Katiba Mpya na Janja janja za wenye Maslahi binafsi Madarakani

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
Katiba inabeba msingi mzima wa mahusiano baina ya watu na watu na pia watu na mamlaka katika nchi.

Tuna malalamiko ya msingi kuhusiana na mahusiano haya hapa nchini. Hatuko sawa mbele za haki. Hatuko sawa mbele ya sheria. Pana upendeleo wa wazi ambapo waliopo madarakani kama wawamba ngoma wamejivutia mengi zaidi kwao.

Wao hata kodi hawalipi. Mamlaka zinazotudhulumu sisi zinawajibika kwao.

Watu wa namna hii wanautoa wapi ujasiri wa kutuzungumzia sisi kuhusu kutokuwepo umuhimu wa mustakabala au katiba mpya?

Mnufaika mkuu wa katiba iliyopo sasa hivi ni rais wa JMT na wapambe wake. Wanaupata wapi ujasiri wa kutuongelea sisi kuhusu katiba mpya hawa.

Kistaarabu walipaswa hata kukaa kimya wakatuacha tuliowaathirika wa yaliyopo tukajadili kuona ni mustakabala upi ulio bora kwetu sote.

Tulipo ni wazi kuwa Samia hana nia ya kuwepo kwa mustakabala mpya unaoweza kutatiza adhma yake ya kusalia madarakani baada ya 2025.

Rais Samia ni "loser" yeye binafsi kama "individual" kwa kuridhia katiba mpya au tume huru kabla ya 2025.

Rais Samia na wapambe wake wakiwamo kina Majaliwa hawawezi kuuridhia ujio wa katiba mpya au tume huru kabla ya 2025, kama tutawapa nafasi hiyo.

Options zilizopo ni mbili tu. Hakuna katikati:

1. Kuridhia wanayoyataka wao kuwa hakuna Katiba mpya wala tume huru kabla ya 2025 na kuwaacha wafanye yao kwa starehe zao.

Au,

2. Kusimama imara na kupambana nao kidete kuidai katiba mpya kwa nguvu zote hadi kupatikana sasa.

Michezo ya kukimbizana nao kama paka na panya haiwezi kutulipa.

Muhimu tukafahamiana uchaguzi wetu ni upi baina ya haya mawili.

Tutoke kuvaana nao au tuachane na hii biashara sasa.
 
Katiba inabeba msingi mzima wa mahusiano baina ya watu na watu na pia watu na mamlaka katika nchi.

Tuna malalamiko ya msingi kuhusiana na mahusiano haya hapa nchini. Hatuko sawa mbele za haki. Hatuko sawa mbele ya sheria. Pana upendeleo wa wazi ambapo waliopo madarakani kama wawamba ngoma wamejivutia mengi zaidi kwao.

Wao hata kodi hawalipi. Mamlaka zinazotudhulumu sisi zinawajibika kwao.

Watu wa namna hii wanautoa wapi ujasiri wa kutuzungumzia sisi kuhusu kutokuwepo umuhimu wa mustakabala au katiba mpya?

Mnufaika mkuu wa katiba iliyopo sasa hivi ni rais wa JMT na wapambe wake. Wanaupata wapi ujasiri wa kutuongelea sisi kuhusu katiba mpya hawa.

Kistaarabu walipaswa hata kukaa kimya wakatuacha tuliowaathirika wa yaliyopo tukajadili kuona ni mustakabala upi ulio bora kwetu sote.

Tulipo ni wazi kuwa Samia hana nia ya kuwepo kwa mustakabala mpya unaoweza kutatiza adhma yake ya kusalia madarakani baada ya 2025.

Rais Samia ni "loser" yeye binafsi kama "individual" kwa kuridhia katiba mpya au tume huru kabla ya 2025.

Rais Samia na wapambe wake wakiwamo kina Majaliwa hawawezi kuuridhia ujio wa katiba mpya au tume huru kabla ya 2025.

Options zilizopo ni mbili tu, hakuna katikati:

1. Kuridhia wanayoyataka wao kuwa hakuna Katiba mpya wala tume huru kabla ya 2025 na kuwaacha wafanye yao kwa starehe zao.
2. Kusimama imara na kupambana nao kidete kuidai katiba mpya kwa nguvu zote hadi kupatikana sasa.

Michezo ya kukimbizana nao kama paka na panya haiwezi kutulipa.

Muhimu tukafahamiana uchaguzi wetu ni upi baina ya haya mawili.

Tutoke kuvaana nao au tuachane na hii biashara sasa.
Wakiridhia ombi la wengi la katiba mpya watabarikiwa ila wasipo sikia watalaaniwa.
 
Hawana haja ya mibaraka. Walikoifikisha ngozi ya ngoma hapa duniani haipo mibaraka zaidi.

Ni kuwa katiba mpya au tume huru hawataridhia kabla ya 2025.

Uamuzi uko mikononi mwetu.

Ni vyema tukaamua sasa:

1. Kama vipi tuachane nayo.
2. Kama vipi tukomae vilivyo sasa.

Katikati haipo. Katikati ipi?
 
Nini kisichojulikana kwenye mpambano mtakatifu huu? Ninakazia:

"Tutoke kuvaana nao au tuachane na hii biashara sasa."
 
Hata mimi wakitamka neno "KANDA SIELEWI" huwa nini maana yake!?

Tuwaandalie!

images.jpg

download.jpg
 
Back
Top Bottom