Katiba Mpya Mwarobaini Uchumi wa Viwanda

Nervousity

Member
Nov 3, 2017
21
14
Ni sahihi sana kuhusianisha katiba iliyopo na kukwama kwa maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo maendeleo ya viwanda kwani yapo mambo kadhaa ambayo kwa pamoja huzonga zonga ukuaji na kuendelea kwa jamii. Katika mengi yaliyopo ninaamini katiba inaweza kuchukua nafasi ya kwanza katika ama kukwamisha au kuharakisha maendeleo katika nyanja zote.

Ni muhimu katiba iwe ndio msingi pekee wa kusimamia uwajibikaji wa mihimili yote; yaani dola, bunge na mahakama na kila raia kwa nafasi yake. Ni lazima katiba izibe mianya kwa mtu, taasisi au mhimili wowote katika kurudisha nyuma maendeleo ya jamii katika nyanja za uchumi, siasa, kijamii, kiutamaduni n.k. kwani nyanja zote hizo ni muhimu kwa maisha ya watu.

Ni dhahiri shahiri kuwa nia njema na maono aliyonayo Mh. John Joseph Pombe Magufuli kutaka Tanzania iondokane na utapiamlo wa maendeleo KATIBA MPYA ilipaswa kuwa kipaumbele chake cha kwanza hata kabla ya mambo mengine yote katika awamu hii ya kwanza ya uongozi wake. Katiba hii ingejenga misingi ya uwajibikaji kwa kada zote kuanzia rais mwenyewe hadi mnyonge wa tabaka la chini.

Katiba Mpya ingerejesha Moyo wa Uzalendo kwani jamii yote ya Watanzania ingekuwa sawa chini ya Katiba na chini ya Sheria. Uzalendo ungeimarika tu pale ambapo kila mtanzania angewajibika kwa makosa yake kisheria bila kujali cheo, hali au hadhi na si kwa kuambiwa tuwe wazalendo.

Katiba iliyopo ilitoa mianya mingi ambayo ilisababisha wenye dhamana ya uongozi na maendeleo ya nchi watumie vibaya madaraka yao na kuifanya nchi kuwa shamba la bibi. Kwa sasa ni kama vile nchi imejitawala kwa mara ya kwanza kutoka kwa wakoloni kiasi cha kuanza kuzungumzia umuhimu wa viwanda sasa.

Ili tutoke hapa tulipo tukubali pasi shaka kwamba kuna mahali tulikosea na sasa tuujenge upya mfumo wa uwajibikaji kwa wote kwa kuruhusu na kukubali uhitaji wa KATIBA MPYA sasa kuliko wakati mwingine wowote ule na hivyo kuwepo mazingira ya kila namna yanayoruhusu ukuaji wa uchumi wa viwanda kwani tiba itakuwa ilishapatikana (Mwarobaini).

Ninaamini KATIBA MPYA itakuwa ndio tiba namba moja ya maradhi ya viwanda.
 
Thread yako ni nzuri lakini kwasasa nchi inaongazwa na wa.......
 
Eti mukuu wa mukowa., nirivopita hapa kuomba kura niriahidi katiba mpya.??
 
Back
Top Bottom