usiopingika kwamba pamoja na mambo mengine ya msingi pia inahitajika sana Tume Huru ya Uchaguzi, tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.Ukifuatilia kwa makini sehemu nyingi kulikotokea uvunjifu wa amani ni kwasababu haki uhuru na uwazi vilikosekana.
Kama wadau wa amani na utulivu katika nchi yetu ni vizuri sana kwa kila mpenda haki na kila raia mwema, anayeitakia heri nchi hii akapaza sauti kwa njia yoyote iliyo njema ili kuhakikisha inakuwepo tume huru ya uchaguzi itakayoridhiwa na wadau wote,ambayo haitatiliwa mashaka hata kidogo.
Pamoja na kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni vema ikaendana na mchakato wa kuhakikisha usalama wa hizo kura zitakazopigwa kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi.Tunda la amani na utulivu ni haki,ukiiondoa haki na uwazi ulio dhahiri ni vigumu sana amani na utulivu ikaendelea.Kila mmoja kwa sehemu yake akiweza ashiriki achangie ili tume iwe huru ya uchaguzi ipatikane kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Wakuu salaam.

Kwa upande wa Tdm, atleast leo kumetulia. Hii ni baada ya kuachiwa kwa Diwani na wananchi wengine 80 waliokuwa wakishikiliwa na jeshi la polisi. Ujio wa mbunge wa jimbo hili Mh David Silinde nao umechangia utulivu wa wananchi.

Baada ya utangulizi huo naomba niende kwenye mada moja kwa moja..

Inasemekana wakati wa mkutano wao kati ya kituo cha Demokrasia nchini chini ya John Cheyo na Rais Jakaya Kikwete, walikubaliana pamoja na mambo mengine...

Kuahirisha Bunge maalumu la Katiba (Ambalo hata hivyo halikuahirishwa)
Kupeleka Mswada wa Mabadiriko ya sheria ya uchaguzi ili KUUNDA TUME HURU YA UCHAGUZI

Sasa huo Mswada unapelekwa lini Bungeni? Au ni ktk Bunge hili linaloendelea huko Dodoma? Je kambi ya upinzani Bungeni haioni kwamba inachezewa akili kwa kuahidiwa vitu visivyotekelezwa? (Maana walianza na kutokuahirisha BmK) Je kambi ya Upinzani Bungeni mnachukua hatua gani kwa hili? Je kuendelea kulalamika ni hatua muafaka ya kuendelea kuchukua?. Kama msingi mkuu wa Amani kuelekea Uchaguzi mkuu uko ktk Tume hii (Maana ndiyo inayosimamia chaguzi zote kuanzia, Udiwani,Ubunge mpaka urais) Je Kambi ya upinzani Bungeni haioni kuwa huu ni wakati muafaka wa KUILAZIMISHA Serikali kuchukua hatua madhubuti juu ya jambo hili?

Au tunataka watu wafe wawe vilema. ndipo tuchukue hatua? Hapana huu ni wakati wa kutenda. Tukumbuke huu ni mwezi wa tatu (Tunamiezi saba mpaka sasa kuelekea kwenye uchaguzi) Na Bunge la mwezi wa sita ni Bunge la Budget, mpaka mwezi wa saba (Sidhani kama Mswada husika utapelekwa) Toka hapo kikao kingine cha Bunge ni mpaka mwezi wa tisa (kama siko sahihi) Je wiki mbili zinatosha kujadiri mabadiriko ya sheria husika pamoja na mambo mengine?

Itakuwa ni makosa makubwa sana kwenda kwenye uchaguzi huu, tukiwa na Tume hii ya Jaji Lubuva na Madudu yake. Sote tunafahamu kuanzia utaratibu wa kuhesabu kura mpaka kutangaza matokeo ni Kizungumkuti..!! Na walishatangaza ni marufuku kuhoji popote wala kutaka nakala ya matokeo husika ama kuhakikisha namna kura zilivyopatikana na kuhesabiwa (Hii ni kwa Urais) Je tuko tayari kwenda kwenye uchaguzi na Tume hii??

Tuchukue hatua sahihi.
Wakuu nawasilisha.

BACK TANGANYIKA
 
Sasa huo Mswada unapelekwa lini Bungeni? Au ni ktk Bunge hili linaloendelea huko Dodoma? Je kambi ya upinzani Bungeni haioni kwamba inachezewa akili kwa kuahidiwa vitu visivyotekelezwa? (Maana walianza na kutokuahirisha BmK) Je kambi ya Upinzani Bungeni mnachukua hatua gani kwa hili? Je kuendelea kulalamika ni hatua muafaka ya kuendelea kuchukua?. Kama msingi mkuu wa Amani kuelekea Uchaguzi mkuu uko ktk Tume hii (Maana ndiyo inayosimamia chaguzi zote kuanzia, Udiwani,Ubunge mpaka urais) Je Kambi ya upinzani Bungeni haioni kuwa huu ni wakati muafaka wa KUILAZIMISHA Serikali kuchukua hatua madhubuti juu ya jambo hili?

Hilo jambo ilitakiwa liwemo kwenye katiba mpya.Lakini UKAWA wakatimka.Wengine tulipinga kwa nguvu zetu zote na kulaani kitendo cha UKAWA kususia bunge la katiba kwa sababu tulijua ndani ya bunge lile kulikuwa na mengi yaliyotakiwa kujadiliwa likiwemo hilo la Tume huru ya uchaguzi kuwekwa katika katiba pendekezwa.Lakini UKAWA wakajikita tu kwenye serikali tatu wakatoroka bungeni utadhani Katiba mpya kazi yake ilikuwa kujadili serikali tatu tu!!!

Sasa mleta maada unakumbuka shuka wakati kumekucha.Walisusa bunge la katiba, na wamesema watasusa na kupiga kura ya maoni ya katiba. Naaamini katiba pendekezwa itapita KWA KISHINDO sababu ile si ya vyama vya siasa wala taasisi za dini zinazopiga yowe.Ikipita sijui UKAWA wataingia uchaguzi au watasusa sababu ikishapigiwa kura ya ndiyo ikapita hiyo ndio itatumika uchaguzi ujao.Hapo sasa ndio UKAWA watatafuta kichaka cha kujisaidia.
 
kwani tanzania tatizo ni sheria tatizo ni huo utekelezaji ivi ccm watakubali tume iwe huru huku wakijua kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi?
 
haiko huru kwa maana inaundwa na watu waliochaguliwa na raisi tu!!!

Raisi anachaguliwa na walio wengi waliopiga kura.Na wanampa kura kwa sababu wana imani na maamuzi yake ikiwemo kuunda tume huru ya uchaguzi.Yeye anakuwa kachaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge yeyote na kwa nchi nzima tofauti na mbunge.Hivyo Raisi anakuwa anaaminiwa zaidi na ndio maana kapewa kura na majority kwa kuwa majority wanamwamini.Ulitaka mbunge wa kwahani aliyepata kura mia 300 wakae na mbunge wa kwamtipura aliyepata kura 400 kuingia bungeni ndio wakae waunde tume huru ya uchaguzi?
 
East African Eagle, unatoa hoja as if wewe unaunga mkono juu ya uwepo wa tume hii na hili sishangai maana najua maslahi mpatayo wewe na chama chako (Ingawaje sikupenda kujadiri kuhusiana na uvyama)

Pia tambua Tume huru ya uchaguzi ipo kwenye Katiba inayopendekezwa (Ya wachache) lakini je umeambiwa kwamba hiyo Katiba inayopendekezwa itakapo pita hapo hapo itaanza kufanya kazi? (Hata kama Tume yenyewe imewekwa ndivyo sivyo kwenye katiba yenu) Lakini ninachotambua ni kwamba Hata kama TUME HURU INGEKUWAPO KWA USAHIHI kwenye Katiba husika, KAMWE isingetumika kwenye uchagyzi huu maana ingehitaji sheria mbali mbali kubadirishwa ili kuendana nayo.

Hii ndiomaana Kikwete na Kituo cha Demokrasia walikubaliana kubadirisha sheria husika, Je unadhani walikuwa hamnazo?

Acha propaganda kwenye mambo ya msingi ndugu yangu.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
lakini je umeambiwa kwamba hiyo Katiba inayopendekezwa itakapo pita hapo hapo itaanza kufanya kazi?
Rais alishatamka kuwa ataangalia uwezekano wa katiba mpya kutumika katika uchaguzi ujao kwa kuitisha bunge lipitishe sheria mapema ili uchaguzi ujao ikiwezekana ufanyike chini ya katiba mpya kama itapita.Hilo lipo.
 
Back
Top Bottom