DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 302
- 274
Wanabodi,
Mfumo wa vyama vingi ulianzishwa Tanzania kwa madhumuni ya kuruhusu vyama mbadala kushiriki katika kila chaguzi na kuenzi suala zima la demokrasia kwa kuwa wezesha wananchi kuchagua viongozi wao baada ya kusikiliza na kuelewa sera tofauti tofauti.
Demokrasia zilizo komaa huwezesha mabadiliko mazuri ya kila awamu ya uongozi. Mabadiliko haya ya uongozi yanatakiwa yafanyike vizuri hata katika vipindi ambavyo chama tawala kinashindwa uchaguzi wa urais na hivyo kutakiwa kuruhusu chama cha upinzani kushika wadhifa mkubwa wa uongozi kuliko yote. Lakini je mifumo iliyopo ina uwezo wa kuruhusu mabadiliko haya?
Katika uongozi, aliye katika nafasi ya juu hutegemea sana walio katika nafasi za chini kutekeleza wadhifa wao. Kwasababu hiyo rais yeyote hawezi kufanya kazi yake vizuri bila vyombo mbalimbali vya usalama.
Vyombo hivi ni kama idara ya usalama wa taifa, polisi, jeshi la wananchi bila kusahau watumishi wa umma katika sekta tofauti tofauti serikalini kama vile ofisi ya rais, ofisi ya makamu wa rais, ofisi ya waziri mkuu, ikulu, bunge na wizara zote kwa ujumla.
Swali zito ambalo wote tunatakiwa kujiuliza ni kama waliopo kwenye vyombo hivi wanaweza kuheshimu maamuzi yoyote yanayoweza kufanywa na wananchi na kumpokea mgombea yeyote wa chama chochote madarakani.
Katika demokrasia ya ukweli na demokrasia iliyo komaa, vyombo hivi vyote vinatakiwa kuweza kushirikiana na chama chochote cha siasa na kwasababu hiyo, kuna umuhimu wa kuwa "Neutral" na kusisitiza utanzania kwanza.
Jambo ambalo sisi wananchi hatu fahamu ni kama wahusika wa vyombo hivi wana pendelea zaidi chama tawala kuendelea kubaki madarakani. Kama hii ni kweli, basi kuna "Forces" nyingi sana zinazo hakikisha kwamba chama tawala kina endelea kubaki madarakani na demokrasia yetu siyo ya kweli.
Nawasihi wana JF wenzangu waendelee kutafakari haya yote. Labda tume huru ya uchaguzi na katiba mpya havina uhusiano mkubwa katika suala zima la kuwa na siasa zenye ushindani.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.